
Unapoongelea wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao miziki yao na mashairi yao yametoa mchango mkubwa katika kuufanya muziki huo ukubalike na kupewa heshima na nafasi yake katika jamii,bila shaka huwezi kuthubutu kumweka pembeni Joseph Haule au kama anavyojulikana miongoni mwa washabiki na wadau wa muziki; Proffessor Jay,MC Shupavu,The Heavy Weight MC,Jay wa Mtulinga,Mti Mkavu,Jiizeh nk.
Hivi sasa Prof.Jay yupo nchini Marekani akiendelea na tour yake ndani ya taifa hilo ambalo hivi sasa linaongozwa na Barack Obama,Rais wa kwanza mweusi. BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ziara hiyo. Je unataka kujua atatua na kufanya shows katika miji na majimbo gani? Anasemaje kuhusu ambacho ameweza kukiona na kujifunza nchini humo mpaka hivi sasa? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Prof,asante kwa nafasi hii ya mahojiano mafupi.Mambo yanakwendaje?
PROF.JAY: Safi vipi mtu wangu?Na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi hii adimu.
BC: Ni muda sasa umekuwa nchini Marekani kwa ajili ya American Tour yako kiasi kwamba mashabiki wako ambao hawajui uko wapi wamekuwa wakijiuliza maswali yasiyo na majibu ya haraka.Kupitia hapa BC unaweza kuwaeleza kwa sasa hapo Marekani makazi yako ni katika State au Jimbo gani?
PROF.JAY: Asante na naomba niseme samahani kwa wale ambao wamekuwa wakijiuliza kwamba nipo wapi na mambo kama hayo.Kwa sasa hapa nchini Marekani nipo Massachussets nikiwa nimeweka kambi na DJ wangu anayekwenda kwa jina la RICHMAKA.Na sababu ya kuweka kambi hapa ni ili kupata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi kwa pamoja kama team ili shows ninazofanya ziwe katika kiwango cha hali ya juu na mashabiki wangu wapate thamani halisi ya pesa zao watakazotoa ili kuja kwenye shows.
BC: Ni kampuni gani inakusimamia katika hii tour yako hapo nchini Marekani?
PROF.JAY: Kampuni inayonisimamia inaitwa NGOME ENTERTAINMENT.Makao yake makuu yapo Dallas,Texas.Kampuni hii ipo chini ya CEO wake,Kitova Mungai.
BC: Ni miji gani ambako unatarajia kuwa na shows?
PROF JAY: Mpaka hivi sasa nimeshapiga show moja ambayo ilifanyikia pale Houston,Texas tarehe 4 Julai(siku ya kusheherekea Uhuru hapa nchini Marekani) Ratiba ya shows zinazofuatia ni kama ifuatavyo:
- Tarehe 31/8/2010 Washington,D.C
- Tarehe 7/8/2010 Boston,Massachusetts.
- Tarehe 13/8/2010 Dallas,Texas.
- Tarehe 19/8/2010 Kansas City,Missouri.
- Tarehe 20/8/2010 Witchita,Kansas.
- Tarehe 11/9/2010 Atlanta,Georgia.

Mpaka hivi sasa ratiba ndio hiyo. Lakini kuna shows zingine nyingi ambazo zinaweza kutokea kwa sababu Promoters kadhaa wameonyesha nia na kufanya majadiliano ya awali ingawa hatuja-confirm firm tarehe kamili za kufanya kazi. Pia naomba niweke wazi kwamba milango ipo wazi kwa promoters wengine ambao wanataka kubook shows.Wenye nia hiyo wanaweza kuwasiliana na Kitova kwa kutumia nambari ya simu +1 214 455 5082 au DJ Rich Maka kwa nambari +1 413 262 0400.Karibuni sana.
BC: Unawaambia nini mashabiki wako katika miji hiyo?Watarajie nini kutoka kwako?
PROF.JAY: Kama nilivyogusia hapo juu,mashabiki wategemee shows za kiwango cha juu kabisa ambayo hawajawahi kuiona kutoka kwa msanii yeyote kutoka kwenye ukanda wa Afrika Mashariki,kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ninachowaomba wajitokeze kwa wingi ili wasije wakayakosa yale niliyowaandalia.Pia nawaomba wapatapo habari hii wawaambie na wengine.
BC: Waswahili wanasema kutembea kwingi ni kuona mengi pia.Mpaka hivi sasa unaweza kusema umejifunza nini kutokana na ambacho umekiona nchini Marekani iwe ni kwa upande wa sanaa ya muziki au jamii kwa ujumla?
PROF.JAY: Kwanza kabisa nimejifunza professionalism. Huku watu wanaheshimu sana kazi zao. Muda wa kazi ni muda wa kazi. Pia muziki wa huku upo katika kiwango cha juu. Bila shaka na sisi tunahitaji marekebisho mengi sana ili nasi tuboreshe miziki yetu na kazi zetu za sanaa zifikie angalau robo tatu ya kiwango ambacho wenzetu wameshafikia.Nasema hivyo kwa sababu huku muziki ni kazi na ni ajira kubwa sana kwa vijana na hata wasio vijana.Inaheshimika kama kazi nyingine zingine zozote.

