
Kuna kitu nimekipenda katika kuitazama kwa makini picha hii.Bahati mbaya siwezi hata kuelezea vizuri ni kitu gani nilichokipenda katika picha hii ya wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) walipokuwa wakimshangilia mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho,Dr.Wilbrod Slaa,wakati wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho katika viwanja vya Jangwani jijini Dar-es-salaam.
Ni matumaini, ni saa ya ukombozi,ni kwamba tumechoka sasa au?
Picha kwa hisani ya John Bukuku.
Feedback / Comments
3 Responses to “MSISIMKO!”
Leave a Reply


sending...
Wahenga wanaesema mtu mwenye njaa ni mtu mwenye hasira AU kwa lugha yao wenye msemo ni kwamba “An hungry man is an angry man”. Mengine utajaza mwenyewe BC.
sio kila anae kupigia makofi amependa hotuba yako, wengine wanataka umalize mapema. Kuna tofauti ya kushangiliwa na kuwaambia watu wakushangilie, walifanya ivyo baada ya shinikizo la mtoa hotuba Freeman Mbowe kuwaambia warushe ngumi juu kumaanisha nguvu ya watu ”people’s power”
CHADEMA hawana sera zaidi ya ufisadi, sera ambayo wapiga kura wengi walioko vijijini ambako ndio ngome na matarajio ya CCM hawajui ni nini…mjini mtaishiwa kushangiliwa na kubebwa na wamachinga ambao hawajajiandikisha kupiga KURA…mtaisoma namba .
Inaonyesha watu wenye uchu wamaendeleo ambao hawajapewa pilau au kanga kuja kushangilia. Wanashangilia from their heart. I love it! A picture speaks a million words BRAVO!!!