Kuna mtu mmoja aliwahi kuweka wazi kwamba jambo moja zuri kuhusu maisha ni kwamba hakuna kitu ambacho siku zote hubakia kama kilivyo(nothing stays the same). Kuna mabadiliko kibao.Kuna kupanda na kuna kushuka.Ulipo leo hapana maana sana kwani kesho unaweza kuwa juu au kama leo upo juu basi usishangae keshokutwa ukawa chini. Hali hiyo,ya kupanda au kushuka inapotokea,usijilaumu sana.Ndizo sheria za dunia ambazo ni tofauti kabisa na hizi tunazozitunga sisi wanadamu.

Sasa akitokea mtu aliyekuwa na mihela mingi sana akafilisika unamcheka au unamsikitikia?Ni swali ambalo wala sitaki jibu lake kutoka kwako.Kaa nalo moyoni mwako.Jijibu mwenyewe kisha jiangalie vizuri kwamba u-binadamu wa aina gani. Hayo ndio maudhui ya Zilipendwa Friday Session ya BC.Wimbo unaitwa Kufilisika Sio Kilema na ni kutoka kwa Orchestra Makassy ambayo ilikuwa miongoni mwa zile bendi zilizoitwa The Giants Of East Africa.Burudika na furahia wikiendi yako.

Kama una special request,tuma ombi lako kupitia bongocelebrity at gmail.com

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Be Sociable, Share!

Feedback / Comments

Leave a Reply