
Pichani ni Dr.Willbroad Peter Slaa akihutubia mamia ya wananchi waliokwenda kumsikiliza hivi karibuni mjini Arusha.
Hivi karibuni Dr.Slaa alitangazwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambacho kwa muda sasa amekitumikia kama Katibu wake Mkuu.
Tangu ilipotangazwa kwamba Dr.Slaa sio tena candidate wa Ubunge bali Urais,kumekuwa na maoni tofauti tofauti.Kuna ambao wanasema Dr.Slaa asingethubutu kugombea Urais na badala yake angeendelea tu kugombea kiti chake cha Ubunge wa Karatu kwani nafasi ya kumshinda mgombea wa Chama Cha Mapinduzi-Jakaya Mrisho Kikwete ni ndogo sana.
Wanaounga mkono hoja hiyo wanasema,kwa sababu uwezekano wa Dr.Slaa kumshinda Kikwete ni mdogo,hiyo ina maana kule Bungeni kutakuwa kumepungukiwa na mbunge makini na ambaye kwa muda wa miaka mitano iliyopita,aliwapa tabu na challenge kubwa,wabunge na viongozi wa chama tawala cha CCM.
Kwa upande mwingine,wale wanaounga mkono uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Dr.Slaa katika kuwania Urais,wanasema ni kitu kizuri kwa ukuaji wa demokrasia na wanaamini kwamba Dr.Slaa atamshinda Jakaya Mrisho Kikwete na kwa maana hiyo he will become our next President.
Tungependa kupata maoni yako.Je,unakubaliana na wale wa kundi la kwanza au la pili? Will Dr.Slaa become our next President?
BC iliwahi kufanya naye mahojiano ya kina na Dr.Slaa.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.
Feedback / Comments
103 Responses to “DR.SLAA:THE NEXT PRESIDENT?”
Leave a Reply


sending...
Mimi nakubaliana na wale wa kundi la pili.
Kwanza tuelewe kuwa Dr hakuzaliwa kama mbunge bali ni kwa kujifunza na uelewa wake ndio maana amekuwa mbunge makini.Wapo watakaoziba pengo lake.
Pili, hii ramli ya kushindwa na kikwete ni maruwe ruwe ya wapunga pepo. Mbona Oboma alimbwaga Hillary Clinton licha ya umaarufu na mtandao wa Bill. Katika 2008 wagombea wote wa democrat walikuwa senior senators na walishagombea, nani alijua someone unpopular and unknown can make the miracle.
Tatu, lengo si slaa kuwa rais tu, hata kama hilo halitatokea, ninaa imani kwa kishindo chake Chadema itaingiza ”Slaa” wengi zaidi mjengoni. Hapa ni sawa na kuuza dhahabu ili upate pesa za kumiliki mgodi.
Mwisho[last],wale wanaosema Dr asigombee watueleze nani agombee, maana demokrasi inayokua haiwezi ruhusu ” eti apite bila kupingwa” who is he!!! kwa madudu ya miaka 5,pamoja na yale ya 15 kama waziri, aachiwe tu! na kuwaficha wezi na mabazazi marafiki,apite tu! lazima tupate jukwaa la kumwambia ”huwezi kazi,stay aside with friends fisadi”
Japokuwa ana rekodi nzuri, lakini ni mapema mno kuweza kumwamini kwa nafasi nyeti kama uraisi wa nchi. Ningekuwa mshauri wake, ningemshauri agombee tena ubunge katika jimbo la Karatu na aendelee kuutumia ubunge kujijenga zaidi kisiasa. Isitoshe anapaswa pia kushirikiana na viongozi wenzake wa Chadema, kuimarisha chama ili kienee sehemu zote za nchi na kiwe na nguvu. Kwa sasa chama bado kina wafuasi wachache katika sehemu nyingi za nchi. Kipimo cha kuanzia ni uchaguzi wa madiwani mwaka huu. Kimetoa madiwani wangapi na katika mikoa gani ya nchi? Je ukiondoa baadhi ya wilaya katika mikoa ya Kilimanajoro, Arusha, Kigoma na Mara kina wabunge katika mkoa gani mwingine wa nchi. Kina ofisi za maana katika mikoa ipi? Mambo hayo ni mhimu kuyatizama. Angeonesha mfano kwanza katika kukijenga chama kikubalike na kuwa na wafuasi wengi nchini kote. Kuwa na wafuasi katika baadhi ya sehemu za nchi kunatia wasiwasi juu ya utaifa na umoja wa chama jambo ambalo ni la msingi sana katika kuchagua raisi.
Bado hana vigezo vya kuwa rais namshauri akagombee ubunge bado hajachelewa maana huko alikojitumbukiza kaenda kupotea kabisa mimi nasikitika kumkosa bungeni muda ujao
Dr Slaa ndiye kiongozi makini anayeifaa Tanzania yetu kwa sasa.Ni mtu serious katika issues mbalimbali na anazisimamia ipasavyo. Tumechoshwa na siasa za ubabaishaji za ccm. Miaka zaidi ya 50 madarakani nchi badala ya kusonga mbele ndio inazidi kurudi nyuma. Wemekaa kulingia rekodi zisizo na kichwa wala miguu.
Suala lisiwe kuchoshwa tu na CCM na kuamua kwa jazba. Uchaguzi wa Raisi ni jambo nyeti sana katika mustakbari wa nchi. Kosa dogo linaweza kutucost kwa miaka mingi.
Nakubali kwamba katika kipindi chake cha ubunge hasa katika miaka mitano iliyopita. mdomo wake na kichwa chake kilitoa mchango mkubwa katika kukosoa serikali. Na hiyo ndiyo kazi kubwa ya upinzania. Ni ukweli pia kwamba kazi hiyo aliifanya pamoja na wabunge wengine wa CCM ambao walikuwa na mtizamo kama yeye. Ni bila shaka siri ya mengi aliyoyalipua ilitoka ndani ya Serikali kutokana na hitilafu zilizojitokeza baada ya uchaguzi mkuu.
Hatuwezi kusema mheshimiwa Kikwete ni safi sana. Kwani kama maraisi waliyomtangulia ana mapungufu yake. Pia ana mazuri mengi aliyoyafanya. Lakini kumuhusisha Kikwete na ufisaji bila shaka ni kumuonea. Ufisadi mwingi uliyojitokeza bungeni ulitokea toka enzi za Mkapa. Mzee Kikwete katika utawala wake ameonesha wazi kuchukia ufisadi kwa vitendo. Tumeona mawaziri wastaafu wenye majina makubwa wakiburuzwa mahakamani bila woga. Tumeona Sheria ya Kuzuia Rushwa ikifanyiwa marekebisho makubwa kuwabana mafisadi. Tumeona Sheria ya Ghalama za Uchaguzi ikitungwa kudhibiti rushwa katika siasa. Tumeona kikosi cha kuzuia na kupambana na rushwa kikiimarishwa.
Japo mapungufu yamejitokeza katika utekelezaji wa Sheria ya Garama za Uchaguzi, nia na dhamila ya serikali inabaki kuwa nzuri. Mapungufu yaliyojitokeza ni changamoto. Sheria itabidi ibadilishwa baadae kuadress hizo changamoto.
Katika uwanja wa siasa Mheshimiwa Kikwete amefaulu sana katika kuimarisha amani na umoja wa kitaifa na kuondoa mgawanyiko Zbar ambao ulichafua hali ya siasa. Amekuwa mvumilivu kwa vyama pinzani kuliko waliomtangulia.
Katika elimu pia kuna mafanikio makubwa sana katika elimu ya msingi, sekondari na chuo kikuu. Mbali ya kuongezeka vyuo vya binafsi vyuo vya serikali pia vimeongezeka bila kusahau chuo kikuu cha Dodoma.
Yapo mapungufu katika uwanja wa siasa ambayo hata yeye mwenyewe anayakubali. Lakini misingi mizuri imewekwa.
Kwa hiyo raisi hajashindwa kiasi cha kutufanya tukurupike
Anatafuta kukolimbuwa kaishavunjika mkono
Mambo ya kukolimbwa kwa maoni yangu hayapo. Kuvunjika mkono ni ajali ya kawaida. Bafuni alikuwa peke yake hadi alipowaita mwenyewe wenzake waje kumsaidia. Kwa mtu wa umri wake siyo ajabu kuteleza na kupata madhara mabubwa kama hayo. Kwa hilo tumuombee Mungu apone haraka.
Jambo moja ningependa kuzungumzia. Slaa amakuwa mbunge kwa muda mfululizo wa miaka kumi na tano. Naamini si mgeni sana katika siasa. Ajabu ni kwamba ameanza kampeni kabla ya muda. Juzi nilikuwepo katika mkutano wake wa hadhara viwanja vya Jangwani.Kilichotokea katika mkutano huo hakiwezi kuwa na tafsiri nyingine zaidi ya kampeni za uraisi. Wengine wanasema hata Kigoma, Arusha, Mwanza na Mtwara alifanya hinvyo hinvyo.
Kwa hilo nimeshindwa kuelewa lengo lake. Siamini kama amejisahahu au amelewa sifa za wapambe wake akaamua kuanza kampeni kabla ya muda. Kwa lugha nyingine amecheza rafu ambayo hata akipewa kadi nyekundu hawezi kulaumu. Inatia shaka kama kweli alikuwa ameshaamua kuacha ubunge na kugombea uraisi. Ndiyo maana kwenye kampeni yake juzi alisema rasmi kwamba “sasa nimekubali kugombea”. Inaonyesha kabla ya hapo alikuwa anatest zali ili baadae arudi katika nafasi yake ya ubunge. Akipewa
Dr. Slaa anafaa sana kuwa raisi, ni wakati sahihi wa yeye kugombea nafasi hiyo, ccm ni uzushi mtupu, madaraka wanapeana kimtandao, kama wewe si mwana mtandao lazima ung’ooke, nilikipenda sana chama hichi, nilikitetea kwa moyo, kumbe ni wababaishaji watupu. Watanzania haswa wafanyakazi wenzangu tuliumizwa sana na kauli ya raisi aliyoitoa kuhusu wafanyakazi, alipaswa kutumia lugha nzuri na tungemuelewa. Natumaini wafanyakazi hamtamwangusha dr.slaa.
Nimemsikiliza sana katika hotuba zake alizozitoa katika mikoa mitano tofauti. Mbali ya kukosoa CCM kwa mambo ya ufisadi sijaona mkakati wowote aliouandaa kuondoa ufisadi na kuiendeleza nchi. Kukosoa ni kitu raisi sana. Leo hii ukinipa ishirini kuikosoa Serikali iliyopo madarakani nitayatumia yote na kuomba masaa mengine ya ziada. Lakini ukinipa nusu saa niongee nitakayo yafanya kama nitapewa serikali naweza kutumia dakika kumi na tano baada ya hapo nikaanza kurudia ama kusisitiza niliyo yasema mwanzo. Ninachomaanisha hapa ni kwamba huwezi kuupata uboro wa kiongozi kwa kigezo cha kukosoa.
Mtu kama Mtikila kwa mfano angekuwa moja katika ya wabunge wa upinzani wa bunge lililopita naamini angekuwa hodari na maarufu kuliko Slaa. Maana, yeye anaufundi na umahiri mkubwa katika kukosoa. Vipi Mrema wakati anajiunga na upinzani? Alikuwa maarufu sana kwa kukosoa. Watanzania tusiwe wepesi wa kumuamini Slaa kwa kuwa anajua kukosoa serikaali iliyopo madarakani. Kwa maoni yangu mtu anayejua kukosoa sana anafaa kuwa mpinzani kuliko kuwa madarakani. Mtu anayefaa kupewa uraisi siyo bingwa wa kukosoa bali bingwa wa kupanga mikakati ya kujenga nchi.
Suala la wafanyakazi nasikitika linachukuliwa kisiasa kuliko ukweli wa mambo. Vyama vya wafanyakazi siyo vyama vya kisiasa na havipaswi kucheza kisiasa. Kauli ya raisi, kwa mtizamo wangu haikuwa na tasfiri kama hiyo. Tatizo lilikuwa ni uchaguzi wa maneno na wala siyo kuwa mbali na wafanyaakazi. Raisi alikuwa anasisitiza kwamba serikali yake haikuwa na uwezo wa kutekeleza matakwa ya wafanyakazi kama yalivyo. Lakini mwisho wa siku alitekeleza aliyoyaweza. Ndio maana mgomo haukufanyika. Siyo kwamba wafanyakazi tulimuogopa raisi bali tulikubaliana na kidogo alichotoa kwa kuzingatia ukweli wa mambo. Sioni jambo lolote la ajabu raisi alilolifanya ukilinganishwa na waliomtangulia mpaka atafsiriwe kama adui wa wafanyakazi.
Kuhusu mizengwe ndani ya chama ni tatizo lipo. Lakini hatua zinachukuliwa kulirekebisha. Kupitishwa Sheria ya Garama za Uchaguzi ilikuwa ni moja ya mikakati ya kuadress tatizo hilo. Dada Dora huna haja ya kukataa tamaa
ki ukweli sion haja hata kidogo ya kuiacha ccm madarakani hawana jipya la kutueleza silaa ni makini san katika mbio hizi za urais tutajuta kumchagua kikwete na mafisadi kwa mara ya pili hana lolote yeye na mafisadi wenzake anasema miaka mitano ilikua ya majaribio hiyo mitano mingine ijayo ci itakua balaaa tuna mpa rais mwenye kujiamin anaejua anafanya nini c huyu bazazi
Kama suala ni CCM, hoja iwe ni kwa namna gani CHADEMA ni makini kuliko au kulingana na CCM. Haihitaji utafiti kuhitimisha kwamba CHADEMA haina umakini wowote. Ingekuwa makini kwa kipindi chote cha miaka kumi na saba ya uhai wake ingekuwa imeshasambaa Tanzania nzima. Kwa hivi sasa CHADEMA ipo Kilimanjaro, Arusha, Kigoma na Manyara. Tanzania inamikoa na wilaya chungu zima. Ni nini inaifanya CHADEMA isijipenyeze na kujiimarisha maeneo yote haya. Chama hakina wabunge wa kuchaguliwa hata zaidi sita nchini lakini kimeshaanza mivutano mikubwa na kuunda makundi miongoni mwa vigogo. Kikizeeka kama CCM itakuwaje?
Bado nasisitiza kwamba DR SLAA na chama chake bado hawajakomaa kuweza kukabidhiwa dola ya viumbe zaidi ya milioni 30. Uongozi na uwezo wa kuzungumza ni vitu tofauti. Uongozi ni timu siyo mtu mmoja. SLAA mwenywe anaweza kuwa na uzuri wake lakini hajakuwa na timu ya kitaifa ya kuweza kuchukuwa dhamana kubwa kama hiyo. Ushauri wangu wa bure kwa CHADEMA ni kwamba nyumba huanza kujengwa kwa msingi. Huwezi kuanza kupauwa kabla hujaweka msingi. Nyumba itakosa hata pa kuangukia. CHADEMA (na vyama vingine vya upinzani) tumieni nguvu, akili na fedha nyini katika kujenga misingi imara ambayo itawapa ubavu wa kuchukua dola. Msiwe na haraka ya kuwa na dola bila ya kuwa na nchi. Ndio maana vyama vingi vya upinzani hawiendelei nchini. Helcopta mnatumia wakati wa kutafuta uraisi badala ya fedha hizo kuzitumia kujenga chama. Kuna mikoa kama Rukwa, Kigoma, Mara, Mbeya na Manyara. Kama CHADEMA wangekuwa makini wangekuwa waneshajihakikishia wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani na wabunge wengi sana na kukiimarisha chama. Wangweka mikakati pia katika mikoa mingine. Lakini kuvizia tu kipindi cha uchaguzi huwezi kujenga chama. CCM itatawala muda mrefu labda wagawanyike wenyewe na kuanzisha chama kingine. Wapinzania watakuwa sawa na fisi mwenye njaa aliyekaa chini akisubiri binaadamu aliangani akatike mkono apate msosi.
Watanzania Ni wagumu Sana Kuelewa Na wepesi Kusahau. Ndugu Zangu CCM Imezeeka HAINA DIRA WALA MWELEKEO. Maneno hayo alisema katibu Mkuu wao mwenyewe ambaye walimwamini na kumpenda Hata kufikia hatua ya kutungiwa wimbo wa kuwa ASIYEMPENDA HORACE KOLIMBA SIO RAIA WA TANZANIA.Kuona ukweli unawekwa hadharani wakamuua. Leo Hii miaka 10 na kitu baadaye mtu na akili zako timamu bado unaendelea kukishabikia kwa HOJA ETI kina misingi, misingi ipi zaidi ya misingi ya kulindana katika kutuibia? Inawezekana vip mtu mwenye kesi ya ubadhirifu wa mali ya umma anaenda kugombea ubunge? Ingekua china angekuwa wapi mtu huyo? Mtu ambaye ana kesi za namna hiyo au hata ana harufu tu ya rushwa hafai hata kusogelea ofisi za nchi hii hadi atuthibitishie kuwa ni safi. Leo hii anasafishwa aliyesema bilion 2 ni vijisent na bado tunasema chama kina misingi na ndo kinachofaa kutuongoza. Mimi hainiingia akilin hata kidogo. Ndo maana Nchi za Ulaya zinatuona kuwa akili zetu sote c timamu na kuja kwa wingi kuendelea kununua migodi yetu kwa bei sawa na bure. POLENI SANA WATANZANIA TENA POLENI SANA MNAOSEMA CHADEMA HAKIKUWA SAWA KUMPELEKA SLAA KUGOMBEA URAISI.Aibu hii iwe nanyi uson kwenu hadi mwisho wa maisha yenu
Bwana Frisk anaweza kutuona hatuna akili, ni uhuru wake wakueleza yaliyo kufuani mwake. Lakini hilo haliufuti ukweli kwamba CHADEMA haijafanya lolote kutufanya tuamini kwamba itafanya mazuri kuliko CCM. Uamuzi wa kumpa mtu au chama dola haupaswi kusukumwa na jazba. Yawezekana kwamba yapo mengi mabaya CCM imeyafanya tuna uhakika gani kwamba huyo Slaa hawezi kufanya mabaya zaidi. Kuna nini la maana CHADEMA na SLAA wamelifanya kutushawishi tuwaone kama ndio suluhisho la matatizo yetu?
Katika maoni yangu nimekuwa nikizingatia mambo mengi na kubwa zaidi ikiwa umoja na usalama wa taifa. Nimekuwa nikisisitiza na sijapingwa na mchangiaji yeyote, kwamba CHADEMA hakijaonesha sura ya kitaifa licha ya kuwepo kwa zaidi ya miaka kumi na tano. CCM licha ya matatizo yote kilichonayo imethibitika kuwa ya kitaifa. Suala hilo limesaidia katika kuimarisha amani na umoja wa kitaifa. CHADEMA na vyama vingine wanahitaji kujipenyeza na kujiimarisha katika sehemu zote za nchi ili kionekane kuwa chama cha kitaifa. Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakitizama chama cha CHADEMA katika sura ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha, kwanini wasiondoe hiyo dhana kwanza kwa kujiimarisha nchi nzima?
Watanzania tunapaswa kulitizama suala la uchaguzi katika jicho la upevu. Mchangiaji anamzungumzia SLAA wakati kuna viongozi wengine zaidi ya wanne nje ya CCM wanaogombea uraisi. Kwa nini Slaa? Ili kuboresha mjadala na kuwasaidia watu kupata picha kamili angetuonesha ni mikakati gani ya maana SLAA na CHADEMA yake aliyoweka ili kufanya vizuri zaidi ya CCM.
Ningewaomba wachangiaji tujadili kwa lengo la kuelimishna na kujenga na kwa maslahi ya taifa. Na pia ningewaomba tuvumiliane kwa kutumia lugha isiyoweza kuamsha hisia mbaya.
Binaadamu tunatofautiana kimtizamo na maono. Yawezekana ikawa kuna sehemu kutokana na upeo wangu wa ufahamu na taarifa nilizo nazo nikawa nimekosea. Lakini ningefurahi sana kama ungeonesha kosa langu na kunipa hoja unayodhani kuwa sahihi. Maneno kama “mtu mwenye akili timamu…” hawezi kuona DR SLAA hafai yanakatisha tamaa. Hamna aibu yoyote katika kutoa maoni unayoyaamini kuwa ni sahihi hata kama Ulaya na Marekani watakushangaa.
Kumbuka kwamba siyo wapiga kura wote wana elimu na ufahamu mkubwa kama wewe katika uchambuzi wa mambo ya siasa. Kuwalaumu tu na kuwapa pole bila kueleza mazuri na mikakati ya CHADEMA hakuondoa “ujinga” wao na nia yao unayoidhani kuwa siyo sahihi ya kuichagua CCM
Watu huogopa sana mabadiliko kwa sababu hata ambazo si za msingi, mifano iliyopo ya chuki thidi ya ufisadi haikidhi sifa ya chuki kwa ufisadi… Mangapi yanapita kiaina ambapo kila mwenye akili timamu atashangaa tunafanya nini watanzania … Usanii??? tena kwenye mambo yanayolitafuna taifa…. Guys, let spade be spade tusirembe mambo kama hayarembeki….
Kwani Mheshimiwa alichakuliwa kwa CV ipi tukuka? au ni nyota ndo zatuongoza? Angalieni vitendo vinavyotawala maisha ya mtu ili kuona mfano wa yale ayaelezayo na angalau kuuhisi ukweli kupitia historia ya mtu….
Mabadiliko yapo ili kuleta changamoto za maendeleo. Badiliko likileta shida linatolewa ili kuleta sura muafaka kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu. Lakini hili nalo litalindwa vema iwapo katiba yetu itaundwa upya kuweka maangalizo ya sehemu za kupenyea iwapo tunafanya uchaguzi wenye makosa.
Hivi sacrifice aliyoifanya Slaa ina mfano hapa nchini… Toka fununu za money loundery BOT??
Tuwe wepesi wa kuona….
Inashangaza sana kama bado watanzania wanazidi kuikumbatia C.C.M, kama watu wenye ufahamu bado wanamuunga mkono Kikwete pamoja ana ahadi zake za uongo kila siku, maisha bora kwa kila Mtanzania imekuwa ni wimbo mzuri kuusikiliza lakini matokeo yake yamekuwa ni kinyume kabisa, angalia hali ilivyokuwa mbaya, barabarani foleni za kukatisha tamaa, hospitali huduma mbovu, tra,trc, kama kuna mtu alisikiliza hotuba ya Dr slaa siku ya ufunguzi wa kampeni zake, then alimsikiliza alivyokuwa akitoa hoja nzito bungeni then bado anasupport CCM lazima atakuwa anafaidika na matunda ya ufisadi, but hata kama unaona unafaidika ujue ni kwa muda tu lakini in long run kila mtu anaumizwa na uongozi mbaya sana wa kifisadi under CCM, nafikiri Watanzania tumerogwa, inatia hasira sana kuona watu wanatetea ufisadi wazi wazi, Mabavu ya CCM yana mwisho, hebu fikiria watu walivyochoka na kuamua kuwapiga waandishi wa TBC waliokatisha hotuba ya Dr slaa alipokuwa akifungua kampeni, CCM hawataki Watanzania wajue ukweli, Kikao cha CCM cha kumteua kikwete CCM wametumia TBC kwa masaa zaidi 7 kila siku kwa siku nzima lakini Dr Slaa anapewa dakika chache ili Watanzania wasijue mabaya ya CCM, ppo open ur mind, CCM inaiangamiza nchi.
Nionavyo mimi suala siyo mabadiliko bali ni uwezo wa kuleta hayo mabadiliko. Ilani za vyama vyote vya upinzani ni kupiga vita ufisati na kuleta katiba mpya. Mimi nimewasikiliza wagombea wote wa uraisi ambao wameshazindua kampeni zao. Sikumsikiliza Slaa peke yake. Alichozungumza Slaa na Professor Lipumba tofauti ni staili ya kuongea na kutia msisitizo. Wote wanazungumza kitu kimoja. Pia ukiondoa msisitizo katika kupambana na ufisadi sijaona kitu kipya katika vipaumbele vya wapinzani zaidi ya uchaguzi wa maneno. Huyu anasema “kilimo kwanza” huyu ansema “kilimo bora”. Kiutekelezaji maneno “kilimo bora” hayawezi kumzuia mtu asikifanye kilimo kuwa kwanza wala kinyume chake.
Uwezo wa kuongea na utekelezaji kwa maoni yangu ni vitu viwili tofauti. Mtu anaweza kuwa jasiri sana wa kukosoa na kulipua mabomu ya udhaifu wa serikali lakini akawa mbovu sana katika uongozi. Mwanzo wa upinzania tulikuwa na waongeaji na wakosoaji wazuri tu wa serikali. Tulikuwa na mheshimiwa Mrema ambaye alijitoa mhanga kwa kukubali kupoteza uwaziri na kupasua mabomu ya udhaifu wa serikali. Kama alivyo Slaa, alizungukwa na wanasheria mahili akiwemo mheshimiwa Marando huyuhuyu. Walikuwepo akina profesa Malima ambao walitoa mhanga uwaziri na kuingia upinzani kupasua mabomu ya udhaifu wa serikali ya CCM. Wapo pia wengine waliyokuwa na umahiri mkubwa wa kujenga hoja na kuivua nguo serikali katika majukwaa ya kisiasa kwa ushawishi mkubwa lakini baada ya arubaini walirudi CCM wakafyata mkia. Bahati nzuri watanzania hatukuwa na haraka kuwapa dola kabla ya kujipa muda wa kujiridhisha na uwezo wao.
Kama alivyo DR SLAA na vyama vingine vya ubinzania, mashujaa waliyomtangulia walishindwa kujenga vyama vyenye sura ya kitaifa na hivyo wananchi wakawa radhi kuendelea na serikali ya chama tawala licha ya mapungufu yake. Mashujaa hao wa zamani historia inaweza kuwasamehe kutokana na uchanga wa demokrasia ya vyama vingi. Hivi leo upinzania karibu unafikia umri wa kuowa bado tunarudia yale yale. Namaanisha kwamba DR SLAA na chama chake ameshindwa ama hajafanikiwa kukipa chama sura ya kitaifa. Hilo limejidhihirisha kwa kushindwa hata kuweka wagombea wa ubunge kwa kiwango cha asilimia 50% ukiacha wenyeviti wa serikali za mitaa na madiwani ambayo idadi ni ya chini zaidi.
Watanzania tumpe nafasi DK SLAA ya kujenga chama kiwe katika hadhi ya kitaifa kabla hatujathubutu kumpa uraisi.
Wachangiaji wenzangu wanazungumzia foleni barabarani. Hilo ni tatizo linalowakabili section ndogo sana ya watanzania wanaoishi sehemu chache sana za nchi. Tatizo hilo pia ni tatizo la kipindi cha mpito. Tunajua kwamba kutoka na kuingia kwa mfumo wa soko huria kumekuwa na mafuliko ya watu kuingiza bidhaa, ikiwemo magari toka nje. Mafuliko haya ni matokeo ya mabadiliko na ni kitu kigeni kwetu. Kipindi cha mfumo wa soko la umma magari nchini yalikuwa yanahesabika. Japo barabara zilikuwa mbaya sana lakini hapakuwa na foleni ya magari. Pengine kwa mtizamo wa wachaniaji wenzangu hayo yanaweza kuchukuliwa kama maendeleo ya mfumo wa ujamaa. Hivi sasa kuna foleni ya magari yanayotoka na kuingia mijini kutoka vijini. Wakati wa mfumo wa umma magari ya abiria na mengine nchini zima yalikuwa yanahesabika. Barabara zilikuwa za kuegesha kiasi kwamba kutoka Dar hadi Musoma ungesafiri kwa wiki nzima wakati sasa unasafiri kwa masaa. Hayo ni madhaifu ya serikali ya CCM. Vyakula villikuwa vinaoza Sumbawanga wakati mkoa jilani wa Tabora watu wanakufa na njaa. Kwa sasa ndani ya siku mbili chakula kinatoka Sumbawanga hadi Mtwara. Hayo yote ni mapungufu ya serikali ya CCM. Mambo yote haya yamefanyika katika kipindi ambacho vyama vya upinzani vilishazaliwa.
George na watanzania wengine kama ulivyo wewe naomba muelewe kuwa kuna WATANZANIA wengi wanaoishi ktk maisha magumu tena yasiyoelezeka,na waliyochoshwa na uongozi wa chama cha CCM nami nawaunga mkono kuwa mabadiliko hayaletwi kwa maneno mengi ya uongo na ubadhirifu /ufisadi wa nchi huku tukikandamizwa kwa sera mbovu tena zisizofaa.
NAWAOMBA WATANZANIA TUFUMBUKE MACHO TUANGALIE WAPI TUNAENDA, TUCHAGUE KIONGOZI MAKINI ASIYE NA SHAKA,TENA ALIYE JITOA KWA MAISHA YA MASIKINI WA TANZANIA. ni kweli DR.SLAA sasa ni wakati wake wa kupewa nafasi ya kuongoza nchi, watanzania tumechoshwa na ufisadi wa serikali yetu,tubadilike tuchague viongozi wanaopenda maendeleo ya nchi na siyo hawa wanaojilimbikizia mali ya nchi na kuacha wananchi wakinyanyasika na kufa kutokana na hali ngumu ya maisha tuliyo nayo.
kwa ukweli mimi sioni haja ya kuwapa mafisadi nchi waendelee kuimaliza-angakieni karibia kila siku wanasafiri na kufanya mabo meengi ili kujinufaisha wao wenyewe eti maisha bora kwa kila mtanzania wakati mtoto na mke wa masikini wanakufa kila leo kwa kukosa matibabu,elimu na huduma muhimu kama za kujifungua, ukitaka kupona basi uwe na uwezo wa kwenda hospitali za private au basi Mungu ndo akunusuru.
Rushwa imetawala kila sekta sasa wanatufumba macho kwa kipindi hiki maalum cha kuchagua viongozi, basi ngoja wapewe nchi uone itakavyo kuwa kimnya, eti TUMEFANYA MENGI MAZURI,na SASA TUTAJENGA BARABARA JUU YA BARABARA wapi jamani acheni kutufanya wote wendawazimu.
WATANZANIA WOTE TUBADILIKE/ TUWE WEPESI WA KUELEWA NA KUONA PIA.TUMCHAGUE DR.SLAA ANAFAA KUWA KIONGOZI ni msomi na ni mtu makini sana.
Ndugu yangu Kimaro najua sana kwamba kuna watanzania wenzangu wanaoishi maisha ya tabu na wamekuwepo wengi zaidi ya hao katika kipindi cha nyuma. Ninafahamu pia kwamba Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi za kiafrika ni maskini. Lakini kama tutafanya tathimini kwa uaminifu bila kuegemea upande wowote tunaona wazi kwamba serikali iliyopo madarakani imefanya mengi mazuri tofauti na wapinzani wanavyotaka ionekane mbele ya watu. Mtu yeyote mkweli hawezi kuilaumu serikali kwamba imeshindwa kujenga barabara au kuboresha miundo mbinu. Serikali kwa kipindi kifupi sana imefanya mapinduzi makubwa katika sector ya usafiri kiasi kwamba asilimia kubwa ya nchi imeunganishwa kwa barabara ya kiwango cha lami. Serikali imefanya makubwa zaidi katika sekita ya elimu. Mwanzani elimu ya sekondari ilipatikana kwa watu wachache walikuwa mijini na kanda zilizopendelewa na mkoloni kwa sababu za kihistoria. Mkoa ninakotoka mimi kwa mfano, hadi mwaka 1991, ikiwa ni miaka 30 toka uhuru tulikuwa na sekondari za serikali tatu na za binafsi zisizozidi tatu. Kwa sasa kila kata kuna japokuwa shule moja ya sekondari ya serikali ambapo watoto wa wakulima wenzangu wanasoma. Tulikuwa na vyuo vikuu vya viwili lakini sasa tunavyo zaidi ya 30 na vya serikali peke yake vikizidi kumi. Kasi hiyo kubwa ya maendeleo haiwezi kubezwa.
Maeneo ya vijiji hali ya maisha pia imebadilika ukilinganisha na mwanzo. Elimu imesogezwa zaidi kwao pamoja na huduma ya maji. Kilimo pia kimeboreshwa kwa wakulima kusambaziwa mbolea na mbegu. Bei ya mazao na upatikanaji wa masoko ya karibu vimeboreshwa sana kuliko ilivyokuwa nyuma. Mtoto wa kijijini wa miaka ya tisini ni tofauti sana na wasasa. Mkulima wa leo ni tofauti sana na mkulima wa zamani. Katika wilaya yangu nimeshuhudia vijana wengi wadogowakitajilika kutokana na shughuli za kilimo jambo ambalo zamani halikuwepo. Serikali kwa sera yake ya kilimo kwanza imeshaanza kuweka mikakati inayoonekana ya kuboresha kilimo kwa kuanzia na matrekta ya kukokota na mikono. Ni mwanzo mzuri japo ndugu zangu akina Kimaro wanaubeza.
Pamoja na yote niliyoyasema nakubali kwamba yapo mapungufu katika serikali ya CCM. Hoja yangu ni kwamba bwana KIMARO pamoja na ndugu zangu wengine walio katika kambi yake ya kimawazo wanavigezo gani vya kuonesha kwamba DR SLAA na chama chake wanauwezo wa kufanya mazuri kama ya CCM au zaidi yake? Kama suala ni kutaka chama cha upinzani kwa nini siyo LIPUMBA wa CUF au Rungu wa NSSR MAGEUZI? Kama tatizo ni CCM Rungu na Lipumba hawana mizizi sana ya CCM kama DR SLAA ambae alikuwa moja wa vingunge wa CCM kabla hajaingia CHADEMA. Kuna mapungufu mengi ya msingi ambayo nimekuwa nikiyabainisha kuonesha kwamba DR SLAA hana maandalizi ya kuwa raisi. Ndugu yangu Kimaro hajayazungumzia wala hajatoa hoja mbadala ya kuonesha uwezo na umakini wa SLAA na chama chake.
Watanzania hatuwezi kuchagua raisi kwa kubahatisha kwamba pengine atakuwa mzuri kuliko raisi aliyepo.
Urais ni ofisi sio mtu.(hata Dr Slaa anafaa saaaana kwani hamna chama kilichosomea uraisi)Mategemeo ya watanzania wote ni kuona rasilimali za nchi zinatumika kwa wote sio mtu mmoja na marafiki zake. Mungu alitupa rasilimali nyingi na nchi yetu sote tunajua kuwa ni tajiri kuliko nchi nyingi duniani lakini umasikini wetu umekuwa ndani ya vichwa vyetu.Tunahitaji mkombozi ambaye atatuletea maendeleo na keki yetu tukagawana wote kwa usawa hataka haitakuwa nusu kwa nusu lakini angalao japo kiduchu.
CCM tumewapa nchi miaka 50 umri wa mtu mzima na wameomba ridhaa mara kadhaa sasa ifike mahali tujaribu na wengine tuwe kama wajapani walivyoamua kuwatosa chama tawala pamoja na kwamba kilikuwa kinafanya mengi na maendeleo yao yakapaa, lakini wakasema basi tuwape na vyama vingine.
Mazuri mliyoyafanya ndiyo tuliyoyataka kwani mlituomba mtutumikie sio tuwatumikie. Kufanya vema ni wajibu na ni sahihi kabisa hatukuwapa nchi iwe jangwa la sahara na mabaya mliyoyafanya mmetukosea sana mlitakiwa tuwawajibishe kwa kuwapa chungu chetu (BOT) mkadokoa nyama zote sasa umebaki ugali.Serikali ya ccm isijitape kwa lolote lile, ile ilikuwa ni wajibu na mtu akitimiza wajibu wake ni vyema na ilikuwa ni lazima utimize na zaidi ya hapo, sio kuhemea maana sisi sio masikini.(Baba ulienda kuhemea na watu zaidi ya 50 na mabilioni mliotumia kuhemea mengine hayatalipika maana mlimalizia njiani mkafikisha robo. vita yenu ya malaria ni ya kusadikika sio halisi, msitugeuze kuwa dampo la vyandarua feki.
ccm hamna sababu ya kujidai. Je mnajili-nganisha na nani kwani mmepora kila kitu mmetuuzia kwenye nchi yetu wenyewe huku tukiwapa ridhaa ya kutuongoza nyie mkatutawala mtajibu siku ya mwisho na wanyang’anyi wote ndio wako ccm na ndio wanaogombea ubunge na udiwani je mnatuelezaje wananchi katika hili!!!!!!! je hamuoi haya??????????????? IMETOSHA IMETOSHA LAZIMA MABADILIKO HAKUNA ALIYEZALIWA NA URAIS AU UBUNGE nchi ni yetu wote bila kujali vyama. (kwa nini ccm wanaogopa mgombea binafsi???) jibu kama wanaume hahahaha.
Kazi yenu imekwisha sasa subirini tuwape wengine ili na nyinyi mjifunze mazuri ya wenzenu ili mpate pa kukosolea. Jamani nchi imenunuliwa na ccm miaka 50 tutajifunza nini kutoka kwa wapinzani? wapeni tuwaone wakitushinda baada ya miaka 5 tunawatupilia mbali. Nyinyi ccm mlikuwa na kila kitu lakini mmeshindwa kuongoza waachieni na wengine hakuna katiba iliyoandikwa kuwa rais lazima atimize miaka 10 hakuna tumewachoka na sera zenu zilezile hazitupeleki kwenye nchi ya asali na maziwa. JE RAIS WETU BAADA YA MIAKA 5 UKIMALIZA TUTAMUULIZA NANI KAMA HUKUTEKELEZA UHAYOYAHAIDI SASA!!!!!! TUJIULIZE/TUWAULIZE NDUGU ZANGUNI.
MMETIMIZA WAJIBU WENU WAPISHENI NA WENZENU JAMANI!!!!! MUNGU IBARIKI TANZANIA.
DR.SLAA songa mbele,nothing impossible under the sun.Tuko nyuma yako mpaka kieleweke.Peoples Power(MUNGU IBARIKI TANZANIA)
jamani slaa muongo sana, tunapotea watanzania
Dr. Ana kipaji cha kuelimisha uma kwa rika zote ni vile tu watanzania ni wepesi wa kusahau na kuridhika na kilichopo lakini maumivu yakifika mahala pake tunaanza kulalama wakati treni limeshaondoka! Tuanze kuwadhamirisha watoto wetu toka shule za awali, kuwa na roho au dhamira ya kitaifa kizalendo. ‘niliwahi kufika Uswis, nikakaribishwa na rafiki yangu ambaye ni mwalimu, akaniomba niandike maneno machache ya kiswahili ubaoni ili wanafunzi wake wasome, wakati naandika kipande kidogo cha chaki kikameguka, mimi sikujali wala haikunigusa lakini nilipoiganyaga! darasa zima walipiga kelele nami nikashangaa! mwalimu wao akaniambia wanalalamika juu ya uharibifu wa kodi ya wazazi wao’ Je ni watanzania wangapi wenye roho ya kizalendo na uchungu wa rasilimali yao! Nani yuko tayari kumsema jirani anayeharibu vianzo vya maji kijijini! Nani anathubutu kumsahihisha nesi anayezembea kazi yake, nani yuko tayari kumkemea kiongozi anayevunja sheria ya nchi! utasikia oh mtoto wa fulani mwizi! mara utaambiwa wamesuluhishwa kinyumbani! mara wamepatanishwa! Zaidi utaambiwa naogopa kulogwa na jirani yangu nikimkosoa au nikimkaripia mtoto wake katika maovu! Haya na mengineyo mengi ndo yaloua dhamiri zetu watanzania! Tumekosa ujasiri, uzalendo na utu wema. Tumekufa kiroho kiasi kwamba tunauza watu kama bidhaa, tunaamini maisha rahisi kwa njia ya ushirikiana! hii yote imetokana na uvivu wa kufikiri na kuwa wabinifu kwa kutmia akili na maarifa! Tunatumia njia fupi kanakwamba muujiza kufanikisha mambo! Yaani nataka gari basi litokee kwa garama yoyote ile hata kama kumwua mwanangu au ndugu yangu afe tu ilimradi nipata! kifo hiki cha dhamiri kilianza polepole! Inabidi tuwe na kiongozi wa kutusafisha kwa namna yoyote ile. Ili kuondoa ugonjwa wa kichaa cha mbwa lazima mbwa wote wenye kichaa wauawe! Tuataka kiongozi wa kuteketeza dhamiri zote mbya zisizo na uzalendo! Tuweze kuwa na Roho ya kitaifa.
Roho ya kizalendo! MF. Migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu (UDSM) ni wa ukweli na haki tupu lakini wangapi wanabaki mpaka mwisho! nini kinakosekana! roho ya udhati! Sauti ya uma ni sauti ya Mungu! Tatizo kubwa ni kwamba watz tuko kwenye matabaka! 1. tabaka la kwanza ni la wale wasionacho na la pili ni la wale walionacho (Maskini na matajiri) sasa tubiri vita kati ya mafukaramalofa na matajiri werevu! Ni vita mbaya sana kwani ni kati ya ndugu na ndugu! Ndugu fukara na Ndugu tajiri je nani ataamua vita vya ndugu?
MIMI NAMWUNGA DR. SLAA KWA ASILIMIA 100% JE NI WATANZANIA WANGAPI WANAOPATA NAFASI YA KUSHIRIKI DARASA LA DR SLAA NA KUELEWA? ONA NI WATANZANIA WANGAPIM WENYE TAALUMA NA VIPAWA VYA UBUNIFU WAKAKWAMISHWA NA SASA WANAFANYA KAZI NJE YA NCHI KWA UMAKINI NA HESHIMA! UKIMKUTA MTAZ KULE UJERUMANI, USWISS AU AMERIKA HANA MUDA WA KUPOTEZA NA WEWE, HAHITAJI SAA NZIMA KWA LUNCH KAMA HAPA BONGO. LAITI MTANZANI MOJA ANGEKUWA ANAFANYAKAZI ANGALAU KWA MASAA MANNE KILA SIKU TUNGEKUWA MBALI SANA! SIO OFISINI WALA MASHAMBANI TUNAZURURA SANA KIASI KWAMBA AKILI ZINALALA TUNABAKI KUPIGA DOMO MCHNA KUTWA TUKISUBIRI KWENDA KWA KALIMAZILA KUPATA DAWA YA UTAJIRI TUKAVUMBUA VIUNGO VYA ALBINO NA WATOTO WACHANGA! MAMA WEWEEEEE TUMEKWISHA
dr slaa is my right president,i blve in him,n every person in tanzania is going to appriciate changes that are going to happen,u i’ll never regret why u selected him,now wake up an pink up ur bag prepare to collect wat ur av lost 4 several years,
TANE READY FOR CHANGES NOTZANIA WE AR BLAABLAA
Nakubali kwa uraisi ni ofisi na wala si mtu binafsi. Hoja yangu ni kwamba DR SLAA na chama chake cha CHEDEMA kwa kushindwa kujidhihirisha kama chama chenye sura ya kitaifa licha ya kuwepo zaidi ya miaka kumi na tano, hakijaweza kujiandaa vya kutosha ili kuaminiwa na kupewa dola. Chama ambacho kimesimamisha wagombea ubunge chini ya asilimia 40%, madiwani chini ya asilimia 30%, kina wenyeviti wa serikali za mitaa chini ya asilimia 10 akuihitajiki utafiti kuthibitisha kwamba hakina maandalizi kushika dola.
Katika kipaupele chake mheshimiwa DR SLAA ameahidi Katiba mpya katika kipindi cha siku 100. Utaratibu wa uandikishaji katiba unajulikana na mwisho wa siku Bunge katika nafasi yake ya Bunge la KAtiba (Constuent Assembly) ndicho chombo pekee kinachoweza kupitisha, kwa niaba ya wananchi, Katiba mpya. Sasa Dr Slaa hata kama wabunge wake wote watashinda hawezi hata kutoa japo asilimia mia moja ya wabunge. Na mabadiliko ya katiba yanahitaji japokuwa asilimia 75% ya wabunge wote. Sasa kwa mtaji huu CHADEMA wana uwezo gani wa kutekeleza ahadi zake.
Wachangiaji wengi wanamuunga mkono DR SLAA wanasema tu kwamba anafaa lakini hawatoi vigezi kwanini SLAA? Kama tatizo ni rushwa CCM kwanini SLAA sio Lipumba au Rungwe?
Nakubali pia kwamba kuiletea nchi maendeleo ni wajibu sio hisani. Hoja ni kwamba serikali ya CCM inapaswa kuenziwa na sio kubezwa kwa mazuri iliyofanya kwani kutekeleza wajibu ni kigezo cha kupewa tena nafasi. Uzuri wa serikali ya CCM ni kwamba mapungufu yanayozungumziwa na wapinzani kama suala la rushwa wanaungama kwamba yapo, na wanaahidi kuendelea kuyashughulikia. Mtu yeyote mkweli atakubaliana nami kwamba mikakati mingi na juhudi kubwa zimefanywa na serikali kukabiliana na rushwa ikiwemo kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za kupambana na rushwa na kuwafikisha hata vigogo kwenye vyombo vya sheria. Katika level ya chama tumeona mabadiliko makubwa ambayo yanawacost hata wao wenyewe. Japo mapungufu yameonekana lakini ni mambo ya kawaida katika hatua za mwanzo za kutekeleza mambo.
Wazungumzaji wengine wameniadress mimi kama mwana CCM. Kwa bahati mbaya au nzuri mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote japo napenda kujadiliana na kushauliana juu ya mambo ya siasa na mstakbari wa nchi yetu.
Pia mimi ni mmoja kati ya wale wanaopenda mabadiliko tofauti na wengine wanavyonidhania. Ila napenda mabadiliko muafaka na sahihi. Uwepo wa vyama vya upinzani Tanzania naufurahia kwa kuwa umeleta changamoto kubwa kwa serikali na mwamko mkubwa wa kisiasa kwa wananchi. Japo wapinzani wanapoikosoa serikali mara nyingine hujibiwa kwa kejeli, lakini kwa vitendo serikali inakubali makosa na kufanyia kazi maoni ya wapinzani.
Mtizamo wangu ni kwamba kwa sasa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani havijakuwa na utayari wa kuchukua dola. Vinahitaji kutumia muda mwingi na resources nyingi kujenga chama kiwe cha kitaifa. Juhudi zionekane katika vipindi vyote sio kusubiri wakati wa uchaguzi. Juhudi nyingi sielekezwe vijijini kwenye wapiga kura wengi sio mijini tu na mikoa kadhaa. Wakifanya hivyo wanaweza kuchukua dola kwani dola ya Tanzania haikuwekwa kwaajili ya chama kimoja tu. Bila kufanya hivyo haaitakuwa busara kuriski nchi na kukipa dola chama kisicho na sura ya kitaifa. Uraisi hauwezi kutolewa kwa majaribio au bahati na sibu.
PIGA UA HUISHA NYOA AU SUKA DR. SLAA ANAUWEZO, DHAMIRA YA DHATI. YOTE TISA, KUMI TUWE NA SERA ZA KITAIFA NA SIYO SERA ZA KICHAMA.
MTU PEKKE AMBAYE ATAWEKA SERA ZA KITAIFA NI DR. SLAA.
Si tu wakati umepita mno wa Tanzania kuamua kuwa wakweli kwa hali halisi ya nchi, bali kuisi katika mazingira ya ukweli.
OMBINA USHAURI NA OMBI LANGU:
Kwanza:
Vyama vya upinzania viumgane pamoja badala ya kugawana KURA na kupelekea kwa kushidwa kwa Mgombea Mpinzani kupata kura chache.
Pili:
Uaminifu uzingatiwe ipasavyo katika kupiga na kuhesabu kura, na matokeo ya kura yatangazwe mara moja.
Suala la kuawa Albinos bila kutafutiwa ufumbuzi wa uhakika, linanipa simanzi kubwa. Jibu lipo peupe sana, ni kuweka camera mahali mbali mbali na kuwanasa wahusika.
Suala la umaskini Tanzania, nchi iliyojaa utajiri wa ajabu ambao madini mengine na wanyama pori hawapo mahali popote duniani isipokuwa Bwana Mungu kaipendelea Tanzania na kujaza maliasli hizo, lakini bado Wananchi tunasota na ufukara wa aibu!
BWANA MUNGU IOKOE TANZANIA! AMINA! AMRN!
•Naungana kwa mikono miwili na Bwana George kwamba Slaa hajawa na uwezo wa kuwa Raisi wa nchi kwa sababu chama chake bado kinaonekana cha kikanda.
•Naungana na John pia kwamba Slaa ana kipaji cha kuelimisha. Bila shaka ndio maana akaitwa daktari. Madaktari wengi duniani wana kipaji cha kuelimisha. Naongezea kwamba wapo viongozi wengi wa kisiasa hapa nchini wenye vipaji vya kuelimisha kama na hata kumzidi Slaa. Yatosha kutoa mfano wa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye kwa mtizamo wangu kama uwezo wa kuelimisha watu ingekuwa sifa ya uraisi angekwisha kuwa raisi wa Tanzania siku nyingi. Nahitimisha nukta hii kwa kusema kazi ya uraisi na ualimu ni vitu viwili tofauti.
•Juu ya watanzania wengi wanaofanya kazi nje mimi ninasema hilo sio tatizo. Wapo watu toka nchi nyingi wanaofanya kazi nje. Serikali haiwezi kuwazuia watu kwenda nje kutafuta maisha na wala haiwezi kwa mda mfupi ikaifanya Tanzania kuwa sawa na Ulaya. Naongezea hata hapa Tanzania wapo wageni wengi wanaojitafutia maisha wengine kutoka nchi zenye maendeleo zaidi yetu.
•Sauti ya watu ni sauti ya Mungu, ni kweli. Chama chenye watu wengi kila kona ya nchi ni CCM. Ikifikia CHADEMA au chama kingine chochote kikawa na watu wengi zaidi ya vyama vyote ni lazima kitatwaa madaraka.
•CCM wamekaa zaidi ya miaka 50, ni sawa. Nakataa kufanya majaribio kwa kuwapa wengine uraisi ambao vyama vyao bado ni vya kikanda au mikoa. Katika miaka yao yote 50 CCM wameweza kulinda amani na umoja wa kitaifa. Hiyo ni amana ya taifa. Chama kinachotaka ufunguo wa Ikulu lazima kuonyeshe wazi kwamba kina sura ya kitaifa. Vinginevyo tutafanya makosa makubwa kukipa ufunguo wa Ikulu chama cha kikanda.
•Mwisho watanzania tusifanye makosa kukipigia chama kilicho bado katika kipindi cha mpito toka ukanda kwenda utaifa. Tusubiri kama kitafanikiwa kufika katika safari yake salama
Aliyoongea ndugu Madaraka na Kibibi nayakubali kimsingi. Bwana Madaraka amefanya uchambuzi wa kisomi na yakinifu kuhusiana na hali ya siasa ya Tanzania kwa wakati wetu. Amekuwa wazi kwamba matatizo katika serikali yapo lakini hayajawa makubwa kiasi cha kuriski amani na usalama wa nchi kwa kukipa chama ambacho bado kina sura ya ukanda dola.
Kibibi naungana naye kwa mambo makuu matatu. Mosi umhimu wa wapinzani kuungana ili wawe na nguvu. Maoni yake yanatokana na ukweli kwamba vyama vya upinzani licha ya kuwa vingi kama utitiri bado vina wafuasi wachache sana na baadhi ya sehemu ya nchi hata uwepo wake haujulikani. Ili kuwa na nguvu ni bora vingeweka dhamira ya kuungana. Tatizo linalijitokeza ni kwamba badala ya vyama vya upinzani kushindana na chama tawala vinashindana vyenyewe ili nani aonekane chama kibabe cha ubinzani. Kuwa chama kibabe cha upinzani kinakinufaisha chama pia katika kupata ruzuku.
Nakubaliana nae pia tatizo na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi linaabisha taifa. Hata hivyo, ninaipongeza serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kukabiliana na tatizo hili.
Umasikini ni tatizo kubwa kama anavyosema Kibibi. Serikali imefanya juhudi pia katika kukabiliana na umaskini licha ya mapungufu. Kupanua elimu, kuboresha miundo mbinu na kuboresha kilimo ni mambo ya msingi katika kuondoa umaskini na serikali inayafanya kwa kiwango chake. Juhudi zaidi zinahitajika.
Tumuombe Mungu uchaguzi uwe wa haki na amani
watanzania tuamke, mtu yeyote mwenye busara ya kuona na kuelewa atajitambua kwa kujilinganisha, tujilinganishe na mataifa yaliyopata uhuru wakati wa tanganyika/tanzania ’1961′ mmoja kati ya nchi hizo ni indonesia “1959″, leo ipo ya 18 katika chati za maendeleo duniani; taifa letu lipo miongoni mwa mataifa masikini kabisa duniani ndani ya nchi chache sana zinazotegemea moja kwa moja misaada hata kwa bajeti na gharama mbalimbali kujiendesha, hivi hao wenzetu pamoja na mataifa yaliyosaidiwa na tanzania kujikomboa toka ukoloni na uongozi mbaya nyingi zikiwa barani afrika na leo chumi zao ziko juu yetu kwa mbali hili tu halitoshi kuona kuwa mfumo wetu wa uongozi ni mbovu na unahitaji ukarabati mkubwa; na ukarabati huu kama si kwa kubadili uongozi uliochoka; mbaya zaidi unazidi tu kujikita kwa kudanganya raia; ati nasi tukazidi tu kuushangilia kama sisi hatuwezi kuona hili tutaona lipi? Wabongo wenzangu wakati umefika wa kutodanganyika; badiliko linahitajika sasa na namna bora popote duniani ni kwa kupiga kura za ndiyo kwa upinzani unaoonesha matumaini kwa njia ya dr. slaa na vyama vingine; vinginevyo ccm haitafahamu kwama raia tumeamka watazidi tu kama kawaida yao kutamba ushindi wa sunami wakati mama na watoto wa tanzania wazidi kula saumu isiyopona kama mtu mwenye kidonda ndugu au saratani asiyetambua anakufa wakati akishangilia kama mzuzu anavyosema baba wa taifa kwa mfano wake wa mtu aliyedanganywa na vipande vya chupa akiambiwa ni almasi… “Enough is Enough my dear tanzanians let’s save our nation from public corruption of few stealing our tax in our poor economy”
barhe thy r
Naomba comments zangu nilizoandika kurespond kuhusiana na mfanano wa maendeleo kati ya Indonesia na Tanzania zirudishwa kama inawezekana. Kwa bahati mbaya nilituma kabla ya kuweka jina langu na email address
kwa wapenda mabadiliko na wasiotekwa namfumo wa kifisadi uliofanywa na CCM kuwa stahili mpya ya maisha ya watanzania, bila shaka hataacha kupiga kura kumpa mwanamapinduzi wa kweli Dr. Slaa(Kwangu mie namuita “Mnyoofu”. Yeyote anayetambua msimamo wa Dr.Slaa katika utendaji wake na utekelezaji wa majukumu yake ndani na nje ya bunge bila shaka Dr. Slaa ndiyo chaguo la watanzania 2010.
Ni sababu zipi zitakazotufanya kuendelea kukumbatia utawala wa watu wajanja wajanja? watu ambao kiti cha urais kwao ni fahari ya maisha na sio sehemu ya kutekeleza mjukumu ya watanzania maskini na Tanzania iliyotajiri bali utajiri wake hauna manufaa kwa watui wake.
Dr. Slaa ndiyo chaguo laetu. Tumwache JK amechoka, amelemewa, tumpumzishe kti cha Ikulu kwake ni kizito mno,Jk anapwaya!
Mmbogo.
Kwa Author Madaraka Uhuru Sept. 11 2010
Pamoja na wachangiaji wote wa “Blog” hii, ninayo machache ambayo ni kumbukumbu hai
za wakati tuliipo:
Kwa heshima na taadhima kwa Bwana Madaraka nina haya ya kumjibu:
“Kwamba CHADEMA ni chama cha mkoa ama bado hakijawa na wanachama wengi ukilinganisha na CCM!” Napenda kusema hivi:
Wingi wa wanachama si hoja, na wala tusidanganyike hata siku moja kwamba wanachama wanapopiga zumali na vigelegele kwenye mikutno ya hadhara ndio wingi wa KURA!
Kumbuka ktk uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi nchini TZ, ambao wengi walikuwa na matumaini kwamba Mzee Lyatonga
(with all my respect due to Hon. August Lyatonga Mrema)angeshindwa!?
Tunakumbuka ktk mikutano yake ya hadhara pale jangwani watu wanasukuma gari lake bila injini kuwashwa! Hamasa hizo zote zilimweka hali bayana kuwa sasa Tz itapata Raisi mpya!
Matokeo yake wote tunayajua na kuyajutia hadi leo hii. Kwa hiyo ndugu zangu wingi wa wanachama na umarufu wa chama si dira halisi ya upigaji wa KURA! Kura ni siri ya mtu binafsi itaendana na uamuzi wa ROHONI mwa mtu binafsi.
Mfano mwingine hai ni pale Mzee Dr. Hastings Kamuzu Banda alipoangushwa katika “Referandum” iliyopelekea Malawi kuingia ktk mfumo wa vyama vingi.
Ktk kampeni yake mara kwa mara utasikia!
“Tili pambuyo panu Angwazi!” tuko nyuma yako Mkombozi.
Dr. Banda alipiga kampeni nakusikia slogan hiyo hadi siku ya mwisho! Matokeo yake yalimshangaza mno na kushidwa kuamini alichokiona yaani kupata 30% ya kura zote.
Lakini alikuwa muungwana na kukiri kushindwa.
Point nyingine ni kuh. uzoefu:
Nani anazaliwa na uzoefu? Uzoefu unakuja na vitendo.
Mfano mwingine hai ni kuh.
Raisi wa 44 Barack Obama.
Wakati wa kampeni 2008 mpinzani wake Bibi Clinton alimuasa ajiunge naye ili awe mgombea mwenza (kwa maana kwamba hajulikani)na hana “experience”
Kijana alikataa na kutangaza wazi kwamba yeye anagomea Uraisi siyo Umakamu wa Raisi.
Baada ya kuteuliwa rasmi na chama chake kuwa Mgombea, ktk moja ya mahojiano na mshindani wake; Mh. John McCainn, aliuliza tena kwa jazba,”Who is Barack Obama? What does he know?”
Suala la kutokuwa na uzoevu “experience” lilijitokeza hasa ktk kampeni!
Kijana alijibu kwa utulivu kabisa na kusema hivi: “Labda sijui, kwa mfano siji kwa nini tunapigana vita Iraq?”
Kuh. uchanga wa chama cha Dr. Slaa na pamoja na yeye mwenye kutokuwa na uzoefu wa uongozi kuwa raisi
Ahsante Ndugu Madaraka, Ndugu Kibibi na akina George Jinasa kwa kuchangia vizuri katika mjadala huu wa “Dr. Slaa na nani hasa anafaa kwenda Ikulu 2010, ni Chama gani hasa kina watu wengi!”
1. Nikianza kwa Bwana Madaraka- Nchi hii ina watanzania wanaozidi milioni arobaini, kati ya hao wapiga kura kwa uchaguzi wa 2005 walikuwa milioni 16tu na mwaka huu wa uchaguzi 2010 watanzania milioni 19 na ushehe wamejiandikisha kupiga kura.
Hoja yangu ni kwamba katika wapiga kura wote hawa hakuna hata chama kimoja chenye wanachama hata robo asilimia(CCM wanaosema wanawanachama milioni nne hawajafika hata robo hiyo- (wana asilimia 21tu kama wanasema kweli ama ni danganya toto!) ukweli ni kwamba katika tafiti mbalimbali zinaonyesha wapiga kura ni asilimia 13 tu ya watanzania ndio wanachama wa vyama vya siasa vyote hapa nchini na asilimia iliyobaki, 87 hawako na wala si wanchama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania.Hivyo basi suala la ushindi wa CCM kwa kuwa na wanachama wengi ni jambo la kujidanganya kwa maana hatma ya nchi hii haiko kwa wanachama wa vyama vya siasa bali ni kwa watanzania wengi wanaopenda mabadiliko ya kweli katika nchi yao.
2. Suala la kuwa na Kiongozi wa Majaribio, tumeona jinsi nchi hii ilivyojaribiwa na viongozi wetu walioko kwenye mamlaka leo hii kwani hatujaona la maana zaidi walilofanya zaidi ya pengine kuwashukuru wanamageuzi na wapenda mabadiliko na maendeleo ya nchi yao akina SLAA kwa kutoa miongozo mbalimbali ya kuinusuru nchi hii kwa viongozi hawa ambao kwangu mimi ndio na amini ni wa majaribio.
3. “Chama Kidogo” na “Chama Cha Mkoa” Kwa Madaraka na Watanzania wengine wa namna hii napenda kuwaasa kuwa tuachane na “FIKRA MGANDO” za kutoa hoja bila tafiti- Chama kidogo maana yake nini? Chama cha mkoa maana yake nini? CHADEMA na vyama vingine kama CUF si vyama vidogo wala si vya mikoa ni vyama ambavyo leo hii viko mahali pote Tanzania bara na Visiwani. Mtanzania yeyote leo hii ahta mtoto mdogo anajua salaam ya vidole viwili kuwa ni ya chama gani, najua unaposema Nguvu ya umma unamaanisha cham gani. Ni jambo la kushangaza sana kwa mtu mwenye akili timamu kuanza kupotosha umma kwa kusema eti hivi ni vyama vya mkoa! Ndugu yangu Madaraka, Je, tukikupa nchi wewe si utaendelea kuwadanya watanzania kuwa hii ni nchi maskini sana na ina viongozi makini sana wakati watanzania wanaangamia si kwa sababu nchi yao ni maskini bali viongozi wao ni wajuzi wa kujilimbikizia mali?
Turudi nyuma, tujiulize na tutafakari hivi kwa nini wenye mamlaka ya kuongoza nchi hii wanaogopa hata midahalo kwa wananchi wao wanaowaongoza? Wamewakosea nini wananchi hawa? CCM ina dhambi gani hata kuogopa kuulizwa maswali ya ana kwa ana na watanzania hawa wenye dhikli ya mlo mmoja kwa siku?
Kwa nini baba mwenye nyumba anajitangaza kwa gharama kubwa ya mabango ya kifahari kwa watoto wake ndani ya nyumba aliyomo kila siku? Tena mabango yenyewe ati ni ya kutoka nje ya nchi kwa gharama ya sh. 1.5 Bilioni wakati watoto wanaugulia njaa hapa ndani ya nyumba. Kibaya zaidi ni kwamba baba ametumia sh.1.5 bilioni na anarudi kwa watoto wake kwamba mniite baba, na safari hii mkiniita baba nitawanunulia pipi na nitawapa kofia nyingi sana mjikinge na jua linalowaletea njaa!
DR.SLAA, ndiyo Rais wetu! Ni mwadilifu, ni mpenda maendeleo ni Msema kweli!Mchague yeye tarehe 31 Oktoba ili tushuhudie mabadiliko makubwa ya maisha ya watanzania.
Watanzania tusifanye makosa kwa kuwapa kura CCM ni sawa na kuangamiza familia zetu na vizazi vyetu! Wachekeeni, nendeni kwenye mikutano yao, ila jengeni fikra kuwa hao si wenzenu wamejenga ukuta na wamesahau daraja kwamba ndio kiungo muhimu kati yao na ninyi.
KURA NI SIRI YAKO HAKUNA ANAYAWEZA KUKUTISHA
wawekeni pembeni ili wajifunje namna maisha ya watanzania yalivyo ya tabu!
“SLAA ANAWEZA!
Kwamba CHADEMA hakijafikia kiwango cha kuwa chama cha kitaifa limejidhihirisha kwa kushindwa kusimamisha hata asilimia 40 ya viti vyote vya ubunge Tanzania na alau asilimia 30 ya viti vyote vya udiwani. Hilo mnajibu vipi?
Pili CHADEMA haina ofisi sehemu nyingi za nch wakati CCM ina ofisi kila kijiji hapa nchini. Chama ambacho kimeshindwa hata kusimamisha wagombea asilimia 30 ya udiwani ni nchi kwa akili ya kawaida ni chama cha kutawala leo?
Hoja yangu sio kuwa na mashabiki wengi katika mikutano kwani kwa hilo hata CHADEMA na CUF wamefanikiwa katika baadhi ya sehemu. Hoja yangu ni kukisambaza chama nchi nzima na kuweka uwakilishi katika kila sehemu. Nakubali kwamba ni kitu kimoja kuweka wagombea na kitu kingine kushinda. Lakini kwa hali ya kawaida kabisa chama chochote chenye sura ya kitaifa kisingeshindwa kuweka alau asilimia 50 ya wagombea wa ubunge na udiwaani. CCM imeweka asilimia 100 na majimbo mengine imepita kwa kususiwa. Sasa CHADEMA inapata wapi hadhi ya kuweza kushindana na CCM leo. Mambo ya kesho na kesho kutwa siwezi kuyasemea kwani binafsi sina tatizo na CHADEMA kama CHADEMA au CUF kama CUF. Tatizo langu ni kushindwa kwao kuvifanya vyama viwe vya kitaifa. Pindipo watafanikiwa kuwa na sura ya kitaifa na kuweka sera nzuri, mimi binafsi naweza kuwaunga mkono.
Kitu kimoja kidogo kinaweza kudhihirisha kwamba CHADEMA bado cha ukanda. Kwamba kati ya wabunge saba walipata nafasi hio kwa viti maalumu sita wanatoka Kilimanjaro. Kama CHADEMA wangekuwa na mkakati wa kukifanya chama kuwa cha kitaifa, bila shaka uteuzi wa wabunge hao ungezingatia uwiano wa kikanda.
DR SLAA anapewa sifa ya mtu safi mnyoofu. Wachangiaji hawesemi wagombea wengine kama DR Kikwete, Prof Lipumba, Hashimu Rungwa na Dovutwa ni wachafu au sio wanyoofu. Hawasemi kigezo kipi wanatumia kumpa mtu daraja la usafi au unyoofu mbali ya ushabiki wao binafsi wa kisiasa. Katika jukwaa kama hili ambalo hatujuani hitikadi na ushabiki wetu wa kisiasa ni bora mtu unapotamka DR SLAA ni safi ukatoa vigezo vya usafi wake ukimlinganisha na nani?
Kwamba viongozi waliopo madarakani wanaogopa midahalo mimi sioni kama ni suala la msingi. Suala la midaharo linategemea mambo mengi. Kwa mfano, nani kauandaa huo mdahalo? Mnarumbana na watu wa aina gani? Katika mazingira ambayo wagombea wanatumia personal attack badala ya kujenga na kuvunja hoja, mgombea mwenye heshima zake anaweza kusita kushiriki.
Suala la Obama halifanani hata kidogo na hali halisi iliyopo Tanzania. Tofauti na DR SLAA, OBAMA anawakilisha chama chenye sura ya kitaifa na chenye uzoefu mkubwa.
Bado nasisitiza kwamba DR SLAA na chama chake bado ni cha kikanda na hivyo hakijapata sifa ya kuchukua dola. Cha kikada kwa msingi kwamba hakijaenea nchi nzima wala hakijaweza kuweka wawakilishi japo asilimia 40 katika nafasi za wagombea ubunge, udiwani na serikali za mitaa. Hicho ni kipimo tosha cha udhaifu wa DR SLAA na chama chake. Kwani kama ameshindwa kukifanya chama chake kiwe cha kitaifa ataweza kuifanya dola ikawa ya kitaifa kama akipewa? Kuna haja gani ya kucheza kamali katika mazingira yaliyo wazi kama haya?
Namalizia kwa kutoa pongezi zangu za dhati kwa wachangiaji wenzangu kama akina MMBOGO, MADARAKA, KIBIBI, BARHE na wengineo kwa kutoa michango iliyojengwa katika misingi ya hoja na katika hali ya kuvumiliana na kuheshimiana. Nawaomba tuendelee kufanya hivyo kwani nyumba yetu wengi wanajifunza.
HAPO UMENENA KAKA GEORGE JINASA. KINACHOTAKIWA SIO TU KUSEMA DR SLAA SAFI BALI KUTOA VIGEZO VYA USAFI WAKE. VINGINEVYO MJADALA WETU HAUTAKUWA TOFAUTI NA KAMPENI ZA SIASA. KAMA KILA MTU ATASEMA MGOMBEA ANAEMPENDA NI SAFI BILA KUTOA KIGEZO TUTABAKI KUWA NA WAGOMBEA WOTE SAFI NA WOTE WACHAFU.
LAWAMA KWAMBA CCM NI MAFISADI KUTOKANA NA BAADHI YA WANA CCM KUJIHUSISHA NA UFISADI HAZINA MSINGI. UFISADI KAMA ILIVYO UHALIFU WAWOTE NI TABIA YA MTU WALA SI SERA ZA CHAMA. HATA KATIKA CHADEMA WAPO MAFISADI WENGI NA HATA WATETEZI WAO. HILO HATA HIVYO HALIKIFANYI CHAMA CHA CHADEMA KUWA CHA KIFISAJI MAANA SERA ZAKE KAMA ZILIVYO ZA VYAMA VYOTE VYA SIASA HAZITETEI UFISADI.
NENO UFISADI NI PANA LINAWEZA KUHUSISHA HATA UFISADI WA KIMAADILI YA KIMAHUSIANO. NI SUALA AMBALO LINATUMIKA SANA NA LIMEKUWA LIKUTUMIKA SANA NA VYAMA VYA UPINZANI KATIKA KUIKOSOA CCM KWA KUWA NDIO CHAMA KILICHO MADARAKANI. KWA KIPINDI CHA MIAKA MINGI KILIOSHIKILIA MADARAKA HAKIWEZI KUKOSA MAPUNGUFU. KINA MAPUNGUFU MENGI TU. MWL NYERERE ALIWAHI KUUNGAMA MBELE YA UMMA KWAMBA YEYE NA CHAMA CHAKE KAMA BINAADAMU YAPO MENGI MAZURI WALIYOYAFANYA LAKINI PIA YAPO YA KIJINGA ALIYOYAFANYA. WAPINZANI HAWAWEZI KUONGELEA MAZURI YA CCM MAANA KUYAFANYA NI JUKUMU LAO. LAKINI WANANCHI WANA MACHO YA KUWEZA KUYAONA MAZURI MENGI TU YALIYOFANYWA NA CCM.
LAWAMA ZA UFISADI ZINGEKUWA NA MAANA KAMA SERIKALI YA CCM INGEKUWA HAICHUKUI HATUA YOYOTE. LAKINI HISTORIA ITASHUHUDIA JUHUDI NA MIKAKATI MIKUBWA SANA ILIYOWEKWA NA SERIKALI YA CCM KATIKA KIPINDI KIFUPI KUPAMBANA NA UFISADI KUANZIA NDANI YA VYAMA NA KATIKA SEHEMU NYINGINE.
Bwana MMBOGO anasema hamna cha maana walichofanya CCM. Mimi siamini kama hiyo kauli ni ya kweli au ya kisiasa tu. Haoni miundo mbinu ilivyoimarika, juhudi na mapinduzi makubwa yaliyofanywa katika elimu. Mashule kila kata Tanzania nzima kwa kipindi cha miaka michache ni kasi kubwa sana. Tunakubali bado matokeo ya shule nyingi za kata sio mazuri kutokana na mapungufu ya waalimu na vitendea kazi. Hilo ni jambo la kawaida katika kipindi cha mwanzo cha mabadiliko. Huwezi kuanzisha mashule katika kila kata na mwaka huo huo yakawa na walimu na vitendea kazi sawa na mashule yaliyokuwepo miaka mia iliyopita. Ni wazi kwamba itachukua muda kwa shule hizo kufikia kiwango cha kawaida. Ndio maana hata huko nyuma serikali ilivyoanzishwa “Universal Primary Education” hakusita kuongeza idadi ya wanafunzi kwa kuwa hapakuwa na walimu na vitendea kazi vya kutosha. Ili bidi vijana waliomaliza darasa la saba wenye uelewa mzuri kuajiliwa kufundisha shule za msingi huku wakiendelezwa kidogo kidogo kabla walimu wa kutosha hawajapatikana. Hivi sasa baadhi ya walimu hao wa Upe wana elimu ya udakitari wa falsafa.
Ni kwa namna hiyo hiyo serikali katika hatua za mwanzo ililazimika kuwachukua vijana waliomaliza form six na kuwapa mafunzo mafupi kabla ya kuwapa madarasa kufundisha huku wakijiendeleza na mikakati mingine ya kupata waalimu zaidi ikiendelea. Vijana hao wengi wamejisajili katika Chuo Kikuu Huria kwa ajili ya elimu ya ualimu na wengine wameshapata shahada. Serikali imesomesha wanafunzi wengi ualimu katika vyuo mbalimabli katika kipindi hicho kifupi kukabiliana na mabadiliko. Kubwa zaidi imechenga kwa nguvu zake yenyewe chuo kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati cha Dodoma ambacho kina shule maalumu ya ualimu. Ndani ya miaka michache ijayo walimu wenye shahada watapatikana sio tu katika shule zote za sekondari bali hata shule za msingi. Kwa nini tusikubali kwamba DR KIKWETE na chama chama chake kimefanya mapinduzi makubwa. Hivi kwa mtanzania wa leo aliezungukwa na technologia ya mawasiliano atashindwa kuliona hili?
Ni jambo la mhimu kuzingatia kwamba serikali imeendelea kufanya mapinduzi makubwa licha ya dunia kukumbwa na mtikisiko wa uchumi.
Ndugu zangu watanzania, ingawa si rahisi kusema ccm haikufanya kitu lakini ni kweli kusema imefanya kidogo sana, maana chochote mwanadamu anachofanya na kusema kinapaswa kulinganishwa na wengine na kwa maana hii nchi ambazo zilipata uhuru wake katika urika na Tanganyika yaani nchi kama Indonesia na Malaysia. Hivi hao wamekuwa na muujiza gani hata nchi zao zinaenda kasi ya kuwa mataifa bingwa kiuchumi duniani nasi Tanzania ati tuhesabiwe daima kuwa miongoni mwa nchi masikini duniani?
Pili wanaosema Chadema bado hawaelewi maana ya demokrasia, hivi democrasia ni umangimeza na urasimu wa kulinda tu walio madarakani? Je tuseme hao wanalinda ufalme fulani, nini maana ya demokrasia ya vyama vingi? Majuzi hapa Mbulu, wananchi wanaondoka na kumwacha mgombea wa ccm wa Urais, kwa kuanza kukashifu vyama vya upinzani na baadaye ati vyombo vya usalama kutumia bomu za machozi ati kuzuia wasiondoke tena baada ya saa kumi na mbili jioni, hivi serikali inataka kufanya nini? Demokrasia ni Autocracy? Ukiunda sheria wewe mwenyewe ndiye tena mvunjaji? Tunataka nchi yetu ielewekeje, je demokrasia ni kulazimisha, nini maana ya uhuru wa kutoa maoni? Kama mtu hapendi kukusikia unamlazimisha? Kwanza saa zenyewe za kuchelewa nje ya muda halali na baadaye wananchi wanaondoka unawazuia kwa mabomu ya machozi ndiyo hiyo demokrasia?
CCM ieleze sera na isilazimishe wananchi kwa kutumia nguvu za Dola, na pia chombo cha habari cha Umma TBC I na TBC Taifa watumie haki sawa kwa wagombea wote, serikali ifahamu kuwa Watanzania ndiyo wenye chombo hicho kwa mujibu wa kodi zao, na pia haki yao kikatiba; na katiba wala si ya chama kimoja, kwa hiyo wana haki kuwasikiliza wagombea wote wa vyama ili wawachague wanaowafaa na si tu wa chama tawala iliyodumu kwa Takriban miaka 50 ya maendeleo duni na sasa yanayojaa ufisadi, mbaya zaidi ufisadi huo na utawala bora kulindwa kwa nguvu za dola.
Kwa wanaodanganyika kwa mizengwe yeyote ile wafahamu hawaipeleki nchi pazuri na pia amani haina maana kulinda maslahi ya viongozi walio madarakani wanaojaza mifuko yao, na mbaya zaidi ni kukosa ubunifu na ulinganishi ulio wa kweli; maana Uongozi ulio madarakani sasa ulipanda jukwaani kuongoza wakati mfumuko wa bei ukiwa asilimia 7% tu, na sasa ni tunapoelekea uchaguzi tuko asilimia 17% hii ni fedheha, yaani wananchi wengi wanashindwa kununua hata mafuta taa na matumizi mengine muhimu ya maisha na bado watanzania wanakaa kwa amani bado majukwaani tuzidi tu ati kuwatukana kwa kuita vyama vingine ni carbon copy ila CCM ni chama halisi hii ni kuwafanya watanzania mabunju wasiofikiri, tukazidi tu kuwakamua kodi zao. Kwa haki uongozi kama huo unapaswa kupelekwa mahakamani kwa kushindwa kuwajibika.
Isitoshe kama vile tunaonekana hatufikiri ati Rais aliye madarakani anatafuta kura anastahili kufanya hivyo, lakini mkewe anatumia kipengee kipi cha katiba ya taifa hili naye kuzunguka nchi kwa gharama za taifa na baadaye ati tudanganywe anatumia mfuko maalum, upi huo na kwa katiba ipi? Maana ziara zake zilishaanza hata wakati uongozi uko madarakani.
barhe.
why not!
naelekeza comment yangu katika kurasa huu wa jamii; iwe wazi kwa wote!
rthyBarhe
Kulinganisha Tanzania na nchi kama Indonesia na Malysia nadhani sio sahihi. Kwanza, sio kweli kwamba nchi hizi zilipata uhuru sawa na Tanzania. Indonesia kwa mfano ilipata uhuru toka mwaka 1949. Isitoshe ukoloni uliokuwepo katika nchi hizi ni tofauti sana. Tofauti na Tanzania, katika nchi hizi dola za kikoloni hazikuvunja nguvu za kiuchumi za makabila makubwa kama waarabu na wachina ambao walikuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi hata kabla ya kuja kwa wakoloni wa kijerumani. Katika kipindi chote cha ukoloni sehemu kubwa ya nchi hizi ziliachwa zikiendelea na mifumo yake ya kiuchumi kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni.
Indonesia yenye visiwa 13,000, ardhi nzuri kwa asilimia 80, yenye utajiri mkubwa wa petroli, gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya silver, dhahabu, copper nakadhalika yenye watu zaidi ya milioni 230 ina mambo mengi kijografia, uchumi na historia yanayotofautiana kimsingi na Tanzania.
Ikumbukwe kuwa baada ya serikali ya Generali Soeharto kuingia madarakani mwaka 1966 na kuanzisha serikali ya kiimla iliyodumu hadi 1997, kulikuwa na uwekezaji mkubwa toka nchi za magharibi uliosaidia pia kukuwa zaidi kwa uchumi. Sidhani kama ni sahihi kusema serikali haikafanya lolote kwa kutokuwa sawa kimaendeleo au kuikaribia Indosyia. Na hata tukichukulia mfano wa nchi kama Afrika ya Kusini iliyopata uhuru wake juzi juzi tu tena kwa kusaidiwa na Tanzania, huwezi kusema kwamba maendeleo yake makubwa ya uchumi yamechangiwa na utawala na sera nzuri tu bila kuangalia historia na geografia ya nchi hiyo.
Kwamba serikali imefanya machache sana, nashindwa kuelewa msingi wa hoja hiyo. Katika maelezo yangu ya mwanzo nimetoa mifano wa maeneo mengi tu ya maendeleo ambayo yamefikiwa na nchi yetu kwa kipindi kifupi. Sijua ndugu yangu Barhe anatumia kigezo gani kupima wingi au uchache wa maendeleo. Lakini kwa upande mwingine hatuambii CHADEMA kwa kipindi cha miaka 17 imefanya maendeleo gani hata katika level ya chama. Imejenga maofisi mangapi ya chama katika ngazi zipi. Naelewa kwa muda mrefu ofisi yao imeendelea kuwa katika nyumba ndogo ya makazi iliyopo Kinondoni ambayo haina hata eneo la kupaki magari matatu. Sina uhakika kama nyumba hiyo ni ya kupanga au yao. Mara nyingi usafi huanzia nyumbani kwako. Kwa chama chenye uongozi mzuri na muelekeo mzuri tungetarajia wangekuwa japo wamenunua hata nyumba kubwa ya kutosha maofisi ya watendaji wao kitaifa. Hawawezi kusema hawana fedha kwakuwa pesa za ruzuku wanapata kila mwaka na ndege wanakodi.
Angalia chama kama CUF. Wao japokuwa wameonesha seriousness kwa kujenga nyumba yao wenyewe ya ghorofa pale Buguruni. Kuna maeneo ya kutosha ofisi nyingi na parking ya magari.
Kuhusiana na tuhuma kwamba serikali imewalazimisha watu kumsikiliza Kikwete siwezi kulisemea sana maana sina taarifa za kutosha. Pia nashindwa kumwamini moja kwa moja ndugu Barthe kwakuwa sina uhakika kama hana maslai binafsi na chama cha Chadema. Kama ni kweli serikali imefanya hivyo imekosea sana. Lakini tujiulize hivi serikali pia iliwalazimisha wananch kwenda kwa wingi katika mkutano wa mgombea wao?
Suala la mfumuko wa bei tusilitizame kwa makengeza. Tutizame pia upande wa pili kwamba ni muda mfupi uliopita dunia ilikumbwa na mtikisiko wa uchumi. Tanzania sio kisiwa ni sehemu ya dunia. Mfumuko wa bei tunaouona una uhusiano mkubwa na mtikisiko wa uchumi. Tunajua kwa kiasi gani mtikisiko wa uchumi uliathiri sekta ya utalii na madini kama ilivyoathiri biashara ya kimataifa. Naamini isingekuwa mtikisiko wa uchumi suala la mfumuko wa bei tusingekuwa tunalizungumzia.
Kuita vyama vingine ni photokopi wala sio matusi bali ni uchambuzi wa CCM wa sera za vyama vya upinzani. CCM wanaziona sera za vyama vya upinzani kama marudio ya sera za CCM katika namna tofauti. Ndio maana Mh Kikwete anaviona vyama vya upinzani kama photokopi na anawataka wananchi wachague original badala ya photokopi. Kama kauli hii ni sahihi au la kinachotakiwa ni kuonesha kwa hoja. Nategemea mchangiaji angetofautisha katika ya Sera za vyama vya upinzani na CCM ili kukanusha madai kwamba ni photokopi. Hapa kwa upeo wa macho yangu sioni matusi yoyote.
Kwamba mke wa Raisi anatumia fedha za umma kutetea CCM, kiongozi wa kampeni wa CCM alikanusha kwa ushahidi. Ningetarajia mchangiaji angetoa ushahidi kama kweli anatumia fedha za umma. Vinginevyo, mke wa Raisi kama mwanachama na mpenzi wa CCM ana haki ya kukipigia chama chake kampeni kama ilivyo kwa wake wa wagombea wote. Ndio maana hata DR SLAA alikuwa anatambulisha mke wake katika kampeni zake za uraisi na hilo halina ubaya.
Kwamba vyombo vya habari vya umma visiwe na upendeleo, nakubaliana kabisa na Barhe. Naongezea kwamba hata vyombo vya habari binafsi havipaswi kuripoti kwa upendeleo na ushabiki. Naamini TBC wamekuwa wakiripoti kwa uaminifu mkubwa bila upendeleo. Ndio maana mdahalo wa wagombea unaendelea japo CCM wamesusia.
Tunaosema CHADEMA bado tunajua nini maana ya demokrasia. Kwa kusema hivyo hatusemi kwamba CHADEMA wasishiriki katika kugombea uraisi na ubunge bali tunawataka wakazane ili kufanya chama chao kiwe cha kitaifa. Msingi wa demokrasia ni utashi na uwakilishi wa watu. Chama kilichoshindwa kujipenyeza sehemu zote za nchi na kuweka hata asilimia 40 ya wawakilishi bado hakijakuwa tayari kuchukua dola. Hiyo haihitaji ujuzi mkubwa wa wa siasa kulijua. Kila jambo lina muda wake, lakini kwa mtaji huo muda wa CHADEMA kupewa dola haujafika.
KODI ZA WAVUJA JASHO Tanzania zinawageukia kuwapiga risasi za machoni walazimishwe kubakia mkanoni wa CCM kusikia jinsi CCM inavyowakaba koo kutoa kodi hata kama mke wake mjamzito hawezi kupata hela ya daladala! CCM inawalazimisha waendelee kuiweka madarakani ili wamalizie zaidi kile kidogo kilcholindwa na kinachosalia ktk BoT na maliasli kwa jumla! Kwa maana hiyo CCM haiwezi kuona madhara na aibu ya nchi tajiri kama Tz. kugeuka Omba Omba> Ni kweli
Ufisadi haunaaibu, ni kweli katabia ka uchouchoyo na ubinafsi kamejenga mizizi na sasa tunavuna matunda yake.
Tukiendelea kuachilia uoza huu kuendelea, hatimaye matunda hapo yanakomaa na kuzalisha mbegu na kuendelea kuimarika nchi nzima kuwa na Serika;i za Wafisadi tangu vitongojini. vojijini hadi taifa.
Barbe, please keep it up!
ALUTA CONTINUA A A A!!!!
Nimepitia mahojiano ya Dr. Slaa na BC, ktk mahojiano marefu na ya kina BC imemuuliza kuwa CHADEMA nao wanasemekana wana Matumizi ya fedha isiyoeleweka chanzo chake, swali kama hilo, Dr. Slaa ameeleza tena kwa ufafanuzi kamili kwamba, ni kweli pesa iliyotumika ktk kukodi helicopter walikopa kwa Mwenekiti wao
Mbowe na kwamba wanalipa pole pale.
Lakini fedha ambayo CCM inatumia kwenye kampeni zake, imetoka wapi? Kama ni bageti ya serikalini imeidhinishwa na nai ktk kikao kipi kilichoomba ridhaa kwa wananchi wavuja jasho na walalo na njaa!!! Kama siyo Serikali ya mabavu na ukandamizaji, ni nini basi?
Udikteta unaanza vivyo hivyo taratibu taratibu kwa maneno laini na ngonjera na hatimaye kutumia ubabe na mabavu ya Dola.
Kaeni chonjo!
Hivi kama katika mahojiano yake kwa kina na BBC angesema hizo pesa katoa mfukoni mwake kungekuwa na tofauti? Mahojiano hayo hata mimi niliyasikiliza. Hakuonesha mkataba wao na Mbowe wala kiasi cha fedha walichokopa. Hawakuonesha zinalipwa vipi na zimeshalipwa vipi? Kama Mbowe ameweka masharti ya kupewa uwaziri mkuu au masharti yoyote yenye madhara kwa umma hamna anaejuwa hata baada ya mahojiano marrefu na BBC.
Kwamba CCM wanapata wapi fedha zao, iko wazi katika kumbu kumbu zao za fedha. CCM wamekuwa wakizungumzia repoti zao za fedha kila mwaka na wanakaguliwa na maodita wa nje. BBC haiwezi kuwahoji wagombea wote kwa wakati mmoja. Kwa hiyo kuhojiwa kwa DR SLAA na kuelezea chanzo chake cha fedha haina maana kwamba CCM wategemea fedha za serikali au hawana uwezo wa kuelezea chanzo chao cha fedha BBC au katika chombo chochote cha habari.
Kwamba serikali wanatumia fedha za wapiga kura kupiga watu mabomu ya machozi na kuwalazimisha wawachague nashindwa kuelewa. Hata DR SLAA sijamsikia akitoa kauli hiyo. Juzi nimemsikia Prof Lipumba akilisifia jeshi la polisi kufanya kazi yao kwa uadilifu katika kipindi hiki cha uchaguzi. Kauli yake haijapingwa na kiongozi yeyote wa upinzani na aliitoa katika press conference. Nionavyo mimi, sio vizuri kulihusisha jeshi la polisi katika ushabiki wetu wa kisiasa bila kuwa na ushahidi kamili. Jeshi la polisi na dola kwa ujumla ni ya wote sio CCM. CCM ni chama tawala tu, ni chama kama vyama vingine. Inawezekana siku nyingine dola ikawa chini ya chama kingine. Lakini dola itabaki ile ile na jeshi la polisi pamoja na majeshi mengine yatatii mkuu wa dola mpya.
Kwamba wananch tukae chonjo kuna udikteta unakuja ni kauli ya kutishna ambayo haipaswi kuwepo katika kipindi hiki cha uchaguzi. Serikali imeonesha uadilifu mkubwa kwa vyama vyote vya siasa. Kama kuna dosari yoyote katika chama binafsi cha siasa, lawana zisiende kwa vyombo vya dola. Tuiombee nchi yetu iendelee kuwa na amani wala tusidumbukie kwenye shimo la udikteta.
Jana nilikuwa napitia magazeti ya miezi michache iliyopita. Nikakutana na habari iliyokuwa inazungumzia uamuzi wa aliekuwa Mbunge wa Maswa Mh John Shibuda kujiondoa katika kugombea kuteuliwa na CCM kuwa mgombea Uraisi. Kwa uchache Mh Shibuda alisema kwamba ameamua kujitoa kwa sababu Kikwete amefanya mambo mengi sana kiasi kwamba hamna mtu yoyote anaeweza kusimama na kupambana nae. Kauli yake hiyo ilijengwa katika hoja zenye mantiki zikiungwa mkono na takwimu. Baadae nikapitia magazeti yakiwa na stori za yeye kushindwa katika kura za maoni. Kwa wakati mmoja anatoa matamshi kwamba hana mpango wa kutoka CCM. Baadae tena tunamsoma magazetini ametoka CCM na kujiunga na CHADEMA na kupewa nafasi kubwa katika chama. Nafasi kubwa kiasi kwamba kila palipo na msafara wa mgombea uraisi wa CHADEMA lazima awepo na kila wanapozungumza viongozi watatu wa CHADEMA yeye ni wa nne wao. Baadae namsikia akimponda Kikwete kwa kutokuwa na uwezo wa kuongoza nchi kiasi cha kushindana na DR SLAA. Anatoa kmaneno haya kwa macho makavu bila hata kurekebisha au kufafanua matamshi yake ya nyuma. Ajabu ni kwamba anashangiliwa na umati wa watu bila kuhoji msimamo wa mtu huyu na ukweli wake.
Tukio kama hili linaweza kutoa picha tofauti kabisa kwa chama cha CHADEMA. Kweli ni chama makini? Kweli hakina tofauti ki mtizamo, maamuzi na mitizamo na kada wake mkuu Shibuda? Kama Shibuda yuko tayari kuzungumza yaliyo kinyume na imani yake ili mradi kuunga mkono chama alicho nacho kwa wakati fulani CHADEMA nao hawawezi kuwa na sura kama hiyo? Hivi Kikwete wa mwezi wa saba ni tofauti na Kikwete wa mwezi wa nane mwaka huu huu? Hivi maneno ya Shibuda kwamba Kikwete hana mfano kwa uwezo wake yalikuwa kweli alipokuwa CCM na maneno Kikwete hana uwezo yakawa pia kweli alipohamia CHADEMA? Kama chama kinachotaka kwenda ikulu kinalea usanii huu wa wazi wa kisiasa kitaaminiwa vipi kama kinaweza kuleta mabadiliko nchini? Naomba kukosolewa.
DU MZEE JINASA UNA KIPAJI KIKUBWA CHA KUCHANGANUA MAMBO. KUSEMA KWELI MIMI UMENIPANUA SANA KUIFAHAMU HALI HALISI YA KISIASA YA NCHI YETU.
HIVI HILI LA CHADEMA KUANDIKA KATIBA NDANI YA SIKU MIA UNALICHUKULIAJE? HUKO KENYA ANAKOZUNGUMZIA WALITUMIA ANAJUA MCHAKATO KUANDIKA KATIBA UMECHUKUA MUDA GANI? MUDA HUO USINGETOSHA HATA KUANDIKA KATIBA MPYA YA CHADEMA NINAVYOJUA MIMI. NI MUDA GANI ATATUMIA KUKUSANYA MAONI YA WATU JUU YA KATIBA WANAOITAKA? NI MUDA GANI ATATUMIA KUCHAMBUA HAYO MAWAZO? MUDA GANI UTATUMIKA KUANDIKA RASMU YA KATIBA MPYA? NI MUDA GANI UTATUMIKA KUIJADILI HIYO RASMU KATIKA BUNGE? NA HILO BUNGO LINALOUNGA MKONO SERA YAKE ATALIPATA WAPI WAKATI WAGOMBEA UBUNGE ALIOSIMAMISHA HAWAFIKI HATA ASILIMIA 40? HIVI WEWE MPIGA KURA ULIWAHI KUKAA CHINI NA KUTAFAKARI HAYA?
Jinasa naona kweli jinase kwenye hoja na siyo maslahi, kama wewe
wategemea ruzuku mimi naandika kwa kuenzi haki za uraia wa watanzania
wote na ruzuku ama takrima kamwe! Mimi sitegemei takrima ilivyozoeleka
kwa baadhi ya viongozi wetu, hilo limefanya raia masikini wasahau haki
zao.
Umesemea madini ya Indonesia; je haya ya Tanzania siyo madini ama kwa
kuwa yako bongo hayawezi kuuzwa, bali tuyatoe kama nyanya mbovu sokoni
sio? Kwa sababu ya uongozi mbovu unaoulindwa kwa vyombo vya dola,
ambavyo kila raia analipia kodi; ati tuwezeshe demokrasia mali ya
kundi ama chama fulani? Ingawa nakubaliana nawe Indonesia ilipata
uhuru 1948 mara baada ya vita vya pili hiyo ni miongo miwili tu kabla
ya Tanganyika 1961, je wao wanapoingia Ulimwengu wa kwanza kiuchumi,
sisi walau tungepaswa kuwa ulimwengu wa pili? Hapo ningeelewana nawe.
Kidogo nakusikitikia maana unasema Chadema hawana ofisi sijui, hiyo
hoja inasaidia nini maana hata baba wa Taifa mpaka anatoka madarakani
hakuwa na nyumba ya familia, maana hakuwa anaanza na ubinafsi bali
utaifa na uzalendo. Kwako wewe uongozi uanze na ubinafsi hakika huo
ndio ulioulemaza taifa letu, viongozi wanufaisha maslahi binafsi dhidi
ya maslahi ya Taifa na raia, na ndiyo maana nguvu kubwa za dola
yatumika kulinda ukiritimba na urasimu huo bila kujali maslahi ya
masikini wa walipa kodi mathalan chama tawala kutumia bilioni hamsini
yamaanisha nini katika umasikini huu ambao raia washindwa kupata tiba,
maji, na mahitaji muhimu kama barabara na elimu, chama kinatembeza
helikopta tatu, wakati Chadema walipoanza moja wailalamikia; wakati
huo huo katika muda tu wa miaka 5 nchi kiuchumi yarudi nyuma badala ya
kuendelea, kiasi kuwa pale alipofikisha Rais wa Awamu ya Tatu sasa ni
ndoto tu! Na ingawa naona upeo wako wa kuelewa uchumi nautilia shaka,
maana hali mbaya ya kiuchumi haikuwa kwa Tanzania tu bali ulimwengu
mzima, je mbona umasikini wetu unakuwa tofauti na mataifa mengine? Je
ni Rais wa Jamhuri ipi duniani anakuwa na ziara nje ya nchi kama
mkakati muhimu hata kiasi cha kuyumbisha bajeti ya taifa, rejea
mkutano wa mwisho wa bajeti gharama za ziara hizo zilikuwa ngapi?
Rejea uone hali ya maisha ya mtanzania, hapa nanukuu, kambi ya
upinzani wakieleza hali halisi, soma uelewe,
“18: Mheshimiwa Spika, Mathalan, wananchi wengi wameacha kunywa chai
kwa vile Sukari sasa imekuwa bidhaa ya anasa wastani wa Tshs 1,200/=
hadi 1,800/- wakati mwaka 2005 ilikuwa shs 500/= hadi 600/=, mikate
iliyokuwa kimbilio la walala hoi hasa mijini imekuwa haishikiki tena
kwa vile bei ya mkate unakimbilia shs 1,500/= hadi 2,000/=. Nyama
inazidi kuwa hadithi ya kusadikika kwa Watanzania wengi kwani bei ya
kilo inakimbilia zaidi ya shs 4,500-5,000/- katika maeneo mengi.
Mchele ambao ukiacha mahindi unakuwa chakula cha Watanzania wengi
unakimbilia Tshs 1,500/ kwa kilo” Dr. Slaa kwa niaba ya upinzani
bungeni, kwa kuwa niko vijijini, niongezee hata mafuta ya taa
yaliyowezekana kwa watanzania wengi kununua kwa serikali ya awamu ya
kwanza leo ni ndoto kwa kaya nyingi vijiji, wanawasha gogo ili
waangaze kaya.
Ndugu labda nikuite mhe. Maana tunakutana kwenye mtandao naona walau
unaelewa kuuchapa, lakini wenzako tumepitia media, kama mtaalam huwezi
kutangaza kwa upendeleo wakati huu wa kampeni, kama watangaza kwa
chama kimoja unapaswa kufanya kwa wote wanaogombania uongozi, habari
ya kuwa jamani fisadi aitwe kondoo siyo kweli; hapo mnawafanya
watanzania zezeta, wanayo haki kutaka kujua ya viongozi wao ili
wawachague viongozi bora na si bora tu kiongozi, kama wewe umeibia
taifa hatuwezi kamwe kukusilimisha, au kukubatiza mtakatifu;
haiwezekani, hapo chombo cha habari kinapokata matangazo tena cha uma
kinachochea vurugu zisizo za lazima, na kamwe tusiimbe amani maana
amani siyo kulinda maslahi ya vyama Fulani na maovu yao, bali utawala
bora na maadili ya viongozi kwa faida ya raia. Hivi sasa TBC inapaswa
kuchunga uzalendo na utawala bora kwa manufaa ya Taifa na si maslahi
ya kundi na viongozi Fulani tu! Wenyewe ni chombo cha uma yaani walipa
kodi wote, wenye vyama na uma mkubwa zaidi usio na wala chama maadam
ni raia wa nchi hii wenye haki sawa kikatiba.
Ya anayejifahamisha ni mama wa taifa, kule marekani sawa; je kwa
katiba ya Tanzania yameandikwa wapi tusiende kwa vionjo bali kwa
katiba dola haiongozi kwa ndoto bali katiba; watanzania tuna haki
kuipigia kelele swala hilo mpaka katiba iwe wazi kwa hilo na katiba
siyo siri sirini ni kwa raia wote, ndiyo maana enzi za mzee Ruksa,
Mwalimu ameshakemea uongozi akisema mkeo anakuambia neno, nawe kesho
yake waileta hadharani ati ndiyo sera ya wapi hiyo; huo ni uswahili na
sio uongozi, kamwe!
Kwako wewe naona uongozi labda ni aina ya ibada hata ukikosea
usikosolewe, je tunaongozwa na malaika sio? Kwa maana demokrasia
sahihi uongozi huchaguliwa, maana yake hutumwa na raia kwa kazi maalum
ya muda Fulani unaoelekezwa na katiba ya nchi husika je hapa kwetu
tuulinde kwa mtutu ili ubaki tu; hata kama unakosea? Je siyo haki ya
wananchi kukuacha jukwaani kama mawazo yako hayakidhi haja zao
kimaendeleo? Nini maana ya uhuru wa kujieleza unaotajwa katika katiba
ya nchi Ibara ya 20, aya ya 4. Pole unasema unashindwa kuzungumzia
yaliyotokea Mbulu kwa sababu yanaingilia maslahi unayoonesha kulinda
na kuyapigania na ambayo mimi nasema si ya kidemokrasia
Mwisho hata yale majina magumu ya Russia huwa hayakosewi jina langu
BARHE ni haki yangu toka kwa wazazi liandike vizuri na kamwe kwa
maswala ya katiba ya nchi na uraia wangu sitanii, mi kwanza raia na
baadaye mengine! niliona uhuru wa Taifa langu toka kwa wakoloni, na
kamwe sibabaiki nao hata kama wanatokea wakoloni weusi mamboleo hao ni
wabaya zaidi maana wanadidimiza nchi; raia wakabaki waombaji katika
nchi yao, nao wakatumia umasikini kama tija yao kubakia madarakani kwa
kugawa mali ile ile ile iliyo kodi ya wavuja jasho na wakesha bure…
kama mawazo yanawasha pole ni haki yangu kikatiba kuzungumzia
yanayohusu nchi yangu kwa ajili ya wale ambao hawakubahatika kupata
elimu hiyo ya kiraia ambayo ni haki yao; mwisho nawaambia viongozi
wanaogombania wa ccm watokee hadharani mbele ya waandishi wa TBC
walumbane na wenzao wanaoitwa wa vyama ati vya upinzani, si vya
upinzani bali vyama mbadala kuongoza chama tawala kinapotukwamisha
kama sasa; maendeleo kiduchu, na kujaza ubinafsi kwa kuiita ati soko
huria…. na mengineyo….
special menu for georgejinasa…
Mheshimiwa Barhe kwamza niwie radhi kwa kukosea jina lako. Pili niwie radhi kwa makosa mengine ya kilugha.
Pia naomba kuweka wazi kwamba nemesikitishwa kwa kuitwa majina mabaya kama mpenda Takrima kwa sababu tu ya tofauti zetu za msingi za kimitizamo ya kisiasa. Ningeshauri ili tuboreshe mjadala wetu tujilazimishe kuvumiliana.
Hamna anaesema kwamba CCM haina mapungufu. Ninachosema ni kwamba CCM imefanya mambo mengi mazuri licha ya mapungufu yake. Mimi sichukii CHADEMA wala chama chochote cha upinzani. Ninachopingana na washabiki wa DR SLAA ni kwamba DR SLAA na CHADEMA bado hawajaonesha uwezo wa kukabidhiwa dola na sababu kubwa ikiwa ni kwamba chama chao bado hakijawa na sura ya kitaifa. Naomba urejee maandiko yangu.
Tofauti ya Indonesia na Tanzania niliitoa kwa makusudi mazima ya kuhoji mantiki ya kupima mafanikio ya serikali ya CCM kwa kufananisha na Indonesia. Hoja ya msingi haikuwa tu tarehe ya kupata uhuru bali kuna nukta nyingi mhimu nilizozigusia. Nimejaribu kugusia historia ya uchumi na siasa kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni na tofauti yake na Tanzania. Aidha, nimegusia abarikio wao wa ardhi nzuri, madini, mafuta, gesi ya asili, maji, idadi kubwa ya watu na mambo mengi ambayo hayawezi kufananishwa na Tanzania.
Kama ilivyo kweli kwamba Tanzania ya mwaka 1985 haiwezi kufananishwa na Indonesia ya mwaka huo, ni ukweli huo huo kwamba Tanzania ya mwaka 2010 haiwezi kulinganishwa na Indonesia ya mwaka 2010. Sio Kikwete wala Mkapa anaweza kulaumiwa wa tofauti hiyo. Hata kama mwalimu Nyerere angetawala hadi leo Tanzania ya leo isingeweza kulinganishwa na Indonesia. Nimemtaja baba wa Taifa kwa makusudi kabisa kwa kuwa sera ya CHADEMA ni kuirudisha Tanzania kama enzi za mwalimu.
Kongo ni moja kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa utajili wa madini na ni moja kati ya nchi tano masikini kuliko zote duniani. Leo ikitokea Serikali nzuri ikatawala kwa kipindi cha miaka mitano inaweza ikalaumiwa kwa kutokuwa sawa na Tanzania bila kuangalia historia ya nchi?
Mimi sio mtaalamu wa uchumi ni kweli. Hata hivyo, ninataarifa za kutosha kuunga mkono ukweli kwamba mfumuko wa bei tulionao leo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na mtikisiko wa uchumi ulioikumba dunia hivi karibuni. Nafahamu kwamba nchi nyingine nyingi za kiafrika zinakumbana na tatizo hili japo kwa kiwango tofauti. Kwa mtu anaefuatilia vizuri maendeleo ya nchi atagundua kwamba mfumuko wa bei Tanzania umebaki katika tarakimu moja toka 2000 hadi mwanzoni mwa 2008. Ongezeko kubwa la mfumuko wa bei lilianzia mwaka 2008, mwaka ambao mtikisiko wa uchumi duniani ulianza kusambaa katika sehemu nyingi za dunia. Moja kati ya sekta zilizoathiriwa sana na mfumuko wa bei ni sekta ya madini ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.
Kupigani uundwaji wa Katiba mpya ni jambo jema ambalo hata mimi naliunga mkono. Tofauti yangu na DR SLAA ni kwamba hawezi kuwahakikishia wananchi kuandika Katiba kwa muda wa siku mia wakati hajasimamisha wagombea ubunge hata asilimia 40. Pia muda wenyewe wa siku 100 hautoshi kuandika Katiba mpya. Katiba ya kuandikwa kwa papala namna hiyo bila kupata maoni ya kutosha ya watu haina maana yoyote. Uganda waliokuwa wa kwanza kuandika katiba mpya Afrika mashariki toka dunia ilipoingia upepo wa mabadiliko ya siasa wako wapi kidemokrasia kama suala nikukimbilia kuandika Katiba mpya bila kuweka misingi mizuri?
Suala la Mbulu hoja yangu ilikuwa ni fupi. Kwamba sina taarifa za kutosha kuweza kulijadili, Nililiacha kwa wachangia wenye taarifa kulijadili kwani sio vizuri kujadili suala usilolijua. Sikuweza kukuamini au kutokuamini katika madai yako kutokana na ushabiki wako kwa CHADEMA na DR SLAA.
Mimi sipendelei CCM wala siichukii CHADEMA tofauti na madai yako. Tofauti yangu nawe ni kwamba kwa mtizamo wangu CHADEMA bado hakijawa na uwezo wa kuchukua dola maana bado hakijaweza kuchukua sura ya kitaifa. Nimekuwa nikishauri siku zote kwamba CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wajizatiti ili wawezi kijipenyeza katika sehemu zote za nchi badala ya kungojea kipindi cha uchaguzi. Mtu mwenye chuki na CHADEMA au upinzani hawezi kutoa ushauri mzuri kama huo.
Suala la CHADEMA kutokuwa na ofisi ya kuridhisha ya kitaifa na katika mkoa nimelizungumzia katika kujenga hoja kwamba viongozi wa CHADEMA hawajawa makini.Mahali unapofanyia kazi ndio mtaji wenyewe wa chama. Huwezi kutegemea kuchukua dola kama ofisi za chama katika sehemu nyingi za nchi ni magari yanayopita kipindi cha kampeni na vipaza sauti. Ofisi ya makao makuu ya chama inatakiwa kufanana fananana na chama kinachotaka kuchukua nchi katika dunia ya leo. Nyerere kutokuwa na nyumba ya familia hata kama ni kweli hakuhusiani na hoja yangu maana CCM imekuwa na ofisi zake nzuri katika sehemu zote za nchi palipo na watu.
Vyama kutumia ndege kwaajili ya kampeni katika nchi masikini kama Tanzania na vyama masikini kama CCM na CHADEMA nakubaliana nawewe haileti picha nzuri. Mamilioni hayo ya fedha kama wangepewa wagombea wa ubunge na udiwani wangefika sehemu nyingi za nchi, Nawashauri CCM na CHADEMA katika uchaguzi ujao waachane na midege na wapite kwa njia ya nchi na maji katika sehemu zote za nchi ili waone hali halisi.
TBC kukatisha matangazo ya kampeni za CHADEMA maelezo mengi tofauti yameshatolewa. Viongozi wa Chadema na TBC walikaa na kuongea wanayoyajua wenyewe hatimaye matangazo yakaendelea. Naamini TBC wamekusikia na kama walifanya makusudi watajirekebisha. Ushauri wangu kwa TBC na vyombo vingine vya dola ni kutoa habari bila upendeleo wala ushabiki wowote wa kisiasa.
Mawazo yako hayawashi bali yanatoa changamoto na kuchangamsha mjadala. Napenda nikuponeze kwa dhati kwa kujenga hoja zenye mantiki. Naomba tuendelee kupanuana mawazo na nakubaliana na wewe kwamba katika mjadala wetu kipaumbele kiwe ni uzalendo na maslahi ya Taifa.
Namshukuru mungu kuwa kuna watu wanao weza kutathmini na kupima mambo muhimu nchi hii na hatimaye kutoa mchango wao Mungu atusaidie
Mimi naungana na bwana george,madaraka na kibibi na wengine wote wanao ona kuwa CCM bado inanafasi na uwezo wa kipekee kuiongoza nchi hii tofauti na chama kingine chochote cha upinzani kwa sasa.
Nikiingia kwenye hoja naanza kwa kusema mwalimu mzuri ni yule anayemfundisha asiyejua ili ajue haijalishi baya au zuri mradi tu kafundisha, pili ii hali niionayo ya kukosoa serikali iliyopo madarakani kwa wanaodhani wapo sawa ina ukweli mmja tu kuwa wanakosoa vitu vilivyo tendeka na vinaonekana isitoshe ni vingi mno ndio maana sitegemei kama wata maliza kwa kipindi hiki tu cha kampain. so bwana george usiogope wao kubeza nikwakuwa vipo vya kubezwa japo kinafki, nimemfuatilia sana Dr. ukweli nikuwa hana mkakati thabit wa kuiletea maendeleo hii nchi zaidi sana ana vipaumbele vitatu rasilimali ya nchi ufisadi na katiba. Dr. anapaswa kuelewa kuwa nchi ni zaidi ya hayo na sio suala la kuamka tu na kuigeuza tanzania kuwa peponi, jambo zito kama katiba linahitaji watu makini na wasio na pupa kwani linahitaji fikra zilizo komaa na muda wa kufanya uamuzi sahihi, na sio kusukumwa na hoja laini za mtu moja. Pili J.K ameonyesha njia kwa walao kuyashawishi makampuni ya wawekezaji kulipa kodi, jambo ambalo halikuwepo hapo awali, natamani watu wangeruhusiwa kuona mikataba J.K aliyoikuta mezani naamini yeye mwenyewe alistaajabu nakujiuliza kama kweli waliofanya vile ni watanzani kweli au la?, kwasababu kuigusa ni kuifilisi nchi au kuiingiza nchi kwenye hasara ya milele hivyo basi alicho kifanya kuwaita na kuwaomba ni jambo la kiungwana na tunapaswa kumuunga mkono Raisi wetu. Nionavyo mimi Dr. na mbwembwe hizi lazma angechemsha.
Hebu fikiria EU imechukua zaidi ya miaka 60 kuwa hivi ilivyo leo kwani naona wengi wana watukuza sana hawa jamaa, itakuwa CCM na mzigo wa idadi ya watu wasio na shule kwa hatua hizi walizofikia? watu wanapaswa kuelewa kwamba idadi ya wasomi inaendelea kuongezeka na hatimaye tutafika tunapo taka kwenda. China ya leo ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa jana nasio malumbano na kutokuwa makini kwa vyama vya upinzani.
Unaweza kusema utakavyo kuhusu CCM lakini jiulize swali hili wewe umefanya nini kuikomboa nchi hii kwa nafasi yako pale ulipoona mapungufu bila kusubiri uchaguzi kwani inawezekana ikaharibika zaidi? Pili kama kweli Dr ana majina na ushaidi wa mafisadi ni kwanini asiwapeleke mahakamani kwakuwa ana uchungu na rasilimali zetu? nitarudi…………
Uvumilivu ilio nao CCM na kwambia hakuna mtu hata mimi si wezi kwani wanao tathmini na kukosa uvumilivu mi naomba ni wakumbushe kuwa sio kwamba CCM na viongo zi wake hawawezi kutenda haya yote ila ni kwa faida ya watu wangapi? na wana mchango gani kwa maendeleo ya nchi hii? hebu fikiri serikali ya CCM imevumilia kusomesha wananchi wake bure ili kuwapata wasomi kwa kuanza watakao shika hatamu na ndio mwendo wake hadi sasa likini eti tu kwakuwa umesoma na sasa unajua kukosoa unakosa subira ya kusubiri zaidi ya asilimia 60% wenzako wasio na shule nao wapate eti tu kwakuwa unataka mabadiliko, naomba muelewe CCM sio mabadiliko inahitaji ila ni mapinduzi ya kuwakomboa hawa 60% kwani ndio wengi na wakisonga hawa nchi imesogea,
Swali kwa wanao ungana na Dr. DR. alipo ingia madarakani 1995 karatu ilikuwa na michango jumla 13,000 kwa mwaka kwa ujumla leo ina jumla ya zaidi yaTsh 193,000 kwa mwaka pili CHADEMA wanapokea ruzuku ya zaidi ya Tsh 320 milioni kutoka serikalini kwa mwezi na hawana hata mfuko wa kusaidia watoto haohao wanao danganya watawasomesha bure? tatu kwanini hata katibu wao wa mkoa wa manyara ngugu…… hawamlipi sababu pesa hazitoshi, nne kwanini hawakumpa mgombea ubunge arumeru magharibi fungu kwa kisingizio kuwa hawatashinda ila ajigharamie kisha watamrudishia akishinda? je pesa hizo ambazo sasa hawana za kumpa watazitoa wapi wakishinda? na je kwakuwa tayari halmashauri kuu ya CHADEMA iliona kuwa haita shinda jihusika ni kwanini wanakubali kumtia mwenzio hasara kwani nikweli hatashinda.
CCM nikweli haijui majibu ya matatizo ya watanzani wote lakini inajua njia bora ya kutafuta sio tu majibu bali suluhisho la muda mrefu na lakudumu la matatizo hayo.
kuna hoja ya kutoa elimu na afya bure Dr akadanganye wengine sio mimi hakuna uendeshaji wowote wa serikali duniani ambao hautegemei kodi kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa kuwa Dr. na timu yake wataongeza kodi kwa sehemu ambazo intresti zao hazipo na kuwaumiza watanzania kwa mlango wa uwani. Kama haitoshi CHADEMA imeshindwa kuwa na uwiano sahihi wa usawa na kitaifa mfano katika viti maalum walivyopewa 12 kati ya 20 ni watu kutoka kilimanjaro sasa kwa misingi hii tujifunze nini kwao?
Ndugu John Samson,
Ni kweli CCM imefanya mengi mazuri mengi, lazidi ni kuiweka Tanzania kuwa Taifa huru, papo hapo umeeleza kuwa Ndugu JK alipoingia madarakani alikuta mizengwe mizani na kutokuamini macho yake kuwa wale waliotia sahihi mkataba hiyo walikuwa w Tanzanai kweli ma…. kujua wazi kwamba wangaliiweka nchi hii kuwa maskini milele…….! Kama nimekunukuu sawa nadhani ni hilo. na kama si sawa, naomba radhi na unisahihishe.
Hoja yangu ni hii;-
Waliotia sahahi mikataba jeneza kwa Tanzania waliomtangulia JK (kulingana na usemi wako)
Ni Wana CCM na CCM ndiye Mdhamini :Steward” wa wale waliomtangulia JK ni pampoja na JK mwenyewe.
JK na CCM wamefanya lipi kurejesha kwa wananchi malizilioporwa na kwa ridhaa yao dhidi ya Wananchi? Wananchi wanasuasua
ktk nchi yao kama Mkimbizi ambaye hajaonyeshwa kambi!
Hapo awali nilisema, …. CCM inaishi ktk Sayari nyingine tofauti kabisa na hapa tulipo kama haioni haya tunayoyaona ya Watanzania kusuasua na maisha ktk nchi yenye neema na madini ya jabu ambayo kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, ameonesha upendeleo wa pekee kwa nchi hii ukilinganisha na cnchi nyibgine.
La ZAIDI NA ZAIDI, NI ROHO YA IMANI NA AMANI
AMANI, AMANI, AMANI AMBAYO NCHI NYINGI ZIMEKOSA.
Kila kukicha Baba/Mama anainua mikono juu na kuomba dua “Anajua Mungu!”
Tusichukulie kwa mzaha neno hili kwamba tunaitwa “An Island of Peace”
Let us not take it for granted without each one and every one fulfilling our noble responsibility to one another”
Siku moja nilipamda ndge iliyopotea njia
tukaenda ufukweni mwa bahari ya Hindi, nilipotupa macho dirishani, sikuamini macho maaju ya yale niliyoona Masaki, na kule kwingineko kama majumba hayo yako Tanzanaia na yanamilikiwa na Watanzania!
Jioni nilikwenda Manzese kuona hali halisi ya Mtanzania, jioni nikaona kwenye TV bomba maji machafu (sewerage) iliyopasuka ina kutana na bomba la maji ya kunywa.
Kipindupindu kimepamba moto, Wana Afya wanatangaza tuchemshe maji ya kunywa, Mama wa Manzese ama Buguruni mwenye famile ya watoto 6 na wtoto wa Marehemu nduguye na ndugu wengine, apate wapi kuni za kuchemshia maji ya kutoshereza famile hiyo, wakati bei ya mafuta ya taa haishikiki!
Mara mmoja anaanza kuharisha, maji ya kusafisha mazingira adimu, anapelekwa hspitali, drip haizipatikani, hadi utoe chau chau kwa mweka drip zaidi na zaidi wamezingirwa na wingi wa wagonjwa, wengi wanafia kwenye stretcher.
Tuseme mangapi?
Rai yangu ni kuipumzisha CCM, kwasababu CCM bin TANU imetuletea U Tanzania, kwa hiyo ni lazima tutawaliwe na CCM daima uli kuonyesha fadhila? Si dhani kama hoja ya msingi ni hiyo.
Malumbano yanaendelea!
Na tutangaze basi kuwa ni chama cha MAISHA kama watawala wengine walivyojitangaza kuwa ni wa MILELE NA MILELE!
Hoja hapa sio kwamba CCM haina mapungufu. Bwana Samson amejitahidi kufafania vizuri kama nilivyofanya hapo kabla kwamba CCM kama vilivyo vyama vyote na serikali zote duniani vina mapungufu. Tofauti ya hoja zetu na za wale wa kambi ya DR SLAA ni kwamba wao wamekuwa wepesi wa kujadili mapungufu tu. Kila tunapoonyesha mafanikio wamekuwa wakifumba macho kana kwamba hawayaoni. Tofauti nyingine wameamua kumfagilia DR SLAA bila kuwa na kigezo chochote cha maana cha uwezo wake na chama chake kuchukua dola. Tumekuwa tukionesha udhaifu wa msingi kabisa wa CHADEMA na DR SLAA bila kupata upinzani wowote kutoka katika kambi ya akina Kibibi.
Lazima tukubaliane kuchukua dola sio suala raisi kama kuongelea uwezo wa kuchukua dola. Ni kosa ambalo linaweza likaigarimu Tanzania kwa miaka mingi. Amani na umoja wa kitaifa japo wengine tunaitamka kiwepesi sana ni kitu chenye thamani na siri kubwa ya maisha yetu watanzania.
Hamna anaesema CCM itatawala milele. Tunachosema ni kwamba CHADEMA kama vilivyo vyama vingine vya upinzani havijaonesha umakini wa kuweza kuaminiwa kukabidhiwa nchi. Kama vitabaki katika hali hiyo kweli CCM itatawala muda mrefu sana.
Ndugu George Jinasa, ktk hoja yako ya Sept 22 2010 ulininukuu kuwa nilisema Ds. Slaa alihojiwa na BBC, la nilisema BC (BongoCelebrity) siyo BBC.
Ndugu Andras Frisk Aug 17 2010 alinukuu maneno ya Hayati Horace Kolimba; nanukuu!
“CCM imezeeka haina dira wala mwelekeo”
Akatungiwa wimbo. nanukuu;
“ASIYEMPENDA HORACE KOLIMBA SIYO RAIA WA TANZANIA” Hajasema ni wasanii gani waliotunga wimbo huu, bila shaka ni wana CCM wenyewe, sijui!
Kolimba yuko wapi sasa?
Nilitaka tu kutoa masahihisho machache juu ya mdahalo wetu.
Ukweli wa mambo ni kwamba Pamoja na mazuri yote yaliyoletwa na CCM, pia tusisahau kuwa
wananchi na imani yao na uvumilivu wao, wao ndio wanaopaswa kushukuriwa kuliko CCM.
CCM ina uwezo wa pekee kumaliza ufukara wote wa Tanzania wangekuwa na mtazamo wa uchungu kwa wanachi “Lacking the POLITICAL WILL!”
ndiyo imetufikisha hapa tulipo.
Jana nimesoma magazeti yanaeleza jinsi wananchi wamelazimishwa kuishi ktk mazingira ya dump pamoja na uoza, ni pamoja na mizoga ya wanyama, kinyesi, na maji machafu, wafanye nini? Waende wapi na wamlilie nani?
Swali langu halima maana ya kukashifu CCM la linatoka moyoni kama mzazi kuwa:Je CCM haioni hayo na imachukua hatua gani kuwalinda na kuwanusuru wananchi wake na majanga yasiyokuwa na lazima ya kuwapata?
Kama kijana wao waliyemweka madarakani kuongoza nchi, amezidiwa na uzito, CCM chama cha nchi nzima, kina Makada kila kona, imeshindwa kweli kudhibiti maovu hayo? Ama haioni kama wengine tunavyoona!Narudia usemi wangu kuwa “Basi CCM inaishi kwenye Sayari nyingine tofauti na hapa tulipo wanachama wake na wanachi wake.
Jambo jingine aliloulizwa Dr. Slaa ktk mahojiano yake na BC, ni kuhusu usalama wake.
(Ni kweli nguvu za Giza zipo).
Kwa imani alijibu, kuwa anamwachia yote Mungu ndiye mlinzi wake, akatoa mfano halisi kuwa Hayati John Kennedy, pamoja na kuzungukwa na FBI na CIA nguvu za Giza zilifanya walichokiwania. Kwa hiyi mimi Kibibi, kwa imani kuu nasema; tumweke
Dr. Slaa mikononi mwake Mwenyezi Mungu AMINA AMEN!
Nimitizamo tu inayo pishana hapa na kambi ya Dr. ndugu yangu Kibibi unapaswa kuelewa kuwa JK alikuwapo ila ana nafasi gani na nguvu gani ya kushauri wakuu wake? unataka kuniambia hakufanya hivyo? Kama ulimsikiliza vizuri Mhe;Rais katika hotuba yake ya kufungua bunge Dec 2005. Utagundua kabisa kuwa Mhe; Rais alikuwa na uchungu na nchi hiii na kuna mambo ambayo aliona kuwa yalifanyika sio kwa kiwango cha juu na yali hitaji kuboreshwa na ndo sababu ya yeye kupitia hayo aliyo ya fanya.
Pili JK sikatai kama hana mapungufu ila ukiweka kwenye mizani yeye ni bora zaidi kuliko aliyemtangulia, hebu fikiri kuhusu mfumuko wa bei ambao JK anahukumiwa? swala hilo sio lake ni la kiuchumi zaidi, MKAPA alishikilia mfumuko wa bei na kuiuza nchi hii kwa asilimia kubwa na alifanya hivyo makusudi kabisa kwakuwa ugumu wa maisha kwa mwanzo kabisa unamgusa mwananchi wa kawaida kwenye fedha. Naomba kibibi na kambi yake ya Dr. waniambie kama Rais ndo anashusha thamani ya shilingi? kwakuwa kama ndiye baai yetu ingekuwa juu mno kwani ni nani anayetaka kuwa chini?
Tatu nimeonyesha ni kwa jinsi kani CHADEMA na viongozi wake walivyo shindwa kubajet ruzuku yao kutoka serikalini pesa hizihizi za walipa kodi wanao taka kutuambia wanawatetea kwa kuzifaidi watu wachache. ninacho kiona kwa CHADEMA ni wazuri wa kukosoa na wajasiri wa kusema kwa hilo na wapongeza, ila ni wabovu kuliko kwenye upangaji na utekelezaji wa mipango yao wenyewe. Nlisema hili kwakuzingatia yafuatayo (a), wameshindwa kujipanga nchi nzima badala yake wanataka kutuburuza tulio wengi kwa matakwa yao. (b), wana mbinu chafu mno za kutafuta madaraka kwa kuwa hadaa walio na nafasi ya kuwasikia na kuwaona kama ambavyo sasa hawapigi kampein wanashindana na SYNOVATE hivi kweli Dr. na kambi yake wameishiwa kiasi wanataka kuwa viongozi wa nchi hii kwa takwimu za maoni ya wachache wenye nafasi ya kukutana na SYNOVATE? hivi kweli wanafikiri tutatawaliwa ushawishi wa maneno yao au na utafiti wa SYNOVATE? Kwanini wasi elekeze muda wao mwingi na nguvu zao kwenda wasikojulikana ambako ni zaidi ya mikoa 25?
Naomba kambi ya slaa ielewe kuwa nchi hii haitaongozwa kwa maamuzi ya watu wachache wenye jazba kutoka mikoa mitano. Kisha kambi ya Dr. wanapaswa kuelewa kuwa inawezekana wao wameona umuhimu wa kubadilika sasa kitu ambacho hata mimi nipo nao kwa hilo. ila sasa tubadilike vipi na kwanini? na nini hasa tukibadilishe na tunataka kiwe na sura ipi? na kwa utaratibu upi? na ni nani wa kuleta mabadiliko hayo? ndo napingana na Dr. na washirika wake, kwakuwa dawa ya tatizo ni kulitatu na sio kulikimbia tatizo kama wanavyo fanya kuondoka CCM na kujiunga CHADEMA kwa kisingizio cha mabadiliko basi haja ya mabadiliko tayari umeshaitimiza kwani kiitikadi tayari umeshabadilika?
Niwazi kuwa mabadiliko ya kweli na mapinduzi yanaweza kufanyika sio tu na CCM chama chochote kinaweza kufanya hivyo ila sasa sio CHADEMA wala CUF labda CCM imguke. Ninachoofia mapinzani wanaweza kubeba dhana ya upinzani hata kwa maendeleo yao wenyewe, kama haitoshi wana weza kushika hatamu halafu kwakuwa tu wana dhana ya upinzani wakatumia muda mwingi kupinga kuliko kupanga na kutekeleza,
nipo
Inashangaza kweli kuona ni jinsi gani watu wengi hawaoni tena mbali (wamekuwa myopic). Kwa sasa, upinzani, hususan Dk. Slaa ndilo tumaini pekee. Utamaduni na utendaji katika serikali ya CCM umeharibika kiasi kwamba haiwezekani marekebisho yakatokea ndani mwao.
Lakini inashangaza kuwa watu wengi hawaoni hivyo! Nadhani hizi ndizo athari za kuporomoka kwa maadili – kwa vile utamaduni wa udanganyifu, rushwa n.k. ili kujitajirisha haraka-haraka umeota mizizi. Hivyo anayedanganywa kwa vijisenti kidogo anapofuka kabisa haoni ukweli!
Haiingii akilini, kwa mfano, mtu aliyesomeshwa bure kwa fedha za Watanzania masikini ndiye akuambie kuwa sera ya elimu bure haitekelezeki! Kama si kwa sababu ya maslahi binafsi mwenye elimimu ya bure ya Mwalimu Nyerere hawezi kuwa na ujasri wa kusema eti elimu bure haiwezekani.
Ndugu zangu mnaosema eti Dk. Slaa hajakomaa, msidanganyike! Labda kama mna maana ya ukomavu katika ufisadi – hapo kweli hajakomaa.
Msidanganike na vijiposho au ulaghai kuwa upinzani ukichaguliwa una “madhara kwa amani na utulivu” ulaghai na kasumba inayoshindiliwa kwenye akili za Watanzania.
2010 HATUDANGANYIKI!
Naomba nitofautishe ugumu wa maisha na serikali ya JK nimeona watu wengi zaidi wakihoji kuhusu ugumu wa maisha na kushabihisha hali hiyo na uongozi uliopo madarakani kwa asilimia 100%, kautafiti kadogo tu nilicho kafanya nimegundu mambo yafuatayo;-
-wengi hawakuweza kukidhi ushindani pale walipo takiwa kufanya hivyo kwa kusudio la kushinda fursa flani iliyotokea. Mfano wengi wa wafuasi wa Dr. ni raia ambao eidha alikosa kitu flani wakati flani alipo jaribu kukitafuta, kama kazi, huduma flani serikalini, au kwa uvivu wake tu wa kufikiri na kubweteka kusubiri muujiza umfikie wa maisha bora bila kujishughulisha anatafuta pa kujituza kwa kisingizio kuwa serikali ndo sababu ya yeye kuwa hivyo. Kitu ambacho ni wazi ni ufinyu wa kutathmini na kupambanua mambo. Huwezi kuacha makusudi shule kwa tamaa ya pesa kisha leo utoe milio ya hakuna kazi hainiingii akilini. Kama hujasoma na huwezi kuwa Daktari au Engineer basi elekea kwenye kazi za mikono kwani ndio halali yako kwa nafasi uliyo nayo, nasio kutumia muda kupiga soga na vijiwe vya uvutaji wa bangi madawa ya kulevya na vinavyo fanana na hivyo,
-wengi wa hao hupenda vitu vya pupa (harakaharaka) ili tu kukidhi haja na matakwa yao bila kujali madhara wanayo weza kusababisha. Mfano kudiriki kutamka kuwa wakikosa Urais hata msituni wataingia. sasa najiuliza ikiwa mtu yupo tayari kuingia madarakani kwa vita ni hali gani ya usalama kwa raia inayo zingatiwa? Hawaoni wanao pigana wanatafuta maridhiano?
- Wengi wa wanao jiita wanaharakati wa upinzani kwakuwa tu hawana shughuli jambo ambalo CCM na serikali yake haihusiki kwani wao wameshatekeleza kwa nafasi yao kwa kuweka FURSA wazi kwa wanao weza wshindanie na kuandaa ardhi kubwa ili kwa sisi ambao makusudi tulikimbia shule tukalime, tusitumie mwanya wa kutokuwa na taaluma kukubali kutumika isivyo. Kwa kushawishiwa kufuatanafuatana kishabiki na mbwembwe nyingi kwamatumaini ya kutatua matatizo yetu, naomba waelewe kuwa ni kwakuwa tu tulio wengi hatutaki kupayuka hovyo na kushindana kwa kupinga na kukashifu na kubeza ukweli ni kuwa tuna muda wa kutathmini na kupiga kura kuchagua viongozi bora hivyo ndugu yangu GEORGE tusonge mbele kaka.
nitarudi bado ni kaubusy na majukumu tu
Nipo na kamuda kidogo naendelea kujenga hoja juu ya ninacho kiona kuwa ni sahihi
bado nipo na Mhe; Rais JK na serikali yake najikita zaidi na timu yake kwa wakati huu ni wazi kuwa Mhe; ana utitiri watu wengi wenye mitizamo na utashi tofauti japo wapo kwenye mashua. Alichokifanya JK ni kuwapunguza mmoja mmoja kwenye system ili kujenga misingi imara ya utekelezaji wa sera sahihi kwa maendeleo ya nchi yetu ona mambo yafuatayo;-
-kuwashawishi vigogo kama akina MUNGAI, MRAMBA, KINGUNGE, DIALO, MEGJI ZAKIA, na wengineo wengi ambao kwa mtazomo wa tusio wajua wameharibu kuondoka ktk system bila kuleta mtafaruku kwani wazi kuwa wana nguvu ndani ya chama nasi tunaliona hilo lazima utakuwa na kipaji cha kipee kulikamilisha hili.
-Haya ndo mambo ambayo naona kuwa Dr. hawezi kufananishwa na JK na Dr. kipaji hiki cha kutenda hana ila ana cha kuzungumza tu, ndo mana hakuna aliyethubutu kuniambia kuwa ruzuku ya zaidi ya 320 milioni wanaitumiaje? kwani nimeeleza ruzuku ya CCM wanavyo rudisha fadhila kwa wananchi wao kama kusomesha watoto kulea, wazee, wajane na kutoa matibabu bure kwa jamii zisizo jiweza haya yote hamwoni! ni kupiga domo tu siku nzima kwa mabaya midomo itazoea alafu mtakuwa mafundi wa kutengeneza mabaya.
-viongozi wengi ndani ya chama sasa wameanza kubadilika na ndicho kitu cha msingi, kuanza kuweka utaifa mbele na maslai ya nchi ni jambo la msingi sana, ieleweke kuwa CCM ina wanachama wengi na viongozi wengi zaidi kuliko chama chochote hapa nchi, hivyo kwa kupendelewa kwa mazingira hayo ni wazi kuwa wasio na nia njema pia idadi yao itakuwa nikubwa kuliko ilivyo kwingine. hivyo huwezi kutoa hukumu ya wabaya 100 kati ya timu ya watu 1,000,000 halafu ukawapongeza wenye wabaya 10 kati ya watu 100. lazma utakuwa huwazi vizuri.
-Japo serikali iliyopo madarakani ina mapungufu yake lakini madhara ni madogo kuliko mapungufu ninayo yaona CHADEMA au CUF yakipewa madaraka ya kuiongoza dola. Ninacho tahadharisha ni ukubwa wa eneo linalo zungumziwa na uwezo wa timu kumili eneo husika.
Ndugu Kibibi hatuichukulii amani ya nchi for granted japo tunajua umhimu wa amani na utulivu katika maisha ya mwanaadamu.
