
Ndoto za mashabiki wa muziki kuwaona tena Nguza Viking(Babu Seya) na Papii Kocha(Mwana wa Mfalme) wakilipanda tena jukwaa la uraiani kutoa burudani,hususani katika wimbo wao maarufu wa Seya,leo zimefikia ukingoni.Rufaa yao imekataliwa.Hata hivyo,kwa mujibu wa mtandao wa Global Publishers,watoto wawili,Francis na Mbangu, wameachiwa huru!
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Natalia Kimaro, Salum Massati baada ya kupitia kwa makini rufaa hiyo, iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Neema Chusi, wamewaachia huru vijana hao baada ya kuridhika na hoja za upande wa utetezi kuwa hawakuhusika katika tukio hilo lililohusisha familia hiyo mwaka 2003.
Kwa maana hiyo,Babu Seya na mwanae mmoja Papii Kocha,wamerudishwa Ukonga kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha inayowakabili.
Picha kwa hisani ya Global Publishers
Feedback / Comments
9 Responses to “BABU SEYA NA PAPII KUTEKETEA JELA;FRANCIS NA MBANGU WAPO HURU”
Leave a Reply


sending...
hakika hao watu wameonewa tena saana inabidi mahakama iangalie upya kama kuna sheria hiyo
Januari 2 niliandika habari kuhusu James Bain (55). Mmarekani ambaye aliachiwa huru baada ya kutumikia miaka 35 kati ya kifungo cha maisha alichohukumiwa akiwa na miaka 19 kwa kukosa la kubaka.
Na ktk bandiko hilo nilinukuu taarifa kuwa “James Bain sasa atalipwa $50,000 kwa kila mwaka aliokaa gerezani. Ina maana Jimbo la Florida litamlipa takribani dola milioni 1.75 muda mfupi ujao”
Na kati ya maswali niliyoulia ni kuwa “Pengine Babu Seya na wanawe wote ni watu huru, ama kati yao kuna aliye / walio huru ama wote wana hatia, lakini kama kipimo hiki (DNA)kingetumika basi tusingekuwa na mgongano wa mawazo uliopo sasa. Watu wamehusisha kesi yake na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sanaa ya muziki na hata kuwahusisha vigogo wa serikalini.
Lakini ni kwanini tusifanye kitu kwa usahii kwa mara ya kwanza? Na kama kuna ambao ni watu huru huko magerezani (na kwa habari nilizokuwa nasikia kuhusu kubambikiziana keshi nina hakika wapo), ni kwa muda gani tutaendelea kuwashikilia? Na siku wakija kugundulika kuwa walifungwa kimakosa ni nania wa kubeba gharama za kuwafidia? ”
“Ni maisha mangapi yanawekwa pasipostahili kwa kuwa tu wenye dhamana hawajali HAKI NA USAWA wa wananchi wao?”
Waweza soma bandiko lote hapa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/01/tunao-wangapi-magerezani-mwetuuu.html)
HEAVEN HELP US ALL
Kitendo cha kuachiwa watoto wawili wa Babu Seya waliofungwa maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti. Kumedhihirisha wazi kuwa, Majaji na Mahakimu wa Mahakama zetu bila ya shaka yoyote, hufunga watu wengi magerezani bila ya makosa.
Kuendelea kuwafunga maisha Babu Seya na mwanaye, kunatuachia maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Lakini bado tunabaki kuwa na imani ya kwamba, Babu Seya alifanyiwa mchezo mbaya, na mchezo huo bado unaendelezwa ili kumkomoa.
Kuachiwa huru kwa wanawe wawili ni kutaka kutuliza hasira za Watanzania wapenda haki, ambao tangu mwanzo wa kesi waliuona wazi uonezi wa wazi kwa Mzee huyo.
