“JOTO HASIRA”-LADY JAY DEE Feat. PROF.JAY(BRAND NEW TRACK)

Kila kizazi kina legends wake. Kama ulizaliwa na kuyaruka majoka enzi zile, basi wanamuziki waliotamba enzi zile ndio legends wako. Of course wapo legends ambao huvuka kutoka kizazi kimoja mpaka kingine na kuendelea kukubalika. Hao ni wachache. Huko kuna majina makubwa kama vile Bob Marley, Michael Jackson, Elvis Presley, Jim Reeves nk.

Katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya, Lady Jay Dee na Professor Jay ni legends. Wamekuwepo kitambo na bado wapo. Muite Lady JayDee, Binti Machozi, Komando nk utakuwa unamzungumzia mwanadada Judith Wambura ambaye leo hii anaweza kabisa kuandika kitabu kuhusu maisha yake katika sanaa ya muziki ndani na nje ya Tanzania na mtu akakinunua na kukisoma bila kuhisi kuibiwa.

Professor Jay (jina kamili Joseph Haule) naye ana historia ndefu hivyo hivyo. Alikuwepo tangu muziki huu wa kizazi kipya unaanza kushika kasi. Wimbo wake ‘”Chemsha Bongo’ alipokuwa na kundi la Hard Blasters unaaminika kuwa wimbo uliowafungua masikio wazazi wengi kiasi kwamba wakaanza kuukubali muziki wa kizazi kipya kama muziki na sio “uhuni”.

Historia inaonyesha kwamba Lady JayDee hawajashirikiana katika nyimbo nyingi. Waliwahi kufanya hivyo katika wimbo wa Professor Jay unaoitwa Bongo Dar-es-Salaam ambao ni miongoni mwa “classics’ za muziki wa kizazi kipya.

Baada ya kimya cha muda mrefu kwa pamoja au katika ushirikiano, hawa hapa tena. Ni Lady JayDee akimshirikisha Professor Jay katika wimbo Joto Hasira. Usikilize hapo chini;

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity