Kwa miaka kadhaa kituo cha Tanzania House of Talent kimejizolea sifa ya kuibua baadhi ya wasanii ambao hii leo wanafanya vizuri katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini mwetu.Hapa nawazungumzia wasanii kama vile Barnaba,Ditto,Linah,Recho nk
Lakini pia ni ukweli kwamba kwa muda sasa ni kama vile wamekuwa kimya na kuendeleza zaidi wale ambao wameshatoka. Pamoja na hayo,nyuma ya pazia,ukweli ni kwamba wamekuwa wakijaribu na kuwatoa wengine.Mfano mzuri ni msanii huyu anayekwenda kwa jina Vumilia au Vumi ambaye kwa wafuatiliaji wa masuala ya muziki na Tanzania wataweza kukumbuka kwamba alishatoka na wimbo Utanikumbuka. Sasa hapa anakuja na wimbo Dushe Dushe ambao licha ya kwamba umerekodiwa pale pale THT bali pia umeandikwa na one of THT’s own,Lameck Ditto.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Feedback / Comments
Leave a Reply




sending...
