Mradi wa Zinduka.Nia ni kutokomeza malaria.Kila mtu analiunga mkono akiwemo Mheshimiwa Rais.Kumbe chini yake kuna mvutano.Mwanamuziki Sugu(Mr.II) ana kampuni yake.Inaitwa Deiwaka.Kwa upande mwingine kuna mfanyabiashara maarufu.Anaitwa Ruge Mutahaba.Anasaidia kuinua vipaji vya wasanii kupitia Tanzania House Of Talent(THT).Mpaka sasa wasanii kibao wameshainua vipaji vyao kupitia kwake. Kuna shirika la Malaria No More kutoka nchini Marekani.Mradi wa Zinduka ni wa nani?
Kama umechanganyikiwa na jinsi nilivyoandika hapo juu,pengine ni kwa sababu kitu chenyewe kinanichanganya hata mimi pia.Labda wasikilize wenyewe wahusika;
Sugu akiongea na waandishi wa habari.
Ruge Mutahaba akijibu mashambulizi ya Sugu
Feedback / Comments
18 Responses to “SUGU Vs RUGE:ZINDUKA NI YA NANI?”
Leave a Reply


sending...
Sugu kaonewa..Ruge mpe mwenzio haki yake yaishe
unajua hawa clouds media group ndio zao, haki ya sugu,
Hii inaonekana kuna kila namna ya kudhulumiana na mikono ya rushwa katika hii kampeni.Tanzania ni nchi ya ajabu sana mtu(Mr Sugu) anapelekewa barua na mahakama na ‘kuombwa’ au kuamuliwa muda wa kushitakiana ili tamasha liliendelee na ili wengine waingize pesa.Naona wakati umefika sasa WaTanzania tunaoishi nje ya nchi kama tukisikia au kuona kuna rushwa au fedha zinatumiwa vibaya na wahisani wanazotuma Tanzania,kwa kufanya ni kushinikiza hizo kampuni au Serikali zao kusimamisha hiyo misaada.Hii inaweza kuwafanya wakabadilika.
Tanzania inanuka kila sehemu rushwa rushwa.Inasikitisha kuona ukisikia kuna kampeni Bongo basi ujue Nchi tajiri wametuma pesa.Lini tutaanza kampeni zetu wenyewe na idea zetu wenyewe kama kampeni za kusafisha mazingira yetu,kufundishana huduma ya kwanza,kujua maarifa kuhusu afya zetu n.k.Hizo kampeni zingeleta maana kama zingefanyika bure wangebana bajeti nadhani ili kupata watu wa kuwalipa katika kila sehemu ya washiriki.Kuna watu waliendesha semina na kozi kutoka nchi za Nordic huko Tanzania na watu waliodhuria kwenye wangepewa chakula tu na hamna posho.Wakaanza kudai posho wale WaNordic wakasema’haya ni maarifa tunawaletea ni kwa faida yenu’kwa nini tuwalipe na posho,tena labda nyie mngetakiwa kutulipa.Kwa hiyo mnashiriki au la!
clouds ndo baba zao wengine mtafuata nyuma tena sana.don try 2 tok about clouds ndo full entertainment..so ukjifanya mjanja kwa clouuds utafulia ka ilivyokua kks.
haya mie macho
Kweli enzi za mwalimu angefunga wote, Mkurugenzi mpaka mfagizi. Clouds redio ya kibwege kabisa!!!!!!!!!!!!
