Pamoja na kwamba inasemekana kampeni za uchaguzi hazijaanza rasmi au hazitakiwi kuwa zimeanza,ukweli ni kwamba kwa namna moja au nyingine,kampeni zimeshaanza.Huu ni ukweli ambao Tume ya Uchaguzi lazima waukubali ili marekebisho yafanyike endapo wanataka kuwa makini zaidi katika kuhakikisha kwamba vyama vyote na wagombea wote wanasubiri mpaka tarehe 20 Augosti siku ambayo ndio kampeni rasmi zinatakiwa kuanza.
Tunathubutu kusema hivyo kwa sababu tayari tumesikia mara kadhaa viongozi/wagombea mbalimbali wakijinadi kwamba wamefanya nini katika miaka mitano iliyopita na wanatarajia kufanya nini endapo wananchi watawapa tena dhamana ya kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano.
Pia tumeshasikia tambo mbalimbali kutoka kwa wanaowania kuunda serikali mpya,wakijinadi kuhusu watakachokifanya tofauti endapo “ngekewa” ya kuwaongoza watanzania itawaangukia wao.Sasa kama tambo hizo sio sehemu ya kampeni,sijui Tume ya Uchaguzi ina tafsiri ipi kuhusu maana ya “kampeni”.
Bila shaka,baada ya kuwasikia wagombea mbalimbali wakijinadi na kutokana na uzoefu wako na jinsi unavyofuatilia shughuli mbalimbali za kisiasa,umeshafanya maamuzi(japo katika fikra tu) kwamba pindi itakapofika mwezi Octoba,kura yako utampa mgombea fulani.Ndio maana tunauliza;Uchaguzi Ungefanyika Leo,Ungemchagua Nani?Kwanini? Wanaogombea nafasi ya Urais kutoka vyama mbalimbali,hawa hapa:

Civic United Front(CUF): Professor Ibrahim Haruna Lipumba(kulia) na mgombea mwenza,Juma Duni Haji.

Chama Cha Mapinduzi(CCM):Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Mwenza,Dr.Gharib Bilal.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
r.Wilbrod Slaa akisalimiana na Mgombea Mwenza,Hamisi Mzee Hamisi.

National Convention for Construction and Reform-Mageuzi(NCCR-Mageuzi)-Hashim Rungwe(kushoto) na Mgombea Mwenza,Ali Juma.
Feedback / Comments
38 Responses to “ENDAPO UCHAGUZI UNGEFANYIKA LEO,UNGEMCHAGUA NANI?”
Leave a Reply


sending...
Ningemchagua Kikwete.Angalau sasa nina rekodi yake.Hao wengine naona wanaganga njaa tu
Chaguo langu lingekuwa Dr.Slaa.Jamaa yupo makini.
JK hana mpinzani.Ushindi kama wa Kagame hivi 92%
kwa ajili ya haki na hadhi ya wa Tz, kura zangu nitampatia Slaa
Dr Slaa anatisha,asiposhinda 2010,basi lazima 2015 awe rais
SLAA IS THE BEST..
Mimi ningempa kura yangu Mh. Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi, kwani ni Lawyer makini na anaouwezo wa kuwaletea watanzania wa chini mabadiliko yanayotakiwa. Ni mtu ambaye ameishi na watu wa chini na anajua matatizo yao kinaga ubaga.
Ndugu wana BC,
Kufuatana na kifungu 0,1a,2001 cha taratibu za habari haba BC, napenda kufikisha malalamiko yangu juu ya ubaguzi wa kisiasa ambao blog yetu pendwa ya BC imetutendea. Tunashangazwa na kupigwa bumbuwazi tukijuiliza, mbona kiongozi wetu wa TLP Mh. Mutamegwa Mganywa hakutokea katika picha ya mbele. Kitendo hiki kimetudhalilisha sana, kimetufedhehesha sana. Tunajua tatizo ni huu urais na tupo tayari ku grant!
