Kila ifikapo tarehe 13 August, yeye hukumbuka na kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alipozaliwa pale jijini Mwanza,kaskazini mwa Tanzania wazazi wake walimpa jina la Fareed. Leo hii kwa wengi anatambulika kama Fid Q.

Kama ambavyo umeshasikia,leo hii,tarehe 25 Feb 2010, album yake inayokwenda kwa jina Propaganda inaingia mtaani.Kwa hiyo leo ukizunguka mitaani,usishangae kukutana na mtu kabeba CD mpya ya Fid Q au ukasikia sauti yake kwenye gari,magari,usafiri wa umma.Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ni kujipatia nakala yako halisi.Hakuna njia nzuri zaidi ya kuunga mkono juhudi za wasanii zaidi ya hiyo!

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza machache na Fid Q kuhusu ujio wa albamu hii ya Propaganda,muungano wa wasanii wa bongo fleva na pia suala zima la nyimbo nyingi za bongo fleva kuwa na maudhui ya mapenzi zaidi ya kitu kingine chochote.Kwanini ameiita album yake Propaganda? Anamaanisha nini? Je unajua Fid Q ana mtazamo gani kuhusu muungano wa wasanii?Je anasemaje kuhusu mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo au kifo cha muziki wa kizazi kipya? Fuatana nami katika mahojiano yafuatayo;

BC: Kwanza hongera kwa album mpya.Labda kwa ujumla tu,album hii umeitengenezea katika studio zipi,itakuwa na nyimbo ngapi na umewashirikisha wasanii gani wengine?

Fid Q: Asante sana kaka.Album hii nimeifanya katika studio 3 tofauti.Nimefanya kwa MJ Records, Tongwe Records na kwa Lamar.Nimewashirikisha wasanii kama AY, NCHA KALI, MZEE ZORRO, JUMA NATURE,QJ, NYLON WA MANZESE CREW, BI KIDUDE na wengine kibao bila kuwasahau MATONYA na MZUNGU KICHAA.

BC: Kwanini umeiita Propaganda?Kuna ujumbe wowote maalumu kutokana na jina la album?

Fid Q: Nimeiita propaganda kwasababu kuna ujumbe maalum ndani yake nadhani hata kava linajieleza vizuri.

BC: Unaweza kunidokezea kidogo kuhusu ujumbe huo?

Fid Q:Kuna mstari (line) ndani ya hiyo nyimbo zinasema NI UCHUNGUZI TU WA KISAYANSI AMBAO HAUKUFANIKIWA/ KAMA ULE WA NG’OMBE KULA NYASI TU HALAFU ANATOA MAZIWA.

BC: Kumekuwepo na malalamiko kadhaa(mimi binafsi nikiwemo) kwamba wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya,wamejikita zaidi katika kuimba nyimbo zenye maudhui ya mapenzi.Najua wewe nyimbo zako nyingi zina falsafa.Lakini unadhani kwanini wasanii wengi wanaimba nyimbo za mapenzi zaidi na kutozingatia mambo mengine yanayoikabili jamii?

Fid Q: Kiukweli jamii yetu inakumbwa na mambo mengi… especially sisi ambao tuko 3rd world(dunia ya tatu) Lakini huwa sishangai kuona watu wanapenda kusikia love song au hata media kuzipromoti zaidi nyimbo zenye ujumbe huo kwa sababu Love is love, love is love is love love namaanisha LOVE IS LOVE,LOVE.LOVE IS LOVE..LOVE.

Binafsi huwa naona ni bora nifanye love song kuliko kufanya party song na nijuavyo mimi kuhusu soko letu la muziki wa Swahili Hip Hop kuna formula inabidi tuifate, ili kuweza kuteka masikio ya wasikilizaji nayo ni Even if you are trying to teach and motivate pia inabidi u-entertain.

Fid Q(kulia) akiwa na Mzungu Kichaa ambaye ni miongoni mwa wasanii aliowashirikisha katika Propaganda.

BC: Una maanisha kwamba wimbo kuhusu mapenzi unapewa kipaumbele zaidi na media kuliko nyimbo kwa mfano inayoongelea jinsi ya kujikomboa kifikra au kutoka katika umasikini?

Fid Q: Exactly.Love Songs zinapewa kipaumbele sana na media.Si unaona hata States; mbona ile ngoma ya HAITI haijahit? Au Bongo kuna ngoma ilifanywa kuhusu maafa ya mafuriko ya Kilosa lakini haijahit pia?

BC: Kwa hiyo ili wasanii wabadilike na kubalance kati ya nyimbo za mapenzi na nyimbo zingine,unachosema ni kwamba media lazima nayo ibadilike.Au sio?

Fid Q: YAP…na ndio maana kuna msemo huwa tunausema REAL HIPHOP

haipigwi radioni.Media zinasema Lil Wayne ndio mwana hiphop bora.Mimi nikimsikliza Lil Wayne naona hana similies, metaphors, words play na vitu vingi tu hata punchlinez zake sio kihiivyo lakini ndio kajinyakulia tuzo kibao mwaka jana na juzi.Media zimeupa kipaumbele uongo kiasi kwamba watoto wa siku hizi sio Afrika tu bali hata ulaya wanaamini RAMBO ndio hero!

BC: Tuje kidogo kwenye suala la umoja na mafanikio miongoni mwa wasanii.Wewe ni msanii ambaye tunaweza kumuita mkongwe.Unadhani ni kitu gani kinachowafanya wasanii msiwe na umoja wenye nguvu ili kuwa na mafanikio zaidi?