Kuwepo kwa majumba ya hali ya juu masaki na mbezi kwa upande mmoja na majumba ya hali ya kimasikini katika sehemu nyingine, ni moja katika changamoto za maisha ambazo hatuwezi kuzikwepa. Ndio maana hata katika CHADEMA kuna matajiri wakubwa kama akina Mboe na Ndesambura wenye majumba makubwa kuliko ya Masaki na pia kuna masikini kupindukia. Hali kama hii ipo katika sehemu zote za dunia na imekuwepo toka zama na zama. Hata wewe Kibibi pamoja na wachangiaji wengine unaweza kuwa tajiri mkubwa ukilinganishwa na mtu mwingine na utajiri wako ukabaki halali.
Uwepo wa majumba Masaki haiwezi kuchukuliwa kama ni kushindwa kwa serikali kutekeleza majukumu yake. Tujaribu kutafakari vizuri. Majumba ya Masaki hayakuzuka katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya Kikwete wala nyumba za kimasikini za Manzese na kwingineko. Isitoshe hizo nyumba za Manzese zikipelekwa katika vijiji vilivyopo wilaya ya Nanyumbu zinaweza kuonekana za kifahari sana. Moshi na Arusha kwa kipindi kirefu wamekuwa na mashule mengi ya msingi na sekondari pamoja na majumba mazuri mpaka vijijini. Mikoa mingine kama Mwanza, Dodoma, Kigoma, Singida, Tabora na kadhalika ilikuwa kwa muda mrefu na shule chache sana. Nyumba za kuishi vijijini zilikuwa duni sana. Lakini hili halikuwafanya wananchi waichukie serikali ya CCM wala TANU.
SERA ZA SOKO HURIA TULIZOANZA KUZITEKELEZA RAMSMI MIAKA YA TISINI, NDIO ZILIZOPELEKEA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA SEKTA YA MADINI.
TUKUBALI KWAMBA WAKATI TUNAJIINGIZA KATIKA UWEKEZAJI MKUBWA WA UCHIMBAJI WA MADINI, NCHI YETU ILIKUWA NA UZOEFU MDOGO SANA. MAPUNGUFU KATIKA MIKATABA HII KWA MTIZAMO WANGU YAMECHANGIWA KWA KIASI KIKUBWA NA UCHANGA WETU KATIKA SEKTA YA UZALISHAJI WA MADINI.
KWA HIVI SASA SERIKALI IMECHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI YA KUPITIA UPYA MIKATABA YA MADINI NA SHERIA MPYA YA MADINI IMESHAANDIKWA.PIA FANI YA MIAMBA NA MADINI IMEANZA KUTOLEWA KWA VIWANGO VIZURI KATIKA VYUO VYAO. HILI LITAPUNGUZA TATIZO. TATIZO LA MADINI SIO TU SUALA LA MIKATABA LAKINI ZAIDI NI LA KIMTAJI NA TEKINOLOGIA. BILA YA KUWA NA MTAJI NA TEKINOLOGIA TUTAENDELEA KUPUNJIKA.
WACHANGIAJI TUNATAKA KUCHUKUA NAFASI YA WATU WENGI KAMA VILE TUNARIDHAA YA KUWASEMEA. HAYA TUNAYOYASEMA NI HOJA NA MITIZAMO YETU BINAFSI NA WATU WENYE MISIMAMO KAMA YETU NA SIO LAZIMA SANA KWAMBA INAUNGWA MKONO NA WANANCH WETU WENGI. KIPIMO CHA YOTE NI WAPIGA KURA.
MIAKA MIWILI HAIJAPITA TOKA TUFANYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA. CHADEMA HAKIKUPATA HATA ASILIMIA NNE YA VIONGOZI WOTE. HALI YA MMWAKA MMOJA ULIOPITA HAIJABADILIKA SANA KULINGANISHA NA YA SASA. TUNAKIGEZO KIPI SAHIHI KWAMBA WANANCHI WAMECHOKA NA CCM NA TOKEA LINI?
Tunamtaka Dr. Slaa hatujali chama,hicho chama chenye miziz na ukomavu na ndevu na mvi ndio hicho kimetufikisha hapa ambapo mtanzania unaona hata aibu kujiita mtanzania ukiwa nje ya nchi. Tafuteni na angalieni sinema ya Darwin Nightmare, nimeiona nikiwa Djibouti, ilionyeshwa na TV ya taifa. Ni ile ya mapanki, hutaweza kuamini kwamba viongozi wetu waliiangalia na haikuwagusa zaidi ya kupiga porojo na lugeuza umasikini, ujinga na dhuluma za watanzania kuwaagenda ya kuzungumzia kwenye kahawa. Ni kama Nigeria wailisikia huko Mali kuna kambi za watumwa, mabinti wa kinaijeria wanatumikishwa kwenye ngono, wakatuma watu kuchunguza, wakathibitisha na hata kuongea na hao mabinti eti wanasema waliwaacha vile vile sasa wanaitisha kikao cha mataifa ya Ecowas kujadili tatizo hilo. Hivi ukimkuta binti yako katekwa nyara anabakwa akiwa kageuzwa kitega uchumi eti utaondoka ukaite kikao cha ukoo kujadili jambo hilo? sisi watanzania sasa hivi tumechoka na hatuna haja na hiyo mijadala ya kisomi inayoishia kwenye karatasi, tunataka watu wanaothubutu na kutangulia mbele kama dr, slaa. Hapa ^hakieleweki kitu, tunampa kura na tunaichukua nchi potelea mbali hatuna cha kupoteza zaidi ya umasikini wetu na aibu.
Ningemuelewa na kurudishia JK heshima kama naye angesema anampigia Dr. Slaa kura, hivi nyie hamuoni maandishi ukutani? wakati tunadai uhuru nyie mngesema bado hatustaili maana hatuna hiki na kile, ni kawaida kuogopa mabadiliko sasa tunasema leo ni keo hatutaki kupoteza nafasi hii. Dr.SLAA NDIYE RAISI AJAYE.
Ndugu yangu bwana UHURU nakushukuru kwa kufafanua jambo ambalo nilishindwa kuliweka sawa jana 30/9/2010 kwa lugha nyingine usione watu wameamua kunyamaza nakutojishughulisha na SIASA ukadhani wana wame ichoka CCM nakueleza ukweli kuwa CCM imefanya kazi nzuri na niimani yangu kuwa JK atapita na zaidi ya asilimia 80% tena kwani ninachokiona nikuwa kelele hizi na ushabiki huu ni aina ya milio iliyo wahi kutolewa 1995 na umaarufu wa MREMA kwani yaleyale yaliyo tokea wakati ule ya mbwembwe nyingi huku ukidhani una watu kumbe wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi ya kujitafutia chochote mifukoni na hatuna pakwenda sasa chochote kilichopo mbele yetu ndo kazi yetu? sijui mtaficha wapi nyuso zenu wakati wa matokeo.
Leo nakuja na udhaifu mwingine wa Dr. Bwana GEORGE atanisaidia kama nitakosea Dr. ni mtu jasiri kweli wa kusema ila sio utekelezaji na sababu zangu ni kwanini asianze yeye kuwafikisha mahakamani yeye wahujumu uchumi wa hii nchi kama kweli majina na ushaidi anao? ana msubiri nani afanye hivyo? nakama hawezi anatafuta taarifa hizo kwa sababu zipi? je tukishajua tufaarifa zisizo na ukeli wala hukumu ya mahakama sisi wananchi zinatusaidiaje? na kama hawezi kutenda jambo la kijasiri kwanafasi aliyo nayo atawezaje kutenda akiwa na majukumu makubwa kama RAIS? ukweli ni kuwa Dr. hana majukumu aliyo nayo Mhe; Rais lakini hathubutu mahakamani kwani anajua kuwa hana analoweza kulifanya na anatafuta umaarufu tu wa kupelekwa mahakamani ili ionekane ati na yeye ana weza kitingisha viongozi, JK ni muelewa na anafahamu kuwa anatafuta umaarufu hivyo hawezi kupoteza muda na timu yake kwa kumshughulikia kiumbe mdogo kama slaa.
Slaa sio msikivu ila ni msemaji kama ambavyo CHADEMA ilivyo watoto wa mjini wanasema wana chonga sana, Imani bila matendo ni bure. Fanyenyi kitu thubutuni kumfunga walao mmoja muone kama hatuta waunga mkono JK amefanya LYUMBA yupo ndani mnatakaje?
Jana na juzi nimemsikia DR SLAA akimuandama Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania kwa tahadhari aliyotoa kwa viongozi wa kisiasa na taasisi mbalimbali. Tamko la Mnadhimu Mkuu alilitowa akiongozana na Kamanda wa Polisi muwakilishi katika kitengo cha operation ambacho nijuavyo mimi kinahusisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi na Usalama wa Taifa.
Kwa namna nilivyomsikia Mnadhimu Mkuu na mazingira yaliyojitokeza kabla ya hapo, sijaona tatizo lolote katika tamko lake. Muelekeo wa majeshi yetu ni kuzuia uvunjifu wa amani badala ya kusubiri kuutibu. Huo ni utaratibu mzuri maana ni vigumu sana kuirejesha amani inapotoweka kuliko kuzuia isitoweke. Na amani inapovunjika, majeshi yetu ndiyo yenye dhamna ya kuirejesha. Na wao ndio wanaojua zaidi ugumu wa kurejesha amani.Kama viongozi wa siasa wanatamka baadhi ya maneno yanayoashilia vita, uasi na uvunjifu wa amani kwa ujumla,ni chombo gani makini cha usalama kitakachokaa kimya?
Ningewashauri viongozi wa kisiasa tujikite katika sera zetu badala ya kujiingiza katika malumbano na vyombo vya ulinzi na usalama bila sababu za msingi. Kama tatizo ni kati ya vyama, kwa nini mvihusishe vyombo vya ulinzi na usalama katika malumbano yenu ya kisiasa? Kwa nini kiongozi wa siasa aanze kutamka hamna cha Jeshi la Wananchi wala Polisi?
Vyombo vya ulinzi na usalama vinajukumu la kutuhakikishia ulinzi na usalama wetu. Kwa hali yoyote lazima viwe kila siku vinafanya uchunguzi kuweza kujua hali halisi ya kiusalama. Wanaposema kwamba wana wasiwasi kwamba baadhi ya mambo yakiachwa yanaweza kuvuluga amani, lazima waaminiwe. Na wanabotoa tahadhari kwa wananchi hatuna haja ya kulumbana nao. Wao ndio wenye dhamana ya ulinzi na wenye taarifa sahihi za kitaalamu kuhusiana na hali yetu ya kiusalama. Na dhamana yao ni kwa wananchi wote na vyama vyote. Vyamna vya siasa havina vyombo vyao vya ulinzi na usalama ambavyo vinaweza kuijua na kuitafsiri hali halisi ya usalama Tanzania zaidi ya majeshi yetu.
Bahati nzuri katika taarifa yao hawakutaja jina la chama cha siasa wala kiongozi yoyote. Wao wametoa tahadhari kwa vyama vyote. Ni vyema vyama vyote vikazingatia ushauri wa Jeshi letu.
BWANA SAMWELI WATANZANIA WALIO NJE WANAJIVUNIA UTANZANIA WAO.WANATEMBEA KIFUA MBELE KWAMBA WANATOKA KATIKA NCHI KISIWA CHA AMANI. WALE WACHACHE WANAOJINASIBISHA NA NCHI NYINGINE KAMA RWANDA, BURUNDI, SOMALIA NA KONGO HAWAFANYI HIVYO KWA SABABU YA UDHALILI WA NCHI YETU, BALI NI KWA KUTAKA WAPATE HADHI YA UKIMBIZI. WANAJUA FIKA KWAMBA WAKIJITAMBULISHA KAMA WATANZANIA HAWAWEZI KUPEWA HADHI YA UKIMBIZI KWA MAANA TANZANIA INATAMBULIKA KUWA KISIWA CHA AMANI.
UZEE WA CCM SIONI KAMA NI TATIZO. HATA HUYO RAISI WAKO DR SLAA HAKUTOKA CCM KWA SABABU YA UZEE WA CHAMA. AMETOKA CCM BAADA YA KUTOPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE. HANA TOFAUTI NA AKINA SHIBUDA NA MPENDAZOE.
Ndugu yangu Samsoni uliyosema ni kweli tupu. DR SLAA kama walivyo viongozi wa upinzani waliomtangulia, analitumia suala la ufisadi kama njia ya kupata umaarufu kisiasa. Ndio maana hata siku moja hawawezi kuipongeza serikali inapochukua hatua za kupambana na ufisadi. Badala yake inalaumiwa tu.
CHEDEMA imezungukwa na lundo la wanasheria mahiri. Kama angekuwa serious katika lawama zake, angeshauriwa namna ya kuwafikisha mafisadi Mahakamani. Kumtuhumu mtu ni visadi ni kitu kingine, na kuthibitika kuwa mtu ni visadi ni kitu kingine. Sio lazima kwamba kila atakayetuhumiwa fisadi ni visadi. Wapo wanaoweza kutuhumiwa mafisadi kwa sababu za maslahi ya kisiasa. Ndo maana chini ya mfumo wetu wa haki, mtu hawezi kusemwa ni mhalifu mpaka mahakama imuone kuwa hivyo.
Serikali na vyombo vyake vya dola inajukumu kuzifanyia kazi tuhuma za uhalifu bila kujali zimetolewa na chama gani. Na ndivyo ilivyofanya na kuwafikisha wale ambao inaushahidi kuwa ni wahalifu Mahakamani. Ni jambo la kujivunia katika historia ya nchi kwamba Serikali imethubutu kuwafikisha katika vyombo vya sheria hata viongozi wake maarufu.
Ni jambo la mhimu kugusia kwamba moja kati ya viongozi waandamizi wa CHADEMA ndio anaeongoza jopo la mawakili wanaotetea watuhumiwa wa ufisadi. Mtu anaweza kudhani kwamba lengo la kiongozi huyo mwandamizi ni watuhumiwa washindwe ili serikali ionekane imeshindwa na CHADEMA kuendelea kupata sifa
Ndugu yangu george yetu hayaishi wala hayataisha kwa mdahalo kwani naamini kuwa serikali yangu iliyopo madarakani haikurupuki nnachotaka kugusia leo ni ujasiri wa Mhe: JK kumyanyua mkono na kuwanadi watu kama Mramba,Rostam,Lowassa na wengineo wengi ambao wanaonekana kama ndo wenye kubeba lawama za yote haya yaliyopo,
Hebu tufikiri pamoja katika hili wamefanya nini? Hata walaumiwe kiasi hiki? Hatuna ushaidi wowote wa kuwatia hatiani watu hawa isipokuwa uzushi tu na roho mbaya za watu fulani kwa misingi ya kuchafuana na wivu wa kwanini wao wanayo na sisi hatuna? Fanya kazi, nenda shule, na uwe mbunifu kwani hamwoni kuwa hata BIBLIA intamka kuwa asiyefanya kazi na asile, na siku zote FUNDI wa LAWAMA huchongoka mdomo kwa kutafuta staili ya kuremba lawama zake.
Mahakama haikumtia hatiani hata mmoja katika uhalifu wowote zaidi sana ni mahakimu wasio rasmi katika baadhi ya magazeti ndo wanao endesha kesi hizo na ni vizuri kwani hata hukumu itakuwa kihabarihabari kama wanavyo fanya. Siioni sababu ya watu wa Dar kuwachaguli Rombo mbunge! nashangaa sana!?? Kama watu hawakuona ubaya wangu unao nipakazia inakukera nini? wanapo endelea kunipa nafasi? na kama we unatamka wakati wote mabaya yangu lakini walio wangu hawakuyaona wanafanya kusikia kutoka kwako, Je undhani wanakuelewaje?
Bwana George misitaki kuzungumzia ya mawakili kwani nafahamu kabisa kwanza wapo kazini, pili hadi wafikie hatua ya kuchukua kesi wameona kabisa kuwa kuna uwezekano wa kushinda kesi nakwamantiki hiyo wameona dalili ya haki ya mtu kuibiwa kwa sababu ya wivu au chuki binafsi.
Mtu kama lowassa anpesa tangu enzi ya mwalimu hadi leo, jamaa anapiga kazi mbaya ni mjasiriamali na kiongozi, mnataka akae tu ili nini? mtalisha familia yake? Monduli mtapeleka maendeleo nyie? kwa taarifa yenu hata mfukoni inapobidi huwa anafanya.
JK ametumia haki ya kikatiba kuwa kama mtu hajawahi KUHUKUMIWA kwa kosa lolote la JINAI
anayo nafasi ya kuwa kiongozi wa nchi hii. nitajieni katika serikali nzima aliyewahi na bado yupo madarakani? kushitakiwa ni tofauti na kuhukumiwa mnapaswa kuelewa hilo, unaweza kushitakiwa kimakosa, au kwa kuonewa sasa tusigeuke kuwa mafundi wa kutoa hukumu kwa sababu za kisiasa au uchochezi au hata mamluki kwakuwa tu unamchukia mtu kwasababu ya alichonacho wakati taaluma hiyo na vigezo vya kuhumu hatufahamu. Tujifunze kujikubali na kwakubali wengine na ikithibitika kuwa wana makosa mahakama itawapa staili yao. sio sisi?
Tunachoweza kufanya sisi ni kuisaidia mahakama kama tunaushaidi tuuwasilishe ilikurahisisha kazi ya mahakama lakini hatupeleki ushaidi matokeo yake tunaanzisha mahakama zetu kwenye majukwaa ilikuwafurahisha wasio na uwezo wala utashiwa kupambanua mambo kwani leo hii hata wale wanao jiita wasomi na mawakili sikia kauli zao
“sisi mesha sema kuwa flani na flani ni mafisadi wahujumu uchumi, mapapa wala rushwa na zaidi ya haya kama wanaona kuwa wameonewa waende mahakamni ushaidi tunao”
sasa ikiwa kweli ushaidi upo kwanini msiwapeleke kwenye vyombo husika? kwa kuiokoa mali yetu inayotumiwa vibaya?
naieleweka kuwa sio kwamba wao hawawezi kwenda mahakamani ila wanaona kamchezo kachafu kakupotezeana muda na kutafuta umaarufu kwa kupitia mgongo wa kiongozi fulani, naukizingatia kuwa wapo kzikazi zaidi muda wamalumbano kwao ni mwiko.
NITASEMA KWELI DAIMA NA FITINA KWANGU NI MWIKO ni kauli ya kiapo kwa makamanda wa CCM sijaona kama kunu mahali wanaapa kulumbana? zaidi ya kuparangana na maisha kwaajili ya kuondoa umasikini. Wanao beza kauli ya MAISHA BIRA KWAKILA MTANZANIA ni walio nafikra finyu kwani unapo mwomba MUNGU afungue milango ukishamaliza kuomba unaenda kulala au unafanya kazi? Nyie jiegesheni kwenye magenge ya kahawa na visheti Msifanye kazi alfu msubiri maisha bora yaje kama muujiza? Hata MUNGU habariki hilo.
Mnao sema kuwa hakuna fursa mmefeli wenyewe na nafsi zenu zinawasuta kwani nchi hii inahitaji MADAKTARI WANASHERIA WAALIMU WAGAVI WAGANI WAUGUZI WAHANDISI na wengineo wengi lakini watu hakuna kwaluwa wataalamu hao hawapo tulio wengi tumekimbia shule pengine leo tungekuwa mmoja kati ya hao na tusinge kuwa na milio ya aina hii ya ugumu wa maisha.
Pinguza lawama ongeza muda wakufanya kazi nautaona mabadiliko na fursa zikitokea utakuwa kwenye nafasi ya kushindania na kushinda kama ambavyo CCM itshinda kwa kishindo.
miruzi ming mara zote ama humchanganya au kumpoteza dog kabisa kwenye site kwan watz mpaka sasa hatujasoma alama za nyakat na kumtambua rais.akiwa jasir na mpinga ufisadi waz waz bila woga cdhan kama kuna cha kudiscuss wandug tukae tu mita tulizoelekezwa kwa upole tukisubir ushindi.
Hivi mnajua Slaa na Mabere Marando wote ni TISS (Usalama)?Hawa jamaa wana kadi za CCM mfukoni (that’s a fact).Tumia e-mail yangu kama unataka ushahidi.Tanzania haijawahi kuwa na mpinzani wala hatakaa awepo siku za karibuni.Nani amemsahau Mzee wa Kiraracha mwaka 1995??Si kazi ilikuwa ile ile ya kutengeneza vuguvugu la uanaharakati??Hawa watu ni wamoja.Jaribu kujiuliza ile siku Richard Kyabo anarudi CCM wale wananchi waliomsapoti ile siku anaanzisha CCJ si walijiona majuha???Kaa fanya kazi zako.I have seen the future.
Muhamed, it’s always better when you prove what you so called a fact, ili kwamba 2ongelee vitu ambavyo vipo,ni kweli kabisa wapinzani wote walitoka ccm kwasababu yo mfumo wa chama kimoja kw wakati ule, but kwa sasa waliotka ccm ndo wanaoleta upinzani, the point is if you really seen the future then vote for the person whom you think put the interest of th epublic first and if your just saying that you have seen the future yet you are voting for those shameless leaders then as per me you haven’t see the future.
Kweli nimegundua ugumu alionao mwalimu kuhusu suala zima lakufundisha na kuhakikisha ukungu unamtoka mtu na hatimaye naye anaonekana na watu kuwa anafaa.
Niwazi kuwa unaweza kudhani ulilifahamu hili tangu zamani ila sio kwa mtizamo wangu, nikirejea kwa aliyewahi kuwa Rais wa marekani ABRAHAM LINCOLIN alisema “huwezi kumwezesha/kumpa mtu nguvu kwa kunyang’anya aliye nazo” mwisho wa kunukuu.
Maana yangu ni hii Demokrasia sio vita, jazba, chuki, kulazimishana, matusi, na mengine mengi yanayo fanana na hayo, ila kwa ufupi tu ni maridhiano/ridhaa/uamuzi wa utashi wa mtu/fursa/haki. Na mambo mengi yanayo fanana na hayo
Demokrasia sio USAWA kwani maisha ya punda hatuwezi kuwa sawa, Shetani ukorofi wake ulianzia kwenye kutaka kuwa SAWA na MUNGU kwasababu tu ya umaarufu wake, Lakini matokeo yake akakabidhiwa LIFE TIME PUNISHMENT, kama unadhani natani jiulize kwanini wewe sio sawa na baba yako? na kwanini CCM sio sawa na CHADEMA? au Kwanini nafasi ya katibu sio sawa na ya M/Kiti?
Ukigundua tu kuwa hatukosawa bali tuna HAKI sawa basi utafahamu kuwa ndani ya haki ndio kuna kinachoitwa usawa, hii ni falsafa ngumu kidogo kwa wale wanaochukulia mambo juu juu, HAKI yetu sote kwa MUNGU ni KUMTUMIKIA YEYE PEKEE, KUISHI KWA MAPENZI YAKE YEYE PEKEE, na USAWA wetu unakuja baada ya kutimiza haki nao ni KUFA.
HAKI ya vyama vyasiasa ni kwanza KUWEPO KWAO KISHERIA, KUWA NA WANACHAMA, KUNADI SERA ZAO, KUPIGA KEMPEIN, n.k . USAWA wao ni SIKU MOJA TU ya kupiga kura wote kwa pamoja. Na KUFUTILIWA MBALI UKIVUNJA SHERIA ILIYOKUWEKA HAI. hizo ndio haki na usawa kwa uchache kwa wano taka sana USAWA bila kuangalia HAKI ZAO. yani minina wanachama milioni 8 wewe una wanachama laki 6 tunawezaje kuwa SAWA? ila inawezekana kuwa na HAKI sawa.
Kwa misingi hiyo CCM haiwezi kuwa sawa na chadema hata mfanye nini kwanza hata majina tu sio sawa, hata kiutendaji pia hawapo sawa. Ndomana CCM imeweka wagombea NCHI NZIMA na chadema chini ya 40% nchi nzima. tayari wameshajitofautisha kiusawa ilhali wana HAKISAWA.
ninachokiona kinfanywa na DR. nikuipa ushauri CCM na serikali yake nini vipewe kipaumbele katika miaka mitano ijayo. Kwani CCM pamoja na sera zao safi huwa sio wachoyo kwa kuenda mbele zaidi na kusaidia hata ambapo hawakukusudia kufanya hivyo?
Nasema huwezi kuwa SERIOUS unataka NCHI na katika TARAFA nzima huna kata ofisa ya balozi, lazima utkuwa UP STAIRS hauko sawa.
Nimemsikia DR akimtaka DR. JK aeleze alikopeleka Trilion 1.7 za Kustahimili Mtikisiko wa uchumi? Kwanza slaa anapaswa kujua kuwa serikali iliyopo madarakani siyo ya chadema ni ya CCM so alichokifanya Dr.JK ni kuwaeleza wenye serikali yao jinsi zilivyo tumika. kwani hata uko pia kuna wabunge tena zaidi ya asilimia 90% kwa maana nyingine akikuwa bungeni.
Leo natamka wazi kuwa Slaa hatafikia hata kura atakazopata PROF. LIPUMBA achana na habari ya JK kwani ni next LEVEL watoto wa mjini wajua hivyo, kwani akimsogelea basi atakuwa amepitwa na milioni 10.
Halafu ii habari ya kuibiwa inatoka wapi? mkishaona mnashindwa msianze kutushawishi kuwa mnaibiwa hizo ni kauli za MFA MAJI.
NA DEMOKRASIA haikamili tu MPINZANI anaposhinda kwani ndio mtizamo wa mlio wengi fanya tathmini na utaona tunao ipenda CCM ni zaidi ya 96% ya watanzania wote.
Bwana Samson umesema kweli. Dalili ya nvua ni mawingu.Huwezi kuzungumzia kuibiwa kura wakati hata uchaguzi wenyewe haujafanyika. Tena ukaenda hatua mbele zaidi na kusema hamna cha polisi wala jeshi la kujenga taifa.
It really is supprising to hear someone aurgue that “serikali inachukua hatua dhidi ya ufisadi”!
Hatua gani zinazochukuliwa? Kesi kubwa zote ziko tu kutumika kama smoke screen – na kuhakikisha kuwa hakuna discussion juu ya kashfa zenyewe kwa vile ‘masuala yako mahakamani’. Wahusika si ndo hao wanagombea kama ‘watu safi’ majimboni kwao?
Nani amewajibishwa au kuadhibiwa kuhusiana na sakata la Richmond (kampuni iliyosemekana haipo na bado inatajwa)? Nani anajulikana kuwa alirudisha mabilioni ya fedha za EPA? (Je mtuhumiwa anayerejesha ni basi kawa safi?) Ni nini uamuzi uliotolewa juu ya Kagoda? Deep Green? Meremeta?
Hatua gani za haraka zimechukuliwa dhidi ya watuhumiwa zaidi ya 50 wa CCM waliohusishwa na rushwa wakati wa kura za maoni?
