Kama unafuatilia programs mbalimbali za TV kutoka nchini Marekani,basi bila shaka unamtambua Jaji maarufu anayejulikana kama Judge Judy (jina kamili Judy Sheindlin).

Basi kuna habari kwamba mapema hivi leo alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya kupata maumivu makali ya tumbo wakati akiwa katika studio yake.

read more

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na utalii wakati alipofanya ziara yake ya kukazi wizarani hapo jana jioni.

Photo/Ikulu

Rapper mkali kutoka nchini Marekani,Lil Wayne ambaye amekuwa katika game tangu akiwa na umri wa miaka 15 tayari ameanza kuzungumzia kustaafu mara atakapofikisha umri wa miaka 35. Lil Wayne ambaye miongoni mwa wafuasi wake kupitia label yake ya  Young Money ni pamoja na Rapper mkali mzaliwa wa Toronto,Canada na rapper machachari wa kike,Nicki Minaj, hivi sasa ana umri wa miaka 28. Kwa maana hiyo Rapper huyo ana miaka mingine 7 tu kusimama imara katika ulingo wa muziki.

Akizungumza na Angie Martinez wa Hot 97, Lil Wayne ambaye mashabiki wake hupenda kumwita “Weezy” alieleza kwamba atahakikisha anajituma kwa kadri ya uwezo wake ili kupumzika atakapotimiza miaka 35. “Hiki ndicho kinachotokea unapofanya kazi sana.Watu wanadhani kwamba unaposema unafanya kazi sana ni kwamba unafanya kazi masaa mawili ya ziadaHaya ni maisha yangu, “alisema. “Ndio maana kustaafu katika umri wa miaka 35 ni sawa sawia kabisa kwangu”

Wakati wasanii wenzake kadhaa waliwahi kutangaza kustaafu na kisha kurudi kwenye game ,kama vile Jay-Z, Lil Wayne anaweka bayana kwamba yeye hatanii anaposema hivyo. “Huu ni mpango madhubuti kabisa na nitautekeleza, ”

Alipoulizwa kama ana mpango wa kuendelea kupata watoto wengine, rapper huyo aliweka wazi kwamba hana mpango huo,”Hapana,nipo sawa kwa sasa.Nina watoto wanne na nadhani wananitosha kwa wakati huu”

Hivi sasa Lil Wayne yupo katika tour “I am Music II tour” pamoja na Nicki Minaj, Rick Ross na Travis Barker na anatarajiwa kuachia album yake mpya ya The Carter IV tarehe 16 Mei mwaka huu.

Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma”Baba ya Muziki”, Muhidin Maalim Gurumo, amelazwa tena katika Hospitali ya Muhimbili.Hiyo ni kwa mujibu wa Blog ya Bongo Weekend ya Khadija Kalili.

Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi sita kwani kama mtakumbuka Maalim Gurumo alilazwa hospitalini hapo mwezi Novemba mwaka jana akisumbuliwa na mapafu kujaa maji. Baadaye alitoka hospitalini hapo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii lakini bila yeye mwenyewe kupanda jukwaani.

Hivi karibuni alihudhuria mpambano wa bendi yake ya Msondo Ngoma na Sikinde pale Diamond Jubilee.

BC inamtakia Muhidini Maalim Gurumo kila la kheri,apone haraka.

Bonyeza hapa kumtembelea mwenyewe ili ujue nini kinachojiri.It’s a Shock!

Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi(pichani), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 31 Machi na tarehe 01 Aprili 2011.Waziri amepanga kuwaona wasanii kwa utaratibu ufuatao:-

31/03/2011 (Alhamisi) Saa 5:00 asubuhi

Wasanii wa Sanaa za Picha Jongevu na Sanaa za Maonyesho

Saa 7:00 Mchana

Wasanii wa Sanaa za Muziki na Sanaa za Ufundi

01/04/2011 (Ijumaa)Saa 3:00 asubuhi

Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya

Izingatiwe kwamba Waziri atawaona wasanii wa muziki kwa siku mbili tofauti. Tarehe 31/03/2011 ataongea na wasanii wa Muziki wote isipokuwa wale wa Kizazi Kipya. Wasanii hao ni pamoja na wale wa Muziki wa Bendi, Taarab, Disco, kwaya na Muziki wa Asili.

Tarehe 01/04/2011 ataongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya tu. Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa hakikisheni wasanii wamepata taarifa na kuhudhuria kwa wakati.

Lengo kuu ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.

Ghonche Materego

KATIBU MTENDAJI


In the next Rolling Stone issue,Rihanna is on the cover.Here is the little bio of her from the Rolling Stone

As a sister company of ZG-Designs that has a large base for marketing in Tanzania, ZG Films presents Zanzibar’s first high quality Bongo Movie, Glamour produced by Javed Jafferji and Directed by Amitabh Aurora which tells the story of young Zanzibari girl who dreams of becoming a model and her trials and tribulations as she leaves her conservative Muslim home to peruse her glamorous new career in the big city, Dar es salaam.

Staring one of Tanzania’s top models, Eva Issac, and celebrated Tanzania couturier, Mustafa Hassanali, this is the film that will undoubtedly appeal to the masses in a country filled with beauty pageants and where becoming a model is a dream of many – both male and female.

Glamour, a Swahili Bongo Film with English subtitles is set to be released across the nation this April. Below is the Official Trailer of the movie;

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mwanamuziki Beyonce Knowles kutoka nchini Marekani ametangaza kwamba hatoendelea kuwa chini ya menejimenti ya Baba yake,Mathew Knowles,katika shughuli zake za kimuziki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake,Yvette Noel-Schure,Beyonce anatengana na baba yake katika masuala ya muziki kutokana na makubaliano yaliyofikiwa pasipo mikwaruzano.

“Namshukuru sana kwa yote aliyonitendea”, alisema Beyonce na kuongeza “Nimekuwa nikiwaona baba yangu na mama yangu wakinitumikia kama mameneja wangu na pia waki-meneji kazi zao.Wote ni wajasiriamali mahiri na natumaini kuendelea kufuata nyayo zao”

Mathew Knowles amekuwa meneja wa Beyonce tangu mkali huyo wa muziki alipoanza kutamba akiwa na kundi la Destiny’s Child katika miaka ya 90 na aliendelea kuwa meneja wake hata pale msanii huyo alipoamua kwenda solo.Mzazi huyo ndio alikuwa akisimamia kila kitu kuhusu Beyonce ikiwemo muziki,mavazi au fashion,ushiriki wake katika filamu nk. Mpaka hivi sasa Beyonce ameshashinda tuzo 16 za Grammys.

Alipoulizwa kuhusu kutengana huko na mwanae,baba mtu,Mathew Beyonce alisema ” Biashara ni biashara na familia ni familia.Nampenda mwanangu na nina kila sababu ya kujisikia kwa jinsi alivyo na kwa mafanikio ambayo ameyapata mpaka hivi sasa.Namtakia kila la kheri katika kazi zake na mafanikio katika siku za mbeleni”.

read more

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page