Kila anapofanya show,umati kumbi na viwanja huwa “vinatapika”.Hapo ilikuwa ndani ya CCM Kirumba-Mwanza.Can you do a count from this photo?
BC: Baada ya Tour yako nchini Marekani unatarajia kuelekea katika nchi nyingine kuendelea na tour au utarudi kwanza nyumbani kupumzika kidogo?
PROF.JAY: Baada ya kukamilisha hii tour,nitarudi nyumbani kwa mapumziko mafupi kisha nitaelekea Ulaya kwa tour nyingine.Mpaka sasa nimeshapata mwaliko kutoka nchi za Scandinavia(Sweden,Norway,Denmark na Finland).Pia nimepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza nchini Uingereza. Nitakaporudi nyumbani ndio nitajua wapi pa kuanzia.Mashabiki na wadau watajulishwa kuhusu tour hizo kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BongoCelebrity.
BC: Mbali na hiyo tour kuna shughuli nyingine unafanya huko Marekani?
PROF.JAY: Ni kweli kabisa.Mbali na tour pia narekodi miziki.Tumeshaongea na kampuni moja ya kutengeneza video ili tuweze kushoot video kadhaa huku huku.Pia nafanya mawasiliano na wanamuziki mbalimbali kutoka nchi nyingine duniani ili kubadlishana mawazo na pia kuangalia uwezekano wa kufanya kazi pamoja.
Mbali na yote hayo,kama unavyofahamu mimi ni Balozi wa MARALIA NO MORE.Wao pia wametumia nafasi hii kunialika New York yalipo makao yao makuu.Nitakuwa huko tarehe 28 na 29 July ili nikutane na staff wote kwa pamoja.Vyombo kadhaa vya habari vitakuwepo na hivyo bila shaka kutakuwa na media coverage.
BC: Kama Balozi wa Malaria No More,unaonaje kuhusiana na vita dhidi ya ugonjwa huo nchini kwetu? Utakuwa na ujumbe wowote maalumu utakapokutana na staff nzima ya Malaria No More?
PROF.JAY: Kwa kweli jitihada za kupambana na ugonjwa wa malaria zinakwenda vizuri.Kwa kutumia muziki,wananchi wengi wamepata nafasi ya kuelewa jinsi ugonjwa huo unavyoenea,mbinu za kupambana nao nk.
Nitakapokutana na staff wa Malaria No More,nitawaeleza zilipofikia jitihada zetu na jinsi tulivyofanikiwa kuwazindua watanzania kuhusiana na ugonjwa huu hatari ambao unaua mamilioni ya watanzania kila mwaka huku wengi wao wakiwa ni watoto chini ya miaka mitano(5) na akina mama wajawazito. Jitihada hizi zinaendelea kufanikiwa kutokana na mchango na support kubwa kutoka kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
BC: Je unatarajia kutoa albamu mpya mwaka huu? Kama sivyo,lini mashabiki wako watarajie album mpya?
PROF.JAY: Ni kweli,it’s about time.Hopefully ambo yote yakienda sawa mwakani mwanzoni nitatoa album mpya. Kwa hiyo mashabiki wangu vuteni subira kidogo. Kazi tumeshazi-record ila tunachozingatia ni lini muda muafaka wa kuzitoa.Nasubiri muongozo kutoka kwa Management yangu.
BC: Shukrani Prof.Tunakutakia kila la kheri katika American Tour yako.
PROF.JAY: Asanteni sana wakuu.
Feedback / Comments
20 Responses to “PROF.JAY ON HIS FIRST AMERICAN TOUR”
Leave a Reply


sending...
Kwakweli jamaa anajitahiidi na nyimbo zake zina mafundisho nimezipenda
Whats up Tanzaian?fine bongo music naukubali coz ujumbe unafika kwa fasta kwa wabongo but haukai muda mrefu unachuja,co kama zilipendwa za kina marijan,leswanyika hadi leo zikipigwa nyimbo zao zinakubalika hii yote coz wanalenga hali halis ya kibongo kwa ujumla,na lika zote wanagusa,then wanahenzi utamaduni wetu,kuliko sas tumemezwa kimaghalibi zaidi,thanks
nice interview!
Huyu bwana namkubali.Very intelligent chap.Naona sasa ameamua kutambaa duniani.Karibu US Prof.
BC,
Nice interview wazee.Prof.nipo Sweden na tunakusubiri kwa hamu huku.Big up mtu wangu.
i lovo your song prf. Jay
prf. Jay panga uje na huku Canada watanzania tunahamu ya live show.Fanya uje mtu wangu tunakusubiri.
E’bwana Jay nakuaminia usisahau kuja finland mazee…..Najua wabongo wanakizimia sana mtu wangu!!
Big up broda.
Nicely interviwed
Big up prof Jizo,keep it up, show zako ni za ukweli, I wish ze best in your tour
you a really heavyweight mc,keep it up but try to make this as you are profesional and a seriously business,when you decide to retire you will have something.lastly respect yourself and show those cowboys waTZ na sisi tuko juu kinoma,see me at masaki tell me nikusaide
Kuna wana TAS Uswiss. Wangeweza kukupokea na kuburudishwa na music wako
maisha muuigo.namuhusudu profesa,asema ya moyoni,na TUZINGATIE.MAISHA daima kuiga,kwa kwali kwa kweli jina lake sio profesa j,AMEIGA.sasa nini maisha tuuige,tufatlize.fujo yenyewe watu hawataki kuuiga mambo ya wa afrika(wabongo)..kila daima bongo si thamani,nusu bin nusu,mark(jina la kuuiga).tuuige.TUFANIKIWE.ombi langu ntaka huyu profesa aimbe kikabila yake.nijue kweli huyu profesa kweli,au sanamu.samahani.mie siwezi kuumba kama yeye nampaka mavi
we profesa.ondoa ukame bongo.sio kelele za sauti tuu
we ni nani mmasai,kafili,au mteja
bongo kuna njaa,wee profesa tuletee.maandazi,ugali na magharagwe.maana wamerikani matajiiri wala kuku na mayai
kaka endelea kukaza mpaka ufike level za kina jay z.
Good work keep up.
uko juu mala nyingi huwa hukosei keep it up