Here is the official video for R.Kelly’s “When A Woman Loves” from his upcoming Love Letters EP to be released soon.When a woman loves…she loves for real.His words,not mine.

Former Big Brother Africa housemates(BBA4),Kevin Chuwang Pam(from Nigeria) and Elizabeth Gupta(from Tanzania) who recently announced their engagement, are now about to move into the really thing;marriage.
According to a source close to the couple, they are planning to tie the knot this coming December in Nigeria.Kevin is expected to visit Tanzania sometimes soon to meet Elizabeth’s family and adhere some customs and traditions before the big day.
Kevin was the winner of BB4 and many Tanzanians still remember how he embraced the Tanzanian flag when he was declared a winner.

Kuna kitu nimekipenda katika kuitazama kwa makini picha hii.Bahati mbaya siwezi hata kuelezea vizuri ni kitu gani nilichokipenda katika picha hii ya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) walipokuwa wakimshangilia mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho,Dr.Wilbrod Slaa,wakati wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho katika viwanja vya Jangwani jijini Dar-es-salaam.
Ni matumaini, ni saa ya ukombozi,ni kwamba tumechoka sasa au?
Picha kwa hisani ya John Bukuku.
“Kama maisha tumejaliwa,kama vipaji tumeshapewa,kwanini leo tuogope?Wanafiki tuwashangae,Wanachekesha”
Si maneno yangu bali maneno kutoka kwa vijana wa TMK Majita.Yamo katika wimbo wao walioutoa hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wanachekesha.Hii ni production kutoka Sound Crafters Studio chini ya Producer Enrico na Muba Touch.Burudika.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

JKN

JK

JKN

Naomba uniwie radhi msomaji wa BC kwa kimya kidogo kilichojitokeza hapa BC.Wiki hii ilikuwa ya majonzi.Nilipatwa na msiba wa kuondokewa na Babu Mkwe wangu Mzee Anselm Lyander(1928-2010).
Kutokana na msiba huo,mambo yakawa mengi na nguvu ya kuandika ikapotea ghafla. Shukrani kwa wote mlionitumia ujumbe kutaka kujua kulikoni.Kwa bahati mbaya sijapata muda wa kuwajibu nyote.Sababu ya msingi ni msiba huo.Maadam Babu amekwisha pumzishwa katika nyumba yake ya milele,hatuna budi kuendelea na maisha.
Tunapoendelea na maisha,tafadhali sikiliza nasi,kibao cha Jabali la Muziki,Hayati Marijani Rajabu na Dar International kiitwacho Rufaa ya Kifo
Kama ingelikuwa binadamu anakata rufaa ya kifo,Oh oh, kinapotokea,mbele ya Mungu na mimi ningekata rufaa, nirudishiwe wangu eeh, niliyempenda hapa duniani lakini nimeshindwa sijui nifanyeje….
Pumzika kwa amani Babu.Bwana alitoa na Bwana ametwaa.Jina lake lihimidiwe.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Jina la Madaraka Nyerere(pichani) sio geni miongoni mwa watanzania.Ukiachilia mbali ukweli kwamba yeye ni mtoto wa sita wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kitu ambacho bila shaka kinampa automatic celebrity status), yeye pia ni mwandishi,mfanyabiashara na mtu ambaye huwa hasiti kuelezea hisia zake kuhusu mambo mbalimbali iwe ni katika nyanja za kisiasa,kijamii na hata kiuchumi kila mara fursa ya kufanya hivyo inapojitokeza.
Mwaka jana mwezi wa nne(April) yeye na Jaffar Amin(mtoto wa Iddi Amin-Rais wa zamani wa Uganda) waliingia katika vitabu vya kumbukumbu vya wapenda amani duniani walipokutana kwa mara ya kwanza ikiwa ni ishara ya amani na usuluhisho barani Afrika na kwingineko.
Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza naye kuhusu mambo kadhaa yakiwemo ya kifamilia na pia kupata maoni yake kuhusu mambo mbalimbali.Je,ni kwanini mpaka leo hii hajajiingiza katika masuala ya siasa au uongozi?Anamuelezeaje Hayati Baba wa Taifa kama baba yake na kama kiongozi?Ana ushauri gani kwa wapiga kura katika mwaka huu wa uchaguzi? Ana mtizamo gani kuhusu viongozi mbalimbali ambao hupenda kumuenzi Baba wa Taifa kwa maneno huku vitendo vyao vikiwa tofauti kabisa? Unataka kujua kwanini alipewa jina la “Madaraka”? Ana ushauri gani kwa vijana kuhusu suala zima la kujiletea maendeleo? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Madaraka,asante sana kwa kukubali kufanya nami mahojiano haya. Kwa faida ya wale ambao hawawajui watoto wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere,nyumbani kwenu mmezaliwa watoto wangapi na wewe ulizaliwa lini,ukasomea wapi na kukulia wapi?
MADARAKA NYERERE: Tuko watoto nane. Mimi wa sita. Nimesoma shule
zifuatazo:
-Shule za msingi: Bunge, Forodhani, Arusha School, Isike (Tabora), Tarime.
-Sekondari: Mzizima, na Tambaza (Dar)
-Post-secondary: Shinyanga Commercial Institute
-Vyuo: Finafrica College (Milan, Italy); Algonquin College (Ottawa, Canada)
BC: Turudishe kidogo wakati wa utoto wako.Ni kitu au tukio gani unalolikumbuka zaidi kuhusu utoto wako?Na ulikuwa na ndoto za kufanya kazi gani utakapokua?
MADARAKA NYERERE: Sina tukio lolote kubwa ninalokumbuka la utotoni. Nahisi baada ya kuanza masomo ya biashara kuanzia kidato cha tatu, tayari nilianza kuwa na mawazo ya kuwa mfanyabiashara. Kabla ya hapo, sikumbuki kama nilikuwa na ndoto za kufanya kazi nyingine.
BC: Uliwahi kuelezwa kwanini ulipozaliwa ulipewa jina la Madaraka?Ilikuwaje kukua kama mtoto wa Rais au katika mazingira ya Ikulu na mambo kama hayo? 

Miss Universe Tanzania 2010,Hellen Dausen,will be onstage tonight to proudly represent Tanzania at the global Miss Universe 2010 beauty pageant.
TheMiss Universe 2010 which is the 59th edition of the pageant,will be held at the Mandalay Bay Events Center in the Mandalay Bay Resort and Casino,Las Vegas-Nevada,US. It will be hosted by Bret Michaels and Natalie Morales.It will be broadcasted Live on NBC starting at 9pm Eastern Standard Time.
Goodluck Hellen.
UPDATE: The Miss Universe Pageant is Live right now on NBC.That comes with a bit bad news;The top 15 contestants have just been announced and Hellen Dausen is not among them!That means,once again,we gonna have to wait and hope for next year.The only contestant from Africa who is in top 15 is Miss Universe-South Africa.
Top 10: Ireland,Albania,Philippines, Jamaica,Mexico,Ukraine,Puerto Rico,South Africa,Guatemala and Australia.
Miss Congeniality: Australia
Miss Photogenic: Thailand
National Costume Award Winner: Thailand
Top 5: Mexico,Jamaica,Ukraine ,Phillipines and Australia
4th Runner Up:Phillipines,
3rd Runner Up: Ukraine
2nd Runner Up: Australia
1st Runner Up: Jamaica
MEXICO WINS MISS UNIVERSE 2010!
Miss Universe 2010: Mexico


sending...
