Zipo habari kuhusu celebrities wetu ambazo huwa nikizisikia kinachonijia kwanza ni masikitiko.Huwa nasikitika ninapoona kwamba watu fulani ambao ni role-models kwa vijana wetu,wanakuwa wanafanya mambo ambayo sio tu yanawavunjia heshima wao wenyewe,bali pia yanaporomosha maadili ya kiungwana na kiutu.

Bila shaka mpaka hivi sasa umeshasikia habari za mcheza kikapu Hasheem Thabeet kumpiga au kupigana na mwanamuziki nyota TID wikiendi iliyopita pale Club Bilicanas jijini Dar. Baada ya vita ya mikono na mateke,vita sasa imebakia kuwa ya maneno.

Kila mmoja, Hasheem na mwenzie TID amekuwa akitoa maelezo tofauti tofauti kuhusu kilichojiri pale Bilicanas.Kwa mujibu wa Gazeti la Amani(la Global Publisherz), Hasheem anasema alichokozwa kupita kiasi na TID. Na TID anasema,kupitia blog yake,kwamba hajui kwanini Hasheem aliamua kumtenda alivyomtenda.TID haweki wazi sana kilichotokea.Anachosema yeye ni kama vile Hasheem aliamua tu kumfanyia “ubabe” na kumdunda.

Katika vita ya maneno,wakati mwingine ni vigumu kupata ukweli.Ukweli halisi wanao Hasheem na TID. Cha msingi kilichopo mbele ni kwamba kwa kuonyeshana ubabe au ego zenu mbele ya kadamnasi,nyote mmekosea. Kama ulichokozwa Hasheem you could have handled it differently. Verbal violence doesn’t have to end with physical violence. Na TID,kama maelezo aliyoyatoa Hasheem katika gazeti la Amani ni ya kweli,tabia ya kupenda kununua ugomvi,haikujengi bali inakubomoa na kukushushia heshima.

Hasheem maliza likizo yako urudi Marekani kuendeleza mchezo wako.You are a role model to many youngsters.Be one.TID zingatia kazi yako muhimu ya  kuburudisha,kuelimisha na kuonya jamii kupitia muziki wako.Pamoja.

Feedback / Comments

13 Responses to “HASHEEM Vs TID:STOP IT!”

  1. Comment by MsA on May 14th, 2010 2:36 pm

    Very sad. I thought it was all a lie when I read it the other day but true?. I don’t know seems like they both have some growing up to do. I have always been told that “The best medicine is walking away”, no matter what people may call you afterward, but walk away, violence isn’t the answer to anything. Hasheem, you may not be in a bigger spotlight like other players in US, but kid your big in Tanzanian communities and every action you take without thinking it will cost you in the long run. Think before you act, that’s my advice to you.

    T.I.D, your grown man why acting like a kid? If Hasheem or you started the none-sense why didn’t you stop it in the first place? You been locked up before cuz of fighting and your doing it again. Focus is what all of them needs.

  2. Comment by mwandiga on May 14th, 2010 4:24 pm

    Mh BC,
    Nakubaliana na wewe kuhusu mtazamo wa role model wetu. Sidhani kuwa u-role model wa kutwangana tunauhitaji. Nigefurahi kuwaona ma-maceleb. wetu wakiungana japo kufanya kitu remarkable kwa taifa masikini na lisilo na mwelekeo kama letu. Hatuhitaji Naomi aje atembelee TMK hospitali wakati celeb. wetu wanatwangana mitama.
    Ni vigumu sana kutoa hukumu isiyo na ushahidi japo ushahidi wa kimazingira unaweza kuonyesha nani mkorofi. Napenda kumuasa Hasheem kuwa mtu akikuita mshenzi basi ukajibu kwa [neno baya]utahukumiwa individually. Mtama haukukujengea heshima zaidi ya kutia dosari. Ulitakiwa u-control hasira kwa vile mwenzako ‘has nothing to lose’! the least to say.
    Historia ni kitu muhimu sana kwa maisha yetu. Hebu turejee historia za hawa watu wawili tunaweza kuwa na jibu hata kama ni la kufikirika.

  3. Comment by nyandaro on May 15th, 2010 4:30 am

    Ushauri mzuri sana hata mimi naona bora arudi,maanayatakuja mengine,hiyo ndio bongoland

  4. Comment by Mr.Degree on May 15th, 2010 4:36 am

    Nilidhani hasheem amekuja kupumzika nyumbani baada ya misukosuko iliyompata huko NBA, kumbe kaja kujirusha! ama kweli ng’ombe wa masikini hazai!

  5. Comment by chachalika on May 16th, 2010 6:20 am

    DU! WABONGO AIBU TUPU YANI HASHEEM ANAKWENDA KUJILUSHA BILCANAS.BADALA AKAE NA KUIELIMISHA TZ, KWAKILE ALICHO KIONA HUKO NA KIJIFUNZA SASA KAWA ………..OYA HASHEEM SHITUKA UNAWEZA UKAPOTEZA MAISHA OR MALENGO YAKO, HUJUI HIV ,JIVINYARI UTIPATA FRESH P

  6. Comment by Patrick on May 16th, 2010 8:33 am

    me nadhani njia nyepesi ni Hasheem kurudi tu Marekani kuliko kulumbana na TID kwa ajili ya maandalizi mazuri ya NBA sidhani ka ameridhika kushushwa hadi DEVELOPMENT LEAGUE.

  7. Comment by wakusepa on May 16th, 2010 1:02 pm

    Eti role model????
    Role model wanjulikana jamani apo hamana role model.

  8. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 16th, 2010 5:53 pm

    …hakuna cha u-role or what….hawa ni vibweka tuuu….akili ni nywele…kila mtu ana zake…lol…

    Sasa tusemeje….inaudhi kweli kweli….

  9. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on May 16th, 2010 5:55 pm

    …miye nafikiri MALEZI yanancahangia….ingawa siwezi jua hawa ma-bwana wawili walilelelewa vipi (and I am not judging them..)….lakini nafikiri kulikuwa na dosari hii ama ile katika malezi na makuzi yao…..

  10. Comment by hamdani on May 17th, 2010 5:26 am

    kwakweli ni jambo la kusikitisha sana lakini naweza kusema ya kwamba kwa kitendo ambacho wamekifanya hawa jamaa sio kizuri hata kidogo ni wa2 wenye heshima zao wanafanyiana mambo ya ajabu mbele ya haraiki ya wa2 kwa kweli wanajishusha baada ya kujipandisha na tid ndio unaongoza kwa ma2kio ya ajabu take care man

  11. Comment by Muddy on May 21st, 2010 8:57 am

    HI BC,
    DAH NIMEFUATILIA KISA CHOTE FROM AMANI NEWS PAPER MPAKA GLOBU YA TID. HUYU DOGO TID MTATA SANA, NA NDIO MAANA MPAKA LEO BADO ANAKAA KWA MAMA YAKE, WE KUBWA ZIMA MPAKA LEO BADO UNAKAA KWENU USWAHILI KINDONI MAWAZO HATA AKILI ZITAKUJAJE. TID HAJAONEWA NA NDIO MAANA HATA UKISOMA KWENYE BLOG YAKE HANA JIPYA LA KUELEZA. HAWA WATOTO WA KISWAHILI SOMETIMES OVYO SANA NA NDIO MAANA HUWA TUNAWAOMBEA HATA WASIPATE VIJISENTI MANAKE HUWA WANAKUWA KERO SANA USWAHILINI. SASA WEWE EMBU ANGALIA NI KITU GANI KINAWAFANYA WADHALILISHANE HAPO CLUB?, HIVI WE TID HUYO ULIYEKUWA NAE NDIO YULE MCHUMBA WAKO ULITUAMBIA ANASOMA URUSI AU BADO UNAENDEKEZA UMALAYA?, MANAKE WACHA TUWE WAWAZI, SISI TUNAINGIA KWENYE SHOO ZAKO ILI UWEZE KWENDA CHOONI KAMA SISI WENYE UWEZO, BADALA YA KUTULIZA AKILI WEWE UNALETA UMBWIGA HAP, KWAKWELI UMENIBOA SANA, NA KUANZIA LEO SIJI TENA KWENYE SHOO ZAKO POMBE WE, UMENITIBUA SANA, BORA UNGEPELEKWA POLISI URUDI LUPANGO, SISI TULIHANGAIKA KUKUOMBEA KWA JAKAYA WEWE UNALETA UPUUZI MPAKA MSHIKAJI ANATUONA HATUNA MAANA ANATUITA NA KUTUUAMBUA KUWA ALITWAMBIA WEWE HAUNA ADABU.

