
Mkali wa Hip-Hop,Sean Kingston, yu mahututi hospitalini(Miami Beach Hospital) huko Miami,Florida kufuatia ajali mbaya ya majini aliyoipata baada ya watercraft aliyokuwa akiiendesha kugonga daraja.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari zinazowahusu celebrities zikiwemo tovuti ya TMZ, Sean Kingston alipata ajali hiyo majira ya saa kumi na mbili jioni akiwa na rafiki yake wa kike ambaye habari zake hazijaweza kupatikana mara moja.Waliokolewa na msamaria mwema.
Pia kwa mujibu wa mwakilishi wake,Sean Kingston mwenye umri wa miaka 21 na ambaye anajulikana zaidi kwa kibao chake cha “Beautiful Girls”, hivi sasa yuko katika chumba cha watu mahututi(ICU) na kwamba familia yake inashukuru wote ambao wamekuwa wakiwatumia salamu za kumpa pole Sean na kumtakia kheri.BC inaungana na wote hao katika kumtakia kila la kheri apone.

The Miss Universe Tanzania beauty pageant has got a new queen. Her name is Nelly Kamwera. She was crowned the new Miss Universe Tanzania 2011 at the event held at Golden Tulip Hotel in Dar-es-salaam last evening. Click here for more photos from the event.

This morning I came across this article that I thought I should share here…especially for the ladies of BC. It fits our Beauty and Health page. Which direction should I wipe?Good question huh?


Millen


Kama wewe ni mdau wa BC,naamini unatambua jinsi gani huwa tunafurahi kutambulisha kwako msanii mpya. Ni kwa sababu tunaunga mkono vipaji vipya.Tunaamini katika kukuza muziki kwa njia ya kuwapa wengine nafasi hususani vijana wapya.
Leo tunaye msanii mpya kutoka pande za Mwanza anayekwenda kwa jina C-SIR MADINI.Jina lake kamili ni Peter Mponeja.Chanzo cha jina lake ni nini? Mwenyewe anasema jina lake lingine la nyumbani ni MASISA.Hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. Kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.
C-SIR MADINI anatokea kule kule Tetemesha Recordz ambapo walitokea Hussein Machozi na baadaye Sajna wasanii ambao kwa upana wake,wanafanya vizuri.
Wimbo unaitwa Kifungo Huru.Ni single yake ya kwanza kutoka katika album ambayo bado ipo jikoni.Video ya wimbo huu ipo mbioni kutoka na imefanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
SONG’S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Every year after the end of the prominent East African Talent show one artist/contestant is afforded a chance of recording with a mogul record label B’Hits Music located in Tanzania. It happened last year with Alpha who recorded a song “Songa Mbele” which went on to be Nominated in various Awards as a foreign origin song. The song also was a big hit in Tanzanian where it was recorded and in Rwanda where Alpha comes from.
This time its Peter Msechu…Remember the character that wrote a seductive song for the same person that was judging his future, Judge Juliana?
Well this time he was thrown a chance to do it with B’Hits Music and it was on. Peter and B’Hits two producers Hermy B & Pancho managed to craft a soul capturing ballad that may make Ne-yo’s pleading sounds like the terminator crying…because it is sweeter than ever.
Peter got assistance from Bella a new RnB sensational in Tanzania and they made sure this song “UNANIUMIZA” becomes as vulnerable as the genre requires.
From here on out its B’Hits and Tusker project Fame to the end of Beautiful music and Talent.
CREDITS:
Song: Unaniumiza
Artist: Peter Msechu Ft Bella
Created and Composed by: Peter Msechu, Hermy B & Pancho Latino
Written By: Peter Msechu
Produced, Recorded, Engineered and Additional instruments By:
Pancho Latino & Hermy B At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Mixed and Mastered By: Hermy B At B’Hits Studio 1, Dar es Salaam.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Original message from B’Hits.Re-printed with permission

Kuna msemo wa Kiswahili usemao; Kimya Kingi Kina Mshindo Mkuu.Sina uhakika kwamba msemo huu una maana moja au la ila naamini kwamba unafanana na ule wa Ukiona Kobe Kainama,jua anatunga sheria! Leo napenda kuihusisha misemo hiyo na kitu ninachotaka kukuletea.
Baada ya kimya cha miaka takribani mitatu,Prof.Jay anarejea tena.
Wimbo unaitwa Kama Ipo(Kupanda na Kushuka).Tofauti na nyimbo nyingi za siku hizi ambazo hugusia sehemu moja tu ya maisha yetu binadamu,Prof.Jay katika wimbo huu anakumbusha,,kuburudisha na kuweka mambo mengi sawa katika suala zima la maisha ambayo kama ujuavyo,yana kupanda na kushuka.
Mtu aliyepo mitamboni katika kuutengeneza wimbo huu ni Producer Lamar kutoka Fishcrab Records ya jijini Dar-es-salaam.Keti chini,usikilize Kama Ipo…
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,jana mchana aliwaongoza viongozi mbalimbali wa serikali na maelfu ya wananchi katika mazishi ya aliyekuwa mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati,Sheikh Yahya Hussein aliyefariki juzi kutokana na maradhi ya moyo.
Mbali na Rais Kikwete,viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo Freeman Mbowe(Mwenyekiti-CHADEMA),John Cheyo(Mwenyekiti-UDP),Prof.Ibrahim Lipumba(Mwenyekiti-CUF) pia walihudhuria mazishi hayo yaliyofanyikia katika makaburi ya Tambaza jijini Dar-es-salaam. Kabla ya hapo dua ya kumuombea ilifanyika katika msikiti wa Manyema.Amefariki akiwa na umri wa miaka 79.Hizi hapa ni baadhi ya picha

Rais Kikwete akitia mchanga katika kaburi la Sheikh Yahya Hussein hapo jana.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa Sheikh Yahya Hussein tayari kwa mazishi.

Baadhi ya wanafunzi wa Sheikh Yahya Hussein wakishiriki katika shughuli nzima ya mazishi yake nyumbani kwake Magomeni Mikumi.

Makamu wa Rais,Dr.Gharib Bilal alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa serikali walioshiriki shughuli ya mazishi ya Sheikh Yahya.Pichani ni Dr.Gharib akimfariji mjane wa marehemu,Kate Yahya Hussein,nyumbani kwao Magomeni Mikumi jijini Dar-es-salaam.

Mnajimu maarufu Afrika Mashariki,Sheikh Yahya Hussein, amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar-es-salaam.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtoto wake, Hassan Yahya Hussein, Sheikh Yahya amefariki dunia nyumbani kwake Magomeni Mwembechai. Alikuwa akisumbuliwa maradhi ya moyo.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jioni hii,Sheikh Yahya anatarajia kuzikwa kesho mchana.
Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho ya Marehemu.


sending...
