IRENE UWOYA Vs JACQUELINE WOLPER:NANI ZAIDI?

Irene Uwoya na Jacqueline Wolper wote ni waigizaji katika Bongo Movies. Na kusema ukweli,kila mmoja ana mvuto wake ndani na nje ya uigizaji. Pamoja na wote kufanya kitu kimoja yaani uigizaji filamu,yasemekana hawaivi.Huwezi kuwaweka katika chungu kimoja.

Mbaya zaidi inasemekana kwamba kila mmoja anamuona mwenzake mbabaishaji linapokuja suala la kuigiza.Irene anasema Jacqueline hana kipaji.Jacqueline naye anasema hivyo hivyo. Wote wamewahi kukaririwa wakisema mwenzake hana kipaji wala uwezo wa kuwa naye katika filamu moja.Sijui kuna ukweli gani katika hili na kama ni kweli hawajawahi kabisa kuigiza katika filamu moja.

Lakini wakati wao wakibishana,yupo mtu ambaye anaweza kuwa mwamuzi mzuri zaidi.Wewe msomaji na mtizamaji wa Bongo Movies zikiwemo zile ambazo wawili hawa wameigiza.Unadhani nani Zaidi?

  1. Mimaah, 19 October, 2015

    h

Copyright © Bongo Celebrity