Kheri iwe kwako msomaji.Natumaini hujambo na wiki hii haikuwa mbaya kwako.Kama ilikuwa na mikwaruzo,basi ni ile ambayo unaweza kuikabili.Kama ilikuwa ngumu sana,basi mwachie Muumba.Yeye anaweza.

Hii ni weekend ya katikati mwa mwezi. Hapa tunaweza kusema kama hesabu za mwanzo wa mwezi zilikwenda kombo,basi leo tanki la mafuta lipo chini ya mstari wa katikati.Usitie shaka,wenzako wakikupigia simu kwamba muongozane kwenda viwanjani,tia  kisingizio cha “dozi ya malaria”. Si unajua hakuna kitu kibaya kama kwenda mahali na kuanza kutumbua huku hesabu kali zikiendelea kichwani.Unaweza kabwa na mnofu wa nyama.Kile kicheko cha bar ya kona kinaota mbawa. Zile mbwembwe za “tuletee kama tulivyo na kisha mwambie jamaa wa jikoni aje” leo sio mahala pake.

Ushauri wangu;weekend hii tumia muda wako nyumbani.Cheza na wanao.Soma nao,cheka nao. Hilo likikushinda (yawezekana hujazoea au watoto wana ratiba zingine za birthday parties nk, basi jisomee.Kama unacho kitabu cha After  4:30 cha David G.Mailu kikamate uso. Kuwa makini,kilipigwa marufuku. Sishauri kukamata remote na kuanza kubadili channel. Ina raha gani kushinda kutwa  ukitazama wenzako wanafanya wanachokipenda na kulipwa ilhali wewe chali?! Aste aste,msaada kwenye tuta.Vyovyote vile iwavyo, usikate tamaa,ni life.Kuna leo na kuna kesho. Unaweza lala masikini ukaamka tajiri.Cheza karata zako vyema.Jitokeze mahali sahihi katika wakati sahihi au muafaka.

Leo katika Zilipendwa tunaelekea Tabora.Kule tunawakuta Tabora Jazz Band.Miaka mingi imeshapita tangu nitembelee mkoa wa Tabora. Leo hii sina hata kumbukumbu nzuri kwamba mara ya mwisho kufika pale ilikuwa lini.Pamoja na hayo, bado ninakumbuka kwamba niliupenda ule mji.Enzi zile,ulikuwa ni mji simple usio na mengi.Watu walijuana vyema.Nakumbuka Chuo cha Uhazili.Kilisifika kwa kutoa makatibu muhtasi wa “ukweli”.Mama zangu wadogo kadhaa wamesoma pale.Nakumbuka shule ya sekondari Uyui.Nilikwenda pale kumsalimia mjomba wangu alipokuwa anasoma pale. Nakumbuka Tabora Girls na Tabora Boys. Mpaka hivi leo nina ndugu wanaishi maeneo ya kule. Nakumbuka disco la pale.Mwana Isungu.Hospitali ya Kitete.Tabora,Tabora,Tabora…nitarudi.

Tukiachana na kumbukumbu yangu inayofifia kuhusu Tabora,Tabora Jazz Band wanao wimbo unaoitwa Tatu Wajidanganya. Kwamba Tatu anadhani kwa sababu anapendwa,basi anayo nguvu ya kumgombanisha jamaa na ndugu zake.Penzi likashinda undugu.Inawezekana?

Wimbo huu ni miongoni mwa zile nyimbo ambazo kwa namna fulani zilikuwa zinatupa kitambulisho cha muziki wa kitanzania ambao ulikuwa ni mchanganyiko mzuri sana wa Afro-Jazz au Afro-Cuban.Jaribu kusikiliza jinsi ala zilivyopangwa.Piga picha jinsi jamaa walivyokuwa jukwaani na zile bugaloo zao.Burudani ya kutosha.Basi burudika  na Tatu Wajidanganya na uwe na weekend njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Msomaji mwenzetu mmoja hapo jana aliomba kuona picha ya Baraza la Mawaziri la sasa baada ya kuona picha ya Baraza la Kwanza la Mawaziri baada ya Muungano katika post iliyopo hapo chini inayomzungumzia Oscar Kambona na Wikipedia.

Kwa bahati mbaya,hatuna picha ya Baraza la Mawaziri lililopo madarakani hivi sasa wakiwa wamesimama au kuketi pamoja. Badala yake tunayo picha hii ambayo tuliitengeneza wenyewe ya Baraza la Mawaziri lililopo madarakani.Kuna fununu kwamba siku si nyingi,Rais Kikwete atafanya mabadiliko katika baraza la mawaziri lililopo.

Sasa badala ya kuweka tu picha na kusema “pichani ni Baraza la Mawaziri na kisha kutoka kushoto kwenda kulia ni yule na yule na yule’,nadhani ni wakati muafaka tukajiuliza,Je unaonaje utendaji wa Mawaziri hawa mpaka hivi sasa?Yupi ambaye unaona anafanya kazi yake ipasavyo na yupi analegalega au kutowajibika kabisa?

Tembelea habari za mtandaoni leo uone habari gani inabamba zaidi hususani kwenye YouTube.Si nyingine bali ni ile ya Rais wa Jamhuri ya Czech kukamatwa na kamera akiiba kalamu “live live” wakati wa ziara yake nchini Chile.Wakati mwenzake yuko “bize” akiongea na waandishi wa habari,jamaa yeye kaona ndio wakati wa kuondoka na kalamu.Tizama video hiyo hapo chini kisha jiulize…What was he thinking?

By the way this is just for your laugh!!

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mwaka juzi niliandika kidogo kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza historia zetu hususani mitandaoni katika zama hizi za maendeleo makubwa na ya kasi ya sayansi na tekinolojia.

Nakumbuka niliandika na kuomba wajuzi wa historia ya nchi yetu,kushiriki katika kuandika na kuitunza historia ya Mwanasiasa Mkongwe,Hayati Bibi Titi Mohammed kupitia mradi wa Wikipedia ambao leo hii unasifika na kuaminika kuwa chanzo cha maarifa mbalimbali.Kwa bahati mbaya,mpaka hivi leo ukurasa wa Bibi Titi Mohammed katika Wikipedia bado una mapungufu.Unahitaji kuendelezwa.Ni kweli kwamba hakuna anayejua kwamba Bibi Titi alizaliwa wapi na kwamba hata tarehe yake ya kuzaliwa haijulikani zaidi ya kwamba alizaliwa mwaka 1926?

Pamoja na utata ambao umekuwa ukijitokeza mara kadhaa kuhusu usahihi wa kinachoandikwa katika Wikipedia,hivi leo inasemekana kwamba wanafunzi wengi,hupata maarifa yao kupitia Wikipedia.

Utata unaojitokeza kuhusu usahihi au kinyume chake katika Wikipedia, unatokana na ukweli kwamba Wikipedia inaandikwa na kila mtu.Wewe na mimi.Kila mtu ana uhuru wa kujiunga na Wikipedia na kuchangia.

Hatari ya uhuru huo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mtu au watu kuandika historia katika jinsi ambayo itakidhi mahitaji yao na hivyo kuandika habari potofu au za uongo.Hilo linaweza kufanyika kwa bahati mbaya au makusudi.

Kama hunipendi mimi Jeff Msangi,basi unaweza ukaingia katika Wikipedia na kuandika unachokitaka wewe mpaka hapo mwingine anayeijua historia yangu kwa jicho lingine,atakapoingia na kusahihisha.Kama mimi mwenyewe nipo hai pia naweza kuwaandikia Wikipedia na kutoa malalamiko yangu na wao watarekebisha.Kwa kawaida,mtu binafsi haruhusiwi kujiunga na Wikipedia na kuandika habari zake binafsi kwa minajili ya kujitangaza na mambo kama hayo.Historia yako inaandikwa na watu wengine.

Sikumbuki nilikuwa nawaza nini leo nilipoamua kujaribu kutafuta habari zinazomhusu Mwanasiasa mkongwe,Marehemu Oscar Kambona(13th August 1928-July 1997). Historia yake,kwa mujibu wa Wikipedia, imeandikwa vizuri na kwa umakini.Nasema kwa umakini kwa sababu imeandikwa kwa nia ya makusudi ya kuelezea maisha ya mwanasiasa huyo katika miale ya kumtaka msomaji kuelewa vizuri historia yake na kile kilichojiri mpaka akaja  kutoelewana na serikali ya awamu ya kwanza  na bila shaka Hayati Baba wa Taifa,Julius Kambarage Nyerere mwenyewe. Lakini kila kitu kilichoandikwa pale ni sahihi? Mtiririko ule wa matukio ndivyo ulivyokuwa? Ni kweli kwamba Kambona na Nyerere walishindwa kuelewana katika suala zima la siasa za Ujamaa na Azimio la Arusha peke yake? (Nyerere aliamini katika Ujamaa wakati Kambona aliamini katika Ubepari)

Baraza la Kwanza la Mawaziri baada ya Muungano.Oscar Kambona ni wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele.

