Je,unaweza kuotea hawa ni kina nani? Dokezo: Ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya.Ukishindwa kuwatambua bonyeza “More” kupata jibu.

??

read more

BC inapenda kuchukua nafasi hii kukutakia mfungo mwema wa Ramadhan wewe,ndugu,jamaa na marafiki zako wote.Tuendelee kupendana,kuheshimiana na kujaliana katika wakati wote huu wa mwezi mtukufu na hata pale utakapomalizika.Asante na Mwenyezi Mungu azidi kukubariki.

Leo nipo katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Kinachotokea hapa ni kitu ambacho nimeona nikiite Serengeti Fiesta 2011 Finale kwani ule msimu wa raha,ule msimu wa Fiesta Serengeti kwa mwaka huu wa 2011 ndio unafikia ukingoni.Hiyo ni baada ya ziara ndefu ya mikoani kama vile kule Mwanza,Tanga,Morogoro,Iringa,Mbeya(kule Mheshimiwa Sugu alitaka kuweka kizingiti,kikafeli)

Jambo la kwanza ambalo sina budi kukwambia ni kwamba Leaders Club is packed.Vijana wamejitokeza haswa! Huo ni upande wa mashabiki.Kwa upande wa wasanii,nimebahatika kuwaona(backstage) takribani kila msanii mwenye jina na ambaye anatambulika kwako kirahisi japo kupitia ala au miziki yake.Of course bado sijamuona nyota wa mchezo wa leo ambaye ni msanii Ludacris kutokea nchini Marekani. Bila shaka hiyo ni kutokana na ukweli kwamba ataletwa baadaye kidogo kukamua na pengine kufunga show.

Pamoja na watu kuwa wengi,kuna ulinzi wa kutosha kabisa.Vijana wanaoitwa Ninjas wapo wa kumwaga.Wametapakaa kila kona.Muda mfupi uliopita nilienda maliwatoni nikakuta jamaa wametuna nje wanahakikisha kuna ulinzi wa uhakika.Hii ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria Finale ya Fiesta. Kwa maana hiyo sio mbaya kama nitaweka wazi baadhi ya mambo yaliyonivutia.Kwanza ni stage.Stage imetengenezwa vizuri na imekaa katika mazingira safi kabisa ambayo yanamwezesha yeyote…yaani mfupi au mrefu kuona vizuri kinachoendelea.

Kule pembezoni mwa viwanja hivi vya Leaders, watu wa msalaba mwekundu ambao wapo tayari kabisa kuokoa maisha ya mtu endapo lolote linaloweza kuhatarisha maisha linaweza kutokea.Yawezekana mtu akazidiwa na “maji” aka pombe ikawa tabu.Bila shaka unajua kwamba unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako. Ninapoandika bado sijapata nafasi ya kuutathmini utaratibu wa kununua vinywaji.Pamoja na hayo,kupitia  matangazo niliyoyaona nje na ndani ya hapa tulipo,msisitizo ulikuwa kwamba pombe haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.This is good.Pombe ina umri wake pia.Ule umri wa kuweza kufanya maamuzi sahihi.

Mpaka sasa wasanii mbalimbali wameshapanda jukwaani. Kuna baadhi ya undergrounds na wengine ambao pamoja na kuwa undergrounds hivi sasa washaanza kupaa. Mfano ni dogo aliyemwambia Ridhiwani amwambie mshua kwamba street kishanuka...si unamjua? Leo ana msemo wake ambao unachengua watu..anasema zomea TANESCO…na mashabiki wanazomea kweli kweli.Well…wana haki…nchi imekuwa gizani kwa muda wa kutosha sasa jamani.

read more

Duh!Jamaa hamuogopi huyo nyoka?Hii ilikuwa wapi?Bonyeza hapa kujua zaidi.

Baada ya kumwania mara mbili bila mafanikio, hatimaye Shirikisho la Soka nchini Marekani hapo jana limefanikiwa kumuajiri aliyewahi kuwa nyota wa soka wa Ujerumani na ulimwenguni, Juergen Klinsmann, kuwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya taifa hilo ili kuisuka upya timu hiyo.

Klinsmann ndiye aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyoishia katika nafasi ya tatu katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006. Tofauti na Steve Sampson, Bruce Arena na Bob Bradley, watangulizi wake wa karibu, alikuwa mchezaji wa kimataifa wa timu ya taifa ya Ujerumani.

Yeye aliajiriwa siku chache baada ya Bradley kutimuliwa.Mechi yake ya kwanza akiwa kocha wa Marekani dhidi ya Mexico katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa tarehe 10 August huko Philadelphia.

Katika taarifa aliyoitoa hapo jana, Klinsman amesema anayo furaha na heshima kubwa ya kukabidhiwa dhamana ya kuinoa timu hiyo hususani inapoanza mchakato wa kujiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zitakazofanyikia nchini Brazil. Klinsmann, ambaye leo Jumamosi anatimiza miaka 47,anaishi na familia yake huko Kusini mwa California.

Ludacris akiongea na waandishi wa habari.

Msanii Ludacris kutoka nchini Marekani na ambaye anasubiriwa kwa hamu kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki hususani wa Hip Hop/Rap,asubuhi hii ameweka wazi mbele ya waandishi wa habari kwamba yupo tayari kabisa kuwapa mashabiki hao burudani ya kipekee na ya aina yake wakati atakapopanda jukwaani hapo kesho katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar-es-salaaam.

Ludacris ambaye alizaliwa huko Champaign,Illinois 11  mwezi September mwaka 1977 ameweka wazi kwamba anazo nyimbo za kutosha kabisa ili kuwapagaisha wapenzi wa muziki.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyikia katika hotel ya Kempinsk Kilimanjaro jijini Dar,Ludacris alionekana mchangamfu na mtu anayejiamini kabisa kwa kitu anachotarajia kufanya hapo kesho. Kazi kwako mpenzi wa muziki.

Mwanamuziki Ludacris (wa pili kutoka kulia) akiwa katika mkutano huo na waandishi mbalimbali.Kulia ni Mkurugenzi wa Clouds FM na PrimeTime Promotions ambao ndio wanaoratibu ujio huu wa Ludacris chini ya udhamini wa Serengeti Premium Lager.Kushoto ni Caroline Ndungu, Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers anayemaliza muda wake  na Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Allan Chonjo.

Kutoka kulia,Ruge Mutahaba kutoka PrimeTime Promotions/Clouds Media Group,Mwanamuziki/Muigizaji Ludacris kutoka Marekani na Allan Chonjo,Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa Fiesta 2011

Photos Courtesy of MichuziJR

Kama tulivyoripoti mapema,mwanamuziki Ludacris ametua mchana huu tayari kabisa kwa Fiesta Serengeti.Hizi hapa chini ni baadhi ya picha tangu kuwasili kwa msanii huyo.Picha zote kwa hisani kubwa ya Ahmad Michuzi toka Jiachie.

Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip Hop,ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Brian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(JKNIA) na kupokelewa na wenyeji wake.

Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini, Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Fiesta 2011, Serengeti Premium Lager

Mwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk Kilimanjaro jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onyesho lake moja ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar.

Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar.

Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Clouds TV jioni ya leo.

Mwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akiwafafanulia jambo wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya leo akitokea nchini Marekani.


From left,Miss Universe Albania 2010,Donald Trump who owns Miss Universe Beauty Pageant,and our Flaviana Matata,Miss Universe Tanzania 2007

For more photos and news on this please visit Miss Jestina George blog by clicking here.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page