Umeshawahi kuhudhuria maonyesho ya Twanga Pepeta?Unasemaje kuhusu mchango wa hawa kina-dada wa Twanga katika kukamilisha burudani?

Lakini je unafahamu kwamba bendi ya Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi za muziki ambazo zimedumu kwa muda mrefu zaidi nchini Tanzania? Bila shaka hayo ni matokeo ya uongozi thabiti wa Asha Baraka,Mkurugenzi wa ASET(African Stars Entertainment Tanzania). Asha Baraka ni miongoni mwa watu ambao ningependa sana kupata fursa ya kufanya naye mahojiano.If you can make it happen,please contact us.

Pichani ni Dr.Willbroad Peter Slaa akihutubia mamia ya wananchi waliokwenda kumsikiliza hivi karibuni mjini Arusha.

Hivi karibuni Dr.Slaa alitangazwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambacho kwa muda sasa amekitumikia kama Katibu wake Mkuu.

Tangu ilipotangazwa kwamba Dr.Slaa sio tena candidate wa Ubunge bali Urais,kumekuwa na maoni tofauti tofauti.Kuna ambao wanasema Dr.Slaa asingethubutu kugombea Urais na badala yake angeendelea tu kugombea kiti chake cha Ubunge wa Karatu kwani nafasi ya kumshinda mgombea wa Chama Cha Mapinduzi-Jakaya Mrisho Kikwete ni ndogo sana.

Wanaounga mkono hoja hiyo wanasema,kwa sababu uwezekano wa Dr.Slaa kumshinda Kikwete ni mdogo,hiyo ina maana kule Bungeni kutakuwa kumepungukiwa na mbunge makini na ambaye kwa muda wa miaka mitano iliyopita,aliwapa tabu na challenge kubwa,wabunge na viongozi wa chama tawala cha CCM.

Kwa upande mwingine,wale wanaounga mkono uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Dr.Slaa katika kuwania Urais,wanasema ni kitu kizuri kwa ukuaji wa demokrasia na wanaamini kwamba Dr.Slaa atamshinda Jakaya Mrisho Kikwete na kwa maana hiyo he will become our next President.

Tungependa kupata maoni yako.Je,unakubaliana na wale wa kundi la kwanza au la pili? Will Dr.Slaa become our next President?

BC iliwahi kufanya naye mahojiano ya kina na Dr.Slaa.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.

Pichani juu ni Dr.Remmy Ongala.Tuliwahi kuandika kwa kirefu historia yake.Unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa. Katika miaka ya nyuma,yeye na Orchestre Super Matimila,ndio walikuwa kitambulisho kizuri cha muziki kutoka Tanzania katika nchi za Ulaya na hata Marekani ya Kaskazini.Alipendwa sana wakati alipokuwa akihudhuria matamasha ya WOMAD.

Mpaka leo hii,watu wengi wa ughaibuni ambao hawatoki Tanzania,hupenda kumuulizia na kutaka kujua yuko wapi na anafanya shughuli gani na kama bado anajishughulisha na muziki.Jibu la maswali hayo linaeleweka;Remmy Ongala siku hizi ni mlokole.Kama bado anajishughulisha na muziki,basi ni ule wa kiroho.Ule wa kumsifu na kumtukuza Muumba.

Remmy Ongala na Orchestre Super Matimila,ndio wanaotupa burudani ya wikiendi hii.Wimbo unaitwa Kipenda Roho.Anasema Kipenda Roho hula nyama mbichi.Kipenda Rohooo…msikilize na furahia mwisho wa wiki.Asante.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Prof.Jay,The Heavy Weight MC

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi(pichani) kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Brazil .

Uteuzi wa Balozi Malambugi umetokana na na kuteuliwa hivi karibuni kwa aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.

Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.

Anaitwa Kida Waziri.Enzi zake aliwahi kutamba sana na Vijana Jazz Band.Bila shaka wengi bado tunamkumbuka kwa wimbo wake Wifi Zangu.

Sasa kwa mujibu wa blog ya Brother John Kitime,Kida is back. Hivi karibuni ataingiza sokoni album mpya ambayo itakuwa na nyimbo 6.

John Kitime anayo habari kamili.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Unapoongelea wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao miziki yao na mashairi yao yametoa mchango mkubwa katika kuufanya muziki huo ukubalike na kupewa heshima na nafasi yake katika jamii,bila shaka huwezi kuthubutu kumweka pembeni Joseph Haule au kama anavyojulikana miongoni mwa washabiki na wadau wa muziki; Proffessor Jay,MC Shupavu,The Heavy Weight MC,Jay wa Mtulinga,Mti Mkavu,Jiizeh nk.

Hivi sasa Prof.Jay yupo nchini Marekani akiendelea na tour yake ndani ya taifa hilo ambalo hivi sasa linaongozwa na Barack Obama,Rais wa kwanza mweusi. BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ziara hiyo. Je unataka kujua atatua na kufanya shows katika miji na majimbo gani? Anasemaje kuhusu ambacho ameweza kukiona na kujifunza nchini humo mpaka hivi sasa? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Prof,asante kwa nafasi hii ya mahojiano mafupi.Mambo yanakwendaje?

PROF.JAY: Safi vipi mtu wangu?Na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi hii adimu.

BC: Ni muda sasa umekuwa nchini Marekani kwa ajili ya American Tour yako kiasi kwamba mashabiki wako ambao hawajui uko wapi wamekuwa wakijiuliza maswali yasiyo na majibu ya haraka.Kupitia hapa BC unaweza kuwaeleza kwa sasa hapo Marekani makazi yako ni katika State au Jimbo gani?

PROF.JAY: Asante na naomba niseme samahani kwa wale ambao wamekuwa wakijiuliza kwamba nipo wapi na mambo kama hayo.Kwa sasa hapa nchini Marekani nipo Massachussets nikiwa nimeweka kambi na DJ wangu anayekwenda kwa jina la RICHMAKA.Na sababu ya kuweka kambi hapa ni ili kupata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi kwa pamoja kama team ili shows ninazofanya ziwe katika kiwango cha hali ya juu na mashabiki wangu wapate thamani halisi ya pesa zao watakazotoa ili kuja kwenye shows.

BC: Ni kampuni gani inakusimamia katika hii tour yako hapo nchini Marekani?

PROF.JAY: Kampuni inayonisimamia inaitwa NGOME ENTERTAINMENT.Makao yake makuu yapo Dallas,Texas.Kampuni hii ipo chini ya CEO wake,Kitova Mungai.

BC: Ni miji gani ambako unatarajia kuwa na shows?

PROF JAY: Mpaka hivi sasa nimeshapiga show moja ambayo ilifanyikia pale Houston,Texas tarehe 4 Julai(siku ya kusheherekea Uhuru hapa nchini Marekani) Ratiba ya shows zinazofuatia ni kama ifuatavyo:

  • Tarehe 31/8/2010 Washington,D.C
  • Tarehe 7/8/2010 Boston,Massachusetts.
  • Tarehe 13/8/2010 Dallas,Texas.
  • Tarehe 19/8/2010 Kansas City,Missouri.
  • Tarehe 20/8/2010 Witchita,Kansas.
  • Tarehe 11/9/2010 Atlanta,Georgia.

Mpaka hivi sasa ratiba ndio hiyo. Lakini kuna shows zingine nyingi ambazo zinaweza kutokea kwa sababu Promoters kadhaa wameonyesha nia na kufanya majadiliano ya awali ingawa hatuja-confirm firm tarehe kamili za kufanya kazi. Pia naomba niweke wazi kwamba milango ipo wazi kwa promoters wengine ambao wanataka kubook shows.Wenye nia hiyo wanaweza kuwasiliana na Kitova kwa kutumia nambari ya simu +1 214 455 5082 au DJ Rich Maka kwa nambari +1 413 262 0400.Karibuni sana.

BC: Unawaambia nini mashabiki wako katika miji hiyo?Watarajie nini kutoka kwako?

PROF.JAY: Kama nilivyogusia hapo juu,mashabiki wategemee shows za kiwango cha juu kabisa ambayo hawajawahi kuiona kutoka kwa msanii yeyote kutoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki,kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Ninachowaomba wajitokeze kwa wingi ili wasije wakayakosa yale niliyowaandalia.Pia nawaomba wapatapo habari hii wawaambie na wengine.

BC: Waswahili wanasema kutembea kwingi ni kuona mengi pia.Mpaka hivi sasa unaweza kusema umejifunza nini kutokana na ambacho umekiona nchini Marekani iwe ni kwa upande wa sanaa ya muziki au jamii kwa ujumla?

PROF.JAY: Kwanza kabisa nimejifunza professionalism. Huku watu wanaheshimu sana kazi zao. Muda wa kazi ni muda wa kazi. Pia muziki wa huku upo katika kiwango cha juu. Bila shaka na sisi tunahitaji marekebisho mengi sana ili nasi tuboreshe miziki yetu na kazi zetu za sanaa zifikie angalau robo tatu ya kiwango ambacho wenzetu wameshafikia.Nasema hivyo kwa sababu huku muziki ni kazi na ni ajira kubwa sana kwa vijana na hata wasio vijana.Inaheshimika kama kazi nyingine zingine zozote.

Kila anapofanya show,umati kumbi na viwanja huwa “vinatapika”.Hapo ilikuwa ndani ya CCM Kirumba-Mwanza.Can you do a count from this photo?

BC: Baada ya Tour yako nchini Marekani unatarajia kuelekea katika nchi nyingine kuendelea na tour au utarudi kwanza nyumbani kupumzika kidogo?

PROF.JAY: Baada ya kukamilisha hii tour,nitarudi nyumbani kwa mapumziko mafupi kisha nitaelekea Ulaya kwa tour nyingine.Mpaka sasa nimeshapata mwaliko kutoka nchi za Scandinavia(Sweden,Norway,Denmark na Finland).Pia nimepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza nchini Uingereza. Nitakaporudi nyumbani ndio nitajua wapi pa kuanzia.Mashabiki na wadau watajulishwa kuhusu tour hizo kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BongoCelebrity.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

BC: Mbali na hiyo tour kuna shughuli nyingine unafanya huko Marekani?

PROF.JAY: Ni kweli kabisa.Mbali na tour pia narekodi miziki.Tumeshaongea na kampuni moja ya kutengeneza video ili tuweze kushoot video kadhaa huku huku.Pia nafanya mawasiliano na wanamuziki mbalimbali kutoka nchi nyingine duniani ili kubadlishana mawazo na pia kuangalia uwezekano wa kufanya kazi pamoja.

Mbali na yote hayo,kama unavyofahamu mimi ni Balozi wa MARALIA NO MORE.Wao pia wametumia nafasi hii kunialika New York yalipo makao yao makuu.Nitakuwa huko tarehe 28 na 29 July ili nikutane na staff wote kwa pamoja.Vyombo kadhaa vya habari vitakuwepo na hivyo bila shaka kutakuwa na media coverage.

BC: Kama Balozi wa Malaria No More,unaonaje kuhusiana na vita dhidi ya ugonjwa huo nchini kwetu? Utakuwa na ujumbe wowote maalumu utakapokutana na staff nzima ya Malaria No More?

PROF.JAY: Kwa kweli jitihada za kupambana na ugonjwa wa malaria zinakwenda vizuri.Kwa kutumia muziki,wananchi wengi wamepata nafasi ya kuelewa jinsi ugonjwa huo unavyoenea,mbinu za kupambana nao nk.

Nitakapokutana na staff wa Malaria No More,nitawaeleza zilipofikia jitihada zetu na jinsi tulivyofanikiwa kuwazindua watanzania kuhusiana na ugonjwa huu hatari ambao unaua mamilioni ya watanzania kila mwaka huku wengi wao wakiwa ni watoto chini ya miaka mitano(5) na akina mama wajawazito. Jitihada hizi zinaendelea kufanikiwa kutokana na mchango na support kubwa kutoka kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

BC: Je unatarajia kutoa albamu mpya mwaka huu? Kama sivyo,lini mashabiki wako watarajie album mpya?

PROF.JAY: Ni kweli,it’s about time.Hopefully ambo yote yakienda sawa mwakani mwanzoni nitatoa album mpya. Kwa hiyo mashabiki wangu vuteni subira kidogo. Kazi tumeshazi-record ila tunachozingatia ni lini muda muafaka wa kuzitoa.Nasubiri muongozo kutoka kwa Management yangu.

BC: Shukrani Prof.Tunakutakia kila la kheri katika American Tour yako.

PROF.JAY: Asanteni sana wakuu.


Unaweza kuwaita FFU ukipenda.Lakini ukiwatambua au kuwatambulisha kama The Ngoma Africa Band,unakuwa hujakosea pia.Ni bendi inayoundwa na watanzania yenye makao yake makuu nchini Ujerumani.

Katika kuendeleza shamrashamra za majira ya kiangazi(summer), Jumamosi tarehe 7 mwezi wa Nane(August) vijana hao machachari watakuwepo jijini Frankfurt,huko huko Ujerumani katika tamasha kubwa linalojulikana kama Afrika & Karibik Festival litakalofanyika katika viwanja vya Robestock Park hapo Frankfurt.

Baada ya hapo FFU hao wanatarajiwa kuwasha moto katika tamasha lingine kubwa mjini Keiserslautern,Ujerumani.Hiyo itakuwa siku ya Jumapili tarehe 8-08-2010.

Kazi kwenu mashabiki wa muziki mliopo Frankfurt na Keiserslautern.Msikose kwenda kuwaunga mkono mabalozi hawa wa Tanzania kupitia muziki.

Unaweza kuwasikiliza The Ngoma Africa Band hapa www.myspace.com/thengomaafrica

Miongoni mwa mambo ambayo yanatia moyo nchini kwetu ni pamoja na kuendelea kukua kwa tasnia ya filamu kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia. Ukuaji huo unakwenda sambamba na kuona kwamba,siku baada ya siku, wapenzi wa filamu za “nyumbani” wanazidi kuongezeka na kwa maana hiyo industry nzima ya filamu inazidi kukua.

Lakini uungwaji mkono huo haukuja bure tu. Umetokana na tabia nzuri ambayo wasanii wengi wa sanaa hiyo wameionyesha.Wamekubali kukosolewa na kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali wa masuala ya filamu na kuyafanyia kazi ipasavyo.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Steven Kanumba ambaye bila shaka sote tunakubaliana kwamba kila kukicha ameonyesha kuwa na bidii kubwa kabisa katika kuboresha kazi zake na uigizaji wake kwa ujumla.

Mwezi ujao(August),Kanumba anatarajia kuendelea kuthibitisha jinsi anavyozidi kukomaa katika sanaa hiyo,itakapotoka filamu ambayo imepewa jina Crazy Love(Part 1 & 2). Kwa mujibu wake yeye mwenyewe kupitia blog yake,ili kuweza kuigiza katika filamu hiyo,ilimbidi kusoma vitabu mbalimbali vya wanafalsafa mashuhuri ulimwenguni kama vile Plato,Karl Max,Alexander The Great,Samuel Taylor nk ili kuelewa zaidi mambo yanayohusu tabia za binadamu,falsafa nk.

Je usomaji huo ulimsaidiaje Kanumba katika Crazy Love?Usikose kununua makala halisi ya filamu hiyo pindi itakapoingia sokoni mwezi ujao.

Photos Courtesy:Kanumba.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page