MBUNGE wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za kugonga na kuua papo hapo mwenda kwa miguu ambaye hakufahamika jina mara moja.

Akimsomea mashitaka yake jana mbele ya Hakimu Mkazi Hassan Momba, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Beatrice Nsana, alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 11 mwaka huu saa 5.30 usiku eneo la Wajenzi, mjini hapa.

Nsana alisema mtuhumiwa Mporogomyi alikuwa akiendesha gari namba T288ASJ aina ya Toyota Land Cruiser akashindwa kusimama amruhusu mwenda kwa miguu huyo avuke barabara, akamgonga.

Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa Mbunge huyo anakabiliwa na mashitaka mawili; kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha kifo.

Alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika; mshitakiwa alikana mashitaka na kusema hamfahamu marehemu wala makazi yake.

Mtuhumiwa alipata dhamana baada ya kukidhi masharti ya Sh milioni 5 na kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 5 mwaka huu itakapotajwa.

Source:Habari Leo.

Photo Courtesy: Tanzania Parliament Website.

Feedback / Comments

2 Responses to “MBUNGE WA KASULU KIZIMBANI KWA KUGONGA NA KUUA!”

  1. Comment by msemakweli on July 14th, 2010 12:41 pm

    Huyu mbunge inafaa sasa anyang’anye leseni yake na apewe adhabu kali, inaelekea anaendesha gari vibaya na bila uangalifu. nakumbuka mwaka 2006 akiwa anaendesha gari yeye mwenyewe alimgonga mtoto mdogo wa shule darasa la 3 pale Chamakweza,Chalinze maskini mtoto wa watu alipoteza maisha palepale na hakuna hatua yoyote kali iliyochukuliwa dhidi yake. Inafaa sasa achunguzwe na apewe adhabu kali na kutopewa ruhusa ya kuendesha gari tena.

  2. Comment by zitto kiaratu on July 15th, 2010 5:14 pm

    huu ni mwisho wa ccm/tanu kwa sababu hata mkimtumia nyerere yeye afadhali hakuuwa mtu/mtoto kina ngombale-mwiru/pius msekwa kwa nini msife tuu, watanzania tunataka kuangalia mbele sio nyuma

Leave a Reply