

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Arsenal,Thierry Henry,anasema kwamba bado inamwia vigumu kuitoa katika kumbukumbu yake timu ya Arsenal kwani kila arejeapo hujisikia kama amerudi “nyumbani”
Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters,Henry ambaye mpaka leo anashikilia rekodi ya kuifungia klabu hiyo magoli mengi zaidi(alifunga magoli 226), anasema bado anaipenda Arsenal.
Muhimu aliyoyaongelea Rais katika hotuba ya mwezi huu ni
- Milipuko ya mabomu Gongo la Mboto-Uchunguzi unaendelea kwa kushirikisha wataalamu wa nje.
- Hali ya Chakula nchini-Upungufu wowote wa chakula utadhibitiwa
- Bei ya sukari-itadhibitiwa ambapo kilo moja itauzwa Tshs/=1,700 na sio zaidi ya hapo kuanzia mwezi May.Kwa sasa,serikali imetoa kibali ili kuagizwa kwa sukari kutoka nje.Haitotozwa ushuru wa forodha ili iweze kuuzwa kwa bei nzuri.
- Hali ya Umeme-Mambo Bado
- Hali ya usalama wa nchi-Aelekeza lawama kwa CHADEMA; Kauli zao,maandamano yao yanachochea ghasia,machafuko.Atoa “shule” kwa viongozi wa CHADEMA juu ya nini cha kufanya baada ya Uchaguzi.Asema CHADEMA wanataka kuipeleka nchi pabaya kwa uchu wao wa madaraka.

For the first time,I was able to predict at least 90% of the winners for this year’s Oscars.I am not sure whether that is a good thing or not but I now know that I still love surprises. That means,to me,this year’s Academy Awards were quite boring even though for there were some touchy moments.Not gonna mention them.
Didn’t you predict King’s Speech to win Best Picture?Then were you real surprised when Colin Firth won Best Actor spot?Now,I am not saying King’s Speech is not a great movie.It is the predictability of the winners and losers that bothers me a bit.You can see the full list of the winners and runner ups here.
On the other hand,there was the Red Carpet.As it is now,there can’t be Oscars without Red Carpet moments.It would be suicidal if it happens.Who wore what? Who dressed to be the best and actually became the best?Who dressed to impress (you know the psychology of dressing,right?)and then ended right at the bottom in your opinion? Click “continue reading ” for our Oscars 2011 Red Carpet Special;

