Majuzi Tanzania imepoteza msanii hodari ambaye wengi tulianza kumsikia kupitia michezo ya radio. Huyo si mwingine bali Mzee Pwagu(Pumzika kwa Amani Mzee wetu). Lakini je,michezo ya radio ingalipo na nini nafasi yake katika jamii ya leo? Ukweli ni kwamba ndio,michezo ya radio ingalipo na bado ina nafasi na jukumu lile lile la kuelimisha,kubudurudisha, kuonya na hata kurekebisha jamii. Mfano mzuri wa michezo hiyo ni ule unaorushwa na Wahapahapa.

WAHAPAHAPA ni mchezo wa radio wenye nia ya kubadili mtazamo wa kimaisha kuwa chanya. Mchezo huu unalenga suala zima la mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, matibabu na uangalizi.

Mchezo huu unarushwa kila wiki kwa namna ya kuvutia na kuelimisha, kwa njia ya mawasiliano ya radio.
Maisha yanayojiri katika mchezo huu yanatokea katika vijiji vya kufikirika vya KALUMBI na MAKATANI vilivyoko sehemu Fulani huko Tanzania.

“Homeboys” ni bendi ya muziki ambayo ndio kiunganishi cha matukio yote yanayojiri katika mchezo huu wa kusisimua. Bendi hii inaundwa na wavulana watano ambao baadae kidogo mwanamuziki wa kike anajiunga nao.

Bendi hii inaamini kuwa ikipiga muziki mzuri itafanikiwa kimaisha na hatimae watakuwa nyota kwa washabiki wao wa nyumbani. Bendi inakutana na changamoto kadhaa zinazokinzana na nia yao ya kuwa vinara wa muziki pamoja na kujitengenezea kipato. Kuna migogoro lakini haikosi suluhisho, maslahi ya bendi ni makubwa zaidi ya maslahi ya mtu mmoja mmoja.

Hatuishii kuona maisha ya wanabendi peke yake bali mchezo unazidi kunoga zaidi pale tunapokaribishwa kuona pia maisha ya ndugu, familia, jamaa, na marafiki wa wanabendi. Tunaona migogo na changamoto inayokabili jamii hii na jinsi inavyoamua kuungana pamoja kupambana kuelekea siku mpya.

Unaweza kuusikiliza mchezo huu wa kuvutia kwa kubonyeza hapa ili kwenda katika tovuti ya wahapahapa.com. Ukifika pale tafuta katika vichwa vya kurasa zilizopo pale utaona Mchezo wa Radio.

Feedback / Comments

4 Responses to “UMEWAHI KUUSIKIA MCHEZO WA RADIO WA WAHAPAHAPA?”

  1. Comment by mamilo on June 8th, 2010 5:38 am

    Napenda kuwapongeza walioweza kubuni na kuandaa kipindi hicho ukweli kinaelimisha jamii ,ninaposikiliza nakumbuka enzi hizo tulizokuwa tunasikiliza kipindi cha mchezo wa redio vilivyokuwa vinarushwa na redio Tanzania hasa walivyokuwa wanaigiza, akina kipara hao katika zile mfano FAHARI KITOVU CHA UZEMBE na vinginevyo hata naanza sahau lakini ingekuwapo filamu ningetunza au hata vitabu mfano vya Penina Mlama havichapishwi tena jamani hapo inakuwaje? walikuwa ni hazina walifanya tupende kusikiliza vipindi hivyo kwa wakati huo,hii inaonyesha jinsi gani watu walivyo na uwezo wa kuigiza redioni.Kama ingewezekana hawa WA HAPA HAPA wangetayarisha filamu ya hayo yanayoendelea katika kipindi hicho. Pia muda nao unatukwaza kama itawezekana kirushwe mara 3 kwa wiki hii itasaidia usipowahi kusikiliza alhamisi au jumapili bado uwe na nafasi kusikiliza tena wakati mwingine kweli ni kipindi kizuri NAWAPA PONGEZI KUNDI ZIMA!!!

  2. Comment by DORICE MCHAU on August 24th, 2010 4:09 am

    BIG UP SANA, NAPENDA SANA KUTOA PONGEZ NYINGI KWA KUWEZA KUTUELIMISHA KUPITIA KIPINDI CHENU CHA WAHAPAHAPA KWELI TUNAELIMIKA SANA NA KINAELIMISHA JAMIIKUHUSU JINSI YA KUISHI KWA MATUMAIN KWA MTU MWENYE VIRUS VYA UKIMWI. ASANTEN SANA

  3. Comment by DORICE MCHAU on August 24th, 2010 4:13 am

    PIA NAOMBA KUTOA PENDEKEZO KUWA MTUONGEZEE MUDA KIDOGO KATIKA KIPINDI.

  4. Comment by Stephen edward on May 8th, 2011 6:20 am

    Naombeni mnisaidie kuniambia hiki kipindi kinarushwa hewani kwa sasa na redio gan maana kimeniacha sehem tamu sana kwan wakat huo kabla ya mwez wa nne nilikua nikikisikiliza radio one lakn sasa hiv cjakisikia naomben mnijibu kwa kutumia email yangu hapo juu

Leave a Reply