Kama unafuatilia masuala ya filamu hususani kutoka Hollywood,bila shaka utakuwa umesikia kuhusu “wazimu” uliowaingia wapenzi wa filamu(wengi wao ni vijana) kuhusu movie mpya inayoingia Theatre hivi leo ya The Twilight Saga:Eclipse. Ni movie kuhusu Vampires. Vijana wengi wa kizungu hupenda sana hadithi na mikasa kuhusu Vampires.Tizama Trailer ya filamu hiyo hapa chini;

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Wenzetu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(zamani ilikuwa inaitwa Zaire),leo wanasheherekea miaka 50 ya Uhuru! D.R.C walipata Uhuru kutoka kwa mkoloni Mbelgiji.Tunawapongeza.

Pichani ni Patrice Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Zaire. Yeye ndiye aliyeongoza harakati za kujipatia uhuru.Wiki chache tu baada ya Uhuru na kuwa madarakani,aliuawa.Unaweza kusoma zaidi kuhusu historia yake kwa kubonyeza hapa.

Katika siku chache zijazo,nitafanya mahojiano na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond.

Je una swali au maswali ambayo ungependa niyajumuishe katika maswali yangu kwa msanii huyo ambaye mapema mwaka huu alibeba Tuzo 3 za Kilimanjaro (Kilimanjaro Music Awards).

Unaweza kutuma swali au maswali yako kupitia bongocelebrity at gmail dot com au info at bongocelebrity dot com. Asante.

Burudika kidogo na wimbo wake Kamwambie

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Okay,kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi nchini Tanzania,kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu wa 2010 hazijaanza rasmi au zinatakiwa kuwa katika “mute mode” kwa sasa.

Asikudanganye mtu,kampeni zimeshaanza.Kama una mpango wa kuchukua “jimbo” fulani na mpaka leo bado unasubiri tarehe rasmi ya kampeni kuanza,angalia.Unaweza kuwa umechelewa kidoogo!Isitoshe zimebakia siku kama 125 hivi kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Katika pitia pitia yangu mtandaoni,nilipita kwa Dr.Faustine na kukuta kwamba Rais Jakaya Mrisho Kikwete,tayari ameanza kujizatiti katika matumizi ya Zama Mpya za Habari na Mawasiliano za Kijamii(New Social Media) ili kuhakikisha kwamba watanzania wanampa tena dhamana ya kuwaongoza kwa miaka mingine mitano(5). Zama za ari mpya,kwa kasi mpya na nini tena ndio anazipa kisogo.Mambo ni Kilimo Kwanza. Unaweza kuzisoma Nguzo Kumi za Kilimo Kwanza kwa kubonyeza hapa.

Tayari ipo blog maalumu kwa ajili ya kampeni yake na pia Ukurasa wa Twitter mahsusi kwa ajili ya kuripoti kila anachokifanya.

Kama utakumbuka Rais wa Marekani, Barack Obama, ndiye anasifika kuwa “muasisi” wa kampeni za kisiasa zinazotumia New Social Media au vyombo vya habari vya kijamii.

Obama alitumia vitu kama Facebook(BC ina ukurasa wake wa Facebook,ukitaka kujiunga nasi,bonyeza hapa),Twitter,YouTube,DailyMotion,MySpace nk kwa mafanikio makubwa wakati wa Kampeni yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2008 nchini Marekani. Matokeo ya kampeni hizo sote tunayajua.Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo linalopenda ubabe,mtu mweusi aliingia Ikulu(White House)

Je,Kikwete ataweza kuwafikishia ujumbe wake(kampeni zake bila shaka zitaongozwa na kauli mbio ya Kilimo Kwanza) watanzania waliotapakaa ulimwenguni kote na hususani wanaozitumia nyanja hizo za mawasiliano? Na vipi kuhusu suala la maoni (comments) katika blog la Mheshimiwa Rais?Uhuru wa kutoa maoni utazingatiwa? Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo tutakuwa tukiyaangalia.

Bila shaka uliona sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA yanayoendelea nchini Afrika Kusini.Kama jibu ni ndio,bila shaka unakumbuka wimbo alioimba R.Kelly akishirikiana na Soweto Gospel Choir.Hii hapa ni Official video ya wimbo huo;Burudika

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Unaweza kusema alikuwa na mchango gani katika ukuzaji wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania?

Kama jana ulipata muda kutizama Tuzo za Kituo cha Televisheni cha BET cha nchini Marekani(BET Awards 2010),bila shaka ulisikia jina la Tanzania likitajwa kama mara mbili au tatu hivi.

