Ni program ya kijamii ambayo inaenda hewani kupitia kituo cha STAR TV kila JUMAPILI saa 12:30 -1:00 jioni. Ni program mzuri sana ambayo inalenga kuburudisha, kuelimisha, kugusa hisia, pamoja na kugawa “vijisenti.”.Watch the part of the first episode below.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

This is how it all went down on the BET Awards 2011 Green Carpet.The carpet was actually green…no joke.It ain’t no more Red stuff..it’s green!

Alicia Keys

Drake

Nicki Minaj

read more

When US First Lady,Michelle Obama, with her daughters,Sasha and Malia met Nelson Mandela Madiba,former President of the Republic of South Africa.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ali Kiba pamoja na madansa wake alfajiri ya jana(Jumapili) wamenusurika vifo kufuatia kupata ajali ya gari katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro walipokuwa safarini kutokea Mbeya kuelekea jijini Dar-es-salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti la Nipashe ambazo BC imeweza kuzithibitisha kutoka kwa Ali Kiba mwenyewe,jumla ya watu saba wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya mkoa Morogoro.Ali Kiba ambaye aliumia mguuni na mkononi  tayari ameruhusiwa kutoka hospitali na amesharejea nyumbani kwake Dar ambapo ameieleza BC kwamba anaendelea vyema. Ali Kiba alikuwa awe miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyikia CCM Kirumba Mwanza hapo jana.

Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijawekwa wazi na polisi tayari wanachunguza.BC inawatakia wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo kupona haraka ili waweze kurejea katika kazi zao.

Endapo unapenda kujua mengi kiasi kuhusu muigizaji Steven Kanumba,sasa papo pahala ambapo unaweza kufanya hivyo kirahisi hata kutoka kwenye simu yako ya kiganjani.Anayo tovuti mpya ambayo kwa mujibu wake mwenyewe,imeboreshwa na kuwa ya kimataifa zaidi.Ni www.kanumba.com. Unaweza kuitembelea kwa kubonyeza hapa.

Naomba nimpongeze Kanumba kwa hatua hii.Natumaini wengine nao watafuata kwani katika ulimwengu wa leo tovuti ni suala muhimu sana katika kujitangaza na kuwasiliana na mashabiki na wanunuzi wa kazi za sanaa kirahisi zaidi.Caution: Hakikisha inakuwa updated mara kwa mara.

Professor Jay

Takribani mwezi mmoja uliopita, Professor Jay(The HeavyWeight MC) aliachia wimbo wake wa kwanza kutoka katika album yake mpya inayotarajiwa kuingia kitaani baadae mwaka huu.Bonyeza hapa kuisikiliza single hiyo kama bado hujafanya hivyo.

Baada ya hapo,na kama ilivyo ada,kilichokuwa kinafuata ni kutengeneza video ya wimbo huo ambao mpaka hivi sasa wapenzi wengi wa muziki wametokea kuupenda na kuukubali(kwanini usiupende?). You heard it,now you’ll have to see it!

Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika sehemu mbalimbali ilipotengenezwa video hii.BC sambamba na EATV na DTV ndivyo vyombo vya habari vilivyopata exclusive access katika location hizo. Video hiyo ambayo inatarajiwa kutoka ndani ya wiki hizi mbili,inatengenezwa na Visual Lab chini ya usimamizi wa Adam Juma(naomba nimuite Mzee wa Next Level).Kama ulivyo wimbo wenyewe,video inatarajiwa kuweka bayana jinsi gani maisha yanaweza kupanda na kushuka.Ukiwa huna hivi leo,usikate tamaa.Fanya kazi kwa bidii kwani kesho yaweza kuwa zamu yako ya kupanda.Na kama leo unazo,basi nenda taratibu ili hata utakaposhuka,isiwe kinoma noma.

When life gives you lemons,you gotta make lemonade!

Maisha mafungu saba…

Prof.Jay with Sheta

Let the work begin…Adam Juma behind the camera

Prof.Jay with people who makes it happen behind the scene.Brothers!

On set..Jay and Happy

On set before the shoot:I can see Chege,Jaffarai and Mwaipopo…

Prof.Jay and Prince Dully Sykes on set

MwanaFA with one of his amid fan and part of the crew,Ray Msangi.

read more

Anaitwa Hamis Mandi au ukipenda na kama anavyofahamika zaidi, B-Dozen au B12.Kituo chake cha kazi ni pale 88.4,Clouds FM. Ukiitazama picha unachokiona yawezekana ndicho au sicho. Alikuwa akifanya nini hapo?Kwanini mbele yake kuna boto kubwa kabisa ya kinywaji cha Serengeti? Bonyeza hapa kufahamau zaidi na kwa undani.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Unaowaona pichani ni baadhi ya waigizaji wa filamu nchini Tanzania.Kuna jina lingine ambalo wanapenda kulitumia wakiwa pamoja.Ni Bongo Movies Stars.Kwa ufupi waigizaji hao ni watu ambao wana umaarufu kwenye jamii.Kuna wengine wana umaarufu kupitia majina yao ya uigizaji kuliko hata majina yao halisi.Je,kwa kuwatazama hapo pichani unaweza kuwataja au ku-tag picha hii?

Pichani ni wiki iliyopita walipokwenda Dodoma kukutana na watunga sheria wa nchi hii.Aliyepo pichani katikati ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko,Dr.Cyril Chami na Mbunge wa Viti Maalumu,Vicky Kamata ambaye pia ni msanii/mwimbaji.

Picha:PMO Office

Lipo jambo ambalo kimsingi,mapromota wanahitaji kulifahamu;kuheshimu mikataba. Kinyume cha hilo,matokeo yake ni aibu kama  iliyojitokeza  juzi jumamosi pale katika Hotel ya Golden Tulip ambapo mwanamuziki maarufu barani Afrika,Hugh Masekela kutoka Afrika Kusini alipogoma kupanda jukwaani kutokana na ukiukwaji wa sehemu muhimu ya mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Abdallah Singano,Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano cha Stanbic Bank ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa tukio hilo, Hugh Masekela aligoma kupanda jukwaani baada ya promota wa show hiyo,Heri Bomani kupitia kampuni yake ya Full Circle Africa Limited kushindwa kumlipa msanii huyo kitu ambacho bila shaka ni ukiukwaji wa kipengele muhimu cha mkataba!

Akiongea na waandishi wa habari jana katika hotel ya Southern Sun,Abdallah Singano amesema wao kama wadhamini wamesikitishwa sana na kitu kilichotokea na wanapanga kuwachukulia hatua za kisheria mwandaaji na kampuni yake.Pia amewataka wote ambao walikuwa wamenunua tiketi za onyesho hilo kumtafuta mwandaaji ili awarejeshee fedha zao.

The show that never was!

Kwa upande mwingine,Sauda Simba,alifanikiwa kutuliza japo kidogo roho za wapenzi wa muziki waliohudhuria kwa onyesho safi kitu ambacho kinazidi kumweka Sauda pazuri hususani miongoni mwa wapenzi wa Jazz.Good job Sauda!

Sauda Simba performing.Photo by Issa Michuzi

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page