Ni Kikwete tu amalize mazuri aliyobakisha na bila kuficha kwamaendeleo yako ni kikwete na sio sera za kufikirika na kusadikika
Jamani mbona hakuna aliemtaja Lipumba au ndo kusema jamaa kaisha kisiasa? mie ningevote for DR. wa ukweli hao wengine porojo tu!! SLAA juu
Uchaguzi sio swala la mzaha!
Mtu unapokwenda kupiga kura ni lazima akili yako iwe makini katika kukielewa unachotaka kukifanya. Unachagua mtu atakaye kusaidia kukuinua hali yako ya maisha katika nyanja nyingi sana.
Waomba kura huja na ahadi kibao ambazo usipokuwa makini unaweza ukaingia mkenge kwa kuwaamini katiaka ahadi zao. Chunguza kwanza ahadi hizo kama kweli zinawezekana kwa kuangalia hali halisi yako mwenyewe na hali halisi ya Watanzania wenzako na serikali kwa ujumla.
Kwa mfano, mgombea anakuja na ahadi ya kuwalipa wafanyakazi wote kima cha chini shilingi laki tatu kila mmoja. Wakati bajeti ya serikali haitoshi kulipa hivyo. Je, unafurahi kupewa ahadi hewa kama hiyo na mgombea huyo?
Nchi nyingi za Ulaya, wananchi wake wengi wako makini sana na wagombea wa aina ya watoa ahadi hewa, na matokeo yake wananchi huwatoa patupu wagombea hao kwa kutokuwapa kura.
Watanzania sasa tumekomaa kisiasa. Tusiendeshwe na wanasiasa uchwara kama hawa wanaoibuka sasa hivi, wanaotaka kuganga njaa zao kwa kupitia migongo yetu. Tuwakatae bila ya huruma wala haya katika sanduku la kura zetu, lakini rushwa zao tuzichukue.
Mtu kakuletea mwenyewe hela yake, kukupa rushwa, kwanini usiichukue?. Takukuru mtuonee huruma sisi wapokea rushwa. Tunazihitaji sana pesa kwa matumizi yetu mbali mbali binafsi. Tutampa kura tumtakaye sisi, na siyo yule anayetupa fedha.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Blackmannen nasikitika kusema kuwa hoja zako hazina msingi wowote! Wewe ni miongoni mwa waTanzania walio wengi, ambao bado wanachelewesha maendeleo ya nchi yetu. CCM wamefanikiwa kuwafanya wananchi kama “Blackmannen” kuamini kuwa serikali yetu haina pesa za kuwalipa wanachi wake kima cha chini cha mihahara inayofanana na gharama za maisha, kitu ambacho si kweli. Katika kukufahamisha kuwa inawezekana wakulipa raia wema wa nchi yetu kima cha chini cha mishahara kuwa laki 3…..naomba ujiulize maswali haya machache ya msingi:
1) Ni pesa kiasi gani tumesikia zimepotea katika masuala ya ufisadi chini ya serikali ya CCM?
2) Je pesa hizo zisingetumika katika kuongeza pato halisi la nchi na hatimaye serikali kuweza kuwalipa wafanyakazi wake kima cha juu cha mishahara tofauti na ilivyo sasa?
3) Ni rasilimali ngapi za nchi yetu hazijatumika kwa ajili ya kumuendeleza mtanzania wa chini, na badala yake wananufaika wawekezaji uchwara, ambao wanakula na vigogo wa CCM?
4) Kuna tofauti gani kati yako wewe unaewashauri wanachi wachukue rushwa za wanasiasa wanaoganga njaa na hao wanasiasa wanaotoa hizo rushwa? Je na wewe haugangi njaa kwa kupokea rushwa? Dawa ya moto sio moto ndugu yangu.
