WANAMUZIKI FIVE STARS MODERN TAARAB WAPATA AJALI MBAYA,WATU 12 WAFARIKI!

Habari ambazo zimethibitishwa ndani ya Clouds FM kupitia Mkuu wa Polisi mkoani Morogoro,zinapasha kwamba wanamuziki wa kikundi cha Five Stars Modern Taarab wamepata ajali mbaya ya gari karibu na Mikumi mkoani  na Morogoro na watu 12 wamepoteza maisha yao huku wengi wao wakihofiwa kuwa ni wanamuziki wa kundi hilo lililoanzishwa chini ya miaka mitatu iliyopita.

Wanamuziki hao walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Coaster wakitokea mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma kwa ajili ya shughuli zao za muziki.Inasemekana ajali ilitokea baada ya Coaster hiyo kulivaa lori bovu la mizigo lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabarawakiwemo waimbaji, mafundi mitambo na mkurugenzi wa bendi.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Katika ajali hiyo, alikuwemo pia mwimbaji mkongwe Mwanahawa Ally ambaye alinusurika baada ya kuumia vibaya, aliungana nao kama mwimbaji mwalikwa akitokea Melody ModernTaarab.
Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote na awasaidie waliojeruhiwa waweze kupona haraka na kuwapa nguvu ndugu,jamaa na marafiki wote katika wakati huu mgumu.Amina
Zifuatazo ni picha mbalimbali kuhusiana na ajali hiyo kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo Global Publishers,Issa Michuzi,Dj Choka,nk.ONYO: BAADHI YA PICHA NI ZA KUTISHA.TAFADHALI USIFUNGUE KUANGALIA KAMA HUNA UWEZO WA KUSTAHIMILIPichani ni baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo wakati wa uzinduzi wa kundi hilo July 2009

 1. mashaka kulanga, 22 March, 2011

  tunamuoamba mwenyezi mungu awape amani, faraja na utulivu wafiwa kwa kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa watanzania wote hususani wapenzi wa taarabu.

  tunamuomba mwenyezi mungu kwa huruma na mapenzi yake awalaze mahala pema peponi na awape tahfifu wafiwa wote-Amina

  Mashaka kulanga

 2. Catherine Michael, 22 March, 2011

  mimi ndimi ufufuo na uzima yeye aaminiye ajapokufa atakuwa anaishi(maandiko matakatifu kutoka katika Biblia ( Yohana25:26) poleni five stars, Tufarijiane kwa pamoja kwani kila Roho itaonja mauti, bali tunaamini siku moja tutaishi katika Roho na Kweli, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki FIVE STARS, AMEN!!!!

 3. james lemar, 22 March, 2011

  du nimesikitika sana kibinafsi Mungu awlaze mahali pema amen

 4. saulo kayombo, 22 March, 2011

  Mungu aziweke pema roho za marehemu na zipumzike kwa amani Amina.

 5. Omar Mwagao, 22 March, 2011

  Poleni sana wenzetu TZ
  KWA KUWAPOTEZA WASANII WALIOKUWA NA NIA NA BIDII YA KUINUA MUZIKI WA TAARAB

 6. agape, 22 March, 2011

  pole sana
  MUNGU ATUPE MOYO MKUU KTK KIPINDI HIKI AMBACHO NI KIGUMU NA HUZUNI KWETU KWA YALIYO WAFIKA WENZETU.
  MUNGU AILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMIN.

 7. Mwatambazi, 22 March, 2011

  Natoa pole kwa wote waliofiwa, na mungu awaweke mahala pema marehemu wote, aaaamina.

 8. Mwanamke wa Shoka (UK), 22 March, 2011

  Oh!! Ni huzuni! Mungu azirehemu roho za marehemu mahali pema peponi, AMIN.

 9. Mwanamke wa Shoka (UK), 22 March, 2011

  …oh!! Inatisha…jamaani!!…Mungu awape heri wafiwa…amin

 10. Amina Chombo, 22 March, 2011

  kila nafsi itaonja mauti, Mwenyezi Mungu awarehemu na kuwasamehe madhambi na makosa, Inshaallah roho zao zilale mahala pema peponi.

 11. Rahma, 22 March, 2011

  poleni sana wafiwa na msiba mkubwa

 12. zitto kiaratu, 22 March, 2011

  ina lilahi waina rajuun!!!!! wafiwa wote m-mungu awaongezee uvumilivu na imani.

 13. lucas, 23 March, 2011

  poleni sana,mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.Amen

 14. Siphanesta, 23 March, 2011

  Mwenyezi Mungu apokee roho zao, na poleni sana wanafamilia na ndugu wa marehemu.

