AY AIBUKA MSHINDI TUZO ZA CHANNEL O.

Msanii AY kutoka nchini Tanzania usiku huu ameibuka mshindi katika Tuzo Za Video Za Muziki za Kituo Cha Televisheni Cha Channel O cha nchini Afrika Kusini(Channel O Music Video Awards) zilizorushwa “Live” na kituo hicho kutokea South Africa.
AY ameibuka mshindi katika kipengele cha MOST GIFTED EAST AFRICAN VIDEO OF THE YEAR kutokana na video ya wimbo I Don’t Wanna Be Alone ambao amewashirikisha kundi la Sauti Sol la nchini Kenya.
BC inapenda kuungana na watanzania wote na hususani wapenzi wa muziki wa kizazi kipya katika kumpongeza AY kwa tuzo hiyo.Wengine aliokuwa akiwania nao tuzo hiyo katika kipengele hicho  ni;
  • Keko Feat. Madtraxx – Make You Dance
  • Camp Mulla – Party Don’t Stop
  • AY feat Sauti Soul – I Don’t Want To Be Alone
  • K’Naan Feat. Nas – Nothing To lose
  • Navio – One & Only
Unaweza pia kuona taarifa zao zaidi  kwa kubonyeza hapa.
Hii hapa ndio video ya ushindi
You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity