UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

29 Novemba, 2011

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Shaaban Robert

Mchana wa leo nilikuwa na majadiliano na kijana mmoja mdogo ambaye yungali shuleni akitafuta elimu na maarifa.Katika mazungumzo yetu,ilitokea akaniuliza kama nimeshawahi kuona picha ya Shaaban Robert yule mtunzi na mwandishi aliyetukuka.Aliniuliza swali hilo kwa sababu yeye anasema,japokuwa anapenda sana mashairi na utunzi wa Hayati Shaaban Robert, hajabahatika kuona picha ya gwiji huyo!

Kwa faida yake(nilimuahidi kumwekea picha hii) na wengineo wengi bila shaka,hiyo hapo juu ni taswira ya Marehemu Shaaban Robert.Unaweza kupata historia yake kwa ufupi kupitia ukurasa huu wa Wikipedia.

Msanii Fareed Kubanda al maarufu kama Fid Q anacho kipindi cha kwenye luninga ambacho mimi binafsi hukipenda sana.Ni ajabu ya kweli kwamba so far sijawahi kuandika chochote kuhusu CheusiDawa TV ambalo ndio jina la kipindi au Luninga hiyo.

Ni wiki ya 14 sasa na Fid Q katika wiki iliyoisha majuzi,alikutana na Hasan Salaam mkazi wa New Jersey nchini Marekani.Ukitaka kujua mengi kuhusu Hasan Salaam basi bonyeza hapa.Lakini ukitaka njia mkato na kwenda moja kwa moja kwenye CheusiDawa TV na Hassan Salaam,basi tizama kipindi hicho hapo chini

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo tarehe 27 Novemba 2011,amekutana na viongozi wa chama kikuu cha upinzani,CHADEMA,Ikulu jijini Dar-es-salaam ili kuzungumza nao juu ya musuada uliopitishwa hivi karibuni Bungeni kuhusu sheria ya kuundwa kwa tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama utakumbuka wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) walisusia upitishwaji wa musuada huo mjini Dodoma.Hii hapa ni SLIDESHOW ya picha mbalimbali kutoka katika mkutano huo ambao bado haijawekwa wazi juu ya yale yaliyoamuliwa.Lakini kutokana na muonekano wa picha tu,yaelekea ulikuwa mkutano mzuri!

Picha zote na Ikulu.Ukitaka kuiona picha katika ukubwa wake,bonyeza juu yake.



Pichani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimshudia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , akinywa kinywa cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa  na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa, wakati wa  uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam juzi tarehe Novemba 25.
Kinachofanyika katika picha hiyo sio kitu kibaya.Ni ishara nzuri ya kuendeleza mila,desturi na tamaduni.Lakini kuna kitu ambacho hakipo sawa sawia katika picha hiyo hususani katika karne hii.Je,unaona ninachokiona?What’s wrong with this photo?

Miezi kadhaa nyuma niliwahi kuuliza swali kuhusu nani aliye zaidi katika ya Steven Kanumba na Ray Kigosi.Mashabiki na wafuatiliaji wa Bongo Movies mkatoa ushirikiano mkubwa na kueleza bayana yule ambaye mnadhani ni zaidi ya mwenzake.Mpaka leo hii bado comments kuhusu hoja ile bado zinaendelea.Hiyo,kwa upande mwingine,inaonyesha ni kwa jinsi gani watu zaidi wanafuatilia sanaa ya filamu nchini Tanzania.Ni jambo zuri.

Leo naomba tuhamie kidogo upande wa waigizaji wa kike kwani ni wazi kabisa na wao wanafanya vizuri sana katika kuendeleza fani hii ambayo kwa miongo kadhaa ilipewa kisogo.Mchango wao ni dhahiri.Hapa naomba niwaweke “kikaangoni” Monalisa (Yvonne Cherryl) na Blandina Chagula maarufu kama Johari. Bila shaka umeshawahi kuwaona katika uigizaji wa aina mbalimbali.Endapo ungekuwa na filamu yako na ukawa unatafuta mwigizaji wa kike(lead actress) ungemchagua nani katika ya Monalisa au Johari.Kwa ufupi unadhani nani zaidi kati yao?Kwanini?

Johari

Kutoka pande za Temeke,Wanaume TMK wanaingiza karata yao.Wimbo unaitwa “Kichwa Kinauma“. Umetengenezwa pale Masaki kwa MJ Records chini ya Producer Marco Chali(Doctor Chali).

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Sina uhakika unaisomea wapi habari hii lakini nahisi unaisomea ukiwa katika mitkasi yako ya kila siku iwe ni kazini au katika sehemu zinginezo za kutafutia riziki.Kwa ufupi unafanya kitu! Lakini je,umeshawahi kuketi chini na kujiuliza kwa undani kabisa kwamba kwanini unafanya unachokifanya? Nini kinakusukuma kufanya hivyo?Unapohisi kukata tamaa na kitu unachokifanya,kwanini unaendelea?

Maudhui kama hayo hapo juu ndio yaliyomo katika wimbo mpya wa Mike Tee(Mnyalu) ambao amemshirikisha Fareed Kubanda au ukipenda Fid Q. Wimbo unazungumzia zaidi sanaa ya muziki.Ni wangapi wanafanya muziki kwa sababu wanapenda au wengi wanafanya kwa “Sababu Ya Njaa”?Msikilize kwa makini Mike Tee hapa.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Photo Courtesy:Get Mziki

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page