Tanzania haikutajwa kwa sababu wasanii wake walikuwemo katika kuwania tuzo hizo.La.Tanzania ilitajwa kwa sababu Mwanamuziki John Legend(pichani) alipokea BET Humanitarian Award kutokana na kazi mbalimbali za kusaidia jamii anazozifanya na hususani nchini Tanzania.

Kupitia mradi wake ujulikanao kama Show Me Campaign,John Legend amekuwa akiingia na kutoka nchini Tanzania kila mara katika kutembelea na kusimamia miradi mbalimbali. Mojawapo ya miradi aliyonayo nchini Tanzania ni pamoja na ile anayoifanya katika kijiji kiitwacho Mbola kilichoko Uyui mkoani Tabora.Unaweza kusoma zaidi kuhusu miradi hiyo kwa kubonyeza hapa. Kama inawezekana,tafadhali muunge mkono.Unaweza fanya hivyo kwa kubonyeza hapa.

Bila shaka utakubaliana nasi kwamba hatuna budi kuwashukuru watu kama hawa kwa jinsi wanavyojitolea katika kuwasaidia ndugu,jamaa na wananchi wenzetu.

Thank You John Legend.We appreciate all you are doing for Mbola and for Tanzania.

Photo/AP

Bila shaka umezipata habari ambazo zimeshaenea sehemu mbalimbali ulimwenguni kuhusu kukamatwa na kisha kuachiwa kwa dhamana(kajiwekea mwenyewe mdhamana)Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Joseph Mbilinyi aka Mr. II alias Sugu.

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo blogs ya Issa Michuzi na Da,Subi(wavuti dot com) sababu za kukamatwa kwake leo na maafisa wa jeshi la Polisi akiwa katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati wa kikao cha kuongelea masuala ya muziki, ni kufuatia mmoja wa viongozi wa kituo kimoja  cha redio ya jijini Dar Es Salaam kumshitaki kuwa anamtishia maisha kwenye wimbo mmoja ambapo Mr. II anasikika akisema “I wanna kill you”. Wimbo huo na nyinginezo zinapatikana katika albamu ya ‘Anti-Virus’ inayosambazwa bure mtaani.

Katika utetezi wake,Mr. II ambaye alitarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania Ubunge mkoani Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA,anasema jambo hilo limemshangaza kwa kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo ni ya kisanii zaidi na yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja.

Amedai alikamatwa na kuhojiwa na maofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo kwa saa kadhaa na kisha kuachiwa kwa dhamana ya kujidhamini mwenywe, na ametakiwa kuripoti kituoni hapo kesho kutwa.

Mr. II pamoja na wasanii wengine wamerekodi nyimbo kadhaa na kuweka kwenye albamu moja ambayo wameiita Anti-Virus, wakielezea hisia zao mbalimbali za kimaisha na kadhia la muziki wa Tanzania.

Je,hii na haki na sahihi(kwa Sugu kufikishwa katika mkono wa sheria)  au ni uonevu? Ni kweli kwamba inawezekana Sugu amekamatwa kutokana na juhudi zake mpya katika ulimwengu wa siasa ambapo hivi karibuni yeye na baadhi ya wasanii walitangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)?

Wikiendi imewasili tena.Ni muda wa kuburudika kupitia hapa BC. Ni muda wa kutuliza akili kidogo na kutafakari yale yaliyojiri katika wiki hii.Ni muda wa kutembeleana,muda wa kuhudhuria vikao mbalimbali vikiwemo vya harusi nk.

Kwa wale ambao mpo ‘ughaibuni”,majira ya joto(summer) ndio yameshawadia.Ni wakati wa kutoka nje na kuota jua!

Wimbo wa leo unaitwa Vigelegele kutoka kwao Western Jazz Band ambayo ni miongoni mwa bendi zilizotamba sana nchini mwetu katika miaka ya 60s sambamba na bendi zingine kama vile Dar-es-salaam Jazz Band na Kilwa Jazz Band.

Wimbo wa leo ni maalumu kwa ajili ya wale ambao wanatarajia kuhudhuria shughuli yeyote ambapo vigelegele hupigwa.Kama unavyojua,majira ya joto huambatana na shughuli kedekede. Kuna harusi,BBQ Parties nk.Ili mradi tu kunakuwa na shughuli kila kukicha. Tunakutakia weekend njema.Burudika.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page