
Here come the collaboration of Young Jeezy and the recent released from jail Rap/Hip Hop King,T.I
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pichani ni mwigizaji maarufu wa filamu.Ni mume wa…..Je unaweza kumtambua?Movie zake zipi ambazo unazikumbuka zaidi au ulizipenda zaidi?

Huyo bwana anaitwa SUNDAY RAMADHANI MANARA aka ‘Computer’ aliyezaliwa miaka 54 iliyopita mjini Kigoma mahali ambapo palikuja kuwa chimbuko la wachezaji wengi nyota kama akina Hamis Askari, Aloo Mwitu, Athuman Juma, Juma Kampala, Abeid Mziba, Makumbi Juma na wengineo.
Mkongwe huyo, ambaye ndugu zake wawili nao walikuwa wanapiga soka yaani Kitwana Manara kaka yake na mdogo wake Kasimu Manara kwa sasa anapatikana maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
MAISHA YA UTOTONI KATIKA SOKA
Sunday anakumbuka maisha yake ya utotoni alianza kuchezea Young Kinya ambayo ilikuwa kama timu ya watoto wa Yanga ingawa ilikuwa kama inajitegemea zaidi na ilikuwa inafanya mazoezi nje ya viwanja vya Kaunda na ilikuwa ukitoka pale unasogea kidogo unakwenda Afrikan Boys ambayo ilikuwa ni timu ya pili ya Yanga na mwanzoni mwa miaka ya 1970 Sunday na wenzie akina Awadhi Kessy, Douglas, Shabaan Ufunguo, Mohamedy Ugando walipandishwa kuichezea Yanga ya wakubwa chini ya kocha Profesa Victor Stanculescu na huko waliwakuta kina Elias Michael, Mohammed Msomali, Hassan Goboss, Boi Iddy, Athuman Kilambo, Maulidi Dilunga, Badi Salehe, Leonard Chitete na wengineo.
MALEZI YAKE KWA STANCULESCU
Sunday, ambaye binafsi anakiri kuwa hajui jina la mashine hiyo yenye kufanya kazi vizuri alipewa na nani zaidi ya kukumbuka tu ni mwaka 1975 alipotoka Zanzibar baada ya kuwapiga Simba mabao 2-0 ila anakubali kuwa maisha waliyokuwa wanalelewa na Mzungu huyo yalimfanya aipende sana Yanga kuliko timu nyingine yeyote ikiwamo Taifa Stars, ambayo walikuwa wachezaji takribani saba, ambao ni kipa Elia Michael, Athuman Kilambo, Hassan Gobboss, Abdulhaman Juma, Kitwana Manara, Gibson Sembuli na yeye mwenyewe.
Ushirikiano ulikuwa mkubwa na ulisababisha kuwa mara zote ni furaha tupu ndani ya mitaa ile ya Jangwani hadi mwaka 1973 ambapo Simba ilifuta uteja kwa kuwafunga bao 1-0 lililowekwa kimiani na nahodha wa Simba wakati huo, Haidar Abeid Muchacho
Kama ulizaliwa miaka ileee niliyozaliwa mimi,unaweza kukumbuka jinsi ilivyokuwa pindi unapomzimia mtu(mara nyingi ni pale mvulana anapomzimia msichana,usiniulize how come).Bila shaka unakumbuka enzi za barua za mapenzi,yes zile zilizokuwa na mwanzo wa Mpendwa nanii,natumaini hujambo.Utakapo kujua hali yangu....Zile enzi za kumtuma mdogo wako akampelekee salamu au kijibarua binti fulani wa mtaani.Enzi za kukutana chemba na kisha “manzi” kuanza kuchimba vishimo kwenye udongo kwa kutumia dole gumba huku akimaliza majani ya maua au miti iliyopo pembeni kwa kujaa “soni”.
Enzi zile maneno hayakuwa mengi.Ukimpenda mwenzio kulikuwa na maneno machache tu kama vile Nakupenda au ili kuonekana umeenda shule kidogo bado unatia I love you huku midomo ikikutetemeka kwa sababu hujui jibu litakalotoka! Kama maneno Nakupenda na I love you huyawezi basi kulikuwa na neno NAKUTAKA.Kidogo lilikuwa harsh lakini ndilo lilikuwa rahisi kupita mengine.
Nimekupa stori za kale kidogo hapo kwa sababu wimbo mpya kutoka kwa msanii Kigwema(pichani) ndio umenikumbusha enzi hizo.Wimbo wake ambao amewashirikisha wasanii Barnaba(THT) na Nyasi,unazo hisia za namna hiyo.Wimbo unaitwa NATAKA.Kwanini unantaka?Nataka kwa sababu hii na ile.Zimewekwa wazi katika wimbo huu ambao naamini siku chache zijazo utasambaa vilivyo katika masikio ya wasikilizaji.
Wimbo umefanywa katika studio za Mpo Africa chini ya Producer Benn Mwamba.Usikilize hapo chini
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Amaya ni Beauty Salon & Spa mpya na ya kisasa kabisa iliyopo katikati ya Jiji la Dar-es-salaam.Ipo nyuma ya jengo la Air Tanzania Corporation(ATC) lililopo katika makutano ya barabara za Ohio Street na Garden Avenue.Amaya Beauty Salon & Spa inajivunia kuwa Beauty Salon & Spa inayotumia bidhaa halisi(original) kutoka Canada na USA huku ikiwa na wafanyakazi waliobobea katika masuala yote yanayohusu urembo kutokea ndani mpaka nje na wenye ujuzi wa kimataifa.
Miongoni mwa huduma zinazopatikana ndani ya Amaya Beauty Salon & Spa ni pamoja na;
- Huduma za nywele kwa aina zote za nywele kuanzia kunyoa au kukata style mbalimbali, kusuka,kuweka dawa,ku-steam, kuchana style mbalimbali,kushonea weaving aina zote,kubandika lace wigs,relaxing,kubandika kope,ku-bond nywele,kuweka aina zote za rangi kwenye nywele, kusokota dreads,kutinda nyusi kwa uzi,twisser na wembe, etc
- Huduma maalumu(specialized treatments) kwa ajili ya mikono na miguu(Manicure and Pedicure) ikiwemo kuosha miguu kwa kutumia mask na paraffin, kuosha mikono,kupaka rangi,kubandika kucha aina zote za rangi mbalimbali/tips,acrylic powder na gel.
- Tunafanya facial za aina tofauti tofauti ikiwemo kutoa chunusi,madoa ya uso nk
- Pia tunafanya waxing
- Tunapamba maharusi,send off,kitchen party na special days kama vile graduation,ubatizo,kipaimara nk
- Tunauza products mbalimbali kama vile Designers Perfumes kutoka kwa Usher,J-Lo,DKNY etc.Avon Products kama vile Powders,Colognes,body creams,shower gels nk.Make-Up products za Mac kama vile Studio Fix,Powders & Foundations,Eye Shadow,Lipsticks/gloss,perfumes nk
- Pia tunatoa huduma zote zilizotajwa hapo juu katika vyumba maalumu(Private Rooms) na kwa kutumia products maalumu.

Baadhi ya wafanyakazi wa Amaya Beauty Salon & Spa
Amaya Beauty Salon & Spa inayo sehemu kubwa ya maegesho ya magari(Parking) yenye ulinzi wa uhakika.Ipo wazi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi(6am) mpaka saa moja jioni(7pm) Jumatatu mpaka Jumamosi.
Kwa mawasiliano zaidi tumia simu; 0716 604495, 0684 262924 na 0753 262 924
Hivi karibuni Rais wa Marekani,Barack Obama,aliongea na Congressional Black Caucus Foundation.Aliwaambia mambo ambayo naamini tunaweza kuyasikiliza na kuyapa uzito hata sie tusio Wamarekani Weusi bali sisi tunaokumbana na kero zetu(nizitaje?).Mtizame hapo juu

Katika tuzo za muziki za Kilimanjaro(Kilimanjaro Music Awards) mwaka huu, alijinyakulia tuzo tano kwa mpigo na hivyo kuweka historia ya aina yake katika muziki wa kizazi kipya na kwa uhakika tuzo hizo.
Kilichofurahisha zaidi wananchi na hususani wapenzi wa muziki ni kwamba 20 Percent alistahili tuzo hizo kutokana na kuwa na albamu yenye mantiki na utamu halisi wa muziki.Inasemekana kwamba albamu ya Ya Nini Malumbano huenda ndio albamu iliyouzwa zaidi nchini Tanzania kwani hata kabla ya kumpatia tuzo hizo,ilikuwa ikienda kama njugu.
Kama nilivyodokezea hapo juu,kilichokuwa kinaiuza albamu hiyo ni nyimbo kali zenye ujumbe mkali na hivyo kuchukua jukumu la sanaa la kuelimisha,kuburudisha,kuonya,kushawishi,kusifia nk.Binafsi ninaisikiliza mara kwa mara album hii.
Akiendeleza kilichompa tuzo tano za Kili,20 Percent ameachia wimbo mwingine kutoka kwenye album hiyo hiyo ya Ya Nini Malumbano.Wimbo huu ambao uko katika mahadhi ya Reggae unaitwa Si Mfano. Ni production nyingine kutoka Combination Sound.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Pindi tu alipotwaa tuzo zake tano za Kili,nilifanikiwa kufanya mahojiano na 20 Percent.Kama hukuwahi kuyasoma,basi unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa.Mahojiano hayo yalikuja kutumiwa pia na Jarida maarufu la Kitangoma.

Kuna wakati napenda kuwaza(sio mara zote,naomba nikiri).Ninapowaza na kushindwa kupata majibu,sina budi kushirikisha wenzangu.Mara nyingi kimbilio langu huwa ni wewe msomaji.Nathamini mchango wako na naheshimu thamani ya ubongo wako.Nakukubali.Leo nimewaza na kushindwa kupata majibu.Hivi nini chanzo cha majina haya ya mitaa na sehemu mbalimbali za jiji la Dar-es-salaam?Unajua?Unamjua anayejua?Kwanini leo tusitumie muda wetu kujuzana?Eti nini chanzo cha majina haya?Asili yake nini?Mfano;
- Kariakoo
- Magomeni
- Msasani
- Upanga
- Kunduchi
- Buguruni
- Vingunguti
- Tabata
- Mikocheni
- Mbezi
- Kimara
- Tegeta
- Boko
- Kigamboni
- Masaki
- Oysterbay
- Na mengineyo mengi….

Hii imetokea huko Igunga.Mbunge wa Tabora Mjini,Ismail Rage akipanda jukwaani kuomba kura.Unakiona alichonacho kiunoni?
Naamini kwamba unatambua kwamba nchi ya Libya hivi sasa ina kiongozi mpya katika serikali ya mpito.Anaitwa Mustafa Abdel-Jalil.Kiongozi huyo ambaye ameshika usukani wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika baada ya kumng’oa madarakati Kanali Muamar Gaddafi,naye yupo nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa UN na ametumia muda huo kukutana na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete.Hizi hapa baadhi ya picha wakati viongozi hao walipokutana.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya Bw.Mustafa Abdel Jalil

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo mafupi na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya,Bw.Mustafa Abdel-Jalil jijini New York nchini Marekani.Viongozi hao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa 66 wa Umoja wa Mataifa jijini New York

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Balozi wa Tanzania wa kudumu katika Umoja wa Mataifa,H.E Ombeni Sefue kwa Kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya,Bw.Mustafa Abdel-Jalil.


sending...