Jibu moja la ukweli ni kwamba mambo haya yanachelewezshwa ili watu wayasahau tu. Lakini hiyo si lazima iwe dawa. Dawa ni kufanya mabadiliko makubwa’ KWA KURA.
Tukiyaacha hayo. Tungependa kuona watu makini wakioongoza taifa letu. Wenye mtizamo wa mbali (vision). Ni mradi upi mkubwa unaweza ku-justify matumizi ya fedha za walipa kodi? Elimu wanachangia, Afya wanachangia n.k., lakini hakuna Reli mpya au matengenezo makubwa kwa zile za zamani! Wimbo ni barabara – kana kwamba barabara ni zawadi kwa wananchi – kumbe ni moja ya haki zao!
Pamoja na umaskini tuliokuwa nao, wakati wa MWalimu kulikuwa na mambo makubwa ya kuonekana. Viwanja vya ndege vya kimataifa, Mang’ula Machine tools (kiwanda cha viwanda kilichtelekezwa), Mahospitali (Muhimbili, n.k.), Mashule ya sekondari yaliyokuwa bora, Elimu bure, reli ya Uhuru, Urafiki, Mwatex, n.k. n.k. DHANA KUU ILIKUWA taifa KUJITEGEMEA! Tumepoteza mwelekeo, treni imeacha njia kweli…
Tunahitaji mabadiliko makubwa!
Hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya mafisadi ni nyingi. Kuna case chungu nzima zimefunguliwa dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi baadhi yao ni wakiwa viongozi waandaminizi. Kutungwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi kudhibiti rushwa katika uchaguzi. Sheria ya Kuzuia Rushwa imefanyiwa marekebisho ya msingi kwa kuingiza makosa mengi ya ufisadi na kuongeza uwezo kwa kikosi cha kuzuia na kupambana na rushwa.
Kwamba kesi zilizopo mahakamani ni daganya toto, mimi naona ni kauli ya kisiasa. Watuhumiwa wanahaha kila siku kujitetea na wengine wameshatiwa hatiani wanatumikia kifungo bado unasema ni danganya toto. Kutuhumiwa tu hakumfanyi mtu kukosa haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Tuzingatie kwamba nchi hii inatawaliwa chini ya utawala wa sheria na haki za binaadamu. Watoa tuhuma sio miungu mpaka tuhuma zao ziwe na uwezo wa kumtia mtu hatiani kabla hajasikilizwa. Kama angekuwa mtu ameshapatikana na hatia ya ufisadi baadae akagombea nafasi ya ubunge hapo ungekuwa sawa.
Kuhusu Richmund hamna asiyejua kwamba ilianza na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri bila kujali kama kulikuwa na ushiriki wa moja kwa moja au unaotokana na uwajibikaji wa kitimu. Kamati ya Bunge ilitoa mapendekezo yake na sehemu kubwa yalitekelezwa. Na hivi sasa suala la Richmund lipo katika vyombo vya sheria kwaajili ya kubaini ukweli zaidi. Serikali yenye nidhamu haiwezi kuendelea kulizungumzia kabla vyombo vya sheria havijatoa maamuzi katika baadhi ya maswali yanayobishaniwa kuhusiana na Richmund na Dowans.
Raia Mwema pia wanapaswa kujua kwamba sio kila tuhuma itakayotolewa dhidi ya mtu au watu fulani itapelekea kufunguliwa kwa kesi ya jinai. Kufunguliwa au kutofunguliwa kwa kesi ni suala la ushihidi. Serikali haiwezi kushinikiza vyombo vya dola kupeleka kesi Mahakamani hata kama hamna ushahidi. Kuwepo au kutokuwepo kwa ushahidi pia hakutegemeani na kiwango cha malalamiko katika majukwaa ya kisiasa au vyombo vya habari. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka no ofisi huru kama ikiona kuna kesi ya kupeleka mahakamani kuhusiana na Kigoda au Meremeta itapeleka.
Vinginevyo kama wananchi wengine wana ushahidi wa kutosha kuhusiana na tuhuma hizo sheria zetu zina utaratibu ambao wanaweza kuutumia kupeleka tuhuma hizo katika vyombo vya sheria. Ikiwa watu wanaweza kuituhumu sheria kuwa ni batili na wakapata uamuzi mahakamani, itakuwa ni kumtuhumu mtu kuwa fisadi? Vyama vya upinzani vimebalikwa kuwa na wanasheria waliobobea. Kama kuna ushahidi na tunahofia kwamba serikali inalinda mafisadi kwani tusiwatumie wanasheria wetu?
Mchangiaji anakubali mashule yamejengwa, barabara zimejengwa na hospitali zimejengwa lakini anataka kuona Reli. Hayo ni mapenzi yake.
Unafahamu raia mwema kama alivyo Dr. na CHADEMA nzima sio kwamba hawaoni vitu ila ni lawama na ile hulka ya upinzani imeshawaathiri
Bwana George dhana ya upinzani kwa vyama vyetu bado hawajaifahamu vizuri na wana dhani ni kupinga tu, kama nimemwelewa vizuri raia mwema, anataka Mhe; JK awe jaji mkuu na awe DPP, na wakati huo huo awe DIKTETA haiwezekani? nakama huo ndio upeo wako kufikiri napata shida kuelewa utitiri wa watu wanao kuona wewe kama ROLL_MODEL wao wao watakuwa wanfikiri vipi?
Kinachoonekana hapa ni jazba, swali langu kwa RAIA MWEMA ni kuwa kama unaweza kuhoji kuwa nani ameona pesa zikirudishwa je nani aliona zikiibiwa? na kwa nini usimuulize yule aliye kuambia kuwa kuna pesa zimeibiwa mahali fulani kama zimerudishwa? kwani imani yako kwake inaonekana ipo juu. Au kama unadhani bado mbona kafunga mdomo juu ya swala hili?
Inaonekana nyimbo za upinzani ni zilezile za meremeta, kagoda, iptl, richmond, epa, na twin towers sasa swali ikiwa hamkuwapeleka mahakamani na mmeamua kuwashitaki kwa wananchi, Basi sasa na msubiri hukumu ya wananchi juu ya hilo. namwelewe kuwa si kila mtu anaishi kwa taratibu na mawazo yenu CHADEMA, CUF na wengineo la hasha tuna taratibu zetu za kazi na maisha hivyo hayo mnayoyaita mabadiliko sisi tunayafanyia ndani kwa ndani nje ni mapinduzi kabisa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. CHAGUA CCM 2010 JAKAYA MRISHO KIWETE CHAGUO LETU
Alafu katika aya yake ya mwisho RAIA MWEMA anasema wakati wa Nyerere kulikuwa na miradi mingi kama Reli ya Uhuru, Viwanja vya ndege na elimu bure. Nimeshindwa kuelewa alikuwa na maana gani. Anamaanisha hivyo viwanja vya ndege kwa sasa havipo? Anamaanisha hivyo viwanja vya ndege, reli na mashule yalijengwa kutokana na fedha za faida ya hivyo viwanda vya nguo alivyovizungumzia?
RAIA MWEMA hajui kwamba asilimia ndogo sana ya watanzania walipata nafasi ya kujiunga na shule chache za sekondari ambazo nyingi ziliachwa na mkoloni. Haoni mamia ya shule za sekondari zilizojengwa bila misaada toka nje. Haoni chuo kikuu kikubwa kabisa cha kisasa kilichojengwa kwa fedha za ndani. Anataka kusema kwamba miundo mbinu ya usafiri ilikuwa mizuri wakati wa mwalimu kuliko sasa?
RAIA MWEMA anasifia viwanda vya nguo hasemi hivyo viwanda vya nguo na vinginevyo vilikufa kwa sababu gani? Anamaanisha kwamba vilikufa wakati wa Mwinyi, Mkapa au Kikwete? Hajui ni matatizo gani ya msingi yaliyokuwa yanaukabiri mfumo wa soko la umma na jinsi yalivyolazimisha kuwepo mfumo wa soko huria tulionao leo. Hajui kwamba mwalimu alishiriki katika kubariki mfumo wa uchumi huria baada ya kuona kwamba mfumo wa soko la umma umepitwa na wakati? Hajui kwamba mwalimu mpaka anaaga dunia alikuwa bado mwanachama wa Chama cha Mapinduzi? Kama RAIA MWEMA na wanachadema wanasema CCM haijafanya lolote katika miaka zaidi ya 45 ya Uhuru na bado wanasema watafanya aliyofanya mwalimu, wanaelewa kweli wanachokisema?
Hawaoni nchi ilivyopiga hatua katika demokrasia na uhuru wa habari? Hajui kwamba tumepiga hatua kubwa kutoka magazeti matatu nchi nzima (Uhuru, Mzalendo, Daily News, Kiongozi, Mfanyakazi, Lengo)hadi magazeti karibu mia likiwemo gazeti lake la RAIA MWEMA na TANZANIA DAIMA. Kutoka radio moja hadi zaidi ya redio ishirini. Kutoka kituo kimoja cha television cha Zanzibar hadi vituo karibu kumi.
Hao CHADEMA anaowaona makini wamefanya nini cha maana katika kipindi cha miaka 17 ya uhai wao mpaka waonekane wana ubavu wa kuchukua nafasi ya CCM. Mbona wameshindwa kukifanya chama chao kiwepo katika sehemu zote za nchi? Mbona wameshindwa kuondoa dalili za ukanda katika chama chama chao?
baba zimebaki dakika za lala salama nikmchague rais kikwete kuendelea kuingoza nchi
nalia na wanachama wa chama cha mapunduzi tujitokeze kwa wingi kwani ndio mtaji tulionao
JK juu na ushindi ni lazima
leo nina kibwagizo kimoja tu hivi tunavyo wafundisha watoto zaidi sana wakike wasikubali vitu vya bure kwani hakuna bure katika dunia ya leo? je hawa akina kanjanja wanao taka kutupa kila kitu bure wao wanatoa wapi pesa? na wana zirejeshaje?
nawaambia Wa TZ tusifanye makosa 2010 ni JK tu. hata kuku watatozwa kodi slaa akipita.
Eti unisomeshee mtoto! mimi ni kilema? mbona mna vichekesho? chama kina 17 years hata ofisi mmeshindwa kujenga eti itakuwa kusomesha watoto bure kujengea wananchi nyumba!!!! hivi hawa jamaa wana maleria nini?
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
VOTE JK 2010
Tuzungumzie suala la wazee wa iliyokuwa East Afrika. Ni kweli madai yao yamekuwa mahakamani kwa muda mrefu. Lakini kilichotokea hivi karibuni kwa maoni yangu kimetokana na sehemu kubwa wanasiasa kutaka kutumia uelewa wa wazee wetu na matatizo yao kupata huruma ya kisiasa.
Nimesoma magazetini na nimechunguza na kugundua kwamba vuguvugu zilianza kwa jaji wa mwanzo kujitoa baada ya kuona ana maslahi binafsi katika kesi. Huo ni utaratibu wa kawaida na mhimu katika mfumo wa uendeshaji wa haki. Huwezi ukategemea kutoa haki katika mgogoro ambao tayari una maslahi binafsi. Ni sawa na kesi ya ngedere kumpelekea nyani au ya nyani kumpelekea ngedere. Unaweza ukashinda kesi kwa upendeleo au ukashindwa kesi kwa upendeleo maana jaji sio Mungu asiwe na hisia zake binafsi katika mgogoro. Sasa jaji amejitoa, unategemea kesi itapangiwa jaji mwingine siku hiyo hiyo na kusikilizwa.
Jaji kajitoa uongozi wa mahakama umetumia muda wa masaa kumpata jaji mwingine na kuipanga kesi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Kesi zingine kutokana na mrundikano wa kesi na uhaba wa waamuzi zinachukua hadi miezi mitatu toka ahirisho moja hadi lingine. Jaji aliyopangiwa japo ni mgeni katika shauri hilo anatumia mda mchache kulisoma na kulifahamu jalada alafu anasingiliza hoja za upande mmoja hadi zinaisha. Kesi inahusisha mamia ya wadai na inavielelezo chungu nzima. Upande wa pili wanahitaji muda wa kujiandaa kujibu hoja za wadai na mahakama muda wakupitia hoja na vielelezo. Wadai wanataka kila kitu kifanyyike siku hiyo hiyo au muda mchache chini ya wiki mbili.Mahakama inaposisitiza msimamo wake watu wanalala barabarani na wanasiasa wanaunga mkono. Hivyo kweli tunaitendea haki mahakama na mfumo mzima wa utoaji wa haki?
Wazee wetu kutokana na umri, matatizo, na ugeni wao katika uendeshaji wa haki siwezi kuwalaumu. Tatizo ni walio nyuma yao.
Bwana george niungane nawe kimtizamo pia kiuhalisia yangu katika hilo ni kuwa wazee wetu wametumika kisiasa lakini zaidi sana nionavyo mimi ni uelewa mdogo wa masuluala ya sheria na taratibu za mahakama umetumika kama mtaji wa kisiasa bila wao kujua, hili halina tofauti nalile la wafanyakazi.
Tatizo hapa ni wakiti gani hawa wazee wanakusudia kugoma? nakwanini sasaivi wakati nchi nzima ikijiandaa na uchaguzi? je hawaoni kuwa kuishinikiza serikali kipindi ambacho vyombo vya dola agenda zao kuu kila wakiamka ni ulinzi na usalama wa nchi nikama kutumia mwanya wa kampeni kutaka matatizo yao yatatuliwe kwa misingi ya rushwa?
Huwezi kuniambia kuwa nitakutekelezea shida zako sasa halafu TAKUKURU wasinikamte? hiyo itakuwa ni rushwa ya waziwazi na ndo mana watu makini wamekaa kimya. wana waacha waendeleze malumbano then mahakama ikisha amua serikali itatekeleza hukumu kwa nafasi yao.
Nashindwa kuelewa hawa wanao jiita wasomi na wanaharakiti, hivi msoma nini hasa? na kimewasaidiaje? mchango wenu katika maendeleo ya hii nchi ni yapi hasa? kama kweli mmeelewa mafunzo mliyoyapata nikwanini falsafa zenu nyingi ni za kukariri? kimsingi nchi hii haina wasomi walioandaliwa vizuri takriban miongo mmoja sasa, na ndo mana kwa wingi wao wanatumika isivyo. huwezi kuniambia mtu ni mhandisi na anatafuta kazi ya kukaa ofisini,au mtu ni daktari anataka nafasi ya mkurugenzi. zalima kuna mahali kuna tatizo na ni lazima president alipe jicho hili kwa mapana zaidi.
ninacho kiona sasa ni kama mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwani wimbo ni mafisadi, mafisadi na huu mpya wataiba tu, hivi kwanini mshiriki ikiwa mtaibiwa? na kwanini nyimbo za kutaka mpewe jicho la karibu na wasimazi wa nje? mme wahi kujiuliza ni chama gani kina mtaji wa wanachama milioni 8????? zaidi ya CCM
Acheni mbwembwe kama kuna mnachotaka kilindwe ni kura lakisita ikizidi sana labda milioni 1.6 hakuna chazaidi mzee slaa
chukua hii itakusaidia nasisitiza watanzania tufanye kazi sana kwani ndio msingi wa maendeleo yetu pekee sio JK wala slaa watakao kujengea nyumba yako ya kuishi Isipokuwa JK kwa mazingira haya ya kazi yake na fursa hizi nitaweza tu na ndomana namchagua TENA na TENA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
VOTE JK 2010
WABUNGE WA CCM 2010
MADIWANI WA CCM 2010
Umesoma taarifa ya kukamatwa gari mpakani Tunduma likitokea Africa Kusini lenye shehena za makaratasi ya kupigia kura yenye kura za JK 5,000,000? Karatasi hizo zinasemekana zina kura za kumchagua JK tayari!
Tutaendelea baadaye.
Ajuza,
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania,taarifa hizo sio za kweli na mpaka hivi sasa aliyehusika na kusambaza uvumi huo yupo mikononi mwa Polisi.Tafadhali tuwe makini katika kutoa maoni na kusambaza habari.Zingine zinaweza kuwa “sumu” kwa utulivu na usalama wa nchi.Asante.
Nimefurahishwa na comment za mtandao wetu kuhusiana na umhimu wa wachangiaji na wananchi kwa ujumla kuwa makini na taarifa tunazotowa.
Juzi nilimsikia DR SLAA akitoa taarifa hizi za uongo hadharani tena kwa kujiamini na mikogo. Binafsi nilikaa kimya na kupata nafasi zaidi ya kufanya uchunguzi ili nijiridhishe na usahihi wa taarifa hizo. Bahati nzuri, muda si mrefu tulipata uhakika wa uongo na upotoshaji uliopo katika taarifa hiyo. Kwa sasa mhusika wa taarifa hiyo yupo katika vyombo vya dola.
USHAURI WANGU wa bure kwa DR SLAA na viongozi wengine wa kisiasa ni kwamba tunapaswa kuwa makini na kauli zetu. Suala la matu kuingiza masanduku ya kura ni zito sana ambalo linaweza kuleta athari mbaya katika usalama na amani ya nchi yetu. DR SLAA alipaswa kuifanyia kazi taarifa na kujiridhisha na usahihi wake kabla hajachukua dhamana ya kuiwasilisha katika umma. Umakini katika masuala nyeti kama haya ni lazima kwa mtu yeyote anaetaka kuwa kiongozi wa dola.
DR SLAA alifanya kosa hilo hilo wakati akireact kutokana na tamko la Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi. Hata kama Mnadhimu alikosea katika kutoa matamshi yake, haikuwa sahihi wala busara hata kidogo kwa mtu anaepigania kutwaa dola kutoa majibu ya namna hiyo. Baya zaidi ni kwamba DR SLAA alirukia kuihusisha taarifa hiyo na ufisadi bila kuwa na ushahidi wowote na bila kusingatia unyeti wa taarifa hiyo katika usalama wa nchi. DR hakuwa amefanya uchunguzi wowote na kujiridhisha kama jeshi halikuwa na taarifa sahihi ya uwepo wa dalili ya uvunjaji wa amani.
nashukuru kwa kumuelimisha ajuza kuhusu hilo kama nilivyo tangulia kusema awali propaganda zipo na sisi hatuogopi wala hazituvyimi usingizi tuna mtaji wa kura zaidi ya milioni 8 za wanachama hai hivyo siogopi chochote katika hili nashukuru kuwa mzushi wa taarifa hizo yupo mahakamani kwa sasa
Bwana Samson inavyoonekana unapenda ushabiki zaidi bila kuzungumzia ukweli au kuchanganua mambo kama mtu mwenye upeo kidogo wa elimu kama uliyonayo kwani nimeona kuna sehemu umejaribu hata kunukuu maneno ya Rais Mstaafu wa Marekani ‘Lincoln’. Ok, inategemea na mwalimu wako aliyekulisha sumu hiyo maana wengine mnasoma kwa kutumia vimemo na mnafaulu kwa kuiba mitihani hadi mnafikia hatua ya vyuo vikuu. Unapojivunia idadi ya wanachama bila kutazama nguzo za utawala bora kama zimetimizwa na CCM unakuwa hujakamilika. Waambie watanzania ni kwa vipi Kikwete ametimiza nguzo hizi za utawala bora ambazo ni
a) Participation
b) Rule of law
c) Transparency
d) Responsiveness
e) Consensus orientation
f) Equity
g) Effectiveness and efficiency
h) Accountability
i) Strategic vision
Kama utaendelea kuzungumzia idadi ya wanachama basi unatakiwa ujiandae kuizika CCM milele baada ya muda wa miaka isiyozidi 15 kuanzia sasa. Idadi ya wanachama unayozungumzia ni ya wazee na wanawake ambao bahati mbaya walikosa elimu ya msingi kuwawezesha angalau kuelewa ni vitu gani wanavyostahili kutimiziwa na serikali bila kujali ni kidemcrasia au ya kidikteta. Wazee watakapokufa usitegemee vijana ambao wanabahatika kupata elimu hata kwa njia ya vyombo vya habari watakimbilia CCM ya familia ya Kikwete na Vingunge wengine. Hata hivyo mimi siwezi kukulaumu maana ni ukweli usiopingika kuwa “KUSOMA NA KUELIMIKA WAKATI MWINGINE HAKUWEZI KUONDOA UJINGA KWA MHUSIKA”. Good day.
Napenda kwanza kutoa pongezi kwa wachangiaji wote!
Dr SLAA anafaa na nichaguo Sahihi la watanzania kuwamchagua kuwa raisi.Kwa uelewa wangu wa demokrasia na utafiti wangu mwenyewe nimejiridhisha kumchagua kuwa Raisi wangu Vigezo hivyo ni hivihapa.
1>Kwanza Dr Slaa ni mtue makini: Ndugu yangu hata ungekuwa na chama ambacho kina ofisi katika kila familia kama kiongozi sio makinia ni kazi bure!
2.Dr Slaa ni mchapakazi
Kuna ukweli usio fichika kuwa Dr Slaa ni mchapakazi nina haki ya kumchagua ili aweze kuinua maisha ya wananchi.
3>Dr Slaa ni MUADLLIFU.
4>Dr SLAA NI MJASILI
5>DR SLAA ANA UZOEFU MKUBWA
Sasa watanzania tuache itikadi mbaya tumchague slaa,Mbona mimi natoka Iringa -ludewa itikadi ya ukabila inatoka wapi?
Nashukuru sana kwa maoni yenu wachangiaji wa hii mada. Ila kuna jambo limenisukuma nikalazimika na mimi kuchangia walau kwa fikra zangu chache yale yaliyomo ndani ya moyo wangu.
Ninachokiona mimi hapa ni kwamba kuna wachangiaji wanapitiliza mipaka kwa kutumia maneno ambayo yanaelekea kuwa kama vile vitisho au matusi kwa upande mwingine. Ushauri wangu mimi ni kwamba bora kila mchangiaji awe na nidhamu na heshima kwa mwenzie kwa kuchangia hoja na si kuandika matusi au vitisho. Mfano mmojawapo ni hii ya kukosoa kiwango cha elimu cha mtu bila kuzingatia inaweza kumuathiri mtu kwa kiwango gani. Tafadhalini waTanzania wenzangu sisi ni watu wa amani na wastaarabu dunia yote inatujua kwa hilo, kwanini hapa tusibishane kwa hoja? Ya nini kuweka kejeli, vitisho na matusi kwa maoni ya mwenzio. Ikumbukwe katiba yetu ambayo ni sheria mama inamruhusu kila mmoja wetu kutoa maoni yake kwenye kila jambo alimradi tu asivunje sheria. Nawaombeni waTanzania wenzangu tuheshimu hili.
Kuhusu nani anafaa kuongoza Tanzania, kwa maoni yangu CCM sio chama kibaya, bali mgombea wake hana sifa zinazofaa kutuondoa kwenye umaskini huu. Si kweli kwamba Dr. Slaa nae ndie suluhisho la kweli kwenye matatizo yetu haya, lakini kwa kua uchaguzi ni kati ya hawa waliojitokeza (ukiongeza na wale wa vyama vingine), ni yeye pekee Dr. Slaa anaonekana anaafadhali. Ukisoma ilani ya CHADEMA mwaka huu ni kweli utaona wamejiandaa kikamilivu angalau kuanza kutuelekeza kwenye mwelekeo sahihi. Tofauti na ilani ya CCM ambayo kwa mtazamo wangu (na huu ninayo haki wa kuueleza) ni ile ile ya mwaka 2005 ambayo kama itakumbukwa, walishawahi kukiri kwamba haitekelezeki tena, isipokua kwa majumuisho mapya sehemu kadhaa.
Kuhusu elimu ya bure, mi nadhani maana halisia ya sera hii ya CHADEMA haijaeleweka ipasavyo. Huu ni mpango mkakati wa muda mrefu (kwa lugha ya kiingereza – long term plan). Sio eti kwamba wakipewa madaraka kesho basi wataanza hapo hapo kutoa elimu bure kwa watanzania. Ninachoamini ni mpango utakaochukua muda mrefu, isipokua wao tayari watakua na malengo ya kuelekea mwelekeo huu na kwa hili sina jinsi bali nitawapa kura yangu.
Kweli serikali ya CCM imefanya mengi hii tunakubali, kujenga shule za kata, vyuo mbali mbali na kujenga zahanati yote haya tumeyaona. Isipokua hapa ukiangalia vizuri utaona kuna ukweli mwingine uliojificha. Kwanza kabisa shule nyingi zimejengwa lakini hoja nikwamba hazina walimu, vitabu wala maabara, inayopelekea elimu inayotolea humo kuwa ya kiwango duni kupindukia. Leo hii Tanzania nchi ya mwalimu (mungu ailaze roho yake mahali pema peponi),inashika nafasi ya 47 kwa ubora wa elimu barani Afrika. Hii ni wazi kwamba waliopo madarakani wameshindwa kuwa na upeo wa kututoa kwenye shimo hili la umaskini na ujinga, na haya ni baadhi ya matokeo yake. Kwa hili CCM haiwezi kukwepa lawama kwani yenyewe (ikiwa kama TANU na baadae CCM) ndio pekee imeshika dola ya nchi hii tokea uhuru.
Pia kuhusu kesi za mafisadi na hasa hilo neno la ufisadi ni mwimbo ambao unaanza kukosa uelekeo. Nawashauri wapinzania hasa CHADEMA wapite kuwaeleza wananchi mikakati yao ya kututoa kwenye umaskini na sio kueneza chuki ya nani kakwapua nini na wapi. Kwa upande mwingine niwapongeze wapinzani kwa kuwapa changamoto CCM na serikali yake ili wananchi wa Tanzania nchi nnayoipenda mimi, waweze kuihukumu kama kweli inaweka maslahi yao mbele ama la. Inauma sana kuona chombo kikubwa kuliko vyote (pengine chenye mamlaka zaidi ya raisi) cha wananchi kama vile bunge kinakua mlango wa mbele kuzika tuhuma nzito kama vile za Meremeta na Deep Green kwa kisingizio cha maswala ya usalama wa taifa. Taifa hili ni la kwetu sote, bila kujali ushabiki wa vyama, na ulinzi wa taifa letu hili unaanza kwa kila mtanzania akiwa eneo lake analoishi. Kwa mtazamo wangu mimi basi wangeruhusu mjadala wa jambo ili uongelewe kama vile Richmond na Dowans ili wenye kukosa tuwajue kwani ni haki yetu sote kujua yale yanayotokea juu ya kodi zetu. Njia mojawapo ya kumuamini kiongozi wako ni ile ya kujijengea uaminifu kwa kila jambo linalowahusu. Kwa hili serikali ya CCM nasikitika kusema mmepunguza uaminifu wetu kwenu.