Fid Q: Wengi bado tuna njaa ya chips vumbi.Tushakaa sana na kujadili kuhusu suala la umoja lakini mara nyingi kikao huwa kikiisha na harakati zinaishia hapohapo.Unapomwambia mtu kuhusu kukomaa tusifanye show kwa kiasi  hiki cha fedha, bali tufanye kwa kiasi kile wengi huwa hawaamini kwasababu wanahisi mie nishafanikiwa kiaina kwa hiyo labda  nataka kuwapigisha ili wasiyafikie malengo yao.So hakuna atakaye risk on such an outlandish idea regardless of how many mifano ushawaonyesha.

BC: Pamoja na “njaa” za baadhi ya wasanii ambazo unazizungumzia,unadhani serikali kupitia wizara yake ya utamaduni kwa mfano,inaweza kufanya chochote ili kuhakikisha kwamba jasho lenu kama wasanii halipotei bure?

Fid Q: Serikali inabidi ijue kitu kimoja… ikitaka kujua kuhusu matatizo ya wasanii inabidi ikutane na wasanii wenyewe na sio mshika dau yeyote!! Sanaa yetu hii ambayo kila siku wasanii wake wanalia kwa shida na wengine wanadharaulika kama ikipewa kipaumbele inaweza kuzaa ajira zaidi ya milioni mbili ndani yake kama ikipewa kipaumbele.Sidhani kama unahitaji mifano kuhusu hili kaka.

Fareed

BC: Hivi karibuni nimesoma makala moja ambayo ilisema,mfumuko wa studio unachangia katika kudidimiza muziki nchini.Kwamba siku hizi msanii akipata hela kidogo anaenda na kujifunza kupiga keyboard kisha anaanzisha studio yake.Unasemaje kuhusu hilo..

Fid Q: Mimi siamini kama wingi wa studio unaua mziki.Kinachoua mziki ni kile kinachotengenezwa na hizo studio.Unajua mziki ni sanaa… na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka au sio?

BC: Asante kwa muda wako Fid Q.Nakutakia kila la kheri katika uzinduzi mzima wa album yako,mauzo na mitikasi mingine.

Fid Q: Asante sana kaka.Kila la kheri katika kazi zako na wewe pia.

More Questions?

Feedback / Comments

12 Responses to ““REAL HIP HOP HAIPIGWI RADIONI”-FID Q”

  1. Comment by chakamaster on February 26th, 2010 7:32 am

    Kaza Buti Baba!! HIP HOP inalipa basi ni kwamba wabongo bado hawailewa wamengangania kwenye nyimbo za malovedavi! Lakini Farid nakuzimia sana kwa mesegi zako!! Keep it up Bro!

  2. Comment by Hater on February 26th, 2010 9:42 am

    Big up, nimependa ulivyosema nyinyi wasanii mna njaa ya chipsi vumbi.. kwikwikwikwi… najua unamaanisha mnazuzuka na vitu vidogo tu na kusahau vikubwa mnavyopaswa kuwa navyo.. uko deep sana kaka na ndio maana siku zote nitaendelea kuwasisitiza ya kwamba WEWE NI KICHWA,

  3. Comment by Grace on February 27th, 2010 2:23 am

    FID Q The Leading hiphop artist In E-Afrique…. i love this guy….! May ALLAH give u more wisdom, keep on keeping on brother. cant wait to buy ur Album….

  4. Comment by dullah on February 27th, 2010 4:19 am

    poooopanda 4ever
    tongwe rec 4ever
    nimependa interview
    yako… yaonyesha
    jinsi gani ulivyo
    makini na kazi yako
    big up bro

  5. Comment by uweso on March 1st, 2010 5:53 am

    aisee we achatu, bongo hakuna wasanii, wengi ni wasindikizaji lakini fid kyu ndo namba moja ebwana mkuu nakukubali sana upo seriously na kazi yako ya mziki si kama wengine wababaishaji.
    keep it up bro you will achieve the best.

  6. Comment by mzuka boy on March 2nd, 2010 2:31 pm

    hip hop is alive, mchekini msanii mpya anaitwa wakazi

    myspace.com/wakazi

    ila fid q ndo anaongoza njia

  7. Comment by MUD BIZNESS on October 1st, 2010 3:06 am

    kaza but bro gem unaliweza

  8. Comment by One The Incredible on November 8th, 2010 4:09 am

    [...] alipohojiwa na Bongo Celebrity kitambo kidogo. Linalomuuma yeye binafsi na mashabiki wengi ni nyimbo za Hip Hop kutochezwa kwenye vituo vingi vya redio. Ukiuliza watu wengine, watasema hata aina nyingine za nyimbo wanazozipenda [...]

  9. Comment by dublin on December 13th, 2010 5:28 am

    fid kaka nakuzimia ile kishenzi, naamini hakuna msanii mahili wa hip hop kama wewew hapa bongo,album yako nimeisikia imeshiba ile kishenzi,kaza buti kaka

  10. Comment by joseph mazengo on February 11th, 2011 11:58 pm

    Ebwana ngosha mzuka sana dizain kama wakikudis wachunie sio unawaogopa ila unofia kuwa kichwa cha habari gazetini let it one day hip hop itakuja kutouch angle zote its me swila one day u can listen ma song b’ze hip hop never die in ma blood cell

  11. Comment by mbogamasoli on April 13th, 2011 2:35 am

    WEWE NI HIP HOP ICON IN TZ RESPECT YUO SON

  12. Comment by Dosa12 on July 12th, 2011 4:58 am

    Ebwada fid we mkal tunachukiana kwasababu atujajuanat2naogopana kwsababu

Leave a Reply