PICHA HII NA VIDEO HIZI ZINASHIKILIA REKODI YA DUNIA: UNAJUA NI REKODI GANI?

Picha iliyowekwa na timu ya kampeni ya Rais Barack Obama dakika chache tu tangu ilipokuwa dhahiri kwamba Rais huyo amemshinda mpinzani wake, Mitt Romney, katika uchaguzi mkuu wa Marekani 2012, mpaka hivi sasa ndio inayoshikilia rekodi ya Twitter ya kuwa picha ambayo imekuwa retweeted  mara nyingi zaidi katika historia ya mtandao huo wa kijamii. Mpaka juzi Jumapili, kwa mujibu wa jarida la mtandaoni la The Daily Beast, picha hiyo ilikuwa imekuwa retweeted zaidi ya mara 816,000!

Picha hiyo inayomuonyesha Rais Obama akiwa amekumbatiwa vyema na mkewe, Michelle Obama, ilipigwa na mpiga picha wa kampeni ya Obama,Scout Tufankjian, tarehe 15 August,2012 huko Dubuque,Iowa wakati wa kampeni. Picha hiyo iliwekwa katika mtandao wa Twitter ikiwa na maneno “Four More Years” kumaanisha kwamba Obama ataendelea kuwa Rais wa Marekani kwa kipindi kingine cha miaka mine baada ya kuibuka mshindi.

Picha hiyo pia mpaka hivi sasa imeweka rekodi ya kuwa picha “iliyopendwa” zaidi katika mtandao mwingine wa kijamii,Facebook. Tangu siku hiyo ya uchaguzi(Novemba 6) picha hiyo imependwa zaidi ya mara 4.5 milioni.

Kwa upande wa video za mtandaoni na hususani mtandao maarufu wa video za mtandaoni wa YouTube, video ya mwanamuziki Justin Bieber,(mzaliwa wa Canada) ya wimbo Baby ambamo amemshirikisha Ludacris mpaka sasa unashikilia rekodi ya kuwa video ambayo imetazamwa mara nyingi zaidi. Mpaka ninapoandika post hii(Jumatatu tarehe 19 November,2012), video hiyo imeshatizamwa mara 801,803,802. Hii ni habari njema kwa wanangu Ray na Nelson ambao ni wapenzi wakubwa wa wimbo huu!

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 Kwa karibu video ambayo inaikaribia ya Bieber na inatazamwa kwa karibu kama video ambayo itakuja kuvunja rekodi ni ile ya mwanamuziki Psy kutoka nchini Korea Kusini na wimbo wake wa Gangnam Style. Mpaka ninapoandika post hii, video hiyo imetizamwa mara 768,449,959.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 Unaijua video kutoka Tanzania ambayo imetizamwa mara nyingi zaidi mtandaoni?Utafiti unaendelea…

 

 

 

 

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity