
Za mwizi arobaini. Bila shaka ushausikia msemo huo.Sina uhakika sana na idadi ya siku (40) lakini nina uhakika kwamba msemo huo humaanisha kwamba uovu una kikomo.Ipo siku utakamatwa.Inaweza kuwa sio ndani ya siku arobaini(40) lakini ipo siku tu!
Lakini inakuwaje siku ukimfumania mtu ambaye haibi kunde na choroko zako shambani bali anaiba penzi au mpenzi wako? Utapigana au utamuacha aende zake.Yaani namaanisha utayamaliza kistaarabu tu au mtaani patakuwa hapatoshi kwa vurumai au songombingo utakalolianzisha?
Sijui utafanyaje…lakini Hussein Machozi(pichani) anasimulia jinsi siku za mwizi(wa penzi,mali au hali) zinavyofikia ukingoni.Baada ya siku arobaini mambo yanawekwa hadharani.Tyler Perry,yule muongoza sinema maarufu kutoka nchini Marekani,anao mchezo(play) unaoitwa What is Done In The Dark…Must Come Out to Light. Labda Hussein Machozi anamaanisha hivyo pia.
Wimbo unaitwa Za Mwizi 40,unapatikana katika album yake ya Kwa Ajili Yako. Hii ni single yake ya 3 kutoka katika album hiyo, single mbili zilizotangulia ni pamoja na Kwa Ajili Yako na Utaipenda.Usikilize hapo chini;
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
SONG’S DETAILS
Track Name: ZA MWIZI 40
Singer: HUSSEIN MACHOZI
Produced by: AMBA & KID BWOY
Written by: HUSSEIN MACHOZI
Song Arranged by: HUSSEIN MACHOZI & KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ / AB RECORDS
Feedback / Comments
7 Responses to “ZA MWIZI 40,UKIMFUMANIA UTAFANYAJE?”
Leave a Reply


MKUBWA BC HUO WIMBO VIPI?uerkebishe vizuri basi tuusikie,maana umekiambia kwa sekunde tano tu
Ally,
Asante.Ngoja niucheki tena nione inakuwaje.
Ni lini tutabadilika jamani… zile nyimbo zake mbili za kwanza niliona huyu anabadilika vizuri, lakiini sasa hii ni nini jamani… wasanii tunaishiwa ubunifu mapema hivi kweli???
Amujaribu katufikirisha kiaina lakini ni udhanifu sana, mwana weka mambo kiuyakinifu
Amejaribu kutufikirisha kiaina lakini ni ya kiudhanifu sana, mwana weka mambo kiuyakinifu, pia mbona jamii ina matataizo mengi sana tuseme wasaniii hawawezi kutufikirisha kutatua mambo hayo kama ufisadi, uongozi mbovu, kukosekana kwa demokrasia ya kweli.umaskini ,magonjwa , uzembe, madawa ya kulevya , pombe za kupindukia , ajali za bararbarani, mimba za utotoni, dhuluma ya utandawazi kwa nchi za dunia ya tatu,
thus cool kijana mm nakukubali mwanzo mwisho
Tunapozungumzia muziki hatuegemei sehemu moja tu! Wasanii wetu wengi wana tatizo hilo! Pia ma~producer wanaudhaifu mkubwa! Kwa kweli nadhani wasanii wetu wengi wanakosa msaada wa ushauri wa ma~producer! Wasanii wanaandika mashairi na kuimba tu kihorelahorela ubunifu unakosekana, midundo ya muziki haiendani na ile ladha ya uimbaji basi nyimbo inaimbwa ili mradi kuimbwe tu!