
Mshindi wa taji la ulimbwende nchini Tanzania kwa mwaka 2010(Miss Tanzania 2010),Genevieve Emmanuel, asubuhi ya leo hii(kwa saa za Tanzania) amekabidhiwa rasmi bendera ya Tanzania tayari kabisa kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya ulimbwende ya dunia(Miss World 2010) yanayotarajiwa kufanyika huko Sanya nchini China tarehe 30 Oktoba 2010.Anatarajiwa kuondoka nchini kesho.
Shughuli ya kumkabidhi bendera mrembo huyo ilifanyikia katika viwanja vya Tanzania Investment Centre(TIC) jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa kituo hicho cha uwekezaji,Bw.Emmanuel Ole Naiko, Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald, Mratibu wa Miss Tanzania,Hasheem Lundenga,wawakilishi wa wadhamini wa shindano la Miss Tanzania kutoka kampuni ya mawasiliano,Vodacom na wengineo.

Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel(kushoto) na Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald.
Mashindano ya mwaka huu yanaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.Awali mashindano ya mwaka huu yalikuwa yafanyikie nchini Vietnam lakini nchi hiyo ilijiondoa katika uandaaji huo na hivyo China kupewa nafasi ya kuyaandaa.
Picha:MichuziJR

Kama kuna jambo ambalo Mheshimiwa Kikwete anaonekana kuwatoa nalo jasho wagombea wengine wa Urais na nafasi nyinginezo za uwakilishi katika Uchaguzi wa mwaka huu-2010, basi bila shaka jambo hilo ni pamoja na kujitahidi kuwa karibu zaidi na wananchi.Mifano ya jambo hili ipo mingi.
Bahati nzuri ni kwamba Mheshimiwa Kikwete amekuwa akifanya hivyo sio tu wakati wa kampeni bali hata pale kampeni zilipofikia kikomo na yeye kuingia ikulu(2005).Hiyo inaonyesha kwamba hii ni hulka yake na sio jambo analolifanya kwa sababu tu anataka kura ya mtu au watu fulani.
Hili ni jambo ambalo viongozi wengine(wakiwemo viongozi wenzake ndani ya CCM) hawana budi kujifunza.Wote wakijifunza kuwa karibu na wananchi,bila shaka wataelewa kwa undani zaidi kuhusu matatizo yanayowakabili wananchi na hivyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi katika kuunda au kusimamia sera na mbinu za kuboresha maisha ya wananchi. Wakifanya hivyo,wataweza kumsaidia Rais katika kutimiza malengo kwa pamoja(collectively)
Pichani ni Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni wa Wilaya ya Makete,mkoani Iringa wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.

12 years ago, two young fellas named Sergey M.Brin and Lawrence E.Page decided to implement their dream(s).Today,all of us are part of that dream and the reality part of it.We call it Google.
In twelve years, they have achieved almost everything they dream of and even some of the things that had never crossed their minds.To me,that is a true power and magic of Thinking Big.
As we continue being part of that dream in one way or another,BC joins millions of people worldwide to wish Google a Happy 12th Birthday.Click here to see the timeline of Google.
Kampeni bado zinaendelea. Sasa ni mwendo wa ama zao,ama zetu.Ngumi hazipigwi ila vijembe vinarushwa.Maneno,ushabiki,kukaziana sura.Usintishe,sikutishi.Kila mtu na hamsini zake.Kama hutaki hamsini basi chukua arobaini.
Kama kawaida ya siasa zetu,kuna mapungufu katika suala zima la sera. Natega sikio lakini sisikii.Ushindani uko kwenye taratibu zaidi ya kuelezea sera nzuri. Wengine wanawaasa wananchi “wasahau yaliyopita,wagange yajayo”.Mhhh..yaani kirahisi rahisi tu mtu anarudi zake Bungeni.Kule anasinzia au yuko bize na kilongalonga chake.Mzigo umeshatua bandarini.Njoo haraka sana.Itabidi kesho nimwambie mheshimiwa spika kwamba nauguliwa.Deal!
Bado vijembe vya “chumbani” vipo.Vya nini? Ah!Unajifanya huelewi.Integrity.Viongozi safi.Hakuna “nyumba ndogo”.Mke mmoja,mume mmoja.Hivi kile kipindi cha ughaibuni cha televisheni cha “cheat….nini vile…kinakuja lini Bongo?Balaa hilo mtu wangu.Ushajua utampigia kura ya NDIYO nani? Ah…fanya kweli bwana.
Sie, leo tumejituliza kama Kasuku. Kama vile walivyoimba Les Wanyika.Hii ni mojawapo ya bendi ambazo sio tu zilitamba sana Afrika Mashariki bali mpaka hivi leo heshima yao ipo pale pale. Isome historia yao utaona kwanini nasema hivyo.Ushirikiano uliokwenda shule.Mipaka haikuwa mali kitu.Vijana kutoka Tanzania wakaungana na vijana kutoka Kenya.Matokeo yake ni kitu kizuri.Burudika la wimbo Kasuku. Zingatia ushauri.Kama vipi,Jitulize kwako kama Kasuku.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Pia unaweza kusikiliza kibao chao kingine cha Sina Makosa kwa kubonyeza hapa.

