
Hivi karibuni Kituo Cha Televisheni cha EATV au Channel 5,waliendesha zoezi la kuwasaka wachekeshaji (comedians) wapya ili kuziba nafasi iliyoachwa na kundi lile la mwanzo baada ya mambo kuingiliana.Wakati wale wengine hivi sasa wapo TBC,hawa Ze Comedy wapya wataendeleza pale wenzao walipoachia hapo hapo EATV. Jumla ya vijana takribani 500(sikujua kama Tanzania tuna vijana wengi hivyo wanaoamini kwamba wana kipaji cha kuwavunja watu mbavu) walijitokeza wakati wa zoezi hilo la kusaka jumla ya wasanii wapya 7 tu.
Je unajua ni kina nani wamechaguliwa kuunda kundi hilo jipya?Bonyeza hapa.

Majuzi Tanzania imepoteza msanii hodari ambaye wengi tulianza kumsikia kupitia michezo ya radio. Huyo si mwingine bali Mzee Pwagu(Pumzika kwa Amani Mzee wetu). Lakini je,michezo ya radio ingalipo na nini nafasi yake katika jamii ya leo? Ukweli ni kwamba ndio,michezo ya radio ingalipo na bado ina nafasi na jukumu lile lile la kuelimisha,kubudurudisha, kuonya na hata kurekebisha jamii. Mfano mzuri wa michezo hiyo ni ule unaorushwa na Wahapahapa.
WAHAPAHAPA ni mchezo wa radio wenye nia ya kubadili mtazamo wa kimaisha kuwa chanya. Mchezo huu unalenga suala zima la mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, matibabu na uangalizi.
Mchezo huu unarushwa kila wiki kwa namna ya kuvutia na kuelimisha, kwa njia ya mawasiliano ya radio.
Maisha yanayojiri katika mchezo huu yanatokea katika vijiji vya kufikirika vya KALUMBI na MAKATANI vilivyoko sehemu Fulani huko Tanzania.
“Homeboys” ni bendi ya muziki ambayo ndio kiunganishi cha matukio yote yanayojiri katika mchezo huu wa kusisimua. Bendi hii inaundwa na wavulana watano ambao baadae kidogo mwanamuziki wa kike anajiunga nao.
Bendi hii inaamini kuwa ikipiga muziki mzuri itafanikiwa kimaisha na hatimae watakuwa nyota kwa washabiki wao wa nyumbani. Bendi inakutana na changamoto kadhaa zinazokinzana na nia yao ya kuwa vinara wa muziki pamoja na kujitengenezea kipato. Kuna migogoro lakini haikosi suluhisho, maslahi ya bendi ni makubwa zaidi ya maslahi ya mtu mmoja mmoja.
Hatuishii kuona maisha ya wanabendi peke yake bali mchezo unazidi kunoga zaidi pale tunapokaribishwa kuona pia maisha ya ndugu, familia, jamaa, na marafiki wa wanabendi. Tunaona migogo na changamoto inayokabili jamii hii na jinsi inavyoamua kuungana pamoja kupambana kuelekea siku mpya.
Unaweza kuusikiliza mchezo huu wa kuvutia kwa kubonyeza hapa ili kwenda katika tovuti ya wahapahapa.com. Ukifika pale tafuta katika vichwa vya kurasa zilizopo pale utaona Mchezo wa Radio.

Habari ambazo tumezipata hivi punde zinaeleza kwamba mwigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Marekani, Gary Coleman, amefariki dunia katika kituo cha Afya kiitwacho Utah Valley Regional Medical Center huko Provo,Utah nchini Marekani.
Gary Coleman ambaye alijizolea umaarufu tangu alipoanza kuigiza akiwa bado mtoto, amefariki kutokana na ugonjwa wa ini.Alijipatia umaarufu zaidi katika sitcom iliyokwenda kwa jina Different Strokes.Humo aliigiza kama Arnold Jackson, mtoto mtundu(mweusi) ambaye amekuwa adopted na familia ya wazungu matajiri wa Manhattan,New York.
Muigizaji huyo alizaliwa huko Zion,Illinois tarehe 8 February 1968. Amefariki akiwa na umri wa miaka 42. Ameacha mke,Shannon Price,aliyefunga naye ndoa miaka miwili iliyopita. Rest in Peace Gary.What Are You Talking About Willis?

Msanii maarufu wa vipindi vya redio,maarufu kama Mzee Pwagu(jina lake halisi ni Rajab Kibwana Hatia),amefariki dunia hivi leo katika Hospitali ya Amana jijini Dar-es-salaam alipokuwa amelazwa kwa muda,akisumbuliwa na ugonjwa wa kwikwi(hiccups) pamoja na matatizo mengine yatokanayo na uzee.
Kama utakumbuka, kabla ya ujio wa televisheni au luninga nchini Tanzania kila mtu alikuwa akitegemea Radio Tanzania Dar-es-salaam(RTD) katika kupata habari,burudani na elimu kupitia sanaa ya kuigiza kupitia kitu kilichojulikana kama “michezo ya redio”. Hapo ndipo vipindi kama vya Pwagu na Pwaguzi vilipotamba.
Kipindi cha Pwagu na Pwaguzi kilikuwa kinarushwa hewani hewani kila Jumamosi kuanzia saa 11:45 hadi 12;00 jioni na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) tangu mwaka 1966 mpaka miaka ya 1980.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Kaole ambapo marehemu alikuwa mwanachama(kama mshauri) mpaka alipofariki, mazishi yanaweza yakafanyika kesho. Shughuli zote za msiba zinafanyikia nyumbani kwake maeneo ya Kigogo Mbuyuni jijini Dar-es-salaam.
Mzee Pwagu alizaliwa mwaka 1923 mjini Tabora. Ameacha mke na watoto wawili. Mmoja kati ya watoto wake ndiye mama mzazi wa msanii chipukizi Abdul Ahmad Salum maarufu kwa jina la Mr Benny wa kundi la Sanaa la Kaole.
Mwenzake,Pwaguzi, ambaye jina lake kamili ni Ali Said Keto,naye alishafariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,AMINA.
Picha na sehemu za habari/Habari Leo Ukitaka kujikumbusha kidogo mchezo wa Pwagu na Pwaguzi,Bonyeza hapa.

Kuna mtu kaniuliza swali ambalo sikuweza kuwa na jibu lake.Sasa kama unavyojua,BC ina watu.Watu kama wewe.Ninapokuwa sina jibu la swali au maswali,naomba msaada kutoka kwako.Ndio raha ya kuzungukwa na jamii.Penye wengi hapaharibiki neno. Mwenzetu kauliza;
Eti ni kweli Irene Uwoya na Jacquiline Wolper wanafanana kiasi kwamba wengine kuthubutu kumuita Jacquline kuwa ni pacha wa Irene Uwoya?
Pichani aliyepo kushoto ni Irene Uwoya na kulia ni Jacquiline Wolper.Wewe unasemaje?Wamefanana?
Kiungo mchezeshaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ghana na klabu ya Chelsea ya Uingereza,Michael Essien(pichani), atazikosa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Chama cha Soka cha Ghana(GFA),kiungo huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti,hatoweza kupona mpaka hapo mwishoni mwa mwezi wa saba(Julai) na hivyo kumaliza kabisa matumaini ya kuweza kucheza katika fainali hizo.
Uamuzi wa mwisho wa kumuondoa Essien katika kikosi cha Ghana(Black Stars) ulifikiwa na chama hicho cha soka kwa kushauriana kwa karibu na timu yake ya Chelsea pamoja na daktari wake na pia madaktari wa Timu ya Taifa ya Ghana.
Pamoja na kwamba hatocheza,habari zinazidi kupasha kwamba Michael Essien ataambatana na timu hiyo kwenda Afrika Kusini na kwamba atasaidia katika masuala mengine ya kiufundi.Ghana wapo kundi D pamoja na Ujerumani, Australia na Serbia. Wataingia uwanjani kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni kupambana na Serbia.
Hii ingekuwa mara ya pili kwa kiungo huyo kucheza katika fainali za Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo miaka minne iliyopita katika fainali zilizofanyikia nchini Ujerumani. Je,Ghana wataweza kufanya vizuri bila kiungo wao mahiri Michael Essien?

Bila shaka unaelewa kwamba kwa waafrika wengi,unene ndio deal.Ukiwa umekondeana au mwembamba,mara nyingi utadhaniwa kwamba umejawa na matatizo,umechacha,unaumwa nk.
Hali ni tofauti katika nchi za ughaibuni.Ukinenepeana ndio unaonekana una matatizo.Ukiingia tu kwa daktari wako swali lake linaweza kuwa “What is wrong,you have gained so much weight”. Suala la unene=afya na kupungua/kukonda=matatizo, ni mjadala ambao hata tukiamua kuuanza hivi leo hautoisha.
Ila kama wewe unaamini kwamba kupunguza uzito ndio afya(mimi naamini katika kuwa wastani) au unataka kupungua uzito kwa sababu zozote zile,basi unaweza kujifunza kutoka kwa mwanamuziki na mcheza filamu,Curtis Jackson au maarufu kama 50Cent.Pichani unaona jinsi alivyopungua.
Kwa mujibu wa mtandao wa ThisIs50.com, amepungua kwa ajili ya role ya filamu iitwayo Things Fall Apart(hakuna uhusiano na kitabu cha Things Fall Apart cha Achebe).Katika filamu hiyo,50 anaigiza kama mcheza Football(American Football-inatumia zaidi mikono) aliye na ugonjwa wa kansa. 50 Cent ameweza kupungua kutoka Paundi 214 mpaka Paundi 160(takribani kutoka kilo 97 mpaka kilo 72.5 hivi). Ametumia nini? Anasema ni Liquid Diet na kukimbia kwenye treadmill kwa masaa matatu kila siku kwa wiki tisa mfululizo!

