KANUMBA VS KIGOSI:NANI ZAIDI?

Ingawa historia ya filamu za kitanzania au Kiswahili ina historia ndefu(tangu enzi za kina Yombayomba,Chale Mwembamba na Mnene,Maangamizi nk),hakuna ubishi kwamba unapoongelea masuala ya sanaa hiyo hivi sasa,ni vigumu kuwaweka kapuni vijana wawili;Steven Kanumba na Ray Kigosi(kama wanavyoonekana hapo juu pichani).Kwa sababu mbalimbali,zikiwemo wingi wa filamu walizocheza na kuongoza(hili bado halinipi amani ya kweli),ndizo zinazowaweka mbele ya wenzao.

Mbaya au zuri ni kwamba Kanumba na Kigosi ni marafiki.Wenyewe wanapenda kutumia neno “swahiba” wanapotajana iwe ni hadharani au katika blog zao(Ya Kanumba hii hapa na ya Kigosi hii hapa).Pamoja na urafiki walionao,ninavyojua mimi Ray na Kanumba ni washindani. Wamewahi wenyewe kuongelea suala na “kufunikana” kama filamu.Kwamba mimi ni zaidi ya wewe na mambo kama hayo.

Hilo ndilo linalonifanya leo nikuletee wewe msomaji (natumaini u-mpenzi wa filamu za kitanzania[bongo films/movies]) nafasi ya kuwa jaji.Kwa mtizamo wako na kwa jinsi ambavyo umekuwa ukifuatilia filamu au uigizaji wa Steven Kanumba na Ray Kigosi nani unadhani ni zaidi ya mwenzake? Na je unaweza kusema ni kwanini unadhani huyo unayesema ni zaidi ni zaidi ya mwenzake?Una ushauri gani kwake au kwao?

 1. jimmy, 21 July, 2012

  kanumba z da great……but ray z da greatest,ray ndo kamfundsha kanumba kuact……….RAY YO DA BEST.

 2. jimmy, 21 July, 2012

  yeah…….acha amuandae mwingie.

 3. andy lee, 25 August, 2012

  Tnese guys are good at what they do, why lie. Ray is obviously talentd as a producer while Kanumba was talentd as an actor.

  Thus as to who is better than the other, your guess is as good as mine.

 4. idrissa, 19 October, 2012

  Wotew kabisa wanafa lakina kigosi djowamana sababu yuko uhayi

 5. Banny Mlengwa, 02 November, 2012

  NIMEAMINI KWAMBA NABII HANA HESHIMA KWAO ILA UGENINI. HATA SIKU MOJA USIJE UKAMLINGANISHE S.KANUMBA NA V.KIGOSI. NA SIDHANI KAMA WA TANZANIA MTAWAHI KUMPATA MSANII WA FILAMU KAMA S. KANUMBA. LABDA BAADA YA MIAKA 100. MIMI NI MKONGO, NAISHI CALIFORNIA/ USA. TULIMPENDA SANA S. KANUMBA.

 6. Charles da Valencia, 29 November, 2012

  Kanumba ndo msanii aliyenifanya niwe natazama bongo movies,kwa kweli alikuwa anajua kuact,chezea devils kingdom wewe.r.i.p kaka.

 7. muro king, 20 December, 2012

  kanumba ndio raisi wa bongo movies

 8. Aliasu Mlengwa, 20 December, 2012

  Huyo v.kigosi, tangu anzekuigiza, hajawai hatasiku moja kuashirikisha wasani wa inje ya inchi. Ila tulimshuhudia S.kanumba akishirikiana na wasani waki Nigeria, hata huko Ghana alifika akiwa pamoja na Dada MONALISA. na ndio ilimfanya S.kanumba awe msanii bora na mwenye uwezo mkubwa kuliko wengine wote hapo kwenu Tanzania. sisi wa DRC(congo), tulimkubali Kanumba.

 9. Amadi lyama, 16 January, 2013

  Jamani tuache ushabiki wa kukurupuka,ukweli ni kwamba vincent kigos nimkali sana,angali oprah,joharg,offside nazingine yeye ndiye aliyekuwa director,pili anajuwa kuvaa,kanumba alifunzwa na ray.tazama picha zao zilizo watowa,kanumba alikuwa choka mbaya,chunusi,vichati virefu.lakini ray anafahamu kuvaha.kanumba alizaraulisha wanaume wote alipo vaha jinzi na suti.ray usijali kaza buti uliyo mfanyiya kanumba kwaku mwinuwa leao watu wanalinganisha mwalimu na mwanafunzi.ray ni mwalimu

 10. justinah, 25 February, 2013

  napendezwa sana na michezo ya vin na steph waendelee vovyo hivyo ur the best of all actors

 11. DERICK, 02 March, 2013

  Kanumba alikuwa juuu sana uyo ray tume mjua uku DRcongo kupitiya kanumba na anakubaliwa sana uku congo nasiyo tu congo mu east africa yote ina mukubali banumba alikuwa baba wa film ya tanz na tangu afariki film za bongo zime pita nazimika atuzioni tena zime enda wapi?

 12. Francine, 03 March, 2013

  Tuna mukumbuka sana acter wetu kanumba r.i.p ndiye aliye weka bongo movies ju nasiyo mwengine ila mujuwe kama mwanafunzi anakujaka kumpita mwalimu ndivyo kanumba alivyo fanya tangu afariki tume baki na upweke mwingi wa bongo movies uku RWANDA HOOO kanumba ume enda wapi?

 13. Ramadhan, 14 March, 2013

  Wote wapo juu ila The late Kanumba The Great alikuwa anatambulika kimataifa zaidi kuliko Ray bt wote wako kuu coz Kanumba kafariki Ray kaza msuli

 14. NICK, 22 June, 2013

  mwanzo mwisho KANUMBA

 15. jeanbush, 17 September, 2013

  kanumba ume enda wapi kaka yangu mbona unatuima rah ndugu yangu tuna ku miss sana kaka yangu njo basi utowe basi japo filamu moja tu tukuone yamara mwisho

 16. clackbyluz nyembwe, 04 July, 2014

  mimi na penda mu ni tuminiye ba videa ya filme ya tanzania ni na yi pendaka sana

 17. clackbyluz nyembwe, 04 July, 2014

  nina pendaka kabila ya swahili sana

 18. clackbyluz nyembwe, 04 July, 2014

  ba film ya afrika iko nzuri sana ku pita ya bulayi

 19. clackbyluz nyembwe, 04 July, 2014

  dunia iko na mambo ya mingi bashi bantu nzo beku mubaya fazi yote bantu ba zuri banakalaka ba mubaya aba psake

 20. Tobias nombo, 02 February, 2015

  Kenya ndo dunia? Hapa zambia wanamjua tu ray. Ubishi unaweza ukawa ukwel kama upande wa pili wanadanganya. Mzuri zaidi anapikwa na ataonekana tu.

 21. Nurayn, 04 August, 2015

  RIP “THE GREAT KANUMBA”. Ila kwa kweli kwa mtazamo wangu RAY alikuwa na yuko juu kwa sasa.Hii ni kwa sababu ya ustadi wa kuzidhihiri hisia halisi katika matukio sahihi kwenye filamu zake. Marehemu Kanumba alikuwa mzuri kuigiza pia lakini kwa kiwango cha chini kidogo kulinganisha na sifa hizo za Ray. Shukran.

Copyright © Bongo Celebrity