BREAKING NEWS: MBUNGE NA WAZIRI WA ZAMANI,JACKSON MAKWETA,AFARIKI DUNIA!

Mbunge wa Njombe wa muda mrefu  na mwanasiasa wa siku nyingi nchini, Mzee Jackson Myangila Makweta,amefariki  dunia jioni hii jijini Dar-es-salaam, kutokana na matatizo ya moyo  ambayo yalikuwa yakimsumbua.

Mbali ya kuwa miongoni mwa wabunge walioongoza majimbo yao kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Tanzania, Jackson Makweta pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikalini ya Tanzania zikiwemo zile za uwaziri(wa wizara mbalimbali),

BC inapenda kuungana na watanzania wote katika kuomboleza msiba huu na kutoa pole nyingi kwa ndugu,jamaa na marafiki na hususani familia yake. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amen

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity