
Tungo zao mara nyingi zimekuwa na tabia ya kugeuka na kuwa misemo ya mjini,gumzo la mitaani na hata kutumiwa “kibiashara” na makampuni kadhaa ya biashara. Bila shaka unakumbuka chanzo cha misemo kama vile Habari Ndio Hiyo,Nangoja Ageuke, Unaoa lini:Bado nipo nipo,Bed and Breakfast nk
Ni vijana ambao mpaka hivi sasa wanaweza kusema ‘wana mafanikio” fulani kutokana na kazi zao za muziki.Walianzia East Coast na mara kundi hilo lililokuwa na makazi yake pale Upanga-Dar-es-salaam,liliposambaratika wao wameendelea kuwa pamoja kama marafiki na pia wasanii wanaoshirikiana.
Tunawaongelea Mwana FA na A.Y ambaye siku chache zilizopita alipata tuzo ya Teenz kutoka nchini Kenya kama Favourite Artist wa East Africa. Safari hii wimbo unaitwa Usije Mjini. Kwanini nisije mjini wakati mjini nasikia ndio mambo yote? Kila mtu anataka kuja mjini.Mjini hata kwa kuuza maji tu unaweza kujipatia kipato.Mjini kuna starehe zote…inaaminika. Sasa kwanini A.Y na Mwana FA wanasema Usije Mjini? Sikiliza kwa makini tungo hizi;
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Photo/Binamu13.com

Umeshawahi kujiuliza kwamba ingekuwa vipi endapo ungejua jinsi siku ya kesho itakavyokuwa? Ingekuwaje ungejua kila kitu kitakachotokea wiki ijayo au mwezi ujao? Endapo ungejua siku utakayorudi kwa Muumba? Mimi nahisi maisha yangekosa hamasa fulani.
Ile hali ya kutojua kesho inajenga imani na msisimko wa aina yake.Inaleta matumaini kwamba kama leo ni “hovyo” basi huenda kesho ikawa ‘safi”. Inakupa sababu ya kudamka asubuhi na mapema,kupambana na foleni ya asubuhi ya jijini Dar-es-salaam kwa mfano,kuwahi kibaruani huku kichwa kikiwa na ndoto kemkem kwamba hapo baadaye huenda na wewe ukasindikizwa na ving’ora na kupishwa na kila atumiaye barabara huku ukiwa “umekunja nne” full kipupwe ukipitia vichwa vya habari vilivyopamba kurasa za magazetini.
Mr.Misosi,yule yule aliyetoka na “Nitoke Vipi” kabla hajakamata vizuri na “Mabinti wa Ki-Tanga” anakuja na wimbo wenye maudhui hayo hapo juu.Unaitwa Huwezi Jua. Kwamba endelea kupigana kwani maisha hupanga Mola na huwezi jua kesho itakuwa vipi.Usikate tamaa. Mr.Msosi amemshirikisha mkali wa sheng,Jua Kali msanii kutoka Kenya. Wimbo umepikwa pale Fishcrab Records kwa mtaalam Lamar. Usikilize hapo chini.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Photo/TID
Leo taifa la Tanzania limetimiza miaka 46! Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika sherehe za kukumbuka siku Tanganyika ilipoungana na Zanzibar zilizofanyikia kitaifa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam.

Rais Jakaya Kikwete(kushoto) akiwapungia mkono wananchi.Kulia ni General Davis Mwamunyange,Mkuu wa Majeshi Tanzania.

Viongozi.

Wananchi,Viongozi mbalimbali wa vyama na serikali.

Hatimaye mrembo wa Miss Universe Tanzania 2010/11 amepatikana. Ni mrembo Hellen Dausen(pichani) mwenye umri wa miaka ishirini na tatu (23) kutoka mkoani Arusha.Nafasi ya pili ilikwenda kwa Rose Shayo kutokea Dodoma wakati ya tatu ilikwenda kwa Mwajuma Juma kutokea Mwanza.
Pichani ni Hellen akipunga mkono baada ya kutwaa taji la umalkia huo nchini katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku wa kuamkia jana.Hongera Hellen.
Picha kwa hisani ya Mrocky.
Mapenzi bila visa na mikasa ni mapenzi yaliyokosa chachu.Ni kama vile maisha yasiyo na kupanda wala kushuka.Yanakosa msisimko au kwa kizungu wanasema ‘boring”.Lakini inakuwaje kama visa na mikasa katika mapenzi baina ya wawili yanakuwa yamejaa visa vya kudanganyana,kunyanyasana,kutoheshimiana? Mbaya zaidi ni kwamba visa na mikasa hiyo haina mapumziko.Kila kukicha kuna msala mpya.Ukiambiwa usamehe utakubali?Ukiambiwa vumilia tu utakubali?Ukipewa ahadi kwamba “nitajaribu” kufanya au kuwa sahihi utaiamini?
Maudhui kama hayo ndiyo yaliyomo katika wimbo mpya kutoka kwa mwanamuziki maarufu Jean Piere aka Kidum kutoka nchini Burundi akishirikiana na mwana wa kwetu,Lady JayDee au ukipenda Judith Wambura.Wimbo umesimamiwa na Hermy B kutoka B’Hits Music Group ambaye hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi na Kidum ingawa ameshafanya kazi kadhaa na Lady JayDee zikiwemo nyimbo Mtarimbo Doro na Teja. Usikilize hapo chini.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
CREDITS:
Song: Nitafanya
Artist: Kidum & Lady JD
Composed by: Kidum
Written By: Kidum & Lady JD
Recorded, Engineered and Additional instruments By: Hermy B At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Mixed and Mastered By: Hermy B At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Kesho ndio kesho. Mshindi lazima apatikane.Mwakilishi wetu katika mashindano ya ngazi ya dunia ya Miss Universe atajulikana hapo kesho tarehe 23/4/2010 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 20 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania,wameteuliwa kuwania taji hilo ambalo bila shaka sote tunakubaliana kwamba ni miongoni mwa mataji ambayo mpaka sasa yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania na kuiletea sifa kimataifa.
Tukio la kesho litasindikizwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii kama vile Nameless kutoka Kenya,Nakaaya, Mama Afrika Circus na wengineo kibao.
Hizi hapa ni picha za warembo wanaotarajiwa kushiriki hapo kesho.Photography by Moiz Hussein, Stylist and designer Farouque Abdela, Make up – Oriflame International. Unadhani mrembo yupi ataibuka mshindi?
Kama bado hujajipatia ticket yako, tafadhali piga simu 0784 305122 au nenda pale Shear Illusions shops ndani ya Millennium Towers na Mlimani City.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Tabia-anatokea Dodoma na aliyepo kulia anaitwa Selina kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Sanje-anatokea Dodoma na aliyepo kulia anaitwa Rose kutokea Dodoma.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Redempta-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Neema kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Nasra-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Mwajabu kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Maureen-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Mary kutokea Morogoro.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Josephine-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Immaculata kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Hellen-anatokea Arusha na aliyepo kulia anaitwa Halima kutokea Arusha.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Gaudencia-anatokea Morogoro na aliyepo kulia anaitwa Demitria kutokea Dar-es-salaam.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Fatma-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Esther kutokea Mwanza.

Mrembo aliyepo kushoto mwa picha anaitwa Devotha-anatokea Dar-es-salaam na aliyepo kulia anaitwa Anna kutokea Dar-es-salaam.

KESI ya kushambulia na kuharibu mali iliyokuwa inamkabili Miss Tanzania, Miriam Gerard, pamoja na rafiki yake imefutwa na wawili hao pamoja na mtu wanae shitakiana nae sasa watamalizana nje ya mahakama.
Kwa mujibu wa blog ya Father Kidevu, Uamuzi huo umefikiwa leo katika Mahakama ya Kinondoni ambako kesi hiyo ilifikishwa mwezi Februari.
Bila shaka habari hizi ni njema kwa Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Uncle Hashim Lundenga ambayo kimsingi ndio msimamizi mkuu wa shughuli za kijamii zinazofanywa na mrembo huyo mpaka hapo atakapoachia taji lake.Life goes on.
Hivi karibuni pale nchini Kenya katika ukumbi ujulikanao kama Bomas of Kenya, kulikuwa na hitimisho la Teneez Awards Kenya.Ambwene Yessayah au maarufu kama AY alikuwa akiwania tuzo hizo katika kipengele cha Best East African Artist 2010 kilichokuwa kinawaniwa pia na wasanii Marlaw kutoka Tanzania,Weasel and Radio kutoka nchini Uganda na Blue 3 kutoka nchini Uganda. Mwisho wa kipute,AY ndiye aliyeibuka mshindi.
Hongera AY kwa ushindi huo.

AY akipokea tuzo ya Teneez Awards Kenya.

AY akiburudisha katika tukio hilo.

Familia ya Mzee Gembe wa Upanga Dar-es-salaam na Tabora,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu,jamaa,majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu mtoto wetu,mdogo wetu,dada yetu, Evaline Gembe ambaye alifariki huko Toronto nchini Canada katika hospitali ya Mtakatifu Michael tarehe 30/March/2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 13/Aprili/2010 kijijini Inyonga Mkoa wa Tabora.
Shukrani za pekee tunaomba ziwafikie Jumuiya yote ya watanzania wanaoishi nchini Canada hususani katika Jiji la Toronto na vitongoji vyake. Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili hadi kuusafirisha kwa gharama kubwa kutoka Toronto hadi Dar-es-salaam mnamo tarehe 8/April/2010.Asanteni kwa sala,maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu.Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Evaline kuja Tanzania.
Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani Dar-es-salaam na Tabora katika kutufariji,mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu.Asanteni sana.
Shukrani pia ziuendee Ubalozi wa Tanzania nchini Canada na Jumuiya mbalimbali za ki-Tanzania nchini Marekani na wanablogu wote waliolitoa tangazo la kifo kwenye Blogu zao.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee,tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa ndugu yetu Evaline.Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.
Sisi tulimpenda sana Evaline lakini
Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,
Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen


sending...