 15. Fatuma Mwangala, 23 March, 2011

  Kifo ni njia ya marahaba sote tutaipitia,Mola awape nguvu wote waliofikwa na msiba na kuzilaza roho za marehemu mahala pema peponi

 16. ME, 23 March, 2011

  inna lillahi waina illahi rajiuun. pole kwa wafiwa wote. mimi ni shabiki wa Bi Mwanahawa, mngu akupenda, acha kuimba na urudi kwake. nakutakia nafuu ya haraka.

 17. Sigalla, 23 March, 2011

  MWENYEZI MUNGU AWAPE PUMZIKO LA AMANI KWANI WAMETUACHA KIMWILI LAKINI KIROHO NA KAZI ZAO TU PAMOJA NAO.
  KAZI ZAO NZURI SANA NI SHADA ZURI SANA WALILOTUACHIA. NASI SOTE TUWAOMBEE KWA MWENYEZI MUNGU AWAPE RAHA YA MILELE NA WAPUMZIKE KWA AMANI.

 18. FLORA, 23 March, 2011

  Jamani Mungu awalaze mahali pema hawa wapenzi wetu waliopoteza maisha.

 19. FLORA, 23 March, 2011

  Tuwaombee ndugu zetu ili Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Huruma awapokee katika ufalme wake kwani yeye ndiye ametwaa viumbe wake jina lake lihimidiwe. Amen.

 20. Stella, 23 March, 2011

  Tuwaombee ndugu zetu ili Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Huruma awapokee katika ufalme wake kwani yeye ndiye ametwaa viumbe wake jina lake lihimidiwe. Amen.

 21. jamila, 23 March, 2011

  poleni sana kwa msiba huo ulio watokea nimesikitika kupita kiasi inshallah mungu awa weke mahali pema peponi na wawe waja wagheri inshallah ameeeeeeeeen

 22. mbarouk, 23 March, 2011

  Tuombe husnul khatim!

 23. BAHARI F.M -MOMBASA KENYA, 23 March, 2011

  POLENI SANA NA MUNGU AWAPE FARAJA IPITAYO FAHAMU ZOTE…TUMEPATA KUTANGAMANA NA WAIMBAJI HAWA KATIKA TAMASHA ZETU HUKU KENYA NA HASWA TWAMUOMBEA AFUENI BI MWANAHAWA ALLY

 24. naomi, 23 March, 2011

  poleni sana wafiwa wote na watanzania wote kwa msiba huu. marehemu wote mungu awape pumziko la milele

 25. Ramadhani Abeid, 23 March, 2011

  inalilahi waina rajuun. mwenyezi mungu muumba mbingu na ardhi azirehemu roho za marehemu hawa na inshaallah awaponye majeruhi wote ili waweze kupata ahueni. aidha, awape moyo wa subira wale wote waliotokwa na ndugu, jamaa na marafiki waliofariki katika ajali hii ya kutisha.

 26. noela, 23 March, 2011

  bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.
  kila akifanyacho anakifanya kwa makusudi na mapenzi yake.mapenzi yake yatimizwe

 27. ibrahim kalenje, 23 March, 2011

  mungu azilaze roho za marehem mahali pema peponi Amina..

 28. DENNIS JUMA, 23 March, 2011

  MAY THE LORD REST THEIR SOULS IN PEACE THOSE VICTIMS. GOD GIVES AND TAKES AWAY. ALL ARE PLANS OF GOD. IN BIG SORROW!I PRAY FOR THEM.

 29. DENNIS JUMA, 23 March, 2011

  ITS HARD BUT ALL WE NEED TO PRAY.

 30. irene grumpner, 23 March, 2011

  daah!inasikitisha sana lakini yote hayo ni mapenzi ya mungu nasi sote ni wasafiri ila hso wametutangulia tuwaombee safari njema ya kwenda kwenye makao ya milele MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN!!!!

 31. Atu, 23 March, 2011

  Sijui niseme nini? Nasikia uchungu sana, kikubwa Mwenyezi Mungu azilaze roho zao peponi wapumzike kwa amini.

  Sisi tuliwapenda ila Mwenyezi Mungu kawapenda zaidi.

  Nawapa pole wafiwa wote na MWenyezi Mungu awajalie heri na faraja katika kipindi hiki kigumu, kwauwezo wa sisi binadamu ni vigumu sana kusahau, lakini kwa Mwenyezi Mungu inawezekana.

  Tupo pamoja.

 32. vicky, 23 March, 2011

  Ajali inatisha nawaombea wafiwa wote heri kaitka kipindi hiki kigumu.