Kama utaweza kujibu maswali haya machache kwa ufasaha ndugu yangu Blackmannen utagundua kuwa bado haujawa mkweli katika ushabiki wako wa kisiasa.
mh! shughuli sio ndogo uchaguzi wa mwaka huu coz Kikwete ndo mtetezi wa taji but Dr Slaa yupo juuu so naamini ataleta upinzani mkubwa
Ningemchagua Dr. Slaa coz yupo makini na ameonesha nia ya kutaka kura zetu sisi wafanyakazi watumishi wa nchi hii.
Prof. Lipumba uko juu baba sema basi tu wananchi sio waelewa….wanashabikia watu ambao hata cv zao kuzitaja ni aibu hasa ukiambiwa anataka kuwa raisi wa nchi kama tanzania..
mabadiliko/maendeleo ya kweli hayaji kwa watu tunaowaelewa historia yao ya kushindwa kwa imani eti sasa wameelewa na watajirekebisha.Watanzania mbona hatusemi ukweli kuwa CCM haifai kabisa kuongoza tena? ufisadi na rushwa zenye kuangamiza nchi mbona ndio sera yao?
NAWASIHI SANA NA NDIO CHAGUO LANGU TUMPENI PROF.LIPUMBA ALETE MAENDELEO NA MAFANIKIO.
Dr slaa. manake ni mtu makini katika kufuatilia mambo ya msingi haendani na matukio kwa ushabiki kama JMK
kazi kweli kweli…
Tumepita katika kipindi kigumu sana kwa mchakato wa mageuzi toka chama kimoja kushika hatamu za uongozi mpaka hapa tulipo sasa.Mara nyingi tumewashuhudia wawakilishi wetu bungeni na katika vyombo mbalimbali vya kufanya maamuzi ya kulinda maslahi za wanyonge walio wengi katika taifa hili wakitetea uovu na kuutukuza huku wakisahau kutenda haki inayostahili.
Kana kwamba haitoshi wachache hawa wameamua kujinufaisha wenyewe na kuwatetea wawekezaji wageni kwa nguvu zote ikiwamo matumizi ya nguvu/vyombo vya dola dhidi ya wazawa. Nikisema hivi;tumeshuhudia watu wakazi na wenyeji wa maeneo ya migodini wakipoteza maisha yao kwa kuwatetea wageni wachache. Ni CCM ndio walioshika nchi hii na kusaidia kuigawa tena kwa wakoloni hawa wa KISASA kwa gahrama ya bureeeeeee!
Nikiacha porojo nyingi, tazama kwa kina hoja ya wizi katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) walisema Dk.Slaa ni mwongo uthibitisho uliopo ni aibu kwa kila aliye madarakani. Endelea kutazama minara ile pacha ya BOT mamaaaaaa naumia sana mwenzenu! Tazama migodi ya dhahabu kule Buzwagi, Bulyahulu, North Mara, Geita kisha uchungulie kidogo pale Mererani kuliko na ile tanzanite adimu kabisaaaaa duniani.
Habari ya mchuchuma na makaa ya mawe kule Ludewa na Kiwira yote haya yametetewa kwamba ni maamuzi sahihi na hao walioshika mpini.
Maonevu mengi yanafanyika bila huruma yoyote kisha wananchi wanaletewa kejeli na kudharauliwa hadharani na katika vyombo vikubwa vya habari.”KAMA NI HIZO KURA TU BASI NIKO TAYARI KUZIKOSA” hii ni aibu kwa mtu tuliyempa dhamana kubwa ya maslahi ya watanzania kuwakejeli kiasi hiki!
Dk. Slaa ni mtu makini natamka kwa ujasiri watanzania wenzangu mnisamehe kwa kutumia lugha ya kuazima “HE IS A GREAT BITING WATCH DOG OF OUR RESOURCE, HONOR AND DIGNITY” mwisho wa kuhama lugha. Nawaomba chondechonde watanzania tuache uCCM,uCUF,uTLP,uCHADEMA,uNCCR nk.tumpe ofisi huyu ndugu anaweza kutuongoza kwa kushirikiana na wapenda maendeleo wenzake ili tuvuke daraja hili la umaskini wa kujitakia kwa kuweka uongozi mbovu madarakani.