Ila kimoja na ambacho kinaniumiza nafsi yangu ni kuona kwamba hakuna anayeongelea maswala ya kubadilisha mwelekeo wa uchumi wetu waTanzania. Ni wachache wenu mnaelewa kwamba mwaka 1987 Tanzania ilikumbwa na (mtaniwia radhi) Economic crisis. Hii ilikua ni matokeo ya mfululizo wa makosa ya kiutawala yaliyofanywa mwishoni mwa miaka ya sabini ikiwa ni pamoja na kuruhusu kuvunjika kwa jumuia ya kwanza ya afrika ya mashariki na vita dhidi ya fedhuli Iddi Amin (marehemu). Huu ndio mwanzo wa matatizo yetu yote ya kiuchumi mpaka leo hii tuna uchumi uliotegemezi kupindukia. Sio siri ningependa kuona mpango mkakati wa kuunda upya uchumi wa nchi hii (kama vile wanavyofanya Zimbabwe sasa) na sio hoja za kuimarisha uchumi. Naamini wale wenzangu wajenzi watakubaliana nami kwamba nyumba nzuri ni ile inayojengwa kwenye msingi imara, basi na uchumi wetu kama kweli tuna nia ya kujikomboa na umaskini, ni lazima ujengwe kwenye misingi imara. Wenzetu nchi zilizoendelea kama vile Uingereza (mkoloni) na Marekani, hoja kuu ya uchaguzi wa ngazi yoyote ile ni uchumi. Wananchi wanampigia kura mgombea aliekua na mkakati bora na imara wa kiuchumi na sio chama. Basi na mimi naamini tungelifanya hili kua ndio jambo la msingi kwenye uchaguzi huu na chaguzi zote zinazokuja, watoto wa kihuni husema, “tungetoka”.
Dr. Slaa umeonyesha ulekeo lakini nakuonya usibweteke ukawa kama wenzako wakiingia ikulu wanasahau, nenda pale ukiwa na malengo na maisha ya waTanzania tulioamini kwamba wewe unaweza ukawa kiungo muhimu katika kutuelekeza kule kwenye nchi ya asali na maziwa tuliyo ahidiwa.
Nimalize kwa maneno ya mwalimu Julias K. Nyerere kwamba, “ikulu ni mahali takatifu”, kwa yeyote waTanzania watakae mchagua mwaka huu, namsihi aende mahali pale akiwa na moyo safi kwani matumaini ya waTanzania yako juu yake ila akumbuke akifanya “madudu” atatuangamiza milele.
Nikianza na ndugu HAKI kwanza kabisa sijaridhishwa na namna alivyoanza kujibu hoja za Bwana Samson. Katika mtandao wa kisomi unaoongozwa na nguvu za hoja sio busara kuanza kwa kumkejeri mchangiaji kama elimu yake ameipata kwa kimemo. Yawezekana bwana HAKI ukawa msomi kuliko wote na msomi wa fani zote, lakini bado unapaswa kuwaheshimu wachangiaji wenzio bila kijali tofauti za kimitizamo. Zingatia kwamba bila kuwa na tofauti za kimisimamo na kimitizamo mjadala huu usingekuwepo.
Umetoa vigezo vingi vya utawala bora na wanafalsafa wa siasa wametoa vingi zaidi ya hivyo. Nilitegemea ungeonesha kwa namna gani DR SLAA anakidhi vigezo hivyo au DR KIKWETE hakidhi vigezo hivyo ili tupate pa kuanzia.
Kwamba CCM kama inategemea mtaji wa wanachama wengi itakufa baada ya miaka kumi na tano, huo ni utabiri kama zilivyo tabiri nyingine. Miaka kumi na tano ni mingi sana na chochote kinaweza kutokea kwa hilo naomba nisikubishie wala kukukubalia kama nilisivyoweza kumbishia mtabiri mwingine atakayesema baada ya miaka kumi na tano CHADEMA itakuwa imeshatoweka.
Ndugu zawadi kama walivyo watanzania wengine ana haki zote kabisa kumchagua DR SLAA katika uchaguzi ujao kama mwingine anavyoweza kuwa na haki ya kumchagua KIKWETE, LIPUMBA au DOFUTWA. Hilo katika mjadala huu halina ubishi.
Kwamba DR SLAA ni makini, jasiii, muadilifu na mzoefu bado sio hoja ya maana sana kama haijafafanuliwa kwa kumlinganisha na wagombea wengine zaidi ya watano. Unaposema mzoefu kwa mfano, maswali mengi yanabaki bila majibu. Ni mzoefu wa uraisi? Ni mzoefu wa ugombea uraisi? Ni mzoefu wa ukatibu wa chama? Ni mzoefu kumpita nani katika nafasi gani? Mtu yoyote muadilifu hawezi akabisha tu kwa ujumla kwamba DR SLAA si mzoefu.
Unaposema mjasili ni nani si mjasili? Mjasili katika mambo gani na kwa kigezo kipi? Ukisema muadilifu pia maswali mengi yanajitokeza. Muadilifu kumsizidi nani na kwa kigezo gani? Muadilifu kwa wazazi wake? Muadilifu kwa wanawe? Muadilifu kwa mkewe? Muadilifu kwa majirani zake? Muadilifu kwa chama chake?
Bwana haki unakila sababu ya kutoa maoni yako na kusema uonavyo wewe kuwa ni sahihi, nitangulie tu kusema kifo ni lazima kwa kila kilicho anzishwa kwani CCM haikushushwa na MUNGU hata CHADEMA kitakufa tu inawezekana hata kabla ya CCM kwani ndugu yangu HAKI unaonekana wewe nawe ni miongoni mwa wafuata mkumbo wengi wa unyiriri wa elimu maomboleo.
Unapo ongelea ushirikishwaji labda sikuelewa ulitaka ufuatwe nakuulizwa wewe binafsi kuhusu nini kifanyike na kwa wakati gani? ilimradi tu uridhike nawe pia umesikilizwa, kwa taarifa yako hakuna kilicho fanyika bila kushirikiahwa wananchi kuanzia na mashule yaliyo jengwa na wananchi&serikali yao, miundombinu ya barabara, maji, na mawasiliano, tatizo nikuwa umeshaamua kuwa mpinzani kwahiyo utajifanya tu huoni.
Utawala wa sheria sijui unataka Rais awe jaji mkuu, au aache uozo utendeke tu kwa misingi ya kila mtu ana haki kama jinalako ya kusema tu, sema ila usiseme ovyo ovyo tu bwana haki, inaonekana kuwa taarifa ulizonazo kuhusu serikali ni za mapungufu tu kwani ndio ulizo zitafuta, jaribu kutafuta na za upande wa pili.
JK yupo safi kijana kama angekua mchafu angekuwa msiri na serikali yake, kaacha uhuru watu waseme na wachunguze kisha dolla ichukue mkondo wake, sijui ugne fahamu vipi ngonjera hizo zote zinazo tolewa na wasema ovyo wenzio kama sio jitahada za serikali kuwafungua midomo.
Viongozi wa serikali hii ni watu makini na wamewajibika pale ilipobidi kwa maslahi ya umma, urasimu kwa kiwango kikubwa kimepungua nchi na unliona hili ila kwakuwa tu umeamua kuwa kipofu huoni sasa si ujibadilishe na jina ili uitwe KIPOFU WA MAENDELEO badala ya haki kwani halikufai.
Kwa hili la maamuzi shirikishi ya jumuiya dhani mtizamo wako umekuwa finyu ,mf. kutokuingia EAC kwa hatua ya federation na kutoijumuisha ardhi kama sehemu ya jumuiya sijui yakuwa maamuzi ya JK au ni ya wananchi baada ya kupiga kura ya maoni? naomba nikuulize hilo wewe. uamuzi wa kutekeleza mapendekezo ya kamati ya bunge ya RICHMOND sijui ulikuwa ni wa serikali ya JK au matakwa ya watanzania kupitia BUNGE, na uamuzi wakuwa na serikali ya mseto ZANZIBAR sijui kama ni kuwa CONSENSUS ORIENTAL au la?
Hapa labda kama na wewe unataka kuwa RAIS, maana nadhani kama kuna mtu anataka usawa wa rasilimali watu hadi za nchi ni JK kumbuka haya kwani umesahau kugawa mashamba ya nafko kwa wananchi, kurudisha mgodi wa kiwira serikalini, kuonge nafasi za upendeleo kwa wasichana kwenye sekta ya elimu ilitu kulinganisha japo sio kuwa sawa. kuwajibisha tabaka zote za wananchi bila nafasi pale ulipo shutumiwa au kupatwa na hatia ya dhana nzima ya maadili.
Nawajibika kidogo then nitarejea na majibu ya unayajiita haki/kipofu kwa mtizamo wangu.
kutomchagua Slaa ni kuendeleza ufisani na maovu yote kijamii yaliyokithiri hadi sasa nchini na kutufikisha hapo tulipo; na kupiga tu madebe ya kutuchanganya kijamii ni kuendeleza ufisadi wa akili na upeo wa kuelewa demokrasia ya kweli yaani uongozi unajaa uwazi na ukweli katika maslahi ya jamii na si ya mtu binafsi alivyofanya bb wa taifa.
send to all!
ANAFAA SANA HATA KIKWETE HAONI NDANI
KWANZA KABISA NAOMBA KUITUMIA NAFASI HII KUWAPONGEZA WANAMJADALA.NIKIWA KAMA MTANZANIA NINAEISHI NJE YA NCHI NINAWASIHI WANANCHI WENZANGU KUACHA USHABIKI WA KISIASA KAMA NDUGU YANGU GEOGE NA KUITUMIA HII NAFASI MUHIMU KWA UFASAHA.TUANGALIE MIFANO HALISI IKIWA NI PAMOJA NA UCHAGUZI WA RAIS OBAMA.ILIONEKANA KUWA OBAMA HAKUWA NA UZOEFU UKILINGANISHA NA WENZAKE VILEVILE AMETOKEA KATIKA TABAKA LA CHINI LAKINI ALICHAGULIWA KUTOKANA NA HALI ALISI YA KIUCHUMI ILIYOSABABISWA NA UTAWALA ULIKUWEPO MIAKA MINANE YA BUSH.KWA HIYO ILIWABIDI WACHUJE MBICHI NA MBIVU .JE KWETU SISI WATANZANIA NI LINI TUTAAMKA KUJIKOMBOA KUTOKANA NA SIASA ZA VITISHO?.WEWE NDUGU YANGU UNAESEMA KUWA KUNA MENGI MAZURI YALIYOFANYWA NA KIKWETE,NAKUOMBA UYATAJE.MIMI NGUGU YAKO NINACHOJUA NI KWAMBA AMEYAFANYA MENGI SANA NA YOTE NI MABAYA.NA NIKIPATA NAFASI NITAKUELIMISHA.J.K KAMA MNAVYOMUITA ALIPOCHAGULIWA AWAMU YA KWANZA ALIKUJA WASHINGTON DC AKISEMA KUWA AMEACHIWA PESA NYINGI SANA NA MKAPA,MUDA SIYO MREFU AKAANZA KUOMBA MISAADA KULIPIA HATA MISHAHARA NA ALIPORUDI DC TUKATAKA KUMBANA ILI TUJUE UHALISI WA MAENDELEO AKAAMUA KUTUKIMBIA KABISA NA HATA AKIJA MAREKANI HATAKI KUONANA NASI.NA MIMI NA WENZANGU TUMEKATA TIKETI TUKIWA NJIANI KUJA KUPIGA KURA.SI MANENO MATUPU BALI NA VITENDO PIA.NAWASIHI WENZANGU TUITUMIE NAFASI HII PEKEE KWANI “GOLDEN CHANCE NEVER COME TWICE’
we unayejiita kubwa kuliko angalia usije ukawa mdogo kuliko kwani kila alikwezae hushushwa na kila ajishushae hukwezwa
toa maoni yako lakini watch your mouth na PREASIDENT wetu. we unadhani unalipi hasa la kutu saidia sisi watanzania kwa kuwa kwako marekani? au unafikiri kuwa marekani ndo maendeleo? kwanza inawezekana hata upo uko kwa mkono wa serikali, au wasamaria wema kwa misingi ya scholarship, au hata kwa kuzamia.
nnachoona cha maana katika yako ni uzalendo wa kuja kupiga kura tu. ila JK hawezi kukutolea milio wewe, fanya kilicho kupeleka us na usilipuke hovyo, alafu tukianza kutajiana hapa kuwa tuko wapi? au tulisha fika wapi? unaweza kuchoma hako kaviza kako kijana. lets debate on the reality and not trash gossips just as what your doing.
main issue hapa ni election na sio wewe na mikogo yako nipo state, inawezekana kabisa upo kiembe mbuzi au USA-RIVER ukadai upo state, i want you to know that your not the haedline here so shut you big boast n talk about Dr.SLAA n Hon.J.KIKWETE
GET it you dogokuliko!!
Labda nianze kwa kumpongeza ndugu Mtanzania Msikivu kwa maoni yake yenye hekima na ustaarsbu. Nakubaliana naye kwamba utamu wa majadiliano ni hoja za kistaarabu na sio lugha ya kudhalauriana.
Pili nimeshindwa kumuelewa alivyosema katika wagombea wote aliye afadhali ni DR SLAA. Japo naheshimu haki yake ya kumchagua yeyote amtakaye hata bila kuwa na sababu, lakini naamini kwamba kwenye janvi kama hili lenye watu wengi wenye maoni na mitazamo tofauti ubora wa hoja ni kutoa vigezo unavyotumia kumuona nani ni bora kuliko nani badala ya kutoa hitimisho bila ya takwimu na uchambuzi wake.
Umetambuwa maendeleo yaliyofikiwa na serikali ya CCM katika elimu lakini ukakosoa shule za kata kwa upungufu wa waalimu na vitendea kazi. Kwa maoni yangu kati ya yai na kuku lazima kiwepo kimoja kinachotangilia kingine. Huwezi ukaanza na vyote kwa wakati mmoja. Huwezi kuanza na walimu na vitabu wakati huna shule na wala huwezi kuanza na vyote kwa wakati mmoja. Unakumbuka hata mwalimu alipobuni utaratibu wa elimu ya msingi kwa wote, alianza na madarasa kwanza. Wanafunzi waliomaliza darasa la saba walitumika kuwafundisha wenzao huku serikali ikifanya utaratibu wa kupata waalimu wenye sifa kwa kuwaendelezea hao hao na kusomesha wengine. Ni kweli matokeo mwanzoni yalikuwa mabaya lakini kadili muda ulivyozidi kuenda walipatikana waalimu zaidi na vitendea kazi. Hamna asiyeona juhudi za makusudi serikali inazofanya kwa kuandaa waalimu wenye vyeti, stashaha na shahada. Vyuo vingi vilivyokuwa vya kawaida vya ualimu vimepewa hadhi ya vyuo vikuu. Chuo Kukuu cha Dodoma kina shule nzima ya ualimu. Serikali imegharamia masomo ya waalimu katika vyuo vikuu vya serikali na binafsi. Vijana waliomaliza kidato cha sita wamepewa mafunzo mafupi na kusaidia kufundisha hizi shule za kata. Na kwa mtu anayefanya tathimini kwa uaminifu atakubaliana namimi kwamba kuna mabadiliko makubwa katika shule za kata. Acha mifano inayotolewa na mashabiki wa siasa ambao watakupa mifano tu ya shule zinazofanya vibaya.
Kwamba DR SLAA hajaeleweka katika sera yake ya elimu ya bure nadhani tunamtia maneno mdomoni mwake. DR SLAA amekuwa akiweka wazi kwamba suala la elimu bure ni la mara moja na siyo mipango ya muda mrefu kama unavyosema. Labda iwe ni lugha yako ya kidiplomasia ya kusema kwamba ahadi za DR SLAA ya elimu bure haitekelezeki bila kuwa na mikakati na mipango ya muda mrefu.
Kwamba wapinzani hawajaonesha mikakati ya kubomoa mfumo uliopo wa uchumi na kuleta mfumo mwingine nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa. Nakubaliana nawe kwamba mambo mengi ambayo DR SLAA pamoja na wengine wanayalalamikia yanaotokana na Tanzania kugeuza mfumo wake wa uchumi toka ujamaa kwenda mfumo wa uchumi huria ambao msingi wake ni ubepari. Sababu zilipelekea mabadiliko hayo ni za kihistoria ambazo, kama ulivyosema kwa usahihi ni kushindikana kwa utekelezaji wa mfumo wa ujamaa kutokana na sababu nyingi zilizoanza kujitokeza mwishoni mwa miaka ya sabini. Kabla ya hapo watanzania tulikuwa tunapata elimu bure, afya bure na huduma nyingine nyingi za kijamii. Kuingia kwetu katika mfumo wa kipebari hakukuwa kwa kutaka kwetu bali tuliwekewa misumari katika pande mbili na kuchagua msumari nafuu na tukaona ni kuingia katika ubepari ili tuweze kupata misaada kwa masharti wakubwa watakaotuwekea. Moja wapo ya masharti ilikuwa ni kuchangia huduma za umma, kubinafsisha mashirika ya umma na kuweka masharti rahisi ya uwekezaji wa nje.
Sasa kama Tanzania tuna nguvu na uwezo wa kujichagulia mfumo wetu wa kiuchumi tofauti na sehemu zingine za dunia na kwa kiwango gani si suala la kisiasa tu la kutamka majukwaani bali linataka mambo mengi.
Uwezi ukazungumzia kutoa elimu ya bure, afya bure bila kuwa na mikakati ya kubomoa mfumo wa sekta binafsi ambao unaratibiwa na nchi zilizoendelea na kuweka mfumo wa ujamaa ambao ulikuwa unaratibiwa na nchi zilizoendelea za kijamaa ambazo kwa sasa zimeshasambaratika. Vinginevyo uwaandae watanzania kufunga mikanda.
Ndugu Barhe sina matatizo naye maana yeye kaamua kusimama katika chama chake bila kujali kama hoja tulizozitoa ni za msingi au la. Sababu kubwa aliyotoa kwa kuchukua msimamo huo ni kuogopa kuchanganywa na hoja za wachangiaji. Hata mimi namuombea Mungu asichanganywe na hoja bali apate taarifa sahihi.
Ndugu Kubwa Kuliko simshangai maana yeye anaishu ughaibuni. Bila shaka hali halisi ya Tanzania anaisikia sikia kwa kusimuliwa tu. Hawezi kushindana na sisi ambao mafanikio na mapungufu ya Kikwete tunayaona.
Nilitegemea angesema mazuri aliyoyafanya Kikwete kama tulivyoyarudia mara kwa mara katika hoja zetu hayapo. Ajabu anataka turejee tena kumtajia. Bahati mbaya hasemi ni lini alitoka Tanzania. Asije akawa kama rafiki yangu fulani tuliyesoma naye shule ya msingi kule kijijini baadae akabahatika kweta Ulaya na kusoma hadi kidato cha nne na kozi fupi ya computa. Aliporudi Tanzania nakuja kijijini mwaka juzi alianza kujigamba kwamba yeye amesoma hadi kidato cha nne na kozi fupi ya computa akidhani Tanzania ya leo ni sawa na ile aliyoiacha ambayo mtu alibahatika kusoma hadi kidato cha nne alikuwa akinyoshewa kidole cha kushangaa kila anapokwenda. Leo elimu ya kidato cha nne, kidato cha sita na chuo kikuu ni kitu cha kawaida sana hapa Tanzania.
Rafiki yangu mwingine naye alipotaka kurudi nyumbani alinipigia simu na kunitaka nimfanyie booking ya usafiri wa treni kwenda Nzega kwa sababu alikuwa na wiki moja tu ya kukaa Tanzania na alitaka azitumie vizuri siku sita kwaajili ya usafiri wa kwenda na kurudi Nzega na siku moja kuwasalimu wazee. Nilivyomuambia Nzega siku hizi ni masaa tu kwa basi alinishangaa sana.
Kwamba DR KIKWETE alikuja Washingtone na kutamba kwamba ameachiwa fedha nyingi na Kikwete ni maneno ya kawaida kutamkwa katika majanvi kama haya. Mwingine anaweza kusema Raisi Obama alikuja Tanzania na kutambia fedha alizoachiwa na Bushi tukamsikiliza kwaajili ya kuchangamsha baraza.Sio lazima kila siku tusome habari za kweli siku nyingine tunategemea kusikia nyepesi nyepesi kama hizi kwa wenzetu wanaofaidi maisha huko viwanja.
Katika gazeti la Raia Mwema la wiki hii, DR SLAA ananukuliwa kuwashughulikia vigogo 11 na kuwamaliza ndani ya miezi sita. Wakati huo huo anasema hataingilia vyombo mbali mbali vya serikali vilivyopo na kwamba ataviacha vifanye kazi kwa uhuru.
Tamko hili la DR SLAA linaacha maswali mengi bila majibu. Hivi inawezekana DR SLAA kuwamaliza vigogo hawa ndani ya miezi sita bila kuingilia uhuru wa vyombo vya dola kama vile ofisi ya Mkurugenzi wa Masitaka na Mahakama? Baadhi ya vigogo anaowataja ni mheshimiwa Raisi DR Kikwete na mheshimiwa Raisi Mstaafu Benjamini Mkapa. Hii haiwezi kuleta picha ya visasi vya kisiasa? Hii haiwezi kuashiria nia ya utawala wa kidikteta? Inamaana DR SLAA yeye ni mpelelezi kuliko wapelelezi wote, ni judge kuliko majaji wote na ni shahidi kuliko mashahidi wote? Kwa tafsiri ya kawaida kuwamaliza hao anaowaita vigogo ndani ya miezi sita hakuwezi kumaanisha kwamba ameshawahukumu kabla ya kuwasikiliza na anasubiri rungu tu awashughulikie?
Mimi naamini kwamba ukomavu katika hekima na busara ni sifa ya lazima kwa mtu kustahili nafasi ya uraisi.Kama wagombea wote watasema kwamba wakishinda watawashughulikia wenzao wengine wanaweza hata kuondoa majina yao. Ni bora wagombea wakazungumzia mambo mazuri watakayowafanyia watanzania wenzao pamoja na wagombea wenzao badala ya kuwatabiria virungu.
Bwana George sijui nikupongeze kwa staili ipi? kwani kwa ufafanuzi huu mtu anaweza kudhani kuwa we ni mtu wa miaka mingi sana au umekaa serikalini kwa muda mrefu sana.
Nirudie tu kusema kuwa sitegemei kuona mpinzani yeyote akihubiri mazuri serikali iliyo yafanya, kwasababu tayari wana dhana ya upinzani vichwani mwao,
nina kazi nyingi leo ila nita wasilisha mchango wangu baadae…..
wote mnapiga kelele tuu, yaani kma mnge kuwa mnajua basi, slaa angebaki kucover nafasi ya ubunge ili azidi kuleta changamoto akiungana na ndugu za freeman, ,mrema mropokaji na wengineo sasa ukifuata mkumbo katika taifa dogo kama hili, basi jua unajijengea taifa ombaomba hati vitukuu wako watakao zaliwaa. tanzania ya leo na kesho iko mikononi mwako, pigia kura upinzani kupunguza makali ya mafisadi na ombaomba wakimataifa.
Jamani,muda wa kuongoza nchi ni miaka mitano tu then uchaguzi unafanyika.Kwa nini badala ya kuendelea kuumia tusijaribu kuwapa ruhusa wapinzani tuone hayo mabadiliko wanayodai wataleta kama yatakuja.Ikishindikana tunarudisha Chama tawala.Sio kung’ang’ania tu kuwa wapinzani waongo,tutaendelea kuumia milele na milele…Tuthubutu Kujaribu jamani!
Ndugu yangu Samson nashukuru sana na pia nakupongeza kwa hoja zako nzito zenye kujenga. Nawapongeza na wachangiaji wengine wa upande wa pili hasa wale waliojitahidi kuchangia kwa uvumilivu.
Sisi kama watanzania wazalendo tunajukumu la kuelimisha umma katika mambo nyeti kama haya. Najua baadhi ya watanzania ni wepesi wa kuchoteka na ufundi wa kupinga. Niliwahi kusema huko nyuma kwamba hamna kazi rahisi kama kukosoa serikali iliyopo madarakani. Urahisi huo unatokana na ukweli kwamba serikali zinaongozwa na wanaadamu wenye mapunguvu na hivyo haziwezi kukosa mapungufu.
Wananchi kama wanaelezwa mapungufu bila kuelezwa mazuri wanaweza kuwa na nafasi ndogo ya kuchambua na kuamua ukizingatia kwamba wapinzani wengi wanayachukua mapungufu na kuyatia chunvi.
Kwa upande mwingine wapinzani wana faida ya kwamba hawajawahi kushika dola na hivyo hawana kipimo cha uwezo wao wa kuongoza dola. Mara nyingi utamsikia kila mpinzani akisema jaribu upinzani. Humsikii mpinzani akisema ni mambo gani ya maana aliyoyafanya kwenye chama chake ili japokuwa yatusaidie kumtathimini? Ni uzoefu gani wa uongozi mwingine hata kama nje ya chama tunaoweza kuutumia kumpima. Bahati mbaya katika kampeni zao hawataji waliyoyafanya katika chama wakati CV yao kubwa waliyoingia nayo katika mambo ya uongozi ni ukatibu au wenyeviti wa chama. Sasa kama wewe katibu mkuu wa chama umeshindwa kuweka misingi imara ya chama katika sehemu zote za nchi kwa zaidi ya miaka kumi na tano, utaaminiwa vipi na kupewa dola? Ukisema hilo kwa nia njema kabisa ya kizalendo unaambiwa mshabiki wa CCM.
Kwa ndugu yetu Bwana DJ mtu yoyote anaesema DR SLAA bado anaonekana anapiga kelele.
Ndugu wanamtandao bado tunahesabu masaa kabla hatujatumia haki yetu ya kupiga kura. Naomba nitumie nafasi hii kuwatakieni uchaguzi mwema na wenye amani.Ningeomba tuzingatie yote ya msingi tuliyoyajadili hapa badala ya kuchagua kwa ushabiki tu.
Naomba baada ya uchaguzi tukutane tena kwaajili ya kutathimini matokea ya uchaguzi. Kwa mazingira yalivyo naamini DR KIKWETE atashinda kwa kishindo kikubwa.
Niungane na wanamtandao kumpongeza DR KIKWETE na chama chake kwa ushindi mnono. Na pia niwapongeze wapinzani kwa kutoa upinzani mkubwa
hawezi kuwa rais kwani tatizo ni chama chake kilimumweka agombee nafasi ya urais kwa sababu mboye amekaa kimaslai mno anatakiwa kuwa makini kipindi kijacho lasivyo hatakuta mwana si wake wachaga siyo watu yeye kama dr slaa ni mtu safi bali waliomzunguka.
Dr. Slaa anaweza ila shida ni wenzake kwenye chama kama watamwuunga mkono maana kumbuka chama chake wachaga kibao na ndio mabosi wake je watamruhusu tena?Kumbukeni yaliyomkumba Zitto Kabwe alipotaka kupambana na mbowe kuwania Unyekiti wa CHADEMA na hata alipotaka uongozi wa kambi ya upinzani bungeni.