Miongoni mwa marais barani Afrika ambao walikuwa wananivutia sana ni pamoja na Rais mstaafu wa Ghana,Jerry Rawlings. Kilichonivutia zaidi ni historia yake na jinsi ambavyo alianza kuiongoza nchi ya Ghana.

Hivi leo inaaminika kwamba mafanikio ya kiuchumi na kidemokrasia iliyonayo Ghana ya leo, yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Jerry Rawlings. Hivi leo Ghana ni nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi barani Afrika na hivi karibuni iliingia katika orodha ya nchi zinazozalisha mafuta ulimwenguni. Katika siasa au demokrasia,nchi hiyo inasemekana kuwa na demokrasia iliyokomaa zaidi barani Afrika baada ya kushuhudia mabadiliko kadhaa ya vyama vinavyoongoza. Alipokuwa anaondoka madarakani,chama chake ambacho ndicho kilikuwa chama tawala,kilishindwa kabla ya kuweza kurejea tena madarakani miaka nane iliyofuata.

Jerry Rawlings aliiongoza nchi ya Ghana kwanza kama “dikteta” kuanzia mwaka 1981-1992 kufuatia mapinduzi ya kijeshi aliyoyaongoza hapo awali.

Ilikuwa May 15,mwaka 1979 alipowaongoza maofisa kadhaa wa ngazi za chini kutoka Jeshi la Anga la nchi hiyo(akiwa miongoni mwa maofisa hao). Wakati huo Ghana ilikuwa ikiongozwa kijeshi. Kwa hiyo unaweza kusema yalikuwa mapinduzi ya maofisa wa ngazi za chini dhidi ya maofisa wa ngazi za juu. Kilichomsukuma Rawlings ilikuwa ni kupinga rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma uliokuwa umetapakaa kila kona( Unaweza kuita “ufisadi” ukipenda.)na kuporomoka kwa uchumi.

Jaribio la kufanya mapinduzi halikwenda vizuri.Jerry Rawlings alikamatwa na kupitia mahakama ya kijeshi, akawekwa ndani akisubiri kusikiliza kwa kesi yake. Lakini akiwa jela na kabla hukumu rasmi haijatolewa, kundi lingine la maofisa wa kijeshi lilivamia jela na kumtoa likimtaka awaongoze katika mapinduzi.

Baada ya kutolewa au kutoka jela,Rawlings akatangaza kupitia radio kwamba anaunda Armed Forces Revolutionary Council maalum kwa ajili ya kumuondoa madarakani kiongozi wa kijeshi aliyekuwepo madarakani.Alikuwa akiitwa William Fred Akuffo.

Zoezi hilo lilifanikiwa na Jerry Rawlings aliongoza harakati za aina yake katika “kuisafisha” Ghana ambayo yeye na wenzake waliamini ilikuwa imeoza kwa rushwa na ufisadi. Mghana mmoja ambaye alishuhudia harakati hizo anasema Jerry Rawlings alipewa support kubwa na vijana wasomi kutoka vyuo vikuu  ambao nao walikuwa wamechoshwa na mambo yalivyokuwa.

Vijana hao wakiongozana na maofisa wa kijeshi waliokuwa chini ya Rawlings,wakaingia kila kona ya nchi wakikagua vitabu vya kumbukumbu za kifedha nk. Endapo itaonekana kwamba wewe ndio chanzo cha rushwa na ubadhirifu moja kwa moja unakwenda mahakamani. Kwa sababu wakati huo nchi ilikuwa ni ya kijeshi,wengi miongoni mwa watu waliothibitishwa kuwa chanzo cha rushwa walikuwa maofisa wa kijeshi. Adhabu yao ilikuwa KIFO kwa kutandikwa risasi hadharani!

Miongoni mwa watu waliouawa hadharani ni pamoja na viongozi wa kijeshi waliopita. Hawa kimsingi walikuwa marais waliomtangulia wakiwemo Akwasi Afrifa, Ignatius Acheampong na William Fred Akuffo.

