Nchi ya Brazil ndiyo iliyopewa dhamana ya kuandaa Kombe la Dunia la FIFA kwa mwaka 2014. Hiyo itakuwa ni mara ya 20 kwa fainali hizo kufanyika na itakuwa ni mara ya pili kwa taifa la Brazil kuandaa fainali hizo.Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1950. Hii ni mara ya kwanza kwa fainali hizo kufanyikia katika bara la Amerika Kusini tangu zilipofanyikia huko mwaka 1978.

Jumla ya miji 12 itakuwa na kipute hicho huku fainali zikifanyikia katika uwanja maarufu wa Maracana uliopo katika jiji la Rio de Janeiro. Uwanja huo ulifunguliwa rasmi mwaka 1950 wakati Brazil ilipoandaa mashindano hayo.

The 20th FIFA World Cup will be hosted in Brazil in June and July 2014. It is the second time that the country has hosted the event – the first being in 1950 – and it is the first time that it has been held in South America since 1978.

There are 12 cities that will host games, while the final will be played at the Maracana Stadium, in the city of Rio de Janeiro – a stadium that was inaugurated in 1950. The cities are:

  • Sao Paulo
  • Rio de Janeiro
  • Belo Horizonte
  • Porto Alegre
  • Brasilia
  • Cuiaba
  • Curitiba
  • Fortaleza
  • Manaus
  • Natal
  • Recife
  • Salvador

Draw kwa ajili ya michuano ya awali kuelekea nchini Brazil itafanyika tarehe July 31, 2011.

Hivi karibuni,kupitia vyombo mbalimbali vya habari,ilitangazwa kwamba filamu inayokwenda kwa jina la Off-Side,ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa filamu nchini Tanzania,itazinduliwa rasmi nchini Congo(DRC-Democratic Republic of Congo).Filamu hiyo imechezwa na baadhi ya vinara wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kama vile Steven Kanumba,Ray Kigosi na mwanadada Irene Uwoya.

Mara tu baada ya habari hizo kutoka,baadhi ya mashabiki wa filamu walituandikia kutaka kujua sababu za filamu hiyo kwenda kuzinduliwa rasmi nchini Congo badala ya nyumbani Tanzania ambapo ndipo penye mashabiki wengi zaidi na isitoshe ndio uwanja wa nyumbani.

Ili kupata jibu la swali hilo na mengine,nilimtafuta Steven Kanumba ambaye ni miongoni mwa lead characters ndani ya filamu hiyo nikiwa na maswali yangu;

BC: Mambo vipi Kanumba? Ni kwanini mmeamua kuizindulia filamu hii nchini DRC?

SK: Ee bwana mambo ni poa tu.Tunashukuru Mungu. Kama ambavyo ungetarajia,uamuzi wa kwenda kuizindulia filamu hii nchini Congo haukuwa mwepesi. Tulizingatia mambo kadhaa ikiwemo kujaribu kupanua wigo wa soko la filamu zetu na pia kwa namna moja au nyingine,kuzidi kuitangaza tasnia hii ya filamu zetu nje ya mipaka yetu.

Isitoshe, kule nchini Congo kuna mashabiki wetu wengi sana na wanatupenda sana. Mara baada ya kutuona mimi na Ray katika filamu ya Oprah, walitusihi sana tutengeneze pamoja filamu nyingine. Tuliridhia na maombi yao na matokeo yake ndio hii filamu ya Off Side. Hizo ndizo sababu zilizofanya tuamue kwenda kuizindulia filamu hii nchini Congo.

BC: Je kutakuwa na uzinduzi wa nchini Tanzania?Kama ndio,utafanyikia wapi na lini?

SK: Ndio,kutakuwepo uzinduzi rasmi kwa upande wa Tanzania. Mipango inaendelea na pindi mambo yote yatakapokamilika, tutawajulisha.

BC: Kwa upande wa filamu yenyewe,mashabiki wa filamu nchini Tanzania wategemee nini kutoka katika filamu hii?

SK: Ingawa sio busara sana kujisifia, ninachoweza kusema ni kwamba mashabiki wetu wategemee maajabu na mapinduzi ya kweli. Kwa uhakika hii ni mojawapo ya filamu bora kabisa nilizowahi kushiriki na humo ndani kuna mpambano wa kweli….nimemfundisha adabu humo Ray…ahahaha.

BC: Kila la kheri kaka.

SK: Asante sana Jeff.Kazi njema na wewe pia.


Tuzo za 2010 Soul Train,zilirushwa hewani jana usiku kupitia kituo cha televisheni cha BET.Waimbaji wengi wa R&B na Soul wali-perform.

Miongoni mwa hao aliyekuna wengi bila shaka ni Mwanamuziki R.Kelly ambaye ndiye aliyefungua tuzo hizo zilizokuwa zinaongozwa na waigizaji Terrence Howard na Taraji P.Henson.Mcheki R.Kelly hapo chini;


R. Kelly Medley Live @ 2010 Soul Train Music Awards BMF
Uploaded by BlakMusicFirst. – See the latest featured music videos.

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amehamisha vifaa mbalimbali vya ofisi ya Bunge Jimbo la Nyamagana, kwa madai kuwa alivinunua mwenyewe kipindi uongozi wake. Akizungumza na Mwananchi jana, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, alisema baada ya kutoka Bungeni alikwenda kuingia katika ofisi hiyo, lakini baada ya kukabidhiwa alikuta vitasa vya mlango, simu ya mezani picha ya Rais na samani za kukalia vikiwa zimechukuliwa.

Kwa mujibu wa Wanje, baada ya kufuatilia aliambiwa kuwa vifaa hivyo viliondolewa na Masha kwa madai kwamba, alivinunua kwa fedha zake mwenyewe.

SOMA ZAIDI: Mwananchi

Kwa mara ya tano mfululizo,Timu ya Barcelona,imethibitisha kwamba Timu ya Real Madrid,sio mali kitu kwao.Barcelona imeichakaza Real Madrid kwa jumla ya mabao 5 kwa nunge katika mchezo ambao kwa hakika umeonekana kuwa kama mchezo wa wanaume dhidi ya wavulana(Men Vs Boys) kwa jinsi Barcelona walivyoonekana kuwazidia Real Madrid.

Dalili za kwamba Real Madrid walikuwa wanaelekea kuangukia pua zilianza kuonekana mapema tu tangu mchezo uanze kwa jinsi ambavyo vijana wa Barcelona, wakiongozwa na mshambuliaji wao hatari,Lionel Messi,walivyokuwa wakionana kwa pasi fupi fupi na za uhakika.Licha ya kutokufunga bao katika mchezo huo,Lionel Messi,alionekana wazi kuizidi akili ngome ya Real Madrid,kwa jinsi alivyokuwa akipenya na kutoa pasi za uhakika kwa wenzake.

Iliwachukua Barcelona dakika 10 tu kabla hawajaandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na Xavi. Dakika nane baadaye, alikuwa ni Pedro aliyeweka wavuni bao la pili.Mpaka mapumziko,Barcelona walikuwa wanaongoza kwa bao 2-0.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kigumu kwa vijana wa Jose Mourinho ambapo kunako dakika ya 55,David Villa,alipachika kimiani bao la tatu kabla hajapigilia msumari mwingine dakika tatu baadaye(dakika ya 55). Goli la tano lilifungwa na Jeffren Suarez kunako dakika ya 90 ikiwa ni dakika tatu tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Pedro Rodriquez.

Kwa matokeo hayo, kwa mara ya kwanza ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho imepoteza mchezo baada ya kutokufungwa katika jumla ya mechi 19 tangu alipochukua kazi ya ukocha katika timu hiyo yenye makazi yake jijini Madrid. Matokeo hayo pia yanaendeleza rekodi ya kuridhisha kwa kocha Pep Guardiola ambaye ameiongoza Barcelona katika kushinda michezo mitano mfululizo dhidi ya watani zao hao wa jadi,Real Madrid.

Kocha/Meneja wa timu ya soka ya Arsenal ya Uingereza,Arsene Wenger, amewataka mashabiki wa timu hiyo,maarufu kama Gunners,kuendelea kuwa na imani na kuwa wavumilivu kwa timu hiyo wakati inajiandaa kupambana na timu ya Wigan hapo kesho katika robo fainali ya English League Cup. Wenger anasema timu yake bado ni changa ingawa anaamini kwamba katika siku za usoni,mambo yatakuwa mswano baada ya kukamilisha programu yake ya kukijenga kikosi hicho.

Klabu hiyo yenye makazi yake kaskazini mwa jiji la London,haijashinda ubingwa wowote mkubwa tangu iliponyakua ubingwa wa FA Cup mwaka 2005.

Pamoja na kwamba katika miaka mitano iliyopita,Arsenal wamesifika kwa kutandaza kandanda maridadi, mashabiki wa timu hiyo wanaona kwamba timu yao inapoteza nafasi muhimu katika historia au utamaduni wa kushinda ikilinganishwa na timu zingine kama vile Manchester United au Chelsea na kwamba wameanza kuchoshwa na ahadi za Wenger kwamba katika siku za mbeleni,Arsenal itakuwa tishio.

Mwishoni mwa wiki,Arsenal ilishinda 4-2 dhidi ya Aston Villa kitu ambacho angalau kilipunguza machungu kwani endapo wangeshindwa wangekuwa wamepoteza michezo mitatu mfululizo baada ya kutandikwa na Tottenham Hotspur 3-2(Arsenal waliongoza 2-0 kabla ya kuishia kupokea kipigo hicho mwishoni) na baadaye kuchapwa 2-0 na timu ya Sporting Braga kutoka Portugal katika Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.

Ankal Michuzi (Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.

Pichani juu ni Ankal Michuzi akiwaonyesha wadau wa Jukwaa la Sanaa jinsi ya kuweka video kwenye YouTube.

Pichani ni Baraza la Mawaziri Tanzania katika kikao chake cha kwanza chini ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete(anayeonekana kwa mbali).Kikao hicho kimefanyika hivi leo,Ikulu jijini Dar-es-salaam.(Picha na Freddy Maro-Ikulu)

Jana Jumamosi,katika Hotel ya Movenpick jijini Dar-es-salaam,kulifanyika mdahalo uliowashirikisha ,Kiongozi wa Upinzani Bungeni hivi sasa,Freeman Mbowe(CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliyepita, Hamad Rashid(CUF).

Nia ya mdahalo huo ulioandaliwa na kampuni za Vox Media na East Africa Business & Media Training Insitute (EABMTI), ulikuwa na malengo ya kujadili hatima ya upinzani nchini Tanzania baada ya kuonekana wazi kutokana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza Bungeni hivi karibuni kwamba kambi hiyo ya upinzani inaelekea kuzidi kushindwa kuwa na kauli moja.

Tembelea hapa kutizama baadhi ya video kutoka mdahalo huo.Na pia tembelea hapa kusikiliza audio kutoka kwenye mdahalo huo.Nini maoni yako?Unadhani nini kinaweza kufanyika ili kunusuru nguvu ya upinzani Bungeni ambayo bila shaka sote tunakubaliana kwamba ni muhimu kwa ajili ya maendeleo sio tu ya demokrasia nchini bali pia ya kijamii?


Nyota chipukizi katika Kiwanda cha Filamu Bongo, Esther Flavian(pichani), amesema ubovu wa filamu unaolalamikiwa hivi sasa na mashabiki wa sanaa hiyo nchini unatokana na tamaa ya waandaji wa ‘muvi’ hizo kutaka kupata ‘mkwanja’ wa haraka haraka.

ZAIDI: GLOBAL PUBLISHERS.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page