Mimi sio mtaalamu wa Kiswahili.Ukweli huo ndio unanifanya niwe tayari kujifunza.Ndio sababu ya kuuliza swali lililopo katika kichwa cha habari hapo juu.Najaribu kujifunza.

Unapowaweka viongozi hao watatu pichani(wote,katika nyakati tofauti,waliwahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania) ni sahihi kuwaita wote kuwa ni Waziri au Mawaziri wastaafu? Nauliza swali hili zaidi nikiwa nimemlenga Mheshimiwa Edward Lowassa (Mbunge wa Monduli) ambaye kwa mujibu wa kumbukumbu yangu,alijiuzulu wadhifa wa Uwaziri Mkuu mara baada ya sakata la Richmond kumkalia vibaya.Je kujiuzulu kule kunamaanisha kwamba ni sahihi hivi leo kumuita Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa?

Feedback / Comments

14 Responses to “HAWA WOTE NI WASTAAFU?”

  1. Comment by dullahd on February 15th, 2010 11:51 pm

    unawaita mafisadi

  2. Comment by Kamanzi on February 16th, 2010 12:43 am

    Lowassa alistaafu lini tena? Naomba nielezwe. Huyu Msuya alikuwa demoted toka uPM hadi uwaziri wa viwanda ivyo hakustaafu bali alikuwa demoted. Hapo mstaafu ni Sumaye tu tena nayeye nikwasababu alikuwa PM wakati raisi na bunge walikuwa dhaifu kimaadili. Kiufupi waziri mkuu mstaafu tanzania ni Nyerere, Salim ahmed Salimu full stop. Wengine ni maPM wafukuzwa (kama Lowassa) au PM demoted kama wote waliobakia.

  3. Comment by papai on February 16th, 2010 2:15 am

    jamani mi naona ndugu edward hafai kabisa kuitwa waziri mkuu mstaafu hasa kwa kashfa nyingi alizonazo. Hiyo heshma wanastahili wazee wetu kama simba wa yuda, warioba, mzee wetu sokoine, salim, hakuna namna yoyote ambayo tutamlinganisha ndugu lowasa na hawa wazee wetu waliolitumikia taifa hili kwa moyo wao wote. kumlinganisha lowasa na wao ni kuwakosea heshma. baba wa taifa alituonya kuhusu lowasa lakini hatukusikia na kutokusikia huko kumetutokea puani. alitumbia kabisa tena kwa msisitizo kuwa mtu kama huyo ni wa kuogopa kama ukoma.

  4. Comment by mwanga k. on February 16th, 2010 2:20 am

    Swali hili ni la msingi sana na ahsante kwa kuweka mambo hadharani. Kabla sijajibu hoja napenda kuwafahamisha watanzania kuwa ni nadra sana wakasoma kitu na kukiangalia kwa mtazamo tofauti[different perspective].Kwa ukweli huu ni wachache sana waligundua hili jambo.
    Mfano mzuri ni huu wa Richmond,wakati dana dana inapigwa wa tz walikaa kimya eti wanasubiri utekelezaji,hawakujua huo ni upotezaji muda[buy time], ghafla likachomekwa jambo wote wakaanza kulalamika.
    Mfano wa pili, Richmond hii hii iliundiwa kamati na katibu kiongozi Luhanjo,si mwandishi wa habari au mwananchi aliyewahi kuhoji nini kimetokea.
    Tatu,Waziri mkulo ameunda kamati na hadi leo hajatueleza BoT ni uchafu gani. n.k,n.k
    Haya yote ya kuunda tume,au kuahidi uchunguzi ni janja ya viongozi wanaojua wazi kuwa wa tz si wadadisi na hata ukitaka wanyongwe watakuambia ok ili kulinda amani na utulivu.

    Hoja: Lowasa si kiongozi mstaafu kwa tafsiri ya dictionary yoyote duniani hata zile za enzi za musa. Huyu ni mfanyakazi aliyejiuzulu tu. Lakini pia ni mstaafu kwasababu analipwa stahili zote kama mstaafu.
    Viongozi waliweka hii ikae controversial ili wapate nafasi kama anayotumia Lowasa.
    Ni vigumu kumhukumu kwa namna yoyote kati ya hizo mbili.
    Tatizo li wapi: Katiba yetu ipo kama dudu lisilo na miguu wala kichwa lakini lina uhai.
    Kwamfano,hivi leo Chadema au Cuf wakiwa na wabunge 200 na rais akatoka ccm nchi itatawalika vipi. Sio kwamba hawajui tatizo hili,ila wanasubiri likitokea wataomba muda wa miaka mitano kurekebisha katiba,uchaguzi unakuwa batili.
    Wa tz tuamke,kikundi cha watu wasiozidi 30 kinatunyanyasa miaka nenda miaka rudi.
    Leo hii kuna shule ya makuti isiyo na kuta,lakini wanasema serikali haina fedha. Hatujwahi kuhoji zile Bilioni 3 za kujenga hekalu la Ndulu na mkewe wake zimetoka wapi.!!
    Leo temeke wakina mama wanavichnga wakiwa wamebanana vitandani. Serikali haina pesa! je zinatoka wapi ,milioni 20 kwa kila mbunge, wabunge 220 mwezi oktoba?