Wote waliuliwa hadharani ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu tangu Rawlings na wenzake walipoanza zoezi la “kuisafisha” Ghana. Baada ya kuamini kwamba zoezi la “kuisafisha” Ghana limekamilika, Rawlings alijiweka pembeni na kupisha kuitishwa kwa  uchaguzi wa kitaifa huku yeye akiwa hayumo miongoni mwa wagombea. Yeye alirejea jeshini na kuendelea na kazi yake kama pilot wa ndege za kijeshi kazi ambayo inasemekana aliimudu vizuri sana.

Uchaguzi ulifanyika na Dr.Hilla Limann, akashinda kwa tiketi ya chama cha National People Party(PNP) na hivyo Ghana ikawa imerejeshwa katika serikali ya kawaida. Baada ya muda mfupi tu (September 1979 mpaka December 1981) Jerry Rawlings akaona Dr.Hilla Limann, anairudisha tena nchi kule ilikotoka.Rushwa ikawa imeanza tena kutapakaa. Ufisadi ukaanza tena kuota mizizi. Baada ya kuona hivyo,akaipindua serikali ya Dr.Limann na kutwaa madaraka tarehe siku ya mkesha wa mwaka mpya mwaka 1981.Akaitupilia mbali katiba iliyokuwepo,akalivunja bunge na kuweka sheria kuondoa vyama vya kisiasa.

Jambo la kwanza alilolifanya baada ya kutwaa madaraka ni kuunda   Provisional National Defence Council(PNDC) ukiwa na mchanganyiko wa wajumbe kutoka uraiani na jeshini na yeye Jerry Rawlings akiwa Mwenyekiti.Baraza hilo ndio likawa chama pekee cha kisiasa.

Kazi ya kwanza ya baraza hilo ilikuwa ni kuanzisha mchakato wa kuirudisha Ghana kwenye utawala wa kiraia ambapo kila M-Ghana angejisikia kwamba anacho cha kuchangia katika maendeleo ya nchi. Suala la huduma ya afya kwa wote lilipewa kipaumbele ambapo sera ya kuzuia maradhi ilitiliwa mkazo.

Mwaka 1992, Rawlings alistaafu rasmi kutoka jeshini na kuanzisha rasmi chama cha National Democratic Congress(NDC) baada ya kukubalika kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi kufuatia mchakato uliofanywa na tume ya demokrasia(National Commission for Democracy) aliyoiunda Rawlings.

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika baada ya hapo,Jerry Rawlings alishinda kwa kishindo. Alishinda tena uchaguzi mkuu miaka minne iliyofuata(1996) na hivyo kutokana na katiba akaiongoza tena Ghana kwa kipindi kingine cha miaka minne mpaka mwaka 2001 alipostaafu.

Jerry Rawlings alizaliwa tarehe 22 June mwaka 1947. Baba yake alikuwa ni mkemia kutoka nchini Scotland aliyekwenda kufanya kazi nchini Ghana(wakati huo ilikuwa ikiitwa Gold Coast).Alijiunga na jeshi la anga la nchi hiyo mwaka 1967. Yeye na mke wake Nana Konadu Agyemah-Rawlings wana watoto wanne.

Pichani ni Jerry Rawlings akisalimiana na Rais wetu Dr.Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana hapo juzi nchini Ethiopia wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika(AU).Picha kwa hisani ya Mawasiliano Ikulu.

Mwezi wa kwanza karibuni tunaumaliza.Wafanyabiashara wengi huulalamikia mwezi huu kutokana na mapato yao kupungua sana. Watu wengi huwa wanakuwa katika breki ya “matumizi” baada ya mwezi wa 12 ambao huwa unaaminika kuwa mwezi wa kipato. Matumizi huzidi kipimo. Kuna Xmas,ubarikio,ubatizo nk.Vyote hivyo huhitaji matumizi.

Lakini ukiachana na mwezi huu wa kwanza,wapo wenzetu ambao wao hawajali mwezi wa kwanza wala wa mwisho,wala wa katikati. Kwao kila siku ni muda wa matumizi. Akiingia Bar lazima kila mtu ajue kwamba fulani kaingia.Anapoketi ni pale kaunta. Mezani kuna simu kama tatu hivi.Zote za bei mbaya.Ameunganishwa na mitandao yote mikubwa. Utamuonea huruma zinapoita zote kwa pamoja.Mbaya zaidi ni pale zinapoita kwa pamoja na wote wanaojaribu kumpigia ni vimwana wake tofauti.Aanze na yupi kisha amalizie na yupi?