Ukame wa kuchukua unaoikabili timu ya Arsenal umeendelea hivi leo baada ya kuchapwa magoli 2-1 na timu ya Birmingham katika mchezo wa fainali wa Carling Cup uliofanyikia katika uwanja wa Wembley mapema hivi leo.
Arsenal ikicheza bila nahodha wake,Cesc Fabregas,ilijikuta ikitandikwa bao la kwanza kunako dakika ya 28 kupitia kwa Nikola Zigic. Dakika takribani kumi baadaye Robin van Persie, alisawazisha na hivyo timu zote kwenda mapumzikoni zikiwa zimefungana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kujaribu kumiliki mpira zaidi na kushambulia ingawa ilionekana wazi kwamba vijana wa Arsene Wenger walikuwa hawako makini vya kutosha katika kuzifumania nyavu za Birmingham.
Huku kila mtu akiamini kwamba huenda matokeo yakabakia kuwa 1-1 mpaka dakika 90 zitakapomalizika,mchezaji Obafemi Martins aliyekuwa ameingia dakika 6 tu zilizokuwa zimepita,aliipa Birmigham bao la ushindi kunako dakika ya 89 na hivyo kumaliza kabisa ndoto za Arsenal kukata kiu yao ya kutwaa ubingwa.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya watanzania mtandaoni,bila shaka utakubaliana nasi kwamba miongoni mwa mahali ambapo mengi hutokea na mengi huandikwa kama sio kujadiliwa basi mahali hapo ni katika blog inayokwenda kwa jina la U-turn.
Ni blog ambayo ingawa haina umri mkubwa(ilianzishwa mwaka mmoja na nusu tu uliopita), tayari imefanikiwa kuwa chanzo muhimu cha habari,michapo,maoni,matukio bila kusahau udaku wa hapa na pale.Ni mafanikio ambayo sio ya kubeza.It is what it is!
Mwendeshaji na mmiliki wa U-turn si mwingine bali Mange Kimambi ambaye miaka michache iliyopita ilikuwa ukisikia jina lake basi ilikuwa ni kupitia kurasa mbalimbali za magazeti hususani yale yanayoitwa “magazeti pendwa”. Leo hii mambo ni tofauti. Ni mama,mke,mwanafunzi na blogger mwenye idadi kubwa tu ya wasomaji na wafuatiliaji.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ya kina. Hii ni mara ya kwanza kwa Mange kufanya mahojiano ya kina na chombo chochote cha habari.
Je,Mange ni nani hasa?Ametokea wapi mpaka kufikia alipo hivi sasa ambapo kila siku idadi ya wasomaji na wanaofuatilia maisha yake na anachokiandika inazidi kuongezeka? Ni matukio gani katika maisha yake ambayo kwa namna moja au nyingine yamechangia in making her who she is today?
Nini siri ya mafanikio yake au ya blog yake?Unataka kujua ana maoni gani kuhusu mambo mbalimbali kama vile uongozi wa Rais Jakaya Kikwete?Ana ushauri gani kwa wasichana wadogo(teen girls)? Kwa majibu ya maswali hayo na mengine mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Mange,Karibu sana ndani ya BC.Mambo vipi?
MANGE: Asante sana.Feels good to be here!
BC:
Nimewahi kusoma mahali kwamba maisha yako ni kama vile kitabu kilicho wazi(an open book) ambapo kila anayetaka kusoma anayo nafasi ya kufanya hivyo.Lakini bila shaka utakubaliana nami kwamba wapo ambao hawajui lolote kuhusu historia ya maisha yako.Naomba tuanzie hapo…kwa kifupi tu ulizaliwa wapi,lini,ukasomea na kukulia wapi na mambo kama hayo.
MANGE: Nilizaliwa Hindu Mandal,Hospital- Dar es Salaam.Cheti changu cha kuzaliwa kina mwaka tofauti na passport yangu.According to my passport, I was born in 1980 lakini tukifuata Birth Certificate kuna difference ya 4years.Hii imetokana na kuna wakati mama yangu alitaka kunitoa kwa baba yangu akidai kwamba nina miaka chini ya 7.So kutokana na sheria za Tanzania natakiwa kuishi na mama. Baba yangu naye akawa na documents zake zinazosema nimeshapita miaka 7 kwa hiyo natakiwa kuishi na baba.So mama alikuwa na cheti changu cha kuzaliwa chenye umri tofauti na baba naye na passport yangu yenye umri tofauti.GO FIGURE.
Primary nilisoma Arusha School iliyoko Arusha- the best memories of my childhood came from my time there. Nilifanikiwa kufaulu mitihani ya darasa la 7 na nilichaguliwa kujiunga na Arusha Secondary.Baba yangu alifurahi sana na akanizawadia kwa kunipeleka kusoma Zimbambwe.So niliishi Harare miaka kadhaa kwa masomo yangu ya secondary.
Baada ya hapo nilikwenda Marekani kuanza masomo yangu ya juu.Kwa bahati nzuri (siwezi kusema bahati mbaya) nilijifungua mtoto wa kike,Bhoke, nikiwa Marekani jambo ambalo lilinifanya nirudi nyumbani kujipanga upya.
Then in 2004 nilijiunga na AVU-UDSM ambapo nilipata degree yangu ya Business Administration na sasa nipo Dubai nasoma Masters(MBA)
Mostly nimekulia Dar-es-salaam.
BC: Unakumbuka nini zaidi kuhusu maisha yako ya utotoni?Ulitaka kuwa nani,ulipenda michezo gani na tukio gani la utotoni ambalo hutokaa ulisahau?

Tonight is the biggest night in the film industry.It’s Academy Awards(Oscars) live from Los Angeles,California.It is the night whereby new stars are born or re-born. Someone’s profile goes skyrocketing while someone’s remain where they are with just “Academy Nominee’ additional title in their profile which means a lot anyway!
While the night remains or is supposedly to be strictly for films and talents associated to the industry, we can’t deny the fact that it is also a big night for fashion.For fashion designers who will be lucky to have their designers worn by actresses(and even actors) walking down the red carpet, this is a golden opportunity to sharpen their careers,boost their profile and get an even bigger recognition. No wonder the struggle to bring actresses and actors in their fitting rooms is so intense.

Ni miongoni mwa walinda milango(golikipa) bora kabisa waliowahi kutokea nchini Tanzania.BC inamtafuta kwa ajili ya mahojiano maalumu.Tafadhali kama unajua tunapoweza kumpata Mwameja au kama Mwameja mwenyewe unasoma ujumbe huu,tafadhali tuwasiliane kupitia bongocelebrity at gmail dot com au info at bongocelebrity dot com.
+447527190239,
+447404332910,
+447876126862,
+4407747129987,
+447944473389

Utakuwa ushawahi kusikia mtu akimwambia mwenzake au akikwambia “Unanijua au unanisikia?Mara nyingi huwa inakuwa katika kujitapa au katika ugomvi wa namna fulani.Kila mtu hupenda kuwekwa juu.Ni kama ile hadithi ya mwamba ngoma….
Je,unamjua au unamsikia?Ni swali kutoka kwa Mwana FA katika wimbo wake mpya ambao,kama zilivyo nyingine,zimejaa mistari yenye kuhitaji utulivu fulani ili kuelewa bayana anachokisema.Upo mstari mmoja ambao nimeusikia…usinipigie makofi maana mikono itachoka.Well done Mwana FA.Usikilize hapa
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Credit za wimbo huu ni kama zifuatazo;


sending...