 33. Said mada, 23 March, 2011

  Sisi sote pamoja mombasa twasikitika na msiba uliotokea kwa wana5stars.mola awarehemu wote waliotuacha.tupeni namba ya usaidizi.

 34. maryam, 23 March, 2011

  innalilah waina illah rajioon. mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu wote pema peponi,… amin

 35. Deo Mutta, 23 March, 2011

  Dooo jamani inasikitisha sana Mungu awalaze pema peponi AMINA

 36. SN, 23 March, 2011

  Poleni sana wafiwa na wapenzi wa taarab na muziki wa Tanzania. Tunawaombea faraja…

 37. zainabu ramadhani, 24 March, 2011

  inahuzunisha na kusikitisha yote ni mipango ya ALLAH alitakalo hutimia nawapa pole ndugu wote wa marehem tumshukuru mola

 38. George mzigo, 24 March, 2011

  Poleni sana wafiwa ndugu,jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito uliotupata Sisi tuliwapenda lakini Mungu kawapenda zaidi, Mungu hazilaze mahali pema peponi roho za marehemu Amin.

 39. Frank Charles, 24 March, 2011

  Tuna amini kifo chenu kitasababisha pengo kubwa hususan katika Tathnia hii ya muziki wa Taarabu,,lakini hatuna jinsi BWANA alitoa na BWANA ametwaa,,,,Jiana lake lishkuriwe,,,
  Sisi tuna waombea Dua njema kwa Maanani,,,

  AMINA,,,,,

 40. fabiola, 24 March, 2011

  Poleni sana yote hii ni kazi ya Mungu. Wanandugu naomba muamini kwamba kila binadamu siku yake ya kufa ikifika atakufa msifikirie vinginevyo

 41. Kakamaiko, 24 March, 2011

  Ajali haina KINGA ??

  Pamoja na majonzi na huzuni zetu lakini pia tuna HASIRA na wote waliosababisha tukio hili la kutisha.
  hatutafuti mchawi maana huenda hayupo… lakini hili lori lililoharibika/kusimama liliweka ishara kwa tahadhari ya wanaokuja nyuma ??

  Dereva wa Coaster yu wapi ? Ni mmoja wa marehemu??

 42. mama Latifah, 24 March, 2011

  INNALILAH WAINAILAIHI RAJIUUN… KUL – NAFSI ZALIKATUL-MAUTI. MWENYEZI MUNGU AWAPE MOYO WA SUBIRA NA IIMANI WAFIWA WOTE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
  AMEEN.

 43. Amina Rashid & Kevin Okech, 25 March, 2011

  In all things give thanks knwing that no one knws the tym and place but we celebrate them they came, brought a big impact, torched lives and gladly they went back to the creater…….. Our de
  pest condolesence to their loved ones we will live to remembe ryou Brothers and Sisters

 44. said, 25 March, 2011

  inallilah waina illahi rajiun sisi sote marejeo yetu ni kwa m/mungu

 45. LUCHELE, 28 March, 2011

  Poleni sana five stars,Mwenyezi mungu awaweke mahali pema peponi.Amina.

 46. yosepha, 28 March, 2011

  kwa kweli hizi ni nyakati za nwisho yatupasa tukeshe tukiomba kila siku kwa maana hatujui siku wala saa jamani hii ajali inasikitisha sana,bwana alitoa bwana alitoa jina lake lihimidiwe,mungu awatie nguvu ndugu wa marehemu kwa kipindi chote kigumu wanachopitia kwa sasa.

 47. Issa seif, 02 April, 2011

  Polen sana familia za wafiwa kinachotakiwa kuwaombea mungu wenze2

 48. Katanga(Shimiwi), 06 April, 2011

  It’s hard to believe if they’ve gone but we’ve to force ourselves believing that they’ve gone & joined a lifeafter.Physically we’ren’t with but mentally & spiritually we’re together.They’re all immotally coz of their works.May Allah rests their souls in eternal peace.Amin

 49. Idrees Assaad Abubakar, 24 May, 2011

  Mtume wetu Muhammad SAW atufundisha kua: HAKIKA KATIKA KUFA KUNA KUSHANGAA, NA MMOJA WENU ANAPO LETEWA HABARI YA KIFO CHA NDUGU AU MPENDWA WENU BASI NA ASISHANGAE NA ASEME INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJEOON. Kisha aseme Ewe Mwenyezi Mungu liandike jina lake huyo kwenye kitabu cha watu wema, na umlete mwengine mbora atakae chukua usukani wa kuiedesha familia wakati wa kukosekana kwake. Na utusamehe sisi na yeye siku ya kiama.

Copyright © Bongo Celebrity