Kumbukeni kwa makini maneno ya mwalimu ili tuendelee tunahitaji ARDHI,WATU,SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Tumekosa uongozi bora lakini tunaiona lulu safi (DK.SLAA) ikichezewa na kuchafuliwa na hao wajanja wanaojihami na kuona aibu inayokuja. HIMA WATANZANIA WOOOOOOOOOOOTE! HAYA SHIME TUAMKE TWENDENI TUMPE KURA YA NDIYO SHUJAA NA MTETEZI WETU!
hapa panahitaji utulivu..mmh kazi ipo…
Nampa Dr. Slaa kwasababu zifuatazo: Nimedhibitisha ufanisi wake kwa miaka michache tuliyompa bungeni hakuboronga hata kidogo na alikua makini. Hakuwa kama mtawala bali mwakilishi kwa wananchi waliomtuma. Sitakaa nimpe Kikwete mahali popote atakapojaribu kupigania uongozi kipindi chote nitakachokua hai kwasababu:
Anarudia makosa yale yale waliofanya viongozi waliopita wa chama chake na “huwezi kurudia rudia kitu hicho hicho ukategemea majibu tofauti”. Pili ameonyesha kuwa mtu anayependa kuwa mtawala/kuabudiwa na sio mtumishi wa watu waliomchagua. Hii ni kutokana na kauli zake na matendo yake nafikiri sote tunafahamu details za matamshi yake sitaki kurudia. Hata kama binadamu anakosea niwazi Jk amekua Mungu mtu maana sijawahi kuona ameomba radhi watanzania kwakukurupuka/kudhihaki wafanyakazi etc. Tatu: amezidi kuwaweka watanzania wakawa kwenye matabaka mawili makubwa wenye nacho na wasiokuwa nacho. Nne: Anaonyesha kebehi kwa wananchi pale anapotoa ahadi zauongo na kutoa maelezo kama mtu asiye na elimu mfano: Kusema maendeleo ya nchi yanapimwa kwa wingi wa magari. Tano: ameonyesha kuwa na limited vision kwa nchi ya Tanzania. Haoni mbali bali anafikiria kujilimbikizi mali yeye na baraza alilolichagua pale anaposhindwa kuwajibisha watendaji wake wanapokosea. Naona ya JK nimengi lakini niishie hapo. Hao wengine Lipumba na wa NCCR siwezi kuwa jaji bado maana hakuna nafasi ya kuitumikia jamii tuliyowapa wakafanya tukaweza kuwajaji.Hivi niulize Watanzania tutakua woga mpaka lini? Kweli tunategemea kumpa Kikwete kura alafu tutegemee different results (maendeleo)? Hiyo ni ndoto kabisaa kama ameshindwa mwanzo atawezaje sasa? Tusipoteze wakati, muda ndio huu wakuchagua mtu makini atakayetetea watanzania woote na sio wachache tu. Mungu ibariki Tanzania.
Blackmannen sasa tuambie wewe kaka yetu unasimama wapi?
Chaguo langu ni Dk. Slaa
Ningempa Dr.Slaa jamaa yuko makini kutetea wanyonge
Watanzania ninavyowajua mlivyo watalaamu wa Domogasia ”demokrasia ya mdomo”…asilimia kubwa ya wachangiaji hapo hawajajiandikisha, mtabaki kumsukuma Slaa, then ataona matokeo yatakvyokuwa baadeni,.Slaa angevuta pumzi kwa 2015..sasa ivi bado nyota ya JK inafanza vema japo ”Kijani na Njano” inaboaaaaaa.
Kazi ni ngumu bora apewe dr
I would have voted for Mrisho, I think it is time for over aged people to retire we need fresh blood (youth) should be given priority on the coming MP sits please I am tired of seeing same face over and over time for change it now. I know Mrisho will take over again but please do some changes we want people who can act like you.
Good luck Mr. Mrisho
Good day!
We,, acha tu Kaka hapo hatatoshi na patachimbika kwa kuwa wote ni wazee wa Herikopta lazima pachimbike,,,,
Oh my dear Florah, if you are realy tired of same faces would you realy vote for Mrisho? Be careful not simply of faces but of same unfullfilled promisses. If you realy want changes then why choose people who can act like him?
We need changes, so let us change. Choose someone who can act differently.
no kura kwa ccm,wamuuza kila kitu,wameshindwa hata kuonoea huruma raia,migodi asilimia 3 with no VAT kweli jaman,inauma,wadanganjwe wajinga
kikwete kama kweli wewe ni mzalendo taifisha baadhi ya migodi ukiwemo mwadui diamond mine,maana hauna faida,hvi huoni tunaibiwa au kuna mtu hiyo ni dili yake
kikwete kashinda tokea mbinguni
Kwa mtazamo wa haraka haraka, nimehesabu watoa maoni yao ya dhati kulingana na swali la BC:
“Kama uchaguzi ungefanyika leo, ungemchagua nani?”
Nimepata kura 13 kwa Dr. Slaa na kura 6 kwa Mhe. JK, Mh. Dr. Lipumba 3. Baadhi ya wachangiaji hawajawa wazi ktk maamuzi yao.
Hii ni changamoto nzuri kwa Wapiga kura na kujua dira yetu inaelekea wapi.
Nawapongeza wote walioeleta wazi maafa ya walala hoi na kuhujumiwa kwa mali asli zetu, kunyanyswa kwa wachimba migodi wenye zana hafifu na kuwapendelea wakezaji wageni.
Suala la Meremeta na nk.Hiyo ndiyo hali halisi iliyotufikisha hapa tulipo.
Kila la kheri!
Ajuza
EEBWANA EEH WERAWERA ME NINGEMCHAGUA SLAA COZ ANGESHUGHULIKA NA MAFISADI MBAYA
Nlmerudia tena uchunguzi na hesabu yangu ni kama ifuatavyo:-
Dr Slaa 11+mimi=12
JK 4
Dr.Lipumba 2
NCCR:Rungwe 1
TLP:Mtamegwa 1
Hawajawa wazi ama hawana uhakika yaani hawajaonesha kidhati msimamo, wangemchagua nani kama uchaguzi ungefanyika leo!
Nlmerudia tena uchunguzi na hesabu yangu ni kama ifuatavyo:-
Dr Slaa 11+mimi=12
JK 4
Dr.Lipumba 2
NCCR:Rungwe 1
TLP:Mtamegwa 1
9 hawajawa wazi ama hawana uhakika yaani hawajaonesha kidhati msimamo, wangemchagua nani kama uchaguzi ungefanyika leo!Kulingana na swali la BC.la August 10, 2010.
Nyongeza na sahihisho.
Nilisema wachangiaji wa mada 9 hawajawa wazi hivyo sikuwahesabia kwa mgombea wa chama chochote, ingawa baadhi wametoa maelezo yenye mwelekeo wa aina aina.
Tafadhali unganisho hesabu hiyo ya watu 9.
Asante.
Wewe unayejiita Blackmannen kakae nyumbani ulee watoto.Mapambano ya kulikomboa taifa hili tuachie sisi.Huna hoja.Unaweza tu kuwa yaya wa watoto wako mkeo anapokuwa kazini.Shughuli kubwa kama za ukombozi wa taifa hili linalofirisiwa na mafisadi huziwezi.Tutazifanya wenyewe mpaka tuhakikishe tunalikomboa taifa hili dhidi ya mafisadi.