
Ukumbi umefurika,watu wananyanyua na kushusha mikono.Wanaimba na kucheza.Wengi wamevalia nguo nyekundu.Siku ya siku ni Valentine’s Day au Siku ya Wapendanao.Kila mtu na wake. Ni siku ya kumuonyesha mwenzako kwamba unampenda.Kama alikuwa haamini huenda leo akaamini.Mwanamuziki aliyepo jukwaani ni TID.Mahali ni Platinum Club,Mikocheni.
Ghafla muziki unazimwa.TID anasema kuna kitu anataka sema.Waungwana wakatulia ili kumsikiliza.Anaanza kuongea “Wapendwa, muda umewadia,nataka kuuaga ukapela.Nataka kuoa”. Watu kimyaa, minong’ono ya chini kwa chini,shauku ya kutaka kujua na kusikiliza zaidi!
Kwa mujibu wa John Bukuku wa Full Shangwe,kilichofuata ni TID kumtambulisha mchumba.Anaitwa Kinana(pichani). TID akapiga goti na kutamka “Will You Marry Me”? Binti akakubali.TID and Kinana are engaged.
Hongera TID.Maisha ni hatua.Tunasubiri harusi.Kila la kheri.
Picha na chanzo cha habari:Full Shangwe.
Feedback / Comments
5 Responses to “TID’s SUPRISE ENGAGEMENT PARTY!”
Leave a Reply


sending...
Hongera sana TID kwa kupiga hatua hiyo kubwa ktk maisha ya mwanadamu! pia hongera kwa kazi nzuri ya mziki, kwa kweli mziki wako me unanimaliza! Kanyaga twende babake!
Kweli kijana umepata mtoto mrembo lakini sasa ukae ukijua kwamba ndoa si sawa na muziki inataka utulie na ujue ndoa ni ndoana kwahiyo nakutakia maisha mema ya uchumba.
wow…!! Raha katika roho….manaake mdogo wangu karibu utapata jiko…MUNGU awajalieni heri na yote mema…!! Amin
inafurahisha sana hongereeni sana mzidi kupendana
congrats Top n dar,
huyo sio kinana wa moscow ? au nafananisha mazee