“DADA LEMI”- TABORA JAZZ (ZILIPENDWA)

Kwa mapana na marefu hii imekuwa wiki ngumu sana kwangu. Kuona ya kwamba ningali nadunda na nipo hapa nimeketi na kuanza kuandika hiki ninachoandika, ni ushuhuda tosha kwamba Mwenyezi Mungu bado yungali ana madhumuni na maisha yangu! Ni jambo linalotia faraja.

Wakati nawaza na kujaribu kuchagua wimbo wa kuweka katika segment hii ya kila Ijumaa ya Zilipendwa, nilijishtukia nakumbuka baadhi ya mikoa na bendi kutoka katika mikoa hiyo ambayo niliwahi kutembelea na kuishi. Mojawapo ya mikoa hiyo ni Mkoa wa Tabora ambako mpaka leo bado nina ndugu wengi tu. Nakumbuka babu mmoja aliyekuwa akituuzia “mantalali”. Naikumbuka mitaa ya Isevya, Chuo Cha Uhazili Tabora(Mama zangu wadogo wamesoma pale). Nakatiza toka mjini na kupitia shule ya Sekondari Uyui. Pale nawacheki wajomba wanaosoma pale. Nakatiza mitaa,pembezoni kuna miti ya miembe, jua la mchana limeshakolea.Joto linalotoka kwenye mchanga sio kawaida. Nalihisi vilivyo ingawa nimevaa raba zangu kutoka “Bora” ambazo Babu alinipa kama zawadi ya Christmas…

Nilipowaza Tabora ndipo nikaanza kutafuta wimbo kutoka kwa Tabora Jazz ambayo ni miongoni mwa bendi zilizowahi kutamba vilivyo enzi zile. Nikausikiliza wimbo Dada Lemi(Lemmy)….huu hapa.Na wewe usikilize na uwe na weekend njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha kwa hisani ya Kijiwe Cha Kitime

 1. Kitime, 21 December, 2012

  Nakumbuka siku nimenunua santuri hii, ikiwa na label ya SABASABA. Picha ni ya Tabora Jazz lakini hii ilikuwa awamu kabla ya group iliyorekodi Lemmy

 2. bongocelebrity, 21 December, 2012

  Asante Kitime kwa kupita hapa na kutoa machache…Wewe ni hazina katika historia ya muziki wa hapo awali.I salute you Bro.

 3. Ramadhani KUBIHA, 21 December, 2012

  Nawapa hongera sana wote waliofanya jitihada ya kutuwekea kazi hii azizi hakika nanyi mmefikiri jambo la maana,Dooooh inatukumbusha maisha halisia ya Mtanzania , hongera sana.

 4. Ntayega hamissi, 29 December, 2012

  Segere matata, ndio yenyewe ilikuwa haina mpinzina, ile mipini ya akina Kassim Karuona na shem karenga ilikuwa haina mpinzani

 5. Paul Alphonce, 27 March, 2014

  Asante braza Kitime kwa kutujali

Copyright © Bongo Celebrity