Anaitwa Roma.Msikilize tena na tena katika wimbo huu Mr.President.He is probably the most courageous B’Fleva artist of all time…in my opinion.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Photo:JamiiForums

Na Anastazia Anyimike wa Gazeti la Habari Leo
TECLA Mjata ni mwanamama mwenye kipaji cha hali ya juu katika uigizaji, ni mtu ambaye anaubeba uhusika wake ipasavyo huku akionesha kazi yake ya sanaa ya maigizo kwa kukupa uhalisia wa tukio lenyewe.
Pamoja na umahiri katika kuigiza kwenye filamu na michezo ya redio, Mjata ambaye anapenda kujitambulisha kama mama Mjata amepitia katika milima na mabonde ya maisha halisi hususani ya uigizaji.
Anasema, alianza fani ya uigizaji kati ya miaka ya 1955 na 1960 akiwa mwanafunzi ambapo alikuwa akishiriki katika michezo ya kuigiza wakati wa Siku ya Wazazi iliyokuwa ikifanyika kila mwaka shuleni kwao na hiyo ilitokana na fani ya uigizaji kuwa kwenye damu.
Baada ya kumaliza elimu ya msingi na baadaye chuo cha uwalimu mwaka 1963, alipangiwa kazi ya kufundisha Shule ya Msingi Kwamagome.
Mjata alifundisha shule mbalimbali baadhi yake zikiwa ni Kwamsangazi, Magunga Mombo na baadaye alihamishiwa Dar es Salaam ambapo alipangiwa kufundisha Shule ya Msingi Kisutu na kufuatia na Olimpio.
” Nikiwa ni mwalimu niliendelea na sanaa ya uigizaji kwa kuwafundisha wanafunzi michezo mbalimbali au hadithi, lakini mapenzi yangu zaidi yalikuwa ni mimi mwenyewe kuigiza na si vinginevyo.”
“Sababu hasa ya kuingia kwenye sanaa hii ilikuwa michezo ya kuigiza iliyokuwa ikifanyika Radio Tanzania (kwa sasa TBC1 Taifa), ambapo wasanii kama Ibrahimu Raha (Mzee Jongo), Hamisi Tajili, Tunu Mrisho (Mama Hambiliki), Ali Keto (Pwaguzi au Matuga) na Nyakomba walinivutia na mimi nikasema nikipata nafasi nitafanya vizuri zaidi.”
” Nilianza kuigiza michezo ya redio katika kipindi cha Mahoka na Pwagu na Pwaguzi ambapo tulikuwa tunaigiza vituko vilivyotokea mitaani. Kama utakumbuka yule mtoto aliyeng’olewa meno na koleo za baiskeli basi nilikuwa ni mimi. 




sending...