Baada ya kimya cha takribani miezi mitatu tangu alipokumbwa na kashfa mfululizo juu ya mahusiano yake na “vimwana” nje ya ndoa yake,mcheza golf maarufu ulimwenguni,Tiger Woods, anatarajiwa kuonekana hadharani na kuzungumza na waandishi wa habari juu ya sakata lake.
Kwa mujibu wa wakala wake,Mark Steinberg, mchezaji huyo ataongea na kundi dogo tu la waandishi wa habari siku ya Ijumaa kutokea katika clubhouse ya TPC Sawgrass huko Ponte Vedra Beach jimboni Florida,yalipo makao makuu ya PGA Tour.
Tiger anatarajiwa kuongelea juu ya yaliyojiri,mipango yake ya sasa na baadaye na pia anatarajiwa kuomba msamaha(kwa kinywa chake mwenyewe) juu ya tabia zake. Tayari kuna hisia kwamba Tiger Woods ameamua kujitokeza na kuongea na waandishi wa habari siku hiyo,saa hizo, sio tu kwa sababu anataka kurudi uwanjani,bali pia kwa sababu anataka kuwakomoa waliokuwa wadhamini wake(Accenture) kwani katika muda huo kutakuwa na shindano lililodhaminiwa na Accenture liitwalo Accenture Match Play Championship kutokea Arizona.
Kwa kuongea na waandishi wa habari katika muda huo,matarajio ni kwamba macho na masikio(attention) vitaelekezwa kwake Tiger.Accenture walikuwa wadhamini wa kwanza kutangaza kumtema Tiger Woods mara tu sakata lake lilipoibuka.
Je hiyo ndio kusema Tiger Woods ameamua kurudi tena uwanjani baada ya hapo awali kutangaza kupitia mtandao wake kwamba anapumzika kucheza golf?
Feedback / Comments
6 Responses to “TIGER WOODS KUONGEA KWA MARA YA KWANZA TANGU AKUMBWE NA KASHFA”
Leave a Reply


sending...
Jamani kwa nnchi za wenzetu sijui niseme ni kwamba wamendelea sana kwenye sector ya habari au vipi? Jamaa kwenye mambo yake binafsi waandishi wa habari wamelivalia njuga! Hongera Tiger toka hazarani ongea nao halafu rudi kwenye gemu napia natumaini mkeo ameshakusamehe! Hembu angalia jamaa ni start sasa unategemea vishawishi vitaacha kuwepo? na ukizingatia jamaa ni handsome?? Keep it up Tiger
Tiger woods ni muongo sana. His apology amefanya kwa sababu wale core sponsor wote wamemtema ndio maana public relations officer wake akamwambia aombe msamaha kwa familia na washambiki wako. His apology is not genuine kabisa…ila ndio uzuri wa ulaya public figur ikiboa ma sponsor wanajitoa safi sana i like that…nadhani ingekuwa bongo Tiger woods angepongezwa kwa kuwa na wanawake wengi..maana Zuma anavyopongezwa mhh
Mhhh Mama Liv hapoo juu nimekupata na nimekuelewa….hawa wanaume wakishakuwa na pesa tuu…hawakalishi…hawashikiki….ila hapo sasa kuna hii issue ambayo ndiyo funga kazi…ole wao na ukimwi…
ktk nchi zilizoendelea hawaangalii pesa wala sura, hao kina zuma watambe hukohuko uchochoroni
Ritta eti atambe huko huko uchochoroni..na mie nasoma huku na wa South Africa yaani jamani hawampendi huyo jamaa. Basi siku ana anaomba msamaha kwamba amezaa nje ya ndoa walicheka sana, na kusema huyo jamaa kashatuharibia reputation ya nchi yetu, maana utawala hawezi then hizo extra activities ndio kabisa zinafanya nchi ionekane haipo serious na issues kama Ukimwi ect…maana mimi i thought wa south Afrika ndio wanamsifia kwa kuendeleza traditions lol..Kuhusu Tiger woods hata mimi nilifurahi sana wale core sponsors walivyojitoa, ulaya na mambo yao yote ila wanajaribu kuonyesha moral fulani hivi…maana ma sponsor wanakupa pesa unajifanya zinakupandia kichwani shenzi taip..sasa na shughuli ya zaida kutafuta sponsor ktk wakati huu mgumu ambapo washabiki wameshaboreka na Tiger woods, na scale yake ya kupendwa imeshuka sana atajiju next time akifanya jambo itabidi afikirie kwanza consequence zake..
Sponsor mwingine kamtema Tiger woods…
http://sports.yahoo.com/golf/pga/news?slug=ap-tigerwoods-gatorade&prov=ap&type=lgns