Rafiki yangu mmoja aliponipigia simu na kuniuliza kama nimeiona video ya Naibu Waziri wa Elimu Tanzania akielezea Tanzania kuwa Muungano wa Visiwa Vya Pemba na Zimbabwe na Tanzania Bara yaani Tanganyika, nilidhani ananitania. Akanihakikishia kwamba hatanii. Nilipopata muda nilitulia na mimi mwenyewe kujionea na kisha kuona itakuwa kosa la jinai kutoiweka clip hii hapa ili nawe msomaji(kama hujaiona) upate kufanya hivyo…
Labda niweke wazi kwamba tunaweza kusema kwamba neno “Zimbabwe” ilikuwa ni kuteleza tu kwa ulimi kwani kwenye PowerPoint iliyokuwa inaendelea macho yangu yameona “Zanzibar”.Kilichonigusa zaidi ni aina yenyewe ya Presentation.Yaani kweli kuna haja ya kwenda kote ulikotoka na kwenda kuanza kuwafundisha watu historia ambayo imeandikwa vilivyo na ninaamini idadi kubwa ya wahudhuriaji wanaielewa (pengine kumshinda Naibu Waziri). Na wapi matumizi sahihi ya herufi R na L katika matamshi?Upo wapi weledi wa kuonyesha kwamba huyu ni Naibu Waziri wa Elimu na anajua anachokiongelea?
Na ukitaka kujua tofauti nyingine,tizama tu hotuba au mawasilisho ya Mawaziri wengine wa elimu kutoka nchi zingine waliozungumza katika mkutano huo huo! Kisha #tujipime.
Swali langu linakwenda kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete; hivi watu kama hawa wanapataje kuwa katika kiini cha serikali yako?Unatumia njia gani kuchekecha watu unaowapa dhamana ya kuwa Mawaziri au Manaibu Waziri kama huyu?!
Feedback / Comments
7 Responses to “HUYU NDIYE MDAU NAMBA MBILI WA ELIMU NCHINI MWETU?”
Leave a Reply




sending...

mbaya zaidi alikuwa anasoma…inaelekea hata kusoma hawezi basi. ingekuwa inatoka kichwani madudu yangetisha.
Nimeona sio kipisi ulichokionyesha bali mlolongo mzima wa hotuba zilizotolewa siku hiyo. Tatizo naliona ni la kibinadamu tu hapo, kumbuka alitoa presentation yake baada ya waziri wa Zimbabwe.
Jeff yaani amesema kwa uhakika kabisa, na kama unajisikia mwenyewe basi unachukua fursa hiyo kujirekebisha. Muheshimiwa ametuangusha sana!
Nilipo iyona hii tumbo lilinisokota khafla nikawa ninatapika, duhhh hivi kweli Rais anatuikejeli Tanzania kiasi hichi??? hivi hebu tujiulize swali la kijinga, Rais hutumia kigezo gani kuchagua na kuteuwa mawaziri wake?? Elimu yako au Ukaribu wako?? na kama jawabu ni Elimu yako basi huyu kampiga Rais za kichwa (vyeti kanunua) na kama jawabu ni ukaribu wako na Rais basi haina haja ya Watanzania wengine kupoteza mda wa kusoma kumbe anochaguliwa ni huyu… Kidumu chama cha mapinduzi..!
Nilipo iyona hii tumbo lilinisokota khafla nikawa ninatapika, duhhh hivi kweli Rais anatuikejeli Tanzania kiasi hichi??? hivi hebu tujiulize swali la kijinga, Rais hutumia kigezo gani kuchagua na kuteuwa mawaziri wake?? Elimu yako au Ukaribu wako?? na kama jawabu ni Elimu yako basi huyu kampiga Rais za kichwa (vyeti kanunua) na kama jawabu ni ukaribu wako na Rais basi haina haja ya Watanzania wengine kupoteza mda wa kusoma kumbe anochaguliwa ni huyu… Kidumu chama cha mapinduzi..!
Read more: HUYU NDIYE MDAU NAMBA MBILI WA ELIMU NCHINI MWETU? – BongoCelebrity
Ukipanda mchicha utauvuna huo huo mchicha ulioupanda, ninyi si mmepanda RUSHWA sasa makelele ya nini??
Sijawahi kuona RUSHWA mpaka mochwari,Hospital,posta,barabarani kwa ufupi kila kitu TZ ni Rushwa tu na bado mtajipanga tu na maujinga yenu.
tatizo la nchi yetu,vyeo tunagaiana.hiyo ndio hasara yake.wakati kuna watu wenye uwezo mkubwa kuliko wake wangewakilisha vizuri tu.uongeaji wake,hajiamini kabini kabisa,hapo atajitetea nini?