Wakati suala zima la nani alileta mradi wa Zinduka nchini Tanzania,nani alianzisha idea hiyo na mchakato mzima wa mradi huo likiendelea,nadhani sio vibaya kama tukajionea kile ambacho wasanii waliweza kufanya.
Kimsingi,kampeni hii ina umuhimu wa aina yake.Malaria ni tishio la uhai wa mamilioni ya watu ulimwenguni.Inaua kuliko ugonjwa mwingine wowote.Inaua zaidi ya Ukimwi!Kuna haja ya kuendelea kusambaza ujumbe.Kuna haja ya kuendelea kupeana maarifa kuhusu jinsi ya kupambana na ugonjwa wa malaria.Mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria ni zaidi ya chandarua.Ni suala la mazingira.Vidimbwi vya maji yaliyotuama.Misitu ya majani inayoachwa bila matunzo.Ni pamoja na kutumia kila aina ya kinga zilizopo.Hongera kwa wasanii waliotengeneza na kushiriki katika video hii;Zinduka. Kwa msaada zaidi wa jinsi ya kupambana na malaria,bonyeza hapa.
Feedback / Comments
8 Responses to “ZINDUKA:THE VIDEO”
Leave a Reply


sending...
Beats za wimbo nzuri sana, na ujumbe murua. Hapa hakika pesa za “donors” zimetumika ipasavyo.
Ila video ingeweza kuelimisha jamii zaidi kama wangeonyesha kiufupi nini haswa kuhusu ugonjwa huu wa Malaria, kwa mfano kwa kuonyesha matukio kama vile mbu, madibwi ya maji machafu, mtu mgonjwa na hafifu kwa homa kali, kutapika etc. Walivyoonyesha watu wanacheza ngoma, hii haiilingani na ujumbe wenyewe.
Cheers!
That’s great, very educative!!
good job.wasanii wetu
NIJUILISHE
Ni kweli video haigusi sana malaria.
Kuna haja ya kuandaa video nyingine
Hasa kwa watazamaji wa vijijini na wasio na upeo wa kusikiliza maneno yote watakosa ujumbe kabisa
But its a great song
I love it
Siku zote usanii hasa wa maigizo na nyimbo huitaji sana uhalisia wa kiigizwacho au kiimbwacho! Linapokuja jambo la uhalisia hasa kwetu Tz ndipo ugomv mkubwa! Video is good but mapunguf ya hapa na pale! Big up kwa wote walioshrk na kuiandaa…
Mimi kwa mtazamo wangu pamoja kwa ujumbe walioimba mwanzo wa zinduka hakuna shida ila tatizo lilikuja pale msanii mmojammoja alipoanza kuimba pale ndo palinistua yani walikuwa wanaonyesha shoo ya nyimbo zao ambazo tunazisikia siku zote radion au? hasa huyo RC kile ni nini? mimi nilitegemea wasanii wote ambacho wangeimba kingekuwa juu ya hiyohiyo malaria lakini haikuwa hivyo hapom nadhani haijakaa vizuri.
usipofundishwa na wazazi,utafundishwa na ulimwengu.nawapa HEKO VIJANA,KWA KUKUSANYIKA,na kutoa mwimbo wa somo.nawaonea gele mie kuuimba sijui.tuishi na AFYA,ndio mungu wa karne hii.markniggga salamba australia.