Ninapoandika post hii,Afrika Kusini wapo uwanjani wakimenyana na Mexico.Wanaongoza goli 1-0.
Kwa bahati mbaya,Mzee Madiba ameshindwa kuhudhuria ufunguzi wa fainali hizo kutokana na kifo cha kitukuu wake,Zenani Mandela,kilichotokea jana usiku kwa ajali ya gari.

(AP Photo/Nelson Mandela Foundation, Debbie Yazbek)
Pichani juu ni Mandela na wajukuu zake.Kutoka kushoto ni Thembela Mandela,Zenani Mandela(aliyefariki) na Mbuso Mandela.
Unaweze kutizama video kidogo ya Mandela na kitukuu wake aliyefariki kwa kubonyeza hapa.
UPDATE: Mchezo kati ya South Africa na Mexico umekwisha.Matokeo ni 1-1. Goli la South Africa lilifungwa na Siphiwe Tshabalala kunako dakika ya 55.Mexico walisawazisha kunako dakika ya kwa goli rahisi lililofungwa na Rafael Marquez kunako dakika 79.
Feedback / Comments
One Response to “FAINALI ZIMEANZA,MANDELA ASHINDWA KUHUDHURIA.”
Leave a Reply


sending...
So sad…R.I.P.Jamani kunywa pombe na kuendesha magari noma