
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi(pichani) kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Brazil .
Uteuzi wa Balozi Malambugi umetokana na na kuteuliwa hivi karibuni kwa aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.
Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.
Feedback / Comments
4 Responses to “MALAMBUGI ATEULIWA KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI BRAZIL”
Leave a Reply


sending...
muheshiMalambugi, umeacha sifa yako nzuri hapa ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani, kwani ulikuwa mtete hasa wa wafanyakazi (local staff).na pia umetusaidia sana. kitendo cha mweshimiwa raisi kukutea ni cha kupewa hashima sana.tangu umeondoka hakuna linalofanyika hapa Berlin.
ni kweli, hayo yaliyoandikwa hapo juu, sasa ubalozi wa tz ujerumani hauna heshima hata kidogo, yaani ni kama dangulo,watu wanavuka hasa mipaka, heshima uliyoileta sasa imetoweka hasa
ni kweli, hayo yaliyoandikwa hapo juu, sasa ubalozi wa tz ujerumani hauna heshima hata kidogo, yaani ni kama dangulo,watu wanavuka hasa mipaka, heshima uliyoileta sasa imetoweka hasa
jamani Ngemera ataondoka lini, tumechoka