Hapo ndipo linapokuja tena suala la sisi sote,hususani wale wasomi wa historia,kuwa mstari wa mbele katika kuchangia katika miradi kama Wikipedia.Nia ni kuhakikisha kwamba historia ya nchi yetu,ya watu wetu,inaandikwa kwa usahihi wa kutosha na unaokubalika. Tusipofanya hivyo,tunahatarisha kuzidi kuupoteza ukweli kuhusu historia.Muda ni jambo la ajabu.Hutufanya kusahau.Vizazi vya baadae vitasoma nini na kujifunza kutoka kwa nani juu ya historia yetu?

Shime.Wewe msomi.Jiunge sasa na Wikipedia.Sahihisha.Andika.Historia yetu,za kwetu,za watu wetu ni muhimu zikaandikwa na watu miongoni mwetu.

Whenever I hear that a fellow countryman is recognized somewhere,I feel happy and wish to encourage them as much as I can. That is the case with DJ Tama(photo above) who is a Tanzanian working as a resident DJ at Garage Night Club in Dubai.

According to news posted on 24 Seven 365,this brother entered a DJ-ying competition called Middle East Technical and emerged the winner. While the good news doesn’t give out further details about the competition, we ought to recognized him anyways,Congratulations brother.Keep moving,keep working!

DJ Tama ni Mtanzania anayefanya shughuli zake za Udj katika Club moja ya Dubai inayoitwa Garage Night Club.

Here is another production from EmptySoulz Production. A song titled One Minute.Ever wondered what One Minute can do?I mean 60 seconds.Listen to these young but promising artists from Bongo.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mamaa,nihurumieni sitorudia tena.

Aah jamani,nyie si mnajua raha ya ikulu ilivyo jamani,nisameheni.

Kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ametiwa kizuizini mjini Abidjan na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi wa Umoja wa Mataifa.

Alikamatwa wakati majeshi ya kiongozi anayetambulika kimataifa kuwa Rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara na vifaru vya Ufaransa kuingia kwenye makazi yake.

Bw Gbagbo alikuwa akikataa kukabidhi madaraka, akisema alishinda uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba.

Ufaransa ilisema majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara yalimkamata, lakini washirika wa Bw Gbagbo walisema ni majeshi maalum ya Ufaransa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alisema kukamatwa kwa Bw Gbagbo kumemaliza miezi kadhaa ya ghasia zisizo na sababu, na Umoja wa Mataifa utaunga mkono serikali mpya.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KUPITIA BBC-SWAHILI

Mwishoni mwa wiki,Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) alifanya  “maamuzi magumu” ndani ya chama hicho anachokiongoza.

Maamuzi hayo ambayo yaliwashtua wengi ilikuwa ni pamoja na kuvunja Kamati kuu sekretarieti ya chama hicho iliyokuwa inaongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Yusuf Makamba.

Siku moja baadaye,viongozi wapya walichaguliwa kukiongoza chama hicho hatua ambayo inachukuliwa kama hatua za makusudi katika kukiunda upya chama hicho hususani kuondokana na makundi mbalimbali yaliyokuwa yanazidi kushamiri ndani ya chama hicho tawala.

Pichani juu ni viongozi wapya waliochaguliwa kuongoza Kamati Kuu ya Chama na Sekratarieti ya Chama hicho.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu mpya wa CCM-Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara,Abdulrahman Kinana,Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi,Zakhia Meghji. Mwingine ambaye picha yake hatukuweza kuipata mara moja ni Bi.Rehema Nchimbi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu wa Oganaizesheni.

Bw.Yusuf Makamba-Katibu Mkuu anayeondoka au aliyeondolewa madarakani.

Swali ambalo mimi binafsi najiuliza ni Je huu ni mwanzo wa CCM mpya au ni ile hadithi ya mvinyo mpya katika chupa ya kale? Au pengine ndio mwanzo mpya wa migogoro ndani ya chama ikifuatiwa na kujiengua kwa baadhi ya wanachama wa siku nyingi wa chama hicho?

Timu ya soka ya Yanga(watoto wa Jangwani),jana wamechukua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara baada ya kuichapa timu ya Toto Africa ya Mwanza kwa jumla ya mabao 3-0 na hivyo kuwavua rasmi ubingwa watani wao,timu ya Simba Sports Club kwa tofauti ya magoli.

Tofauti na ligi zilizopita,ligi ya safari hii ilibidi kusubiri mpaka michezo ya mwisho ili kujua nani atatwaa ubingwa.Hongera Yanga!

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page