Je,wacheza filamu wetu wanaweza kuiga mfano huu wa kupungua au kuongezeka ili ufit katika role fulani ya filamu? Changamoto.
Zimebaki takribani siku 15 kabla kipute cha kugombea Kombe la Dunia la Soka hakijaanza huko nchini Afrika Kusini au “bondeni” kama ambavyo wengine wanapaita.
Jumla ya timu 32 zinashiriki fainali za kombe la dunia la mwaka huu ambazo kwa mara ya kwanza kabisa,zinafanyikia barani Afrika. Wawakilishi wa bara la Afrika katika fainali za mwaka huu ni wenyeji Afrika Kusini, Nigeria, Ghana,Ivory Coast, Cameroon na Algeria.
Licha ya hii kuwa mara ya kwanza kwa nchi yeyote ya bara la Afrika kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, hakuna timu ya Afrika iliyowahi kuchukua ubingwa au hata kufikia nusu fainali.Mafanikio ambayo bara la Afrika linajivunia nayo mpaka hivi leo ni kufikia hatua ya robo fainali ambapo Senegal(ilifika hatua ya robo-fainali mwaka 2002 kabla ya kutolewa na Uturuki kwa goli kwa 1-0) na Cameroon(mwaka 1990 ilifikia hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa na Uingereza kwa jumla ya goli 3-2)
Wachambuzi mbalimbali wa soka hawaipi Afrika nafasi ya kufanya vyema japokuwa ni wenyeji kwa sababu mbalimbali kama vile kuwa katika makundi magumu;mfano hapa unatolewa kwa kundi G ambalo ndani yake kuna Ivory Coast,Brazil,Portugal na Korea Kaskazini. Wengi hawaipi Ivory Coast nafasi ya kuendelea raundi ya pili na kwa maana hiyo kuziacha ama timu za Brazil na Portugal ambazo zinapewa zaidi nafasi ya kusonga mbele.
Sababu zingine zinazotolewa ni ukosefu wa uzoefu(Ghana na Ivory Coast zinashiriki kwa mara ya pili wakati Algeria inashiriki kwa mara ya tatu baada ya kutofanya hivyo kwa muda mrefu)
Pamoja na hayo, kwa upande mwingine wale wanaozipa nafasi timu kutoka barani Africa wanajitia moyo wa ushindi kwa sababu ukweli ni kwamba bara la Afrika lina wachezaji lukuki katika ligi za Ulaya jambo ambalo linatuhahakishia kwamba timu za Afrika zilizofuzu zinao wachezaji wengi tu wenye ufundi na uzoefu(skills and experience) na mikikimikiki ya mashindano makubwa kama ya Kombe la Dunia.
Je, Africa tutacheka au tutaendelea kulia na kununa? Miongoni mwa timu hizi ambazo picha zake zipo hapo chini ni ipi ambayo unaishabikia? Ni ipi ambayo unaipa nafasi ya juu kufanya vyema zaidi kuliko zingine? Kwanini unaipa nafasi hiyo?

South Africa

Cameroon

Algeria

Ivory Coast

Ghana

Nigeria
Editor’s Note: World Cup 2010 ni tukio kubwa na la kipekee ambalo bila shaka litafuatiliwa na mabilioni ya watu ukiwemo wewe msomaji na mtembeleaji,msomaji na mchangiaji wetu.Kwa kutambua hilo,BC itakuwa,kwa msaada na ushirikiano wa wapenzi,wataalamu na wafuatiliaji wa soka,itakuwa ikikuletea chambuzi mbalimbali kuhusu fainali hizi.Asanteni

Taifa Stars

Brazil
Brazil are to play Tanzania on 7 June in a World Cup warm-up match ahead of this summer’s finals in South Africa.
The Brazilians have become the first non-African team to schedule a friendly in Africa in the build-up to the tournament, which kicks off on 11 June.
Tanzanian Football Federation (TFF) spokesman Florian Kaijage told BBC Sport that a contract would be signed within the next two to three days. For more information,click here.

Huu hapa ni ujumbe kutoka kwa Zitto Kabwe(MP)
Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi kama invyostahili. Nimeamua kuanzisha blogu hii mpya ili liwe jukwaa la kujadiliana jinsi ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Karibu kwa maoni, ushauri na hata makatazo! Bonyeza hapa kumtembelea.


sending...