Babu Seya au huyo mwanawe mmoja, yawezekana alitenda kosa hilo. Sasa hasira za Majaji na pengine viongozi wetu wa juu, walishindwa kuvumilia kumwona akipewa adhabu inayokuwa na mwisho. Wakaona ni heri na yeye aharibiwe maisha yake yote pamoja na wanawe. Kumkomesha, asitanue katika nchi ya watu.
Majaji, Mahakimu au Viongozi wetu wanajua wazi kuwa katika sheria, mtu hutakiwi usukumwe na hisia zako katika kutoa maamuzi ya adhabu. Maana kwa kufanya hivyo, hutatenda haki kwa binadamu mwenzio. Utakuwa na wewe unatenda kosa linalostahili uhukumiwe kwa kumwadhibu adhabu nzito kuliko kiwango cha kosa la mkosaji.
Tanzania tunao “Utawala Wa Sheria”. Mbona hatuuoni katika macho yetu Utawala wa aina hiyo? Watuhumiwa wa wizi wanahudhuria vikao vya Bunge kama Wabunge wengine. Watuhumiwa wa mauaji, waliothibitishwa hata na tume iliyoundwa na serikali, wanaachiwa huru kwa visingizio kibao.
Watanzania wenzangu, tumaini letu na la uhakika ni kumtegemea Mwenyezi Mungu pekee, ambaye ndiye mwenye Utawala wa Sheria na Haki. Mwenyezi Mungu haangalii rangi, cheo wala kipato. Kila mtu atasimama mbele ya kiti cha HAKI.
This Is Black=Blackmannen
Naungana kabisa na mtoa hoja hapo juu, kwamba DNA test inatakiwa itumike katika kesi hii. DNA test ikitumika naamini kabisa itategua kindendawili ambacho kinaendelea sasa.Mimi nina imani kuwa kwenye hii kesi kuna mkono wa mtu.
Kwenye ile theory ambayo inaendelea mtaani, inasemekana kuwa yule “Mkubwa”, ambaye babu Seya alimkera sana ….na walipambana kwenye viwanja . Naomba tujiulize, hii ni kesi ambayo imewagusa waTanzania wengi sana, na mazingira yake bado ni kizungumkuti mpaka sasa…. Mbona mkuu wa nchi yupo kimnya??!
Hivi kwani na babu Seya hawezi kukata rufaa kwa mara nyingine tena? Nadhani wakili wao ametumia busara kubwa na utaalamu wa kazi yake katika kuwatetea ila kuna mikono michafu inamshikilia mzee wa watu kwa faida binafsi. Mungu awasaidie tu watoke salama na mapema!
RUFAA YA PILI INWEZA KUWATOA, WAMEBAKIWA NARUFAA MOJA NA KETE YA MWISHO YAANI KUANDIKA BARUA KWA RAIS KUOMBA MSAMAHA
Kukataliwa kwa rufaa ya Babu Seya na mwanawe Papii Kocha ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa muziki ingawaje kosa wanalotuhumiwa kulitenda ni baya kwa jamii.
Kiukweli hakuna binadamu binadamu yeyote mwenye haki ya kumuhukumu mwenzie kutokana na kwend kinyume na utaratibu,lakini kutokana na kudumisha ustaarabu sheria zimeundwa ili kudumisha usawa miongoni mwa wanadamu, in any democratic country Judicary is a independence body headed by chief justice but wonderful enough there are some people in Tanzania who have mujch money are above the law due to the weakness fact that money is above the law!.am sure God is able, one day babu seya and his son they will archieve their right!
HII KESI KATIKA MAHAKA YOYOTE DUNIANI ILIYO HURU HAWAWEZI KUFUNGU KWANZA INA USHAHIDI VERY SHAKE AMBAO WALA HAUNA UZITO MBELE YA MACHO HURU YA SHERIA, KWA MTINDO HUO MTU YOYOTE YULE ANAWEZA KUFUNGWA AKIPACHIKWA KOSA KAMA HILO HAPO TANZANIA