RUGE HUWEZI KUFANYA KITU KWA BURE, SWALA HAPO NI PESA, UMEVUTA NA UMEMPIGA KANZU NA GOLI LA KISIGINO MR 2. UNAVYOONGEA TU INAONEKANA KUNA KITU HAPO. HATA VITU VYA CHARITY WATU HULIPWA HAMNA KITU CHA BURE. ALAFU UNASEMA KESI YA MR 2 IKO KATI YAKE YA MALARIA NO MORE YA MAREKANI NA HAINA OFISI HAPO SO KESI IPO MAREKANI SI TANZANIA, HAYO NI MAWAZO YAKO MTU UNAWEZA KUMSHITAKI MAHALA POPOTE PALE DUNIANI PROVIDED AMEFANYIA KOSA HAPO NA KAMA KUNA KESI YA KUJIBU ATAITWA KUJIBU HATA KAMA ANAISHI WAPI, ACHENI KUONEA VIJANA WADOGO NAO WANATAFUTA, WENZIO HIYO NI KAZI AJIRA NDO WANAKOPATIA VIPATO SASA UKITAKA KILA KITU KUKUMBATIA WEWE TU SASA WATOTO WATAPATA WAPI AJIRA, SHAME ON YOU RUGE ULICHOFANYA SI SAHIHI NI AIBU TUPU UNATAKIWA KUOMBA RADHI.
wewe ruge usie na huruma nimejua sasa kwa nini mlikuwa hampigi nyimbo za sugu for over 4 years na all oversudden mkaanza kupiga mwishoni mwaka jana kumbe mlikuwa mnampaka mafuta kwa mgongo wa chupa mnamwibia deal lake, kwa kweli unaitia aibu clouds and whatever company you are dealing with….
Kwakweli Ruge,wewe ni mbaya sana unawaumiza sana vijana wetu,wenyewe wanajitahidi ili kusiwe na ukandamizaji,hongo na kila kitu ambacho kinapigwa vita nyumbani lakini wewe kutokana na pesa zako zinazonuka unawazibia vijana wenye lengo zuri na taifa letu.SUGU KAONEWA PERIOD!!!!!!!!!!.Sijawahi kuona duniani eti unashtaki halafu mahakama inakuomba siku ya kushtaki ili tamasha au chochote mlichoshtakiana kiendelee,huo ni unyonyaji na rushwa inayonuka nchini.Ndio maana hata tukimaliza shule haturudi huko kwasababu hakuna hakiiiiii,yaani mnaniliza sana nyinyi watu wa tanzania wenye kujidai mna vihela vya kuhonga.
jamani naomba umsiwe mnatoa maamuzi bile kujua kinachoendelea haya ishu ishajulikana kuwa mr.2 anatumia jina la president kufanikisha mambo yake na jana kapigwa marufuku kufanya ivyo …..go on clouds mmefanya mambo mazuri kwa miaka mingi na mmetupa burudani za aina yake km kuna anatatizo na clouds kaa kule….na wewe unaesema ukimaliza shule unabaki huko huna akili na mawazo huku ndo kwenu unang’ang’ani kwa watu shame on you…watu siku izi huko tunakuja kutembea na tunarudi zetu bongo(sweetest home)
We Ruge acha uonevu, you have a lot but still you want to take what belongs to sugu.
its not fair, just quit so as to retain ua status.
Actual what ruge did 2 sugu it is unfair thatz iz why for so long his clouds and other radio uchwala used not to play sugu songs,4 myself i think sugu is the father of bongo freva&hip hop even fighting 4 artist rights. so big up sugu keep it up and God bless u we are in ur side for so long since u were the way 4 others best like prof j,wagosi,nature,afande sele,babu,watukutu and de least.
Kweli aliyenacho huchukua na cha mwenzake. Ukweli Sugu anajitahidi kustruggle ila wenye nazo kama ruge hawako tayari kuacha wengine nao wapate. Kwenye tamasha la zinduka wimbo wa taifa uliimbwa vibaya na kabinti kaliwekak madoido ambayo hahyakuwa na maana kabisa. Wimbo wa taifa uheshhimiwe.
haya sasa jamaa kachukua jimbo du!
Sugu kama mvua nyie machende wa clouds hammuwezi jamaa miaka laki 8
Kwanza hao tht wake hata cwaelewi wanaimba nn? na cku Ruge uCombe ukanyage Joberg, Utakuja kuhadithia wenzako nini taleban souljahz (wabongo) walikufanya, , pasop
mambo ya dhuruma siyo mazuri ni vizuri Sugu na Ruge mkakaa meza moja na kulimaliza hili suala.bifu siyo kabisa,mwisho wake kufanyiana noma kama za kina 2pac.
sugu pigania haki yako mpaka mwisho wala usiogope