Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA, John Mnyika ametolewa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa kile kilichodaiwa kushindwa kufuta kauli yake ya kumuita Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni mtu dhaifu. Kufuatia tukio hilo Mheshimiwa Mnyika anasema msimamo wake ni huu hapa chini;

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

 

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

 

Be Sociable, Share!

Feedback / Comments

5 Responses to “MSIMAMO WA JOHN MNYIKA HUU HAPA”

 1. Comment by Junior Martins on June 19th, 2012 2:25 pm

  Namsapoti John Mnyika 100%, Rais wetu amekuwa bubu kwenye masuala mengi na kulaumu mabadiliko na matatizo yote ya nchi kwa watu wengine. Pia ameshailaumu mvua na mungu kwa kutokewepo mvua ili Tanzania iwe na umeme. Huyu ni Rais dhaifu na nadhani ofisi ya uraisi haiwezi. Ni kweli, katika maraisi wote ni huyu ni dhaifu kama Mnyika alivyosema. Hongera Mnyika kwa kuongea ukweli ndio maana umetolewa nje kwa sababu wazungu wanasema una “GUTS” ujasiri wa kusema ukweli.

 2. Comment by neltress on June 21st, 2012 5:48 am

  ongera mnyika kwa kutoa pointi

 3. Comment by Rhino khery on June 21st, 2012 7:30 am

  Mbali na hilo JK hata washauli wake wanachangia ndomana anakosa msimamo.

 4. Comment by kefa on June 21st, 2012 7:34 am

  sijui kwanini watu hawapendi kusikia ukweli…hivi kama leo naibu spika akiambiwa aseme uimara wa raisi wetu,sijui atasema kitu gani..yani huyu raisi is one of the Very weak presidents i have ever heared…hawezi hata kuto matamko mepesi kuhusu nchi..kifupi sioni kazi yake kama raisi,anabaki kupiga trip tu kila siku…am feedup sitaki kusikia jina lake.

 5. Comment by noelminja on June 16th, 2013 10:15 am

  mimi sipendi selekali kuto tambua mungu, kwa nini serekali hainadini?

Leave a Reply