MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Kwa faida ya msomaji ambaye, kwa sababu moja au nyingine hawezi kuwatambua waliopo pichani; Kutoka kushoto ni Kenneth Kaunda,maarufu kama KK(Rais wa Zambia kuanzia mwaka 1964 mpaka 1991),Julius Kambarage Nyerere(Baba wa Taifa la Tanzania na Rais wake kuanzia mwaka 1964 mpaka 1985),Jomo Kenyatta(Rais wa Kenya kuanzia mwaka 1964 mpaka 1978.),Milton Obotte (Rais wa Uganda kuanzia mwaka 1966 mpaka 1971 na kisha mwaka 1980 mpaka 1985)

Je,wewe binafsi unajifunza au umejifunza nini katika kufuatilia jinsi walivyoendesha maisha yao,utumishi wao kwa umma nk? Unadhani kuna yepi ya msingi ambayo sisi kama wananchi na pia viongozi wetu wa hivi sasa tunaweza kujifunza kutoka kwa watu hao?Kumbuka mazuri na mabaya yao kwani kama tulivyo sote,they were not perfect,no one is!

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

7 Responses to “TUNAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKA KWAO?”

  1. Comment by Babukadja Sankofa on February 15th, 2010 6:43 am

    Kwanza kabisa kutoka kwa viongozi wote hawa najifunza kwamba Uongozi Afrika unahitaji zaidi ya vipindi viwili vya miaka kumikumi ili kutimiza azma yako ya uongozi. Ili kiongozi atimize malengo yake ni lazima kuongoza hadi unapojisikia kung’atuka mwenyewe kama Mwalimu, au unapokufa kama Mzee Kenyatta, au unapopinduliwa kama Obote, au watu wanapokuchoka kama Mzee KK.

    Kutoka kwa Rais Kaunda najifunza kwamba upole katika uongozi haumaanishi kuwa huwezi kuongoza, alikuwa mpole sana huyu mzee na alipenda kumaliza ubishi kwa njia ya mazungumzo. Pia alipenda kubeba leso nyeupe kuashiria amani na upendo.

    Kutoka kwa Mzee Kenyatta najifunza ukitaka kuwaongoza watu wako bila kokoro hakikisha unaendeleza misingi ya ukabila, na kama kabila lako lina watu wengi basi utaongoza hadi ufe.

    Kutoka kwa Mzee Obote najifunza kwamba usisikitikie kupinduliwa kwani unaweza kurejea na kupinduliwa tena na bado ikawa poa tu. Lakini pia najifunza kuwa hakuna jambo baya kama kufia nje ya nchi yako, kwani wafa mpweke. Mzee Obete alifia Zambia nadhani (nikosoe kama nimekosea).

    Kutoka kwa Mwalimu najifunza kwamba si vibaya kuwa na falsafa fulani na kuisimamia hata kama unaona haitakwenda kokote, lakini falsafa hiyo ikishindwa kabisa usione aibu kusema “Samahani tulikosea”

    Kutoka kwa wote wanne najifunza kuwa mzungu naye mtu tu usimuogope unapodai chako, na unapoamua kudai hakikisha unadai hadi unakipata. Wazee hawa walikomalia uhuru vizuri sana.

    Kwa ujumla wazee hawa walianza vyema ila wakajikwaa mahala fulani, wapo waliopata nafasi ya kuomba radhi na wengine hawakuipata. Juu ya yote tunawashukuru wamesababisha nimeweza kuzaliwa katika nchi huru.

  2. Comment by bongocelebrity on February 15th, 2010 12:41 pm

    Babukadja,
    Nimekusoma kaka.Masahihisho kidogo tu ni kwamba Milton Obote alifia nchini Afrika Kusini katika jiji la Johanesburg,Guateng tarehe 10 October 2005.Alikuwa na miaka 79.

  3. Comment by chakamaster on February 17th, 2010 10:14 am

    Kwa upande wangu mimi nashindwa kuelewa kwanini hawa viongozi wetu wa sasa hawataki kufuata mienendo ya viongozi wetu waliopita! Sasa hivi nchi zetu za kiafrika zimetawaliwa na kashfa za rushwa tu mpaka wafadhili wametuchoka! Viongozi hawa enzi hizo huwezi sikia rushwa halafu eti kiongozi huyo akaachwa kweli mimi nawasifu sana wazee hawa na pia kwa wale waliotutangulia mbele ya haki nawaombea wapumzike kwa amani na watuombee bara hili la Africa kwa kashfa zinazoendelea kuwepo!!

  4. Comment by Mzee Gadi on February 25th, 2010 10:44 am

    Najifunza kwamba watu hawa walikuwa wanadamu. Wakaishi kama wanadamu, na wakafa kama wanadamu.

  5. Comment by Nigeria Porter on February 26th, 2010 6:10 am

    Kuna mengi ambayo tulijifunza wakati wa uraisi wao. kwanza umuhimu wa ubinadamu, heshima kwa wakubwa na wadogo, elimu, na kuishi pamoja bila mapingano. Kwa kweli mimi bado naomba na Mungu atatujalia kupata viongozi kama tuliokuwa nao zamani…

  6. Comment by Geoffrey on March 5th, 2010 5:30 pm

    Mzee Gadi, mimi nadhani Kenneth Kaunda bado yupo hai, sidhani kama ni marehemu, maana umesema wote wamekufa.

  7. Comment by GERALD SOKA on April 3rd, 2010 9:41 am

    hawa jamma kweli wanastahili kupongezwa katika jitihada walizozifanya mpaka hapo walipofikia, kweli tukubaliane na hili,ila kuna kasoro ndogo ndogo ambazo walifanya wakiwa kama binadamu.Ningependa zaidi kumzungumzia Baba yetu wa Taifa Mwl.J.K Nyerere kweli huyu alikuwa ni kiongozi wa ukweli hapa Tanzania,kwa mimi ninavyoamini na kuona viongozi wetu wa sasa hawatakaa wawe na uzalendo kama wa Mwalimu,Jaribu kutazama nyuma uzalendo ulikuwa katika namna gani ukilinganisha na viongozi wa sasa tulionao. Tunahitaji Mabadiliko.

Leave a Reply