Huyu bwana hali na kunywa peke yake.Sio mchoyo.Nyote mliopo pale mtafaidi.Maagizo yake huwa ni “mpelekee kila mtu aliyepo hapa kinywaji anachotaka”.Ili mradi tu.Fikra kwamba anatakiwa kuwekeza kwa kesho hazipo.Alirithi utajiri na anachojua yeye ni kuutumia vilivyo.Bomoa leo tutajenga kesho.

Leo tunao Juwata Jazz Band au Msondo.Hii ni miongoni mwa bendi kongwe kabisa nchini.Katika wimbo huu,Tupa Tupa,wanatoa usia au ushauri mzuri sana kuhusu maisha.Kuhusu kujilinda na yale ya kesho au keshokutwa.Wanaasa kuhusu kutopenda anasa. Usikilize kwa makini.Enjoy your weekend.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

A sliced Carrot looks like the human eye The pupil, iris and radiating lines look just like the human eye…and YES science now shows that carrots greatly enhance blood flow to and function of the eyes.

A Tomato has four chambers and is red. The heart is red and has four chambers. All of the research shows tomatoes are indeed pure heart and blood food.

Grapes hang in a cluster that has the shape of the heart. Each grape looks like a blood cell and all of the research today shows that grapes are also profound heart and blood vitalizing food .

A Walnut looks like a little brain, a left and right hemisphere, upper cerebrums and lower cerebellums. Even the wrinkles or folds are on the nut just like the neo-cortex. We now know that walnuts help develop over 3 dozen neuron-transmitters for brain function.

Kidney Beans actually heal and help maintain kidney function and yes, they look exactly like the human kidneys .

Celery, Bok Choy, Rhubarb and more look just like bones. These foods specifically target bone strength. Bones are 23% sodium and these foods are 23% sodium. If you don’t have enough sodium in your diet the body pulls it from the bones, making them weak. These foods replenish the skeletal needs of the body.

Eggplant, Avocadoes and Pears target the health and function of the womb and cervix of the female – they look just like these organs. Today’s research shows that when a woman eats 1 avocado a week, it balances hormones, sheds unwanted birth weight and prevents cervical cancers. And how profound is this? …. It takes exactly 9 months to grow an avocado from blossom to ripened fruit. There are over 14,000 photolytic chemical constituents of nutrition in each one of these foods (modern science has only studied and named about 141 of them).

Figs are full of seeds and hang in twos when they grow. Figs increase the motility of male sperm and increase the numbers of Sperm cells to overcome male sterility.

Grapefruits, Oranges, and other Citrus fruits look just like the mammary glands of the female and actually assist the health of the breasts and the movement of lymph in and out of the breasts .

Onions look like body cells. Today’s research shows that onions help clear waste materials from all of the body cells They even produce tears which wash the epithelial layers of the eyes.

Sweet Potatoes look like the pancreas and actually balance the glycemic index of diabetics.

Olives assist the health and function of the ovaries

Source: http://www.islamcan.com/index.shtml

Ni miaka ya 90.Kitu tunachokiita hivi leo Bongo Fleva ndio kwanza kinaanza kushika kasi. Hakikubaliki bado. Wazazi wengi wanasema ni uhuni.Rap,Rap.Maanake nini? Vijana hawaeleweki mbele ya wazazi,ndugu,jamaa na hata baadhi ya marafiki. Yule keshapotea. Siku hizi kila ukikutana naye anarap-rap tu. Pamoja na hayo,zipo sehemu wanazokubalika. Kuna party za ufukweni. Huko wapo watu wanaowaelewa na kuwasikiliza achilia mbali kuwaona “idols”. Hawakukata tamaa. Wakaendelea kujitoa mhanga kwa kuelimisha kupitia sanaa ya muziki. Leo hii,muziki upo ulipo.Unasikilizwa na watu wa rika zote. Kampeni zinaendeshwa zikisindikizwa na muziki huo.

Miongoni mwa vijana waliokuwepo katika kundi hilo la ‘waasisi” ni pamoja na Ahmed Dola(pichani) ambaye kwa jina la kisanii, tulikuja kumjua kama Balozi Dola Soul. Bila shaka unamkumbuka toka enzi zile za The Deplomatz. Alitamba sana na nyimbo kama vile Kwenye Chati, Nje ya Ndoa(akishirikiana na Mabaga Fresh) na zinginezo kibao.

Baada ya mafanikio kadhaa katika muziki ikiwemo tuzo ya kundi bora la Hip Hop akiwa na The Deplomatz mwaka 1999,Balozi aliamua kuhamishia makazi yake nje ya nchi akipitia nchi kama Uingereza na hatimaye Marekani alipo hivi sasa.

Je,amekacha game moja kwa moja?Jibu la wazi ni Hapana. He was busy taking care of other things such as school and family.Now he is back. Anawakumbusha wapenzi wa Bongo Fleva,toka katika generation yake mpaka hii mpya,kwamba bado anaweza na yupo tayari kurejea. Wimbo unaitwa Balozi Wenu. Usikilize hapa chini. Welcome Back Balozi!!

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Kama unafuatilia kwa karibu maendeleo ya Bongo Fleva,bila shaka tayari umeshausikia wimbo huu mpya kutoka kwa AY akiwa amemshirikisha Miss Trinity,mdada mwenye makazi yake huko California nchini Marekani.

Kama bado hujapata nafasi ya kuusikiliza,achilia mbali kuona video yake,ndio maana kuna kitu kama BC ambapo “mteja” ni mfalme.Tunataka uwe up to date na usipitwe na lolote lile kubwa linalotokea.

Baada ya kufanya vizuri mwaka jana,AY anasema ndio kwanza anauanza mwaka 2011.Na kama inavyoonekana hajasahau alikotoka.Nazungumzia kule kulikopelekea tukamwita “Mzee wa Commercial”. Anachoangalia ni ukumbi umefurika,watu wanaruka chini na juu na ngoma iliyopo hewani ni kutoka kwake!

Wimbo huu ambao umepikwa na Hermy B una historia ya Afrika Mashariki kiaina. Wakati audio imepikwa jijini Dar-es-salaam,video imefanyiwa makeke jijini Kampala nchini Uganda. Hapa tunakupa fursa ya kusikiliza kwanza wimbo katika audio, kisha  hapo chini ni video ya Good Look

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

THE OFFICIAL VIDEO

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Pichani ni Jenerali Davis A.Mwamunyange-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania. Amekuwa Mkuu wa Majeshi tangu tarehe 13 Septemba mwaka 2007 na bado anashikilia cheo hicho mpaka hivi sasa.

Ukitaka kujifunza mengi kuhusiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) au kwa Kiingereza Tanzanian’s People Defense Forces(TPDF) ikiwemo historia yake,muundo wake,shughuli zake,jinsi ya kujiunga na jeshi na mengineyo mengi,Tembelea Tovuti ya JWTZ kwa kubonyeza hapa.

In this photo,on the left is Mwalimu Julius Kambarage Nyerere-The Founding Father of the nation of Tanzania with Dr.Kwame Nkrumah, the first president  of Ghana and the first Prime Minister of Ghana.

I know that any attempt to compare leaders like Nyerere and Nkrumah with majority(if not all) of the leaders we have across Africa today always ignites controversial debates, that wouldn’t stop me from asking this question; Is there anything to compare? Really?

Kwa kawaida mwezi wa kwanza huwa mgumu!Niulize kwanini?Sababu ni nyingi.Lakini zile ambazo tumezizoea ni kwamba “mifuko” huwa inakuwa myeupee.Ita uchakavu ukipenda.Baada ya kunywa,kula na kusaza wakati wa Xmas,mwezi wa kwanza huwa ni muda wa kutafakari.Mwezi wa kukuna kichwa ukijiuliza mwisho wa mwezi unafika lini.Ukienda benki yule “teller” asipokuwa makini anaweza akaambulia za uso au matusi.Iweje akaunti yangu ionyeshe sina kitu? Well…matumizi.Ulipitiliza mtu wangu.Ukajifanya tupatupa pale Magomeni,pale Mwembe Yanga,pale “showroom” au Samaki Samaki,pale Keko Mwanga kwa yule mpika “kiti moto” maarufu,pale…

Kwa bahati mbaya hasira huwa zina tabia ya kupelekwa kusiko.Unwaranted Anger.Anatafutwa “victim”  hapo.Aliyepo mbele yako ndio huyo huyo. Unaambiwa umeingia anga zangu. Yaani ni kama vile kuketi kwenye mataluma ya reli na kujifanya husikii honi.

Mambo huweza kwenda kombo victim akawa mpenzi/mke au mume.Ghafla mashavu yanavimba,amani inatoweka,vijembe kwa kwenda mbele,ugomvi usio na mwenyewe.Kisa?Hawala ya fedha. Ukichunguza sana kisa ni kuchacha.Bwana hataki kuketi karibu na Mamaa kwa kuhofia akifanya hivyo ataulizwa kuhusu ile doti ya kitenge kutoka Kongo aliyoahidi. Dawa,kujidai una mawazo mengi kichwani na bize na kazi. Siku hizi wengine wanakimbilia kwenye Facebook. Busy kutwa ku-connect na marafiki.Hakuna anayeweza kuamua ugomvi wa namna hiyo.Majirani wanabakia kuwa “shingo feni”.Wanasikilizia ukutani.

Hakuna anayeweza kuamua isipokuwa wapenzi wenyewe.Hiyo ndio raha na karaha ya mapenzi.Ndio maana unaambiwa wanapogombana wawili wapendanao,usiingilie.Ukijifanya kuingilia mwisho wa siku wenyewe wanapatana kimbembe kinabaki kwako.Unasutwa.Siku hizi nasikia kuna matarumbeta ya kukodishwa kwa ajili ya “kusuta” mtu!

Nyenzo mojawapo zinazotumika katika kupatana kwa wawili wapendanao ni nyimbo.Tangu enzi na enzi nyimbo za mahaba zimekuwa nyingi zaidi.Zina maana yake.Unaweza kuelezea kilichomo moyoni bila kusema sana.Mpenzi nisamehe,sitorudia tena,rudi nyumbani tujenge familia.Ili mradi tu maneno yanayoweza kupenya kwenye ubongo na fikra.

Mfano ni Zilipendwa ya leo.Wimbo unaitwa Nirudie Mama,ni kutoka kwao Moro Jazz Band kutoka ule mji kasoro bahari,kule kwenye Milima ya Uluguru kama inavyoonyesha picha hapo juu.Kama ulivyo ujumbe uliomo katika nyimbo hii,ukikosea au mkikoseana,basi isiwe ngumu sana kuombana msamaha.Kubali yaishe.Ni uungwana na ushujaa.Life goes on.Weekend njema

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Heroin addiction is a growing problem in Zanzibar, and a group called Muamko (meaning ‘Awakening’) was created two years ago by recovering addicts, and a year ago they decided to forge ahead with creating Drug Free Zanzibar – an NGO dedicated to providing education, rehabilitation and recovery facilities for Zanzibaris in need of help to quit the drug.

Explore Zanzibar Co. Ltd has therefore decided to team up with ‘Drug Free Zanzibar’, in association with Vodacom Foundation & the well-known fashion designer Ally Rehmtullah from Dar es Salaam, along with guest designers like Farouque Abdella, Vida Mahimbo and Kihage, together with International belly dancer Tamalyn Dallal who has danced her way around the world to raise funds for the recovery projects run by Drug Free Zanzibar, to take place during a gala dinner at the Zanzibar Serena Hotel on the 8th of February 2011 at 6:30pm.
This event is scheduled to take place during the world famous Sauti Ya Busara week, under the Busara Xtra platform. Busara Xtra is the name given to the variety of fringe cultural shows and activities happening in Zanzibar during this week.

Come and show your support, of an evening full of fashion, style & music while in the meantime raising funds towards the cause.

This event is sponsored by  Vodacom Foundation, Zanzibar Serena Inn, i-View Media, Darling Hair, QMB, Vayle Springs & DarLife.

Tuesday  8th February 2010

Zanzibar Serena Inn: 6:30pm – 10:30pm

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page