    Tatizo wa tz tumefungwa kiakili na hatuangalii mambo kwa mitazamo tofauti,ndio maana Lowasa anajiita mstaafu, mwakapugi anajiita mstaafu!
    BAE na Takukuru wamefanya uchunguzi,eti Hosea yule yule aliyetudanganya Richmonduli anataka kuanza uchunguzi mwingine,upi! anajua kuwa akipiga dana dana kibarua chake kinaendelea. Hakuna mtz atakaye muuliza uchunguzi gani wakati BAE imetaja”mabaka’na ushahidi upo.
    Hakuna mtz anayehoji vipi kiongozi mwenye kashfa aendelee kuchunguza wenye kashafa wenzake!!!
    Hakuna mtz anyehoji kwanini Hosea aliwaita wabunge kuhusu posho mbili,na hajui nini kimetokea KATIKA Rada???

    Angalia mfano mwingine,kwanini wa tz hawajahoji kashfa zote kubwa zina mikono ya wahindi ” why”.
    Fikiria wa tz hawahoji kuna watanzania wangapi ndani ya bunge la China, au bunge la India?Na ni kwanini hakuna mtu mweusi kule? Sijui kama wa tz wanajua hili. Si wadadisi wala wachambuaji.

    Ahasante BC kwa kuwa wachokozi wa mada,tatizo audience ni myopic[ wasioona mbali].

  5. Comment by Wilson R Mwijage on February 16th, 2010 8:16 am

    Kusitaafu ni hali ya kumaliza kipindi cha uongozi unaotumikia na kukabidhi kwa wengine kikatiba. Lowasa hakumaliza kipindi chake cha uongozi kama waziri mkuu na kukabidhi kwa Pinda, sasa iweje aitwe “mstaafu?”

    Nafikiri ingekuwa ni vizuri zaidi kama angekaa nyuma kabisa karibu na Muzihili, kwasababu hakustahili kukaa mbele labda kama hawakukaa ki-itifaki

    Msiangaike Res Ipsa Requitor

  6. Comment by Babukadja Sankofa on February 16th, 2010 8:58 am

    Wote katika picha hii ni “Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu”, hakuna “Waziri Mkuu mstaafu” hapo mzee wa Bongocelebrity.

    Narudia tena, wote hawa ni “Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu”. Naomba kuwasilisha.

    Mzee wa Bongocelebrity nashukuru kwa kunikumbusha kuwa Obote alifia SA, niwe radhi nilichanganya!

  7. Comment by mr degree on February 16th, 2010 12:39 pm

    hakuna mwafrika anayestaafu siasa, hata ungekua wewe usingestaafu. acheni unafiki na wivu!

  8. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on February 17th, 2010 10:47 am

    ….they make me sick….I wanna throw up…!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  9. Comment by Mickey Jones Amos on February 17th, 2010 11:42 am

    NI SAWA KABISA WOTE KUITWA WASTAAFU

    Kifupi kichwa cha habari ni sawa kabisa,mtu anaweza kustaafu kufuatana na umri,kumaliza kipindi cha wadhifa,kusababishwa na ugonjwa au “presha ya muundo wa kuleta stresi” akiwa kazini,tunaweza kukitumia kichwa cha habari kama kilichotumika katika mjadala huu
    Kwa kuwa hakuna haswa anayejuwa kwa nini mhs Lowassa alijiuzuru kabla ya wadhifa wake kumalizika,tunaweza kuwaita waheshimiwa waliotajwa katika mjadala huu kama wasataafu.

    DENMARK

  10. Comment by Chamchana on February 25th, 2010 8:02 am

    WOTE NI WASTAAFU.
    LOWASA ALISTAAFU KWA MANUFAA YA UMMA!!!!

  11. Comment by nancy on February 26th, 2010 1:08 am

    jamani kuna watu wengi ambao wakipewa nafasi wataongoza vyema lakini hao watatuua.sasa basi kwanini waendelee kuwa viongozi baada ya kashfa zote hizo???
    wapuimzike majumbani au ka vp walakalime kwasababu kuna kilimo kwanza siku hizi.

  12. Comment by ritta on February 26th, 2010 9:00 am

    hawa ni mavimpier(vepaya) wakubwa

  13. Comment by Geoffrey on March 6th, 2010 6:24 pm

    Ritta unaweza kueleza kwa nini?

  14. Comment by Tumainiel on March 25th, 2010 6:21 am

    Wote hao kaka ni wazee wa kuenziwa. Wamelitumikia taifa katika namna tofouti ukuachilia mbali madhaifu ambayo mimi na wewe tunayo.Big up to all

Leave a Reply