SIKU 10 za mwanzo za kampeni za urais zilizoanza rasmi, Agosti 21, zimechukua mwelekeo wa malumbano na mvutano mkubwa wa hoja kati ya vyama viwili vya siasa; Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kile cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa malumbano hayo kwa kiwango kikubwa kiini chake ni kile kinachoonekana kuwa ni kuwapo kwa dalili za kuzidi kuimarika kwa ushindani mkali wa majukwaani kati ya wagombea wawili wa urais wa vyama hivyo, Rais Jakaya Kikwete (CCM) na Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA).

Tanzania Daima linayo habari kamili.

Feedback / Comments

22 Responses to “CHADEMA Vs CCM:VITA YA MANENO ISHAANZA”

  1. Comment by mbayumbayu on September 2nd, 2010 5:44 am

    Slaa hana mvuto!

  2. Comment by majuto on September 3rd, 2010 6:07 am

    mbayumbayu wewe unataka mabadiliko au mvuto.ndo maana inasemekana umaskini wa watanzania ni kutokana na ujinga wao wenywew.sio kulogwa wala laana.ni ujinga.

  3. Comment by Riadhi on September 3rd, 2010 8:36 pm

    Tanzania hatuhitaji kiongozi wakuuza sura tunataka utekelezaji wavitendo. CCM hawana jipya ni taarabu tu na mipasho hiyo haitachangia maendeleo yoyote. Acha ujinga wa mvuto ukitaka mvuto nenda kawe model kila kitu na mahali pake.

  4. Comment by JOSEPHAT MAPUNDA on September 4th, 2010 6:29 am

    Watanzania tuachane na mambo ya mvuto kwani hayana tija katika maslahi yetu na taifa kwa ujumla, tuchague vongonzi wenye uwezo..!!

  5. Comment by Zablon Hibwa on September 6th, 2010 6:42 am

    Wenye akili timamu na tunaoitakia mema Tanzania tumpe Dr Slaa kura zetu akomeshe ufisadi nakuleta maendeleo ya kweli.

  6. Comment by agnes francis on September 8th, 2010 8:15 am

    uongozi si kazi ndogo na ni kazi ngumu sana kuweza kuongoza si rahisi kila mmoja kuridhika kama mfikiriavyo, ccm si chama kibaya ila watenda kazi ndo wabaya, na kikwete si kiongozi mbaya malengo yake huwa mazuri na wale wanaopaswa kutekeleza hawatekelezi ipasavyo.

  7. Comment by jastin rweyongeza on September 9th, 2010 4:57 am

    tunaposema kikwete si mbaya bali watendaji wake tuna maana gani?wakati yeye mwenyewe ndo mwenye jukumu la kuwateua viongozi hao na ndo mwenye majukumun ya kuwavua uongozi?watu makini mda ndo huu atuna budi kuchagua kiongozi makini mwenye mamlaka na uongozi wake..NAONA KAZI HII DR SLAA ANAIWEZA

  8. Comment by Patric on September 9th, 2010 6:33 am

    We mbayumbayu uliyeandika hapo juu nafikiri wewe si mtanzania mwenye nia na malengo ya kuendelea. Nahisi hata utakuwa ni aidha mbumbumbu wa mambo anayetegemea kuamua jambo kwa kuangalia rangi na mng’ao wa umbo, ama wewe ni kati ya watoto wa wale waliokula fedha za wavuja jasho hivyo umekulia mazingira ya kijani kama kilivyo chama chako. Vinginevo tunahitaji kiongozi ambaye ana mvuto wa maendeleo sio sura ya kungaa. Tena usirudie tena kutoa statement zenye kuudhi kama hizo. Watu tunafunga na kuomba usiku na mchana Mola atuletee maisha mema kisha wewe unaleta LONGO?

  9. Comment by Kibibi Namkonongo on September 11th, 2010 1:41 am

    Narudia tena rai yangu kwa Wa Tanzania ni kuwa wa kweli na imara kutetea ukweli.

    Vyama vya upinzani wateuwe mgombea mmoja na wote kumuunga mkono badala ya kunyang’anyana kura na kupelekea kushindwa kwa mgombea Mpinzania. Dr, Slaa apewe nyezo zote za duwa kuiokoa Tanzana.

    Ajuza
    (Msichana wa zamani)

  10. Comment by schwan on September 13th, 2010 1:48 pm

    Yap! wabongo mmeanza kuelimika. Hivi we mbayumbayu utakula mvuto kuwa na uelewa na upeo wa kufikiri, ni ndugu zako wangapi wanapigika huko bush afadhali wewe unajua hata kubofya key za computer! Tunahitaji viongozi makini nawenye uchungu na nchi yetu na si lalamu za mdomoni. Fikiri kwa makini kabla hujapiga kura yako 31 november man 4 your life peace celebration na inatokana na maendeleo ya watanzania wote nasi mafisadi.

  11. Comment by zemche on September 14th, 2010 7:19 am

    mvuto uliwahi kukuwekea sahani ya ugali mezani? we mbayuwayu kweli au wa kichina.maana huna mawazo wala hujigusi kama mfu usiejua usemalo.wanapoongea wakubwa we mtoto nyamaza ebo!!

  12. Comment by Sultan Mgimbi on September 14th, 2010 7:34 am

    Chadema juu. Mi ninawashauru viongozi wa Chadema kuweka mawakala zaidi ya mmoja wakati wa kuhesbu kura ili kuepuka kwa wakala kurubuniwa katika kipindi hiki muhimu sana.

  13. Comment by ...Habari on September 17th, 2010 6:28 am

    …pole sana mbayuwayu!!! kama kuna ‘vijisenti’ ulikuwa ukichotewa na huyo ‘kisura’ wako safari hii umeungua!!! TZ watu wameshajanjaruka! boraujirudi mapemaaaa!

    Tanzania bila ufisadi inawezekana, na Tanzania bila CCM imeshawezekana!!! wadau oyeeee!!!

  14. Comment by Emambi on October 11th, 2010 5:41 am

    jamani kwa mtanzania yeyote mwenye akili timamu na mwenye mtazamo chanya wa maisha yake ni wakati wa kumchagua Dk. Slaa.Maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa yakisikika kama ngonjera tu sasa ni wakati wa kunufaika.
    VOTE FOR DK. SLAA FOR DEVELOPMENT THAT IS SUSTAINABLE!!!!

  15. Comment by sultan mgimbi on October 16th, 2010 6:27 am

    Watanzania tuamke. Wakati wa mabadiliko ndio huu. Usifanye makosa, kapige kura. Na usikubali kura yako ipotee kwa kuwapa walioshindwa. Mpigie Dr.Slaa maana anayoyasema yanawezekana na yanatekelezeka. Usidanganywe na mafisadi kwamba haiwezekani.
    Kijana usipoteze kura yako.
    Mpigie kura Slaa kwa Tanzania endelevu na yenye kujali umma kwanza.
    VOTE FOR Dr. SLAA.

  16. Comment by sultan mgimbi on October 18th, 2010 12:32 pm

    Kijana usifanye mzaha na kura yako moja ukadhani kwamba si kitu. Kura yako ina thamani mno katika kuleta mabadiliko katika taifa hili. Usikubali kudanganywa kutokwenda kupiga kura. Shiriki katika kuleta mabadiliko hayo kwa kumpigia kura Dr. SLAA.
    Mchague SLAA kwa Tanzania endelevu yenye kujali na kuheshimu misingi ya Demokrasia, yenye uwajibikaji, yenye kujali maslahi ya WATANZANIA KWANZA na yenye kulinda na kunufaisha watanzania kwa tunu walizojaliwa na MUNGU.
    VOTE FOR SLAA.

  17. Comment by sultan mgimbi on October 19th, 2010 12:39 pm

    Maslahi ya taifa mbele uswahiba baadaye. Mwalimu Nyerere alileta sera nzuri ya usawa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Lakini viongozi wa sasa wa CCM wameibadilisha kuwa ya UNYAMA NA KUJIMEGEA. Hawa wameusaliti utaifa, wametusaliti watanzania weenzao.
    USIDANGANYIKE! AMKA SASA CHAGUA CHADEMA.
    CHAGUA SLAA KWA MAENDELEO NA USTAWI WA TAIFA LA TANZANIA.

  18. Comment by Gabriel pius on October 30th, 2010 5:25 am

    we acha ujinga inawezekana wewe ni ccm au umeshapewa rushwa Dr slaa akiingia madarakani sisi wana nchi tutanufaika umesikia bwana mdogo sisi atuangalii ao ccm wanaojipodoa na mimi kura yangu chadema tu

  19. Comment by abihudi on October 30th, 2010 7:41 am

    Ndugu zangu kesho ndiyo siku yenyewe mnyeezi mungu aliyotupatia kuikoa taifa letu tajiri lakini linaonekana maskini wa kutupwa kawajili ya wachache wasioipenda nchi yetu bali hujali maslahi yao wenyewe,Tuweni na umoja tuipeleke chadema ikulu na tumwombeeni mh,dr slaa ashinde kwa kishindo naye aweze kutekeleza aliyoyaadi, CHAGUA CHADEMA KWA MAENDELEO BORA YA KILA AJIIRTAE MTANZANIA.
    NIWATAKIENI UCHAGUZI MWEMA NA WA AMANI
    MUNGU IBARIKI TANZANIA, AMINA

  20. Comment by abihudi on October 30th, 2010 7:47 am

    Ndugu zangu kesho ndiyo siku yenyewe mnyeezi mungu aliyotupatia kuikoa taifa letu tajiri lakini linaonekana maskini wa kutupwa kwajili ya wachache wasioipenda nchi yetu bali hujali maslahi yao wenyewe,Tuweni na umoja tuipeleke chadema ikulu na tumwombeeni mh,dr slaa ashinde kwa kishindo naye aweze kutekeleza aliyoyahaidi, CHAGUA CHADEMA KWA MAENDELEO BORA YA KILA AJIIRTAE MTANZANIA.
    NIWATAKIENI UCHAGUZI MWEMA NA WA AMANI
    MUNGU IBARIKI TANZANIA, AMINA

  21. Comment by charles on November 28th, 2010 10:06 am

    tunamwitaji dk.slaa

  22. Comment by Kibibi on November 29th, 2010 7:32 pm

    Matatizo ni kule kugawana kura za wapinzani.
    Inawezekanaje wapi watu na akili zetu timamu tusione ama kubaini wakati wa kampeni, kuwa hapa,”Mimi” napwaya hivyo nimuunge mkono mpinzani mwenzangu na kuwahamasisha wanaoniunga mkono kumpigia kura yule ambaye dalili zimejitokeza wazi kuwa ndiye “STAR” wa upinzani? Njaa tupu!Si kwa nia safi ya kuwakomboa Wa Tanzania, ila tu kuganga njaa!
    Ajuza Kibibi

Leave a Reply