Mwanamitindo maarufu ulimwenguni,Naomi Campbell,yaelekea akaingia matatani tena kwani hivi sasa polisi wa jijini New York nchini Marekani,wanamsaka!

Naomi,ambaye mwaka jana alitua nchini Tanzania na kushiriki katika onyesho la hisani kwa ajili ya akina mama, safari hii anatafutwa akikabiliwa na shutuma za kumchapa vibao dereva wake huko New York.

Mwanamitindo huyo ambaye inasemekana ni mpenda ugomvi sio mgeni na vyombo vya usalama.Siku za nyuma amekwisha kutwa na hatia ya kumpiga mfanyakazi wake wa ndani jijini New York, kumpa kibano msaidizi wake jijini Toronto na pia kumwangushia kisago polisi ndani ya ndege katika uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.Katika makosa yote hayo hapo juu,Naomi alikiri makosa yake na alihukumiwa kufanya kazi za kijamii(community services) kwa masaa zaidi ya 200.Kazi kweli kweli.Hivi kwanini kuna baadhi ya watu huwa wanadhani wanayo haki ya kuwaadhibisha watu wengine kiholela tu?Ni matunzo,jamii au?

NB:Hivi unajua Naomi Campbell alipokuwa mdogo alishiriki katika video ya Mfalme wa Reggae,Bob Marley katika wimbo One Love? Mtizame katika video hiyo hapo chini.Alikuwa na umri wa miaka 7 tu na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa katika spotlight.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Feedback / Comments

5 Responses to “NAOMI CAMPBELL ANASAKWA NA POLISI”

  1. Comment by ritta on March 5th, 2010 10:05 am

    hata mimi mtu nisipomuelewa elewa namchapa tu vibao kama naomi big up naomi wachape tu ili wawe na adabu

  2. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 6th, 2010 10:47 pm

    he he he heeeeeeeeeeeee
    SHeria mkononi amaaaaaaaa??

  3. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 8th, 2010 1:13 am

    mhhh huyu naye….mhh pua yake imeniacha hoi….miye naona ana ka ugonjwa ka kuchanganyikiwa…hajatulia vile….

  4. Comment by SS on March 23rd, 2010 10:09 am

    Mwanamke wa shoka mie namuona mzuri sana..ila hivyo vituko vyake jamani tumechoka sasa nae aende akafanye therapy ya hizo hasira zaka khaaa

  5. Comment by amos baganda on April 29th, 2010 6:36 pm

    dats gud,

Leave a Reply