Ijumaa imewadia.Kama kawaida hii ni siku ambayo watu wengi,hususani wanaofanya kazi ya Jumatatu hadi Ijumaa,huwa wanaisubiri kwa hamu. Hapo sijasema kwamba wikiendi hii ni “Mwisho wa Mwezi”.Kila mtu anazo.Bahati nzuri ni kwamba bado tupo katika Mwezi wa Toba kwa hiyo vibweka huko mitaani navyo huwa vinapungua. La sivyo,ungesikia vibweka kutoka katika baa ya kona.Sikia vicheko.Sikia jinsi baa medi anavyokaripiwa akichelewa kuweka bia mezani.Jeuri ipo.Pesa huwa inaongea.
Nasi hapa BC,tupo kwa ajili ya kuendeleza jadi.Ijumaa ni siku ya kujifaragua kidogo.Zamani walikuwa wanasema siku ya “kuruka majoka”.Ni wakati wa Zilipendwa. Leo tungependa kukuhamisha kidogo msomaji na mpenzi wa safu hii ya kila Ijumaa.Hatukupeleki mbali sana.Ni hapo DRC.Zamani iliitwa Zaire.Ilikuwa maarufu sana ulimwenguni hususani baada ya ule mpambano wa ndondi za uzito wa juu baina ya Mohamed Ali na George Foreman mwaka 1974. Enzi za Mobutu Seseseko Nkuku wa Zabanga.
Wimbo unaitwa Mamou(Tu Vois?) kutoka kwa gwiji la magwiji katika Afro-Rumba.Si mwingine bali mzee mzima Francois Luambo Makiadi maarufu kama Franco.Wimbo huu ni hadithi tamu sana.Hadithi ya mapenzi,uongo katika mapenzi,maisha nk. Zamani nakumbuka tulikuwa tukitaniana kwamba wimbo huu na mwingine hivi wa Madilu System,ulikuwa ukiuanza basi unasafiri kutoka Dar-es-salaam mpaka Morogoro na bado unaburudika tu.
Naamini wimbo huu unaweza kukukumbusha mbali.Usiwe mchoyo basi wa kuwaambia wenzako kupitia sehemu ya maoni kwamba Mamou inakukumbusha wapi.Ulikuwa unasakata Rhumba sehemu gani? Nakutakia wikiendi njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Ukitaka kusoma tafsiri ya Kiingereza ya wimbo huu bonyeza hapa.
Feedback / Comments
2 Responses to ““MAMOU (TU VOIS?)”-FRANCO”
Leave a Reply


sending...
Unajua ile unampata mwenzako.. unajipanga ili uoe; mnapatana, mnaelewena na mnapendana sana?
Sasa, baadae, unakuja kugundua kuwa mwandani wako ni mpishi mzuri mno! BONUS…
Basi ndio huu wimbo — nilikuwa naupenda, ila sikujua hadithi yake (tafsiri).
Shukrani na Ijumaa njema!
SN,
Hadithi ya wimbo huu hata mimi mwenyewe ilifurahisha sana mara ya kwanza niliposimuliwa.Kuna mkongo mmoja alinikuta nasikiliza wimbo huu huku,kama kawaida,nikimung’unya maneno.Akaniuliza,”unajua maana au tafsiri ya wimbo huu?”Nikamwambia sijui japokuwa nimekuwa nikiusikiliza na kuupenda tangu nikiwa mdogo.Ndipo akanipa tafsiri na mkasa wenyewe.Napenda zaidi pale kwenye maongezi ya simu…Hallo…the kids are fine except this younger one….