    ALAFU NA WEWE HASHIMU MBONA NAWE UMEKUWA OVYO, HIVI KWELI KULIKUWA NA MAANA GANI KUANDIKA KUWA WEWE UNAKUNYWA KWA KUSAINI, HUO NDIO UTOTO ULIOUNYESHA HAPA. WEWE KILA MTU ANAJUA WEWE SASAHIVI UNAPESA SASA UNASABABU GANI MPAKA KILA MTU AJUE AU NDIO MAMBO YA KIWAHILI SWAHILI TENA?, HASHIMU EMBU BADIRIKA, USILETE YALE MAMBO YAKO YA CHIPS PALE SINZA KWA REMI KWA MAREHEMU SAMBA, SASAHIVI WEWE NI LEVEL NYINGINE. ULIPASWA KUWAAMBIA HATA MABAUNSA WA BILLS WAKUSAIDIE KUMUONDOA HUYO DOGO KULIKO KUFUKUZANA NAE. YAANI HATA WEWE NIMEKUONA OVYO KABISA. KWENDA ZAKO KULE, NDIO MAANA ALISHUSHWA LEAGUE.
    OK POA WOTE NIMEISHAWASAMEHE MSIRUDIE TENA.

    MUDDY NICE,

  12. Comment by Gerald on May 22nd, 2010 6:39 am

    Ebwaana ee!! Kila mtu anamfahamu TID, nI mtu wa magonvi, huyo si mtu wa kwanza kuleteana naye soo, lakini yote kwa yote , kwa THABEET, nilikuwa ninakuamini sana kwamba umetembea na umejifunza mengi hasa kwa wenzetu, ambao wanaamini kuwa nidhamu ya nje ya uwanja na ndani ya uwanja ndiyo silaha pekee, ya mafanikio, sasa kilichopelekea umpige mashuti TID ni nini? kama ungeamua kushiti kwani ingekuwaje? OK, sometimes inabidi utunishe misuli ili usijeonekana mwili wa bure, lakini kwa TID mwenye mwili kama wangu, watu wangemzarau tena ungepanda chati hapa bongo kuliko sasa umetia doa CV yako ambayo ilikuwa iko clean.mi! naona rudi USA, BWana. NA WEWE mjomba TID, Iga mfano wa the DUDU BAYA AMBAPO SASA NI DUDU ZURI, siku hizi amekuwa mtu mzima, ila waswahili wakimwona mtu yuko kimya wanadai amefulia, TID KUWA BWANA, watu wansema unakaa kwenu, mimi sijui, ila kama ini kweli tafuta GHETO UHAME UGALI WA MAMA UNAKUTIA UTOTO, ni sawa na mtoto anayenyonya sikuzote hakui, YANGU NI HAYO TU MAZEE, BIG UP!! BC.

  13. Comment by In the News: Liyumba Found Guilty, Nyerere Declared A Saint « AS I PLEASE on May 24th, 2010 11:54 am

    [...] The blogosphere has exploded with reports that the Memphis Grizzlies Tanzanian Centre, Hasheem Thabeet, allegedly assaulted the Bongo Flava star TID at Bilicanas, a night club in Dar es Salaam two weeks ago. The reason for the alleged altercation remains unclear. [...]

Leave a Reply