Nimemaliza kusikiliza hotuba ya salamu za mwaka mpya toka kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Rais amegusia mambo mbalimbali.Lakini kubwa zaidi ambalo nadhani watu wengi watakuwa wametoka nalo ni lile la kuafiki  kwake kwamba wakati umefika kwa Tanzania kuwa na Katiba Mpya.

Rais amesema anaunda Constitutional Review Commission(Tume ya Kurekebisha Katiba) ambayo itawashirikisha watu wote katika upatikanaji wa mapendekezo na kisha katiba mpya.

Ninapouanza mwaka mpya,hili ndilo ninalosonga nalo mbele.Katiba itakayokidhi mahitaji ya nchi katika karne hii.Hongera Mheshimiwa Rais.Itazame hotuba nzima ya Rais hapo chini;

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Well…kimsingi umaarufu wake huwezi kuunganisha na kitu kimoja kamili…ni mvuto wake,TV reality show yao kama familia au ni umaarufu wa watu aliowahi kutembea nao? Si unakumbuka kwamba umaarufu wake hasa ulianzia pale alipotengeneza “mkanda wa matusi” na mdogo wake Brandy…Ray J? Yote tisa,ukijumlisha moja lingine unapata kumi na hivyo inakuwa kitu na box.Ni maarufu.Upende au usipende.

Hivi leo katika kuhakikisha kwamba mwaka mpya hauishi hivi hivi tu,Kim Kardashian ametoka na msuko wa cornrow(Kiswahili chake ni nini hivi?).Kuna habari kwamba msuko huu ni maalum kabisa kwa ajili ya video ya Kanye West ambayo Kim ataigiza au kuingiza mbwembwe zake.Tusubiri tuone.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania,Mheshimiwa Anna Makinda amesema hatogombea tena nafasi ya Ubunge pindi atakapomaliza muda wake mwaka 2015.

Akiongea katika mahojiano maalumu na blog ya Mohamed Dewji,Mheshimiwa Makinda ambaye ni Mbunge wa Njombe Kusini na mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi ya Spika wa Bunge nchini Tanzania, pia amesema kwa sasa hana mpango wa kugombea nafasi ya Urais ifikapo mwaka 2015.

Unaweza kusoma mahojiano kamili ya Mheshimiwa Spika na Mo Blog kwa kubonyeza hapa.

Photo Credit:Mo Blog

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Jarida la King la nchini Marekani katika issue yao ya mwezi March/April 2011,aliyepo juu ni mwanadada Nicki Minaj ambaye hivi sasa yupo juu katika game la Hip Hop nchini Marekani hususani kwa upande wa kina dada.Ndani ya jarida hilo,Nicki Minaj anaongelea mambo kadhaa ikiwemo uwezekano wa yeye kuingia katika masuala ya filamu.Pia alipoulizwa kuhusu aina ya mwanaume ambaye anamtaka…alisema…zaidi lisubiri jarida la King mwezi March/April..

Classic film. You did mention earlier how everything has been time consuming. But when that time frees up, what kind of guy do you look for to be sentimental and organic with?

Um, I look for someone who is calm, someone who is strong enough to not have to win every argument, someone who allows a woman to be her crazy self and someone with a conscience not to feel less of a man. You know, someone who is able to honor his woman but also bring out the freak in his woman.

Kuna kitu kinaitwa “jeuri ya pesa”.Kama hujawahi kukisikia shauri yako!Majuzi kabla ya Xmas,Rapper maarufu Jay-Z alionyesha jeuri hiyo baada ya kumnunulia  mkewe,Beyonce zawadi mbalimbali zenye thamani ya $350,000 kutoka katika duka la Hermes ambalo ni maarufu kwa kuuza handbags za Birkin ambazo huuzwa kwa bei kati ya $9,000 mpaka $150,000.

Birkin Bag from Hermes

Jay-Z ambaye kama ilivyo kwa celebrities wengine,ali-shop in private katika mojawapo ya maduka ya Hermes lililopo Manhattan jijini New York

Pamoja na zawadi ya Jay-Z kuwa kubwa(eeh,dola laki tatu sio mchezo!) bado zawadi hiyo haikukaribia zawadi kutoka kwa Beyonce kwenda kwa Jay-Z wakati wa siku yake ya kuzaliwa mapema mwezi huu-(Birthday-Jigga alizaliwa tarehe 4 December,1969) ambapo alinunuliwa gari aina ya Bugatti Grand Sport lenye thamani ya dola milioni mbili($2 million). ndilo linasemekana kuwa gari lenye speed kushinda mengine yote!

Bugatti-Veyron-Grand Sport

Mwezi September,wakati wa birthday ya Beyonce(born September 4,1981) Jay-Z,alimnunulia Beyonce kisiwa binafsi(private island) huko Florida kwa dola milioni 20($ 20 million).Naam hiyo ndio inaitwa jeuri ya fedha.

MZEE Small amewarushia makombora wasanii wa filamu za Tanzania akisema kuwa wanatia aibu na asailimia kubwa hawajui wanachokifanya kwenye sanaa hiyo.

Mchekeshaji huyo mkongwe amesema kuwa kazi za wasanii hao nyingi hazina maadili na hazifai kuangaliwa na familia haswa yenye maadili ya kiafrika.

“Wasanii wa filamu wanajitahidi kuigiza kwani ukingalia walipoanzia na hapa walipofikia wamepiga hatua ingawa si kwa kiasi kikubwa kama wanavyojidai,”anasema msanii huyo.

“Tatizo lao kubwa ni maadili, hakuna maadili katika filamu zao ni aibu, kuna filamu mzazi huwezi kukaa na watoto wako kuangalia, wanaigiza mambo ya ajabu, nguzo walizovaa si za heshima, hili jambo waliangalie sana wanapotosha maadili ya mtanzania.

“Nchi hii watu wanaishi kwa maadili na lazima yafuatwe sio watu wanakimbilia mambo ya nje ya nchi waliangalie upya suala hilo huku wakijiuliza hii nchi ina maadili?,” anasema msanii huyo shabiki wa Yanga ya Dar es Salaam….

Zaidi Kuhusu Habari Hii,Bonyeza hapa.

Keshokutwa,siku ya Alhamisi tarehe 30 December,ndani ya Mzalendo Pub jijini Dar-es-salaam,kutafanyika mpambano wa  kukata na shoka baina ya bendi mbili kongwe nchini Tanzania. Ni mpambano wa Mlimani Park Orchestra dhidi ya mahasimu wao Msondo Ngoma.

Kama wewe ni miongoni mwa wale wapenzi wa daima dumu wa muziki wa dansi au watu ambao wamekuwa wakifuatilia muziki wa dansi nchini,ni wazi kwamba ipo bendi,miongoni mwa hizo mbili,ambayo wewe ni “mnazi” wake zaidi.

Mpambano kama huu bila ubishi ni jambo ambalo achilia mbali kwamba ni nadra kutokea,bali ni tukio ambalo sio la kulikosa.Ni Simba na Yanga kwa upande wa muziki.Kama ni ndani ya La Liga,basi ni El Classico(Real Madrid Vs Barcelona).

Kila bendi imeahidi makubwa.Tambo ni zile zile kama zilivyo kwenye utani mwingine wowote wa jadi.Sikinde wamejitamba zaidi kwa kumrudisha nyumbani,Max Bushoke,maalumu kwa mpambano huu!

Ingawa Msondo mpaka hivi sasa hawajaagiza “kifaa” chochote kutokea nje ya nchi,wao wanasema moto wao ni ule ule uliowafanya wakaitwa Baba ya Muziki.

Je,wewe ni shabiki wa Msondo au Sikinde?Unadhani nani ataibuka mshindi?(sijajua utaratibu utakaotumia kumpata mshindi,kama upo).Kwa vyovyote vile,hakuna ubishi kwamba huu utakuwa mpambano wa aina yake na ambao utatoa burudani ya kweli kwa mashabiki watakaohudhuria.Kila la kheri kwa bendi zote? Au unataka kujua mimi ni shabiki wa bendi gani….?

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Majaji wa Mahakama Kuu.Hiyo ilikuwa ni wakati wa shughuli za kumuapisha Jaji Mkuu Mpya,Mohamed Chande Othman,zilizofanyikia katika viwanja vya Ikulu jijini Dar-es-salaam hivi leo.

Jaji Mkuu mpya,Mohamed Chande Othman,akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu anayestaafu,Jaji Augustino